MWANANCHI
Wakati vikao vya juu vya CCM vikikaribia
kuanza mchakato wa kumpata mgombea Urais wa chama hicho, mji wa Dodoma
umeanza kupokea wageni kutoka maeneo mbalimbali.
Uchunguzi uliofanywa na Gazeti la
Mwananchi kwenye maeneo ya katikati ya mji wa Dodoma hadi jana, umebaini
kuwa tayari nyumba nyingi za kulala wageni na hoteli zimeshajaa.
Baadhi ya wajumbe wa vikao hivyo ni
wabunge ambao tayari wako Dodoma wakiendelea na Bunge, wengine ni
wapambe wa makada waliokuja kurejesha fomu za kuwania Urais ambao
hawajaondoka.
Baadhi ya Mameneja wa hoteli hizo
walisema watu hao wataondolewa kuanzia Julai 6 iwapo hawatakuwa miongoni
mwa waliopangiwa vyumba, huku kukionekana pia baadhi ya wenyeji
wameanza kukarabati nyumba zao kwa ajili ya kupangisha wageni
mbalimbali.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, David Misime amewahakikishia wageni kuwa Jeshi lake limejiandaa vizuri kwa ugeni huo mkubwa utakapoingia, kuishi na hadi kuondoka.
MWANANCHI
Hali tete ndani ya Ukumbi wa Bunge jana iliendelea kutanda wakati Spika Anne Makinda
alipolazimika kuahirisha kikao asubuhi kutokana na kelele na baadaye
Wabunge saba wa upinzani kuadhibiwa, wakiwamo watano waliozuiwa
kuhudhuria hadi kumalizika kwa Bunge la 10.
Hali hiyo ndani ya Bunge iliendelea kwa
siku ya pili mfululizo na mara zote kusababisha Spika kuahirisha vikao
baada ya shughuli za Bunge kushindwa kuendelea kutokana na kelele za
wapinzani wanaopinga kitendo cha kuwasilishwa miswada mitatu kwa hati ya
dharura wakidai hakuna haja ya haraka hiyo.
Jana Spika Makinda aliibuka na dawa mpya na kuitumia Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuwaadhibu wabunge hao saba.
Wabunge John Mnyika, Moses Machali, Tundu Lissu, Felix Mkosamali na Paulin Gekul wamefungiwa kushiriki vikao kuanzia leo hadi Bunge litakapovunjwa Julai 9.
Wabunge wengine wawili, Mchungaji Peter Msigwa na Rajab Mbarouk
wamefungiwa kushiriki vikao viwili kuanzia leo baada ya Kamati hiyo
kuwatia hatiani wawakilishi hao wote saba kwa kudharau mamlaka ya Spika.
Wengine watatu, Joseph Selasini, Khalifa Suleiman Khalifa na Rajabu Abdalah walitakiwa kufika mbele ya kamati hiyo leo saa 4:00 baada ya wito wa kuwataka wahudhurie jana kuchelewa.
“Mashtaka yetu yaliendeshwa kwa haraka, hatukupatiwa muda wa kutosha kujieleza wala kumtumia wakili,” alisema Machali baada ya Bunge kuahirishwa.
Mbunge Tundu Lissu alisema ni bora kufukuzwa kuliko kuendelea kushuhudia gesi ya Watanzania ikiuzwa kwa nguvu bila ya huruma… Mchungaji Msigwa alisema hata angefungiwa kushiriki vikao vyote, asingeathirika.
Usisumbuke Mawerenewz.blogspot.com ndio mtandao wako wakipekee unaokupa habari za BURUDANI,MICHEZO, SIASA, na HABARI MBALIMBALI ZA KIMATAIFA pamoja na KITAIFA Endelea kutembelea MTOKA MBALI pia nifuate twitter>>>@mawere3, facebook>>>Mawere Mtoka Mbali, Instagram>>>mawere_mtoka_mbali,