Showing posts with label HEALTH CORNER.. Show all posts
Showing posts with label HEALTH CORNER.. Show all posts

18 February, 2016

High-sugar diet is as 'damaging to your brain as extreme stress or ABUSE'

High-sugar diet is as 'damaging to your brain as extreme stress or ABUSE'

  • Sugar found to be as damaging as early life stress, scientists discover
  • Chronic sugar intake triggers changes to hippocampus the area of the brain, which is important for both memory and stress
  • Experts say changes noted in the brain are of 'great concern' given the high consumption of sugary drinks, particularly among young people
  • Jayanthi Maniam and Professor Margaret Morris were involved in the study at the University of New South Wales, Australia
  •    
    There has been a seismic shift in the dietary landscape in recent years.
    Where once fat was the much maligned enemy, now scientists are turning their attention to sugar.
    It is now widely accepted that more must be done to encourage people to reduce their sugar intake.
    So much so that dietary guidelines in the UK and US have been altered to reflect the changing scientific evidence.
    The World Health Organization recommends no more than 10 per cent of a person's daily energy should come from added sugars, or those found naturally in juices and honey.
    That equates to around 50g or 12 teaspoons a day.
    While the links between a high-sugar diet and obesity are well documented, in light of the mounting evidence, experts are turning their attention to the other ways sugar can affect the body.
    In a recent study, a team at the University of New South Wales in Australia, found sugar is as damaging to the brain as extreme stress or abuse.
    Here research associate, Jayanthi Maniam and profressor of pharmacology, Margaret Morris discuss their findings.
    Sugar is just as damaging to the brain as extreme stress or abuse, experts in Australia have warned 
    We all know that cola and lemonade aren’t great for our waistline or our dental health.
    But our new study has shed light on just how much damage sugary drinks can also do to our brain.
    The changes we observed to the region of the brain that controls emotional behaviour and cognitive function were more extensive than those caused by extreme early life stress.
    It is known that adverse experiences early in life, such as extreme stress or abuse, increase the risk of poor mental health and psychiatric disorders later in life.
    The number of traumatic events - accidents; witnessing an injury; bereavement; natural disasters; physical, sexual and emotional abuse; domestic violence and being a victim of crime - a child is exposed to is associated with elevated concentrations of the major stress hormone, cortisol.
    There is also evidence that childhood maltreatment is associated with reduced brain volume and that these changes may be linked to anxiety.
    Looking at rats, we examined whether the impact of early life stress on the brain was exacerbated by drinking high volumes of sugary drinks after weaning. 
    As females are more likely to experience adverse life events, we studied female Sprague-Dawley rats.
    To model early life trauma or abuse, after rats were born half of the litters were exposed to limited nesting material from days two to nine after birth.
    They then returned to normal bedding until they were weaned. 
    The limited nesting alters maternal behaviour and increases anxiety in the offspring later in life.
    At weaning, half the rats were given unlimited to access to low-fat chow and water to drink, while their sisters were given chow, water and a 25 per cent sugar solution that they could choose to drink.
    Animals exposed to early life stress were smaller at weaning, but this difference disappeared over time. 
    Rats consuming sugar in both groups (control and stress) ate more calories over the experiment.
    Changes  to the brain region  that controls emotional behaviour and cognitive function were more extensive than those caused by early life stressThe rats were followed until they were 15 weeks old, and then their brains were examined. 
    As we know that early life stress can impact mental health and function, we examined a part of the brain called the hippocampus, which is important for both memory and stress. 
    Four groups of rats were studied – control (no stress), control rats drinking sugar, rats exposed to stress, and rats exposed to stress who drank sugar.
    We found that chronic consumption of sugar in rats who were not stressed produced similar changes in the hippocampus as seen in the rats who were stressed but not drinking sugar. 
    Early life stress exposure or sugar drinking led to lower expression of the receptor that binds the major stress hormone cortisol, which may affect the ability to recover from exposure to a stressful situation.
    Another gene that is important for the growth of nerves, Neurod1, was also reduced by both sugar and stress. 
    Other genes important for the growth of nerves were investigated, and just drinking sugar from a young age was sufficient to reduce them.
    The rats were exposed to high sugar intakes during development, and the impact of the sugar is worrying as it may affect brain development, although further work is required to test this.
    In this study, combining sugar intake and early life stress did not produce further changes in the hippocampus, but whether this remains the case over time is unclear.
    These findings suggest future work should consider possible long-term effects of high sugar intake, particularly early in life, on the brain and behaviour, the scientists conclude
    The changes in the brain induced by sugar are of great concern given the high consumption of sugar-sweetened beverages, with particularly high consumption in children aged nine to 16 years. 
    If similar processes are at play in humans to what was found in our rat study, reducing the consumption of sugar across the community is important.
    The fact that drinking sugar or exposure to early life stress reduced the expression of genes critical for brain development and growth is of great concern. 
    While it is impossible to perform such studies in humans, the brain circuits controlling stress responses and feeding are conserved across species.
    People who were exposed to early life trauma have changes in the structure of their hippocampus. In humans, those consuming the most 'western' diet had smaller hippocampal volumes, in line with data from animal models.
    Taken together, these findings suggest future work should consider possible long-term effects of high sugar intake, particularly early in life, on the brain and behaviour.

    10 December, 2015

    Madaktari kupandikiza uume Marekani ili kumuwezesha mgonjwa kufanya tendo la ngono

    post-feature-imageUpasuaji umepangwa kufanyika kwa mara ya kwanza kupandikiza uume nchini Marekani, kwa lengo la kuwasaidia mpiganaji wa zamani. Upasuaji huo wa saa 12- utahusisha ushonaji wa neva muhimu na mishipa ya damu kwa ajili ya kutunza mkojo na kumuwezesha mgonjwa kufanya tendo la ngono.

    Upasuaji huu unafuatia mafanikio ya kwanza kabisa ya upandikizaji wa uume nchini Afrika kusini mwaka jana. Jopo la madaktari kutoka Hospitali ya chuo kikuu cha Hopkins (JHU) wanapanga kumfanyia upasuaji huyo mwanajeshi wa zamani mwenye umri wa miaka 60kama sehemu ya majaribio.

    Hatua ya kwanza ya upasuaji huo itaanza kwa kuondoa uume kutoka kwa kijana aliefariki ambaye alijitolea kutoa uume wake kwa ruhusa ya familia yake. Kwa mujibu wa jopo la madakatari katika JHU matumaini ya mwanajeshi huyo wa zamani ni kwamba hisia za uume wake zitarejea katika muda wa miezi 12.

    Uwezekano wa mgonjwa kupata watoto, utategemea kiwango cha jeraha na mafanikio ya upasuaji huo. Lakini Wanasayansi wanasema kutokana na kwamba ni upasuaji mmoja wa kupandikiza uume uliofanyika, madaktari watakua makini kuhakikisha kuna matumaini ya kweli.

    08 December, 2015

    Utafiti uliofanywa umeonyesha Unene wa mwanaume huathiri mbegu za kiume

    post-feature-image
    Utafiti uliofanywa nchini Denmark umeonyesha uzani wa mwanamume huathiri seli za mbegu za kiume na huenda ukachangia katika kuwafanya watoto wanaozaliwa kuwa wanene

    Seli za mbegu za kiume za wanaume wembamba na wanaume wanene zilikuwa na taarifa tofauti za kijenetiki, jambo ambalo huenda linaathiri utendaji wa chembe za kijenetiki.

    Dkt Romain Barres, aliyesaidia katika utafiti huo alisema awali ilikuwa imebainika kwamba: “Mwanamke anapokuwa mjamzito anafaa kujitunza vyema. Lakini utafiti huu unaonyesha wanaume wanafaa pia kuangalia uzani wao.”

    Utafiti huo ulifanywa kwa wanaume sita walionenepa kupindukia na ambao walikua wakisaidiwa kupunguza uzani. Watafiti walichunguza mbegu za kiume za wanaume hao kabla na baada ya kupunguza uzani baada ya mwaka mmoja.

    Dkt Romain Barres mtafiti mkuu wa ripoti hii amesema waligundua tofauti iliyokuwepo kwa wanaume hao. Utafiti unasema kwamba zeli za mbegu za wanaume walionenepa husababisha mabadiliko ya tabia.

    Aidha ripoti imeonya wanawake walio na mimba kuwa waangalifu sana hasa ikiwa walitunga mimba hizo wakiwa na wanaume walionenepa sana. Dkt Barres amesema wanaume walionenepa sana husababisha jeni zao kuanza kutamani kula chakula kila mara.

    Ameongeza kwamba uzani wa mtu pia unaambatana na ukuaji wa akili. Utafiti huu uliochukua miaka mitano pia ulitofautisha wanaume 13 wenye uzani wa kadiri na 10 walionenepa zaidi. Hapo ikagunduliwa kwamba, wote walikua na tabia tofauti na zilizochochewa na mabadiliko ya seli kwenye mbegu za kiume.

    Utafiti pia unasema uzani wa baba unaweza kusaidia, wanawe. Utafiti unasema kwa kula sana baba watoto pia huwahimiza wanawe kula sana ili wakue kwa haraka. Prof Allan Pacey amesema utafiti huu umebainisha kwamba baadhi ya tabia za watoto zimechangiwa na zilizokua mbegu za kiume za baba yao


    04 December, 2015

    Mwanamke aliyekataa matibabu ya figo kuokoa maisha yake akidai amepoteza mng’ao afariki

    post-feature-imageMwanamke aliyekataa matibabu ya figo kuokoa maisha yake nchini Uingereza, akisema ameshapoteza mng’ao, amefariki. Mwanamke huyo wa umri wa miaka 50 aliyetambuliwa tu kama C, aligonga vichwa vya habari baada ya jaji kuamua kwamba ana haki ya kukataa kupokea matibabu ya kusafisha damu.

    Figo za C ziliharibika baada yake kunywa dawa kupita kiasi akitaka kujiua. Mahakama iliambia kwamba katika maisha yake, C aliangazia zaidi "sura yake, wanaume na vitu vya thamani.”

    Mmoja wa bindi zake aliambia mahakama: “Kupona kwake si kwamba figo zake zianze kufanya kazi tena pekee, bali atahitaji kupata ‘mng’ao’, jambo ambalo anaamini hawezi kuapata tena kutokana na umri wake.”

    Mwaka uliopita, C alikuwa amepatikana na saratani ya matiti lakini akakataa matibabu akisema matibabu hayo yangemfanya kuwa mnene.

    Baada ya kupata matatizo ya figo, wakfu wa Huduma ya Taifa ya Afya Uingereza katika hospitali ya King’s College ulitaka alazimishwe kupokea matibabu. Lakini Jaji MacDonald, kwenye uamuzi alioutoa Novemba 13, alisema C ana uhuru wa kufanya uamuzi.
    House of Entertainment, News, Gossip, Music and Videos!

    31 October, 2015

    Wewe ni mtumiaji wa vilevi? haya ni mambo ya muhimu unayopaswa kufahamu kuhusiana na Vilevi


    “Haiuzwi kwa wenye umri chini ya miaka 18, kunywa kistaarabu” ujumbe huu unapatikana katika matangazo yote ya vilevi, na nadhani hilo linatambulika kwamba pombe si ya vijana chini ya miaka 18. Unywaji wa pombe ni kawaida kwa watu wengi lakini unakunywa kistaarabu? Sina mpango wa kukufundisha kunywa pombe wala kukushawishi uanze kunywa Pombe wote tunajua madhara yanayoletwa kwa unywaji wa pombe wa kupindukia. Leo tuongelee upande wa pili wa shilingi, faida za unywaji wa pombe kwa wastani. Narudi unywaji wa pombe kwa wastani.
    Magonjwa ya Moyo.
    Utafiti kutoka  Harvard University  Marekani, umegundua unywaji wa pombe kwa kiasi cha wastani kinasaidia mzunguko mzuri wa damu,hii inasaidia kuzia matatizo ya moyo na magonjwa ya kiharusi na kupooza (stroke)
    Urefusha Maisha
    Utafiti uliofanywa na Catholic University  huko Campobasso, waligundua kuwa kunywa chupa chini ya 4 au 2 kwa siku kwa mwanamme au mwanamke,  kwa asilimia  18 inaongeza muda wa kuishi kama  ililipotiwa na Reuters. Dr. Giovanni de Gaetano  wa Catholic University  pia alisema sio mbaya kama unaweza kunywa pombe kidogo wakati wa kula. Makala nyingine iliyoandikwa na Mediterranean diet, kuwa mvinyo (wine) ni kinywaji safii wakati wa chakula cha mchana na cha jioni. Lakini usinywe tu pombe wakati wote.
    Inasaidia kuamsha Hisia za Mapenzi
    Kama ilivyo Red Wine inasaidia kupunguza kasi ya magonjwa ya moyo, Mwaka 2009 jarida lililotambulika kama Sexual Medicine, liliandika kwa utafiti waliofanya  asilimia 25 – 30 wanywaji wa pombe hawapati matatizo ya kushindwa kushiriki tendo. Mkuu wa utafiti , Kew-Kim Chew Mtaalamu wa magonjwa ya mlipuko kutoka University of West Australia alifanya utafiti kwa wanaume  1,770 wa Australia,  Chew aliwashauri pia wanaume hao wasitumie pombe kupitiliza sababu bado wanafanya utafiti juu ya swala hilo kwa kina zaidi.

    Pombe huamsha Akili
    Utafiti uliohusisha watu zaidi ya 365,000 toka mwaka 1997 iliripotiwa na jarida la Neuropsychiatric Disease and Treatment watu wanaokunywa kwa wastani wanauwezo wa kuzuia ugonjwa wa Alzheimer na magonjwa mengine ya akili. Kiwango kidogo cha pombe kinafanya seli za ubongo ziwe hai (fit/active) alisema Edward J. Neafsey, Ph.D mwandishi wa Science Daily. alisema pia hawashauri watu wasiokunywa pombe waanza kunywa pombe. Na akasema kama wale wanaokunywa wanakunywa kwa wastani basi itawasaidia.
    Husaidia Tatizo La Mawe kwenye Kibofu
    Kwa wanywaji wa wastani kuna uwezekano wa kupunguza uwezekano wa kupata  tatizo la mawe kwenye kibofu huo ni  utafiti uliofanywa na University of East Anglia, watafiti walisema faida zinaonekana kwa wale wanywaji wa kawaida na sio waywaji wa pombe kupinduki  sababu unywaji wa pombe kupitiliza huleta matatizo ya kiafya
    Ugonjwa wa Sukari
    Tafiti zilizofanywa uholanzi,  watu wenye afya wanao kunywa glass moja au mbili kwa siku wanapunguza uwezekano wa kupata aina ya pili ya kisukari ukiachilia mbali wale wasiokunywa hata kidogo, wale wanaokunywa kidogo wana afya zaidi, walisema watafiti hao kupitia Reuters.
    Angalizo kujua faida hizi za pombe haina maana kama hujaanza kunywa pombe uanze sasa na kama wewe unatumia kilevi basi kunywa kwa kiwango kidogo sababu ni faida kwa afya yako kuliko unywaji wa kupindukia. Kunywa kistaarabu.

    30 August, 2015

    Fahamu kuhusiana na Ugonjwa wa Kipindupindu, Dalili zake na jinsi ya kujikinga

    Kipindupindu ni ugonjwa wa kuharisha na  kutapika unaosababishwa na vimelea vya bacteria vinavyoitwa kwa lugha ya kitaalam “Vibrio cholera”.

    CHANZO CHA UGONJWA


    • Vimelea vilivyomo kwenye kinyesi na matapishi ya mgonjwa wa kipindupindu.
    • Vimelea vilivyomo kwenye kinyesi cha mtu bila yeye binafsi kuonyesha dalili zozote za ugonjwa.


    DALILI ZA UGONJWA WA KIPINDUPINDU.

    Mgonjwa wa Kipindupindu huwa na dalili zifuatazo:

    • Kuharisha mfululizo au mara kwa mara bila tumbo kuuma ambako kunaweza kuambatana na kutapika.
    • Kinyesi au matapishi huwa ya maji maji yasiyo na harufu, yanayofanana na maji yaliyooshewa mchele.
    • Kusikia kiu sana, macho kudidimia na ngozi kusinyaa ambavyo hutokana na upungufu wa maji mwilini.
    • Kuishiwa nguvu, kuhema haraka haraka na kulegea. Hali hii hutokana na upungufu wa maji na madini mwilini.


    KIPINDUPINDU KINAVYOENEA.


    • Kula chakula au kunywa kinywaji chochote kilicho na vimelea vya ugonjwa wa kipindupindu kwa mfano:-


    1. Kunywa maji yasiyochemshwa.
    2. Kula chakula kilichoandaliwa katika mazingira ambayo siyo safi.
    3. Kula matunda yasiyooshwa kwa maji safi na salama.
    4. Kunywa pombe za kienyeji zilizoandaliwa katika mazingira machafu au kunywea katika vyombo vichafu.
    5. Kula mboga za majani, kachumbari na saladi bila kupikwa au kuziosha kwa maji safi na salama.


    • Kula chakula au kumlisha mtoto bila kunawa mikono kwa sabuni na maji safi na salama yanayo tiririka.
    • Kuosha au kuhudumia mwili wa mtu aliyekufa kwa ugonjwa wa kipindupindu bila kujikinga.
    • Kunawa mikono kwenye chombo kimoja kwa mfano ndani ya bakuli au beseni kabla ya kula chakula.
    • Kutotumia choo au utupaji ovyo wa kinyesi.
    • Kutonawa mikono baada ya kutoka chooni.
    • Kuweka mazingira katika hali ya uchafu mfano kutupa taka ovyo bila kuzingatia kanuni za afya..
    • Kula vyakula vilivyopoa na visivyofunikwa.
    • Kutiririsha maji ya chooni ardhini na hivyo kusababisha uchafuzi wa vyanzo vya maji na chakula.

    Inzi huchangia kueneza ugonjwa wa kipindupindu kwa tabia zake za kutua chooni kwenye kinyesi, uchafu na hata vyakula na vinywaji.

    MADHARA YA KIPINDUPINDU


    1. Hofu miongoni mwa jamii katika sehemu yenye mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.
    2. Kifo kutokana na ukosefu wa maji na madini mwilini baada ya kuharisha na kutapika sana.
    3. Kushuka kwa uchumi kutokana na familia/jamii kuacha shughuli za uzalishaji mali ili kumuhudumia mgonjwa na kushiriki katika misiba.
    4. Serikali hutumia fedha nyingi kwa ajili ya dawa, posho kwa watumishi katika kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu.


    JINSI YA KUJIKINGA NA KIPINDUPINDU


    • Kujenga choo bora na kukitumia Ipasavyo
    • Kufunika tundu la choo na kufunga mlango baada ya matumizi yake.
    • Kunawa mikono kwa maji safi na salama kwa kutumia sabuni baada ya:.

    -      kutumia choo.
    -      kumtawaza mtoto na kabla ya kula au kumlisha motto.

    • Kula chakula kikiwa bado moto na kufunika chakula kilichoandaliwa tayari kwa kuliwa.
    • Kunywa maji yaliyochemshwa na kuhifadhiwa katika chombo kisafi na salama.
    • Kusafisha vyakula vinavyoliwa vibichi (kama vile matunda na mboga) kwa kutumia maji safi na salama yanayotiririka.
    • Kuhakikisha usafi wa mazingira ya vilabu/baa, wahudumu na vyombo vitumikavyo. Pombe za kienyeji ziandaliwe kwa maji yaliyochemshwa.
    • Weka mazingira katika hali ya usafi.
    • Kumbuka, kuchuja maji yaliyochemshwa kunaweza kuchafua maji kwa kuingiza vimelea.Hivyo, chuja maji kabla ya kuyachemsha.


    KUHUDUMIA MGONJWA

    Mgonjwa wa kipindupindu hupoteza maji mengi na madini muhimu mwilini anapoharisha na kutapika. Ili kuokoa maisha ya mgonjwa ni muhimu kuchukua hatua zifuatazo:

    • Mpe mgonjwa dawa ya mchanganyiko wa sukari na chumvi(ORS), maji, uji mwepesi, supu nk. mara kwa mara.
    • Mpeleke mgonjwa haraka iwezekanavyo katika kituo cha afya/zahanati/ hospitali au kituo cha kutibu kipindupindu kilicho karibu nawe.
    • Matapishi na kinyesi cha mgonjwa ni hatari kwa afya yako. Kwa hiyo nguo na vitu vingine vilivyochafuliwa na mgonjwa vilowekwe kwenye kemikali maalumu (mfano Jik) au vichemshwe ili kuua vimelea vya kipindupindu na kasha visafishwe kwa sabuni.
    • Ndugu waliokuwa wakiishi na mgonjwa au wale wanaomhudumia wahakikishe wanapata dawa za kinga dhidi ya kipindupindu.

    Angalizo:

    Ni lazima wakati wote kuwa msafi ili kuzuia vimelea vya ugonjwa visiingie kinywani kwako kwa njia zilizotajwa hapo juu.

    Tahadhari:

    Maiti ya mgonjwa wa kipindupindu ni hatari, usijishughulishe na kuosha maiti hiyo bali izikwe haraka kwa kufuatwa ushauri wa wataalam wa afya.

    Madhara ya kula Mayai yasipoiva vizuri kwa Afya

    Mayai ni moja ya vyakula vyenye viini lishe muhimu kwa ajili ya afya ya mwili wa binadamu. Kwa kawaida mayai kabla ya kuliwa, huandaliwa kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuchemshwa, kukaangwa au kuchanganywa na vyakula vingine kama vipande vya viazi mviringo ambavyo ni maarufu kwa jina la chips.

    Pia, kuna baadhi ya watu wanaopendelea kula mayai mabichi kama dawa ya tiba mbadala, kwa ajili ya kulainisha sauti na wengine hupendelea kula mayai ya kukaanga ambayo hayakukaushwa vizuri.
    Ukitembelea migahawa mingi utabaini kuwa watu wanakuwa na mitazamo tofauti na wanavyopenda kula mayai.

    Mfano kuna wanaoagiza watengenezewe mayai kwa mtindo unaojulikana kama ‘macho ya ng’ombe.’ Ukiagiza namna hiyo, mpishi atataka kuuliza kama ni ‘macho ya ng’ombe’ ya kugeuza.

    Ina maana kuwa ‘macho ya ngombe’ ya kugeuzwa ni yale yanayoivishwa pande zote lakini yale ambayo siyo ya kugeuza, huwa linaifa nusu. Upande mmoja unabaki ukiwa mbichi, na ndiyo raha ya baadhi ya watu.

    Hata ukienda kwa wakaanga chipsi, utakuta wanawauliza wateja wao kama wanapokaanga na mayai wakaushe au wasikaushe. Hii inaashiria kuna watu wanataka wale chipsi zikiwa na mayai ambayo halijaiva sawasawa.

    Kuna watu wengine wanaamini kwamba kula mayai mabichi kunafanya sauti inakuwa nyororo, hivyo wale waimbaji huwalazimu kufanya hivyo ili kufanya nyimbo zao zivutie.

    Si hivyo tu, kuna baadhi ya watu huamini pia dawa ya kikohozi ni kunywa yai bichi lililochanganywa na asali. Hizi ni imani ambazo zimejengeka kwenye jamii na watu hufanya hivyo ili kufikia malengo waliyokusudia.

    Katika siku za karibuni, imevuma kuwa mayai ya kwale yanatibu magonjwa sugu kama vile kisukari, shinikizo la damu, saratani na kifua.

    Katika mpango huo, wanapendekeza wahusika kula mayai mabichi ya kwale tena kwa kutafuna hadi kaka lake, yaani ganda la nje.

    Hali hii imesababisha biashara ya mayai ya kwale kuwa kubwa na hata wafugaji wameongezeka mara dufu.

    Wataalamu wanasemaje?

    Baadhi ya tafiti za sayansi ya lishe na afya ya jamii, zinabainisha kuwa ulaji wa mayai katika hali ya namna ya ubichi, unaweza kuhatarisha afya.

    Wakati mwingine, hali ya namna hii, huwa chanzo cha mlipuko wa magonjwa ya tumbo katika jamii. Katika milipuko ya magonjwa hayo, hali inaweza kuwa mbaya zaidi hasa kwa watoto wadogo, wazee, wajawazito na watu wenye upungufu wa kinga mwilini.

    Hii ni kutokana na ukweli kwamba mayai mabichi yanaweza kusababisha maradhi ya kuharisha na homa ya matumbo kutokana na kubeba vimelea vya magonjwa aina ya Salmonella Enteritidis PT4. Vimelea hivi hatari kwa afya, vinaweza kuwa ndani ya yai au juu kwenye ganda la yai bila kuonekana kwa macho. Mgonjwa aliyepata uambukizo wa bakteria wa Salmonella kutokana na kula mayai, anaweza kuwa na homa kali, maumivu makali ya tumbo pamoja na kuharisha ndani ya saa 72 baada ya kula mayai.

    Ugonjwa huu unaweza kudumu kwa siku nne hadi saba na baadhi ya watu huwa na hali mbaya kiasi cha kuhitaji matibabu ya kulazwa hospitalini.

    Kwa baadhi ya watu ambao kinga ya miili yao si imara, vimelea vya Salmonella vinaweza kuingia katika mfumo wa damu na kusambaa mwili mzima. Jambo hilo linaweza kusababisha kifo kwa muda mfupi kama mgonjwa hatapewa matibabu sahihi na kwa haraka.

    Nchini Uingereza ingawa, ugonjwa utokanao na kula mayai yenye uambukizo wa Salmonella umepungua sana, lakini angalizo la watu kuepuka ulaji wa mayai mabichi bado linadumishwa.

    “Ni swala la kujua kwamba hatari bado ipo katika jambo hili, hata kama ni ndogo,” anasema Bob Martin ambaye ni mfanyakazi wa Wakala wa Viwango vya Ubora wa Chakula (The Food Standards Agency) nchini Uingereza.

    Utafiti uliofanyika mwaka 2004-2005 katika maeneo mengi ya Ulaya ulibaini kuwa asilimia 20 ya mashamba makubwa ya kuku wa mayai, yalikuwa na kuku waliokuwa na uambukizo wa Salmonella. Hii ni kwa mujibu wa Richard Lawley katika makala yake yaliyochapishwa Februari mwaka 2013 katika tovuti ya Food Safety Watch.

    Utafiti mwingine uliofanywa na Q.T. Bura na Henry B. Magwisha kutoka katika Wakala wa Maabara za Mifugo Tanzania (TVLA) kwa kushirikiana na profesa Robinson H. Mdegela wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), nao ulibaini kuwa ndege wengi wanaotaga mayai wana maambukizi ya vimelea vya Salmonella. Utafiti huo ulifanyika katika Jiji la Mwanza kati ya Desemba 2013 na Januari 2014.

    Tukiachilia mbali uambukizo wa Salmonella, ulaji wa muda mrefu wa mayai mabichi au yale yasiyoiva vizuri hasa kwa akina mama wajawazito, unaweza kusababisha wazae watoto wanye ulemavu wa viungo vya mwili katika maumbile yao. Utafiti wa Lawrence Sweetman na wenzake uliochapishwa mwaka 1981 katika jarida la Paediatric toleo la 68(4), unabainisha kuwa ulaji wa mayai mabichi au yasiyoiva vizuri, unaweza kusababisha watoto wasiwe na nywele kichwani.

    Utafiti wa Timothy D. Durance wa Chuo Kikuu cha British Columbia nchini Canada, uliochapishwa mwaka 1991 katika jarida la Sayansi za Vyakula (Journal of Food Sciences) toleo la 56(3), unabainisha kuwa ute mweupe wa mayai unaweza kusababisha upungufu wa Biotin mwilini.

    Dr. Durance anaongeza kusema kwamba, ute mweupe wa mayai mabichi una protini aina ya avidin ambayo huzuia Biotin kusharabiwa (kufyonzwa) kutoka katika chakula kinapokuwa tumboni. Utafiti huo pia ulibaini kuwa hata mayai yaliyochemshwa au kukaangwa vizuri, bado ute mweupe huwa na Avidin yenye nguvu kwa asilimia 40.

    Utafiti wa Profesa Hamid Said wa Chuo Kikuu cha California nchini Marekani, nao uliripoti kuwa ute wa mayai yasiyoiva, unasababisha upungufu wa Biotin mwilini. Utafiti huo ulichapishwa katika jarida la sayansi ya lishe katika tiba (American Journal of Clinical Nutrition) toleo la mwaka 2002. Utafiti mwingine ulioongozwa na Donald Mock na kuchapishwa katika jarida la sayansi ya lishe katika tiba la nchini Marekani toleo la 75(2) mwaka 2002, nao ulibainisha kuwa takribani asilimia 50 ya wanawake wajawazito, wana kiwango fulani cha upungufu wa Biotin mwilini hasa katika miezi mitatu ya mwanzo wa mimba.

    Hali hii inafanya wajawazito wanaokula mayai mabichi au yasiyoiva vizuri katika kipindi hiki, kuhatarisha afya zao na za watoto wao walioko tumboni kwa kiasi kikubwa.

    Utumiaji wa mayai ya namna hii kwa muda mrefu, pia unaweza kusababisha upungufu wa damu mwilini na ugonjwa wa mzio wa chakula hasa kwa watoto. Lakini pia utumiaji wa mayai yasiyoiva vizuri kwa muda mrefu, unaweza kusababisha ugonjwa wa kukatika katika kwa ulimi kutokana na upungufu wa vitamini B mwilini.

    Hali ambayo husababisha shida wakati wa kula vyakula vyenye uchachu au vilivyokolezwa viungo vingi vya aina mbalimbali.

    Tahadhari kubwa inahitajika wakati wa kuandaa mayai ili kuhakikisha kuwa chakula hiki muhimu hakigeuki kuwa chanzo cha madhara ya kiafya. Ni vizuri kutunza, kuchagua na kusafisha mayai vizuri kabla ya kuyachemsha au kuyavunja kwa ajili ya maandalizi mbalimbali ya mapishi.

    Vyombo vinavyotumika kukorogea mayai mabichi ni lazima visafishwe kwa maji ya moto na sabuni kabla ya kutumika kwa ajili ya maandalizi ya chakula. Kwa namna yoyote ile mayai yasiliwe ikiwa hayakuiva vizuri au yanapokuwa katika hali ya ubichi.

    Ni wakati kwa jamii kubadili mwelekeo kwa kula mayai ambayo yamepikwa hadi kuiva na kuepuka kula yakiwa mabichi.

    Ni vyema pia ikaeleweka wapikaji wanapaswa kuwaelimisha wateja wao juu ya athari hizi ili kuwafanye wawe na uchaguzi sahihi wa vyakula watakavyotumia.


    Katika jamii yetu, wapika chipsi huwa hawaoshi lile bakuli la kukorogea mayai kabla hayajakaangwa. Hii ni hatari kwa sababu chombo hicho kinaweza kikawa sababu ya kusambaza maradhi kwa watumiaji wa mayai.

    10 August, 2015

    Ugonjwa wa sukari ni chimbuko la chakula kisichofaa

    Ni vigumu kujua aina ya chakula kinachokufaa, bila kujua jinsi mwili wako unavyokichakata. Kimsingi watafiti wamebaini makundi makuu matatu ya watu kuhusiana na jinsi miili inavyochakata chakula.

    Chakula ambacho ni bora kwa mtu mmoja, kinaweza kuwa sumu baridi kwa mtu mwingine na kumletea madhara endelevu katika maisha yake. Kwa muktadha huu basi hakuna chakula bora kwa kila mtu. Chakula ni bora kwa mtu kama baada ya kukitumia mwili utakipokea vizuri, ukafyonza virutubisho na kikasaidia kuimarisha afya ya mlaji.

    Ni vigumu kujua aina ya chakula kinachokufaa, bila kujua jinsi mwili wako unavyokichakata. Kimsingi watafiti wamebaini makundi makuu matatu ya watu kuhusiana na jinsi miili inavyochakata chakula.

    Kundi la kwanza ni la wachakataji wa protini. Hawa miili yao inakubaliana zaidi na vyakula vya protini. Kwa watu wa kundi hili vyakula vya wanga na hususan vile vilivyochakatwa na kuchujwa kwa kiwango kikubwa (highly processed and refined), ni sumu baridi ambayo itawapelekea kuugua maradhi mengi ya kimfumo.

    Kundi la pili ni la wachakataji wa wanga. Hawa miili yao inakubaliana zaidi na vyakula vya wanga. Kwa watu wa kundi hili la vyakula vya protini, hususan vile vilivyochakatwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya kuwa na muda mrefu wa matumizi, ni sumu baridi ambayo itasababisha kuugua maradhi mengi ya kimfumo.

    Kundi la tatu ni la wachakataji wa vyakula vya protini na wanga kwa viwango sawa. Kundi hili kidogo lina bahati, kwa maana, halidhuriwi kwa wepesi na vyakula vilivyoko katika yale makundi mawili ya mwanzo.

    Moja ya magonjwa yanayosababishwa na mkanganyiko huu katika kula ni ugonjwa wa kisukari. Mchakataji wa protini anapokula chakula cha wanga, kasi ya kuchakata wanga huo ni kubwa mno ikilinganishwa na mlaji mwenzake ambaye ni mchakataji wa wanga.

    Kasi hiyo husababisha kiwango cha sukari kinachoingia katika mzunguko wa damu ndani ya muda mfupi kuwa kikubwa sana. Kutokana na hali hii kongosho hulazimika kufanya kazi ya ziada kuzalisha kiwango kikubwa cha kichocheo kinachojulikana kama insulini ili kuondoa sukari kwenye damu na kuipeleka kwenye seli ili itumike kutengenezea nishati.

    Hali hii ikijirudiarudia, kongosho huchoka na kuanza kufanya kazi chini ya kiwango au wakati mwingine vipokezi vya sukari katika seli (receptors) hushindwa kuendana na kasi ya kuletewa sukari kwa ajili ya matumizi ya seli hivyo huishia kuikataa sukari hiyo.

    Hali hii kitaalamu hujulikana kama insulin resistance, au pingamizi dhidi ya insulini kwa tafsiri isiyo rasmi. Kuna baadhi ya nyakati, vyote hutokea kwa wakati mmoja, yaani kongosho linafanya kazi chini ya kiwango, na pia mgonjwa anakabiliwa na pingamizi dhidi ya insulini.

    Hivi karibuni imebainika kuwa moja ya sababu kubwa sana zinazosababisha vipokezi vya seli kushindwa kupokea sukari inayoletwa ni kitu kinachoitwa mfuro (inflammation). Mfuro ni uvimbe kama lengelenge hivi. Mfano wa mfuro ni pale unapojikwaa au kujigonga usoni na mwili ukaumuka na kutengeneza nundu.

    Vichocheo vya kusababisha mfuro kwenye seli viko vingi lakini baadhi ya hivi ni vyakula tunavyokula kila siku. Vyakula hivi ni pamoja na sukari na wanga uiliochakatwa kwa kiwango kikubwa.

    Athari za ugonjwa

    Kisukarini ni ugonjwa ambao unasababisha mololongo wa matatizo mengine ya kiafya mwilini. Matatizo haya ni pamoja na uharibifu wa macho, unaotambulishwa na magonjwa kama glaucoma ambao husababisha uharibifu wa neva za jicho.

    Matatizo mengine ni ugonjwa ujulikanao cataracts ambao unatokana na ukungu kwenye lenzi ya jicho na retinopathy unaosababisha uharibifu katika retina ya jicho.

    Matatizo mengine ni ya miguu yanayotambulishwa na magonjwa kama neurapathy ambayo ni maumivu yatokanayo na uharibifu wa mishipa ya fahamu, vidonda sugu vya tumbo na gangrene ambao ni mkusanyiko wa tishu zilizokufa kutokana na kutofikiwa na mzunguko wa damu.

    Matatizo mengine ni yale ya magonjwa ya ngozi na magonjwa ya moyo.

    Mpango mzuri wa kuudhibiti ugonjwa wa kisukari ni kuufuatilia kwa makini. Hii ina maana kuwa ni muhimu kufanya kipimo kila siku, ikiwezekana hata mara mbili au tatu kwa siku. Kutokana na hali hii gharama za kuufuatilia ugonjwa huu ni kubwa na huathiri kwa kiasi kikubwa hali ya kiuchumi ya mgonjwa.

    Kwa mfano tu, hivi sasa katika zahanati na vituo vingi vya afya, gharama za kupima kisukari kwa mara moja ni kati ya Sh2,000 na Sh2,500.00. Unapomwambia mtu apime mara tatu kwa siku maana yake atumie kati ya Sh6,000 na Sh7,500.00 kila siku.

    Ugonjwa wa kisukari kwa sasa kinaonekana kunyemelea hadhi ya kuwa ni janga la kijamii. Katika pande zote za dunia kisukari kinaongezeka badala ya kupungua. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), dunia inatarajiwa kuwa na wagonjwa wa kisukari milioni 366 mwaka 2030 kutoka wagonjwa milioni 171 waliokuwepo mwaka 2000.

    Mwaka 2000 Tanzania ilikuwa na wagonjwa 201,600 na mwaka 2030 inatarajiwa kuongezeka maradufu na kufikia 605,000. Hili ni sawa na ongezeko la asilimia 66.7.

    Hata hivyo janga la kisukari linaoonekana kuzikumba zaidi zile nchi ambazo raia wao wanapendelea mno vyakula vya wanga katika mitindo tofauti.

    Vyakula hivyo ni soda, pasta, doughnut, keki, mikate, lambalamba, nakadhalika. Nchi kama Italy uwiano kati ya Wataliano wanaoumwa kisukari na wale ambao hawaumwi ni mtu mmoja kati ya 14. Inawezekana sababu kubwa ikawa ni ulaji wa piza, pasta na spaghetti. Hivi ni vyakula vinavyotengenezwa kwa ngano na Wataliano wanapenda kuvila kwa wingi.

    Marekani uwiano wao ni mtu mmoja kwa kila watu 17. Hii nayo ni jamii ambayo inatumia soda, doughnut, chips, pizza, na vyakula vingine vya wanga vilivyochakatwa kwa kiwango cha juu. India uwiano wao ni mtu mmoja kati ya 39. Hawa nao ni mabingwa wa vitu vitamu. Wahindi wanapenda tamutamu za kila aina na sifa kuu ya vitu hivyo ni wingi wa sukari, ngano, mafuta na rangi.

    Tanzania ina uwiano wa mtu mmoja kati ya 238. Huu ni uwiano mzuri sana ukilinganisha na nchi tulizotangulia kuzitaja. Sababu ya uwiano huu mzuri ni nini? Kimsingi sehemu kubwa ya Watanzania ni wala wanga zaidi kutokana na hali zao za kiuchumi?

    Nadhani sababu kubwa ni ukweli kwamba Watanzania wengi ni wakaazi wa vijijini na kimsingi pamoja na kwamba sehemu kuwa ya chakula chao ni wanga, lakini kutokana na sababu za kiuchumi, wanalazimika kuula wanga huo katika mfumo ambao haujachakatwa.

    06 August, 2015

    Utafiti: Ukila vyakula vilivyotiwa viungo kila siku unajiongezea maisha marefu

    post-feature-imageUtafiti mmoja uliofanywa nchini China umebaini kuwa ukila chakula kilichotiwa viungo kila siku unajiongezea maisha marefu.
    Utafiti huo haswa umeonesha kuwa ukila chakula hususan pilipili utaishi maisha marefu zaidi duniani.
    Watafiti mjini Baijing walidadisi maisha na vyakula wanavyokula wenyeji nusu milioni katika kipindi cha utafiti cha miaka 7.

    Utafiti huo ulibaini kuwa wale waliokula chakula kilichojumuisha pilipili walikuwa katika hali bora zaidi kiafya wala hawakuwa katika hatari ya kuaga dunia. Hali yao ya siha ilitofautiana sana ikilinganishwa na wale ambao waliweka viungo katika vyakula vyao chini ya siku moja kwa juma .

    Watafiti hao walitoa tahadhari.
    Wanasema kuwa utafiti huo ulikuwa wa ushahidi tu lakini wakashauri utafiti zaidi ufanyika kwengineko ilikutilia pondo utafiti wao.
    Hata hivyo walibaini kwa uhakika kuwa kiungo kinachopatikana katika pilipili, 'capsaicin' kinauwezo wa kupigana na seli zinazotuma ujumbe kwa ubongo kuwa mtu amezeeka na kusababisha viashiria vya utu uzima.

    05 August, 2015

    Vinywaji vya kusisimua akili, kutia mwili nguvu, vina athari za kiafya

    post-feature-imageWatu hupenda kunywa vinywaji mbalimbali ambavyo huongeza nguvu hasa pale wanapojihisi wamechoka lakini wanataka kuona wanaendelea na kazi.
    Wengine, hasa madereva, hupenda kutumia vinywaji hivi ili kuondoa uchovu na kuwafanya wasipate usingizi. Hufanya hivyo ili wasisinzie na kusababisha wasababishe ajali.

    Kwa upande mwingine pia, wapo wanaokunywa vinywaji hivi vya kuongeza nguvu kama starehe au mbadala pale wanapokuwa hawatumii vilevi.

    Duniani kote matumizi ya vinywaji vya kuongeza nguvu kwa sasa yameongezeka kuliko unavyofikiria. Takwimu zilizotolewa katika utafiti uliochapishwa mwaka 2009 katika jarida la ‘Drug Alcohol Dependence’ toleo la 99(1–3), zinaonyesha kuwa mwaka 2006 pekee, takribani aina mpya 500 za vinywaji hivi ziliingizwa sokoni.

    Ongezeko hili kubwa la vinywaji vya kuongeza nguvu, linazua mashaka kwa wataalamu wa afya kuhusu usalama wa afya ya jamii. Hii ni kutokana na ukweli kuwa, matumizi makubwa ya vinywaji hivi yanaambatana na madhara ya afya ya mwili na akili kwa watumiaji.

    Watanzania wengi hasa vijana kwa sasa wanapendelea kutumia vinywaji hivi kwa wingi. Kwa sasa soko la vinywaji baridi limejaa vinywaji vya kuongeza nguvu. Ni jambo la kawaida kuona watu wazima na watoto wakinywa vinywaji hivi safarini, katika sherehe mbalimbali na katika kumbi za starehe. Vinywaji hivi huuzwa kwa wingi katika maduka makubwa (Super markets), maduka madogo, hotelini na katika migahawa.

    Miongoni wa watumiaji wakubwa wa vinywaji hivi ni wanamichezo na madreva hasa wa magari yanayofanya safari za masafa marefu, ambao wanaamini kuwa kwa kutumia vinywaji hivi huongeza nguvu za mwili, kasi ya vitendo, umakini na kupunguza uwezekano wa kupata usingizi. Watu wengi wanapotumia vinywaji hivi pia huvichanganya na pombe.

    Vinywaji vya kuongeza nguvu, visivyo na kilevi,  kisayansi vinaelezwa vina kiasi kikubwa cha kafeini, vitamini pamoja na kemikali za taurine, glucuronolactone.

    Wakati mwingine pia huongezewa dawa aina ya guarana pamoja na mitishamba aina ya ginseng kwa lengo la kusisimua akili na kuongeza nguvu za mwili.

    Mtafiti wa madhara ya dawa za kulevya wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Dk Stephen Nsimba anasema kwamba vinywaji hivi vina kiasi kikubwa cha kafeini ambayo ni dawa inayosisimua ubongo na kwa kuvichanganya na pombe athari zake kwenye mfumo wa fahamu za mwili huongezeka.

    “Baada ya kuchanganya vinywaji hivi, kafeini katika vinywaji vya kuongeza nguvu, hupunguza athari za kilevi na kumfanya mtumiaji asibaini haraka kuwa amekunywa kiasi kikubwa cha kilevi. Hili ni jambo la hatari” anaonya Dk Nsimba.

    Habari mbaya zaidi ni kwamba baadhi ya watengenezaji wa vinywaji hivi huweka kiasi kikubwa cha kemikali kuliko inavyotazamiwa katika hali ya kawaida na hawaonyeshi katika lebo ama karatasi ya maelezo inayobandikwa kwenye kifungashio.

    April mwaka jana, Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TDFA) ilikamata makopo 1,526 ya vinywaji vya kuongeza nguvu katika soko la Tanzania ambavyo vilikuwa havikidhi viwango vya ubora na usalama kwa matumizi ya binadamu.

    Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya Mkurugezi wa TFDA, Hiiti Sillo aliyoitoa Aprili  3, 2014 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

    Matokeo ya utafiti mmoja yaliyowasilishwa katika mkutano wa mwaka 2013 wa Chama cha Afya ya Moyo cha Marekani (American Heart Association) uliofanyika katika mji wa New Orleans, ilibainika kuwa kunywa kopo moja hadi matatu ya vinywaji vya kuongeza nguvu, kunaweza kusababisha moyo udunde bila mpangilio na kuongeza shinikizo la damu.

    Utafiti huo unaongeza kusema kuwa, hali kama hiyo inaweza kusababisha  kifo cha ghafla au magonjwa sugu kama vile shinikizo la damu, kisukari na kiharusi kwa baadhi ya watu.

    Dk Gordon F. Tomaselli, ambaye ni msemaji wa American Heart Association (AHA) anasema: “Ingawa jambo hili linaoneka kama dogo lakini linaweza kusababisha madhara makubwa kwa baadhi ya watu. Wale walio na magonjwa ya moyo au historia ya magonjwa hayo katika familia zao, ni lazima wajiepushe na utumiaji wa vinywaji vya kuongeza nguvu.”

    Baadhi ya watu wanaokuwa hawana habari kuwa wana magonjwa ya moyo hasa pale, ugonjwa unapokuwa katika hatua za mwanzo, wanaweza kuhatarisha maisha yao kwa kunywa vinywaji vya kuongeza nguvu ambavyo vina kiasi kikubwa cha kafeini.

    Kiasi kikubwa cha kafeini kinaweza kusababisha shinikizo la damu, kuweweseka, kukosa usingizi, maumivu ya kichwa na degedege.

    Baadhi ya watafiti wanabainisha kuwa vinywaji hivi pia vinaweza kusababisha ugonjwa wa kisukari.

    Utafiti wa Dk. D.C. Greenwood na wenzake uliochapishwa katika jarida lijulikanalo kama Europian Journal of Epidemiology, toleo la 25(4) la mwaka 2010, unabainisha kuwa matumizi ya vinywaji vya kuongeza nguvu wakati wa ujauzito, unaweza kusababisha mimba kuharibika, kuzaa mtoto mfu au kuzaa mtoto mwenye uzito pungufu.

    Kina mama wanaonyonyesha pia wanapotumia vinywaji hivi huwasababishia watoto wao matatizo ya kiakili ikiwa ni pamoja na kulia kupita kiasi.

    Vijana wanaotumia vinywaji hivi, pia wanakabiliwa na hatari ya kutumbukia katika matumizi ya dawa za kulevya, tumbaku na ulevi wa pombe wa kupindukia.

    Utafiti wa hivi karibuni nao umebaini kuwa vijana na watoto wanaotumia vinywaji hivi hupata athari za kiakili kiasi kwamba uwezo wao wa kujifunza na kutambua mambo unaathirika.

    Hii ni kwa mujibu wa utafiti wa T. Van Batenburg-Eddes na wenzake uliochapishwa katika jarida la Front Psychology toleo la 5, mwaka 2014.

    Utafiti wa jeshi la Marekana uliochapishwa mwaka jana unabainisha kuwa, wanajeshi wengi wanaokunywa vinywaji vya kuongeza nguvu wanakabiliwa na hatari ya kujiua.

    Utafiti huo unaongeza kusema kuwa wanajeshi wanaochanganya vinywaji vya kuongeza nguvu pamoja na pombe wanakabiliwa na hatari kubwa zaidi ya kujiua. Hii ni kwa mujibu wa utafiti wa H.B. Mash na wenzake uliochapishwa katika jarida la Social Psychiatry and Psychiatric Epidemiology, toleo la 49(9).

    Kutokana na athari za vinywaji hivi kiafya, jamii inashauriwa kupunguza au kujiepusha na matumizi yake.

    Ni busara pia mamlaka za kiserikali na kidini zinazohusika na usalama wa afya ya watoto zikasaidia kuielimisha jamii kwamba watoto na vijana walio chini ya miaka 18 wasitumie vinywaji hivi. Ni vyema vinywaji kama hivi vikapigwa marufuku.

    17 July, 2015

    Je,mbu hutambua vipi mwili wa mwanadamu usiku?


    Utafiti mpya umebaini kwamba mbu hutafuta kitu cha kula kwa kutumia vigezo vitatu,harufu,macho na joto.
    Utafiti huo unasema kuwa mbu anaweza kufahamu aliko mwanadamu kupitia hewa ya kaboni ambayo watu hupumua nje.
    Inasemekana mbu hunusa hewa hii kiasi cha mita 50.
    Wanasayansi wamesema kwamba walimfuatilia mbu mwenye njaa, ndani ya mtaro uliofunikiwa.
    Kisha waligundua kwamba mbu hao walianza kunusa nusa hewa ya kaboni, na kutema mapovu yenye matone meusi yaliowekwa na watafiti hao sakafuni.null
    Imebainika kwamba wakati mbu yuko mita chache karibu na kile anacholenga, huvutiwa sana na joto.
    Hii imebainisha kwamba hata hufuata joto hilo na kisha kumshambulia mwanadamu.
    Huenda ukapata Malaria au ukaponea lakini utakua na vipele pale vya mbu anapokuuma.

    30 June, 2015

    Magonjwa ya zinaa yaongezeka kwa wapenzi wa jinsia moja

    Maradhi ya zinaa yanayosambazwa miongoni mwa wapenzi wanaume wa jinsia moja inatamausha.
    Haya ni kwa mjibu wa shirika la afya ya umma nchini Uingereza.Takwimu za mwaka 2014 zinanonesha kuwa

    15 May, 2015

    Unyanyasaji wa watoto umeendelea kuwa sehemu ya matukio ambayo yamekuwa yakikithiri sana ndani ya familia

    legs
    Unyanyasaji wa watoto umeendelea kuwa sehemu ya matukio ambayo yamekuwa yakikithiri sana ndani ya familia na jamii za watu wengi duniani.Kitendo cha msichana wa kazi kule Uganda kumtesa mtoto wa bosi wake  kwa kumpiga bado hakijasahaulika na mamilioni ya watu duniani baada ya kunaswa na kamera na kusambazwa kwenye mitandano ya kijamii.

    09 May, 2015

    How to keep yourself healthy in Summer


    Summer is a great season for everyone, for children it’s a holiday season that brings lots of fun, travelling and reunion time with uncle, aunt and grandparents. Summer is a great time for elders too as they find some relaxation from sending their kids to school and

    16 April, 2015

    Mapacha watano wa kike wamezaliwa Marekani

    Mapacha watano wa kike wamezaliwa Marekani katika hospitali moja ya wanawake mjini Texas Houston.Wauguzi katika hospitali hiyo wanasema kuwa uzazi huo kutokana na mimba moja ni rekodi mpya ambayo haijawahi kutokea Marekani.

    Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

    KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...