Ali Kiba ni staa mkubwa kwenye muziki wa Bongo Fleva.. kama wewe ni mtumiaji wa Instagram utakuwa umeona kwamba Ali Kiba haja-follow mtu yoyote ukitembelea mitandao ya kijamii ya Ali Kiba utaona ya kuwa ana mashabiki wengi wanaomfuatilia kupitia mitandao hiyo
.
Nimekutana na post ya Instagram kwenye page ya Mseto East Africa ambao walikaa na kupiga stori na Ali Kiba na kumuuliza swali hilo, majibu yake ni haya hapa >>> “Yea
si follow mtu kwasababu, kwanza kabisa nafanya kazi na watu wengi kuna
akina TUVA kuna watu kibao lakini watu wa Media ndio tuko nao
karibu,sasa wengine walikua waki complain nikawa naogopa zile lawama
nilichoshauriwa na hao wenyewe kwamba ni heri ni si follow mtu na vile
vile nilipenda ivyo kutokana na promotion ya ujio wangu ambao ulikuwa
unakuja ili niweze ku concetrate na account yangu nijue mafans wangu
wanataka kitu gani wanani advice kitu gani na pia imesaidia naona jinsi
gani wako serious namimi kwasababu naongea nao,kuna wengine wananipa
challenge kuna matusi uhmm ni vitu vya kawaida na vile vile wanapokuwa
wananisema wananijenga wananitengeneza kiasi fulani,wananibadilisha ni
wapi nimekosea naweza kubadilisha”<<< officialalikiba
No comments:
Post a Comment