15 July, 2016

Unaweza kuyatazama hapa matokeo yote ya kidato cha sita 2016

July 15 2016 Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi imetangaza matokeo ya kidato cha sita, Matokeo yote unaweza kuyatazama kwa kubonyeza HAPA

New Video: Joh Makini f/ Chidinma – Perfect Combo

Joh Makini ameikata kiu ya muda mrefu ya mashabiki waliokuwa wanatamani kuona video ya wimbo wake mpya ‘Perfect Combo’ aliomshirikisha msanii wa Nigeria, Chidinma. Video imeongozwa na Justin Campus wa Afrika Kusini.

Wapinzani wa Yanga Medeama watua Dar

Yanga
Wapinzani wa klabu ya Young Africans, katika michuano ya kuwania Kombe la Shirikisho Barani Afrika, Medeama kutoka Ghana, wametua Dar es Salaam tayari kwa mechi baina ya timu hizo Jumamosi.

Wachezaji hao waliwasili Dar Alhamisi na wakafanya mazoezi katika uwanja wa Karume.
Yanga itaikaribisha Medeama kwa mchezo wa tatu kuwania taji hilo hatua ya makundi katika uwanja wa taifa Dar es Salaam.
Mchezao huo utaanza saa 10.00 jioni
Michezo miwili ya awali ya Yanga katika michuano hiyo ilikuwa ni dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria ambako ilipoteza kwa bao 1-0 kabla ya kupoteza tena dhidi ya TP Mazembe, mechi iliyopigwa jijini Dar es Salaam.
Mchezo wa Jumamosi utachezeshwa na waamuzi kutoka Misri ambao ni Ibrahim Nour El Din atakayekuwa mwamuzi wa kati; akisaidiwa na Ayman Degaish na Samir Gamal Saad wakati mwamuzi wa akiba akiwa ni Mohamed Maarouf Eid Mansour, kwa mujibu wa Shirikisho la Kandanda la Tanzania (TFF).

MPYA: Download ngoma mpya ya Jux-WIVU

Kutoka kwenye kundi la wakacha, hapa namtaja Jux, katuletea ngoma yake mpya iliyopatiwa title ya Wivu. Ngoma imefanyika pale AM Records chini ya producer Bob Manecky, Unaweza kuupata wimbo huu kwa kubofya HAPA.

Sikiliza Wivu

14 July, 2016

Download Music: Shaa – Sawa

Shaa ameachia ngoma yake mpya ‘Sawa’ iliyotayarishwa na Shirko. Hiyo inakuwa kazi ya kwanza kutoka chini ya label yake, SK Musik. Enjoy muzsiki huu kutoka kwa Shaa na Kumbuka pia kuwashirikisha wana kitaa... One love Yoooo!

Manchester United imeorodheshwa ya tano kwa utajiri duniani -Forbes


Klabu ya Manchester United imeorodheshwa ya tano kwa utajiri duniani na jarida la Forbes, thamani yao ikiwa imepanda kwa asilimia saba.
Klabu ya NFL, Dallas Cowboys, ndiyo inayoongoza thamani yake ikiwa $4bn (£3.03bn), na ni mara ya kwanza kwa klabu ambayo haichezi kandanda kuongoza katika orodha hiyo tangu kuanzishwa kwake 2011.

United, walioongoza orodha hiyo 2011 na 2012, wana thamani ya $3.32bn (£2.52bn).
Real Madrid ni wa pili kwa $3.65bn (£2.77bn) na Barcelona wa tatu $3.55bn (£2.69bn).
United, klabu pekee ya Uingereza katika orodha hiyo, walisaidiwa sana na mkataba wao wa £750m na Adidas, jambo lililoongeza thamani yao licha ya kushindwa kufuzu kwa michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Hata hivyo, Manchester United, ndio wenye deni kubwa zaidi miongoni mwa klabu zilizo katika 25 bora.
Arsenal (23), Manchester City (28), Chelsea (36) na Liverpool (41) ndizo klabu hizo nyingine za Uingereza zilizofanikiwa kuwa kwenye orodha hiyo.

Video: Roma ft Darasa na Jos Mtambo-‘kaa tayari‘

Karudi tena kwenye TV na hii mpya ‘kaa tayari‘ na ni ngoma imesukwa pale Tongwe,humu ndani wamesikika  Darasa na Jos Mtambo. Tizama video hiyo kisha mshirikishe mwana kitaa. Kaa tayari.

13 July, 2016

Chombo cha anga NASA Juno kimetuma picha za kwanza za sayari ya Jupiter

Juno

Moja ya hizo, iliyotolewa na NASA Jumanne inaonesha sayari hiyo ikiwa imezungukwa na miezi mitatu kati ya miezi yake minne mikubwa. Miezi inayoonekana ni Lo, Europa na Ganymede. Mwezi huo mwingine uitwao Callisto hauonekani.

Jupiter

Picha ya kwanza ya sayari ya Jupiter


Picha hiyo ilipigwa Jumamosi sayari Juno ilipokuwa inazunguka sayari hiyo ikiwa umbali wa maili milioni tatu.Hata katika umbali huo, Shimo Jekundu, lililosababishwa na dhoruba kali kwenye sayari hiyo karne nyingi zilizopita, linaonekana.

Juno iliingia katika mzingo wa Jupiter wiki iliyopita na kuanza kuizunguka sayari hiyo ambalo pia hufahamika kama Zohali au Zozali.
Safari yake kutoka duniani hadi ilichukua miaka mitano.
Juno itachunguza na kupeleleza sayari hiyo kwa miezi 20, lengo kuu likiwa kusaidia wanasayansi kubaini asili ya sayari hiyo ambayo wanaamini inaweza kuwasaidia kuelewa zaidi asili ya mfumo wa jua.
Chombo hicho cha juu kilipokuwa kinaikaribia Jupiter, kamera zake na mitambo mingine muhimu vilizimwa kuzuia visiharibiwe na miali nururishi. Baadaye, vilifunguliwa.

Wanasayansi wanatarajia picha za karibu zaidi za Jupiter zitapokelewa mwezi ujao.
  • Jupiter ina ukubwa mara 11 kuzidi Dunia na uzito wake ni mara 300 zaidi
  • Sayari hiyo hutumia miaka 12 ya dunia kulizunguka jua; siku moja huko hudumu saa 10.
  • Muundo wake ni kama wa nyota , sana haidrojeni na helium.
  • Nasa inapanga kuitumia Juno hadi Februari 2018.

Unamfahamu Gyptian mkali wa reggae kutoka Jamaica?

Kwa majina yake kamili anajulikana kama Windel Beneto Edwards. Alizaliwa mnamo October 25, 1983 katika kijiji kimoja kinachojulikana kwa jina la King Weston huko Jamaica. Wazazi wake walijulikana kama Pauline(Mama) na Basil(baba) ambaye pia ni Rastafarian. Wazazi wake wote wawili hawakumzuia kijana wao huyu kufanya muziki licha ya Dini yao bali walimpatia kijana wao support na kuhakikisha anatimiza malengo yake.

 Akiwa na umri wa miaka 7, Gyptian alianza kuimba kwaya kanisani. Baada ya wazazi wake kukitambua kipaji cha kijana wao, waliamua kumtambulisha kijana huyo kwa Producer mmoja aliye julikana kwa jina la Mr. Wong kutoka katika studio iliyojulikana kama Portmore, St. Catherine-"Sikulitila jambo hili maanani" Gyptian alisema.

Akiwa chini ya usimamizi wa Mr.Wong na Mpiga guitar maarufu Earl “Chinna” Smith, Gyptian alifanikiwa kushinda shindano moja la kusaka vipaji huko Kingston. Alijipatia jana la GYPTIAN kutokana na tabia yake ya kufunga T-shirt yake kichwani kama walivyokua wakfunga wafalme wa Misri(Egypt) ambao kwa wakati ule walijulikana kama Pharaohs, Hivyo rafiki zake wakaondoa herufi 'E' kwenye jina EGYPT na kumpatia jina GYPTIAN ambalo analitumia mpaka leo hii.

Mnamo mwaka 2005 alifanikiwa kuachia ngoma kali mbili ambazo ni "Is There A Place" na "Serious Times". Na ilipofika mwaka 2006, alichaguliwa katika tuzo zilizojulikana kama "International Reggae and World Music Awards". Jamaa huyu kwanzia hapo alianza kutawala chart mbali mbali huko Jamaica akiwa na ngoma zake nyingine kama vile "Is There a Place","Beautiful Lady" na ile hit kali ya "Mama, Don't Cry".

Mwishoni mwa mwezi May 2010, ngoma yake ya "Hold you" ilichukua nafasi ya 91 kwenye chart za Billboard Hot 100, na namba 33 katika Billboard R&B/Hip-Hop Chart na namba 6 kwenye Billboard R&B/Hip-Hop Chart. Nyimbo hiyo ilizidi kupata umaarufu mkubwa pale alipoifanyia remix ambayo ndani alimshirikisha NickMinaj. Ambapo ngoma hiyo ilirudi tena katika chart za Billord nakuchukua namba 2.

Gyptian pia aliwika vilivyo na ngoma yake maarufu inayojulikana kwa jina la "Nah let go" ambapo ngoma hii ilitoka mnamo mwezi November mwaka huo huo, Ngoma hii ilijipatia umaarufu mkubwa mno UK na pande mbali mbali ulimwenguni.Gyptian aliachilia album yake Nothing to Lose mwaka 2015.

 
Gyptian amepata mafanikio makubwa mno katika muziki huu, amendika nyimbo nyingi mmno ambazo zinapendwa kote ulimwenguni. 'WINE UP' ndio ngoma nayoipenda mimi kutoka kwa jamaa huyu, je we unaipenda ipi kutoka kwa Gyptian?

12 July, 2016

Nyota wa zamani wa Arsenal Henry aondoka Arsenal

HenryThierry Henry ameondoka Arsenal, baada ya kukataa nafasi aliyopewa ya kufundisha wachezaji wa chini ya umri wa miaka 18.
Henry, 38, alipewa nafasi hiyo na meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, ambaye alimuambia kuwa hawezi kuchanganya na kazi yake ya sasa kama mchambuzi wa soka kwenye TV. 

Hata hivyo, Henry ambaye alifanya kazi na wachezaji chipukizi wa Arsenal kama sehemu ya mafunzo ya kupata leseni yake ya ukocha ya Uefa, hakuwa tayari kuacha kazi yake ya uchambuzi wa soka.
Nahodha wa zamani wa Arsenal, Tony Adams, 49, sasa atachukua nafasi hiyo ya vijana chini ya miaka 18. 

Henry sasa lazima atafute timu ya kufundisha ili kukamilisha leseni yake ya ukocha.
Thierry Henry ameajiriwa na shirika la utangazaji la Sky Spors, na alifanya kazi kama mchambuzi wa BBC wakati wa michuano ya Euro 2016.

Music:Pakuwa nyimbo ya Timbulo Ft Malaika- Ngomani

Baada ya Kimya cha muda mrefu, Timbulo leo hii Jun 12 kaachilia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Ngomani, Humu ndani kashirikishwa mwana dada Malaika, ngoma imefanywa na T-touch. Bonyeza HAPA kuupata wimbo huo. Kumbuka kumpatia pia mwana kitaa na yeye uhondo huu kuoka kwa Timbulo.

Video: Kidogo – Diamond Platnumz ft P’square

Baada ya muda mrefu tangu kuthibitishwa ujio wa ngoma hii, Leo Diamond akishirikiana na  P’square kutoka kule Nigeria, wanatuletea Video inayokwenda kwa jina la Kidogo. Video imeongozwa na God Father kutoka kule Africa ya Kusini.

Kifafa chazid Kumtesa Lil Wayne

Star wa muziki nchini Marekani Lil Wayne ameshambuliwa kwa mara nyingine tena na ugonjwa wa kifafa wiki mbili zilizopita.

Kwa mujibu a TMZ, Lil Wayne na timu yake walishusha ndege mara mbili ili rapa huyu apate matibabu na jambo jili liliwekwa siri kwa muda huu wa wiki mbili.
Lil Wayne aliamua kisitisha show zake kwenye club ya TAO mjini Las Vegas na kwa sasa madaktari wake waangali dose bora zaidi itakayo msaidia kuwa sawa na kufanya kazi pia. Wayne anaugulia mjini Miami.

Music: Nay wa Mitego – Pale Kati

Msanii Nay Wamitego ameachia wimbo mpya unaitwa “Pale Kati”, Producer Mr T Touch. Chukua time yako kuusikiliza wimbo huu kisha mshirikishe mwana kitaa.

Tetesi za Soka Barani Ulaya

Chama cha soka cha England, FA, kitazungumza na meneja wa Hull City Steve Bruce, wakati wakiendelea na harakati za kutafuta meneja mpya wa England (Daily Telegraph), uhamisho wa Graziano Pelle kutoka Southampton kwenda Shandong Luneng ya China kunamfanya mshambuliaji huyo, 30, kuwa mchezaji wa sita anayelipwa zaidi duniani akipata pauni 260,000 kwa wiki (Sun).

PelleViungo Juan Mata, 28, na Bastian Schweinsteiger, 31, pamoja na mabeki Marcos Rojo na Daley Blind, 26, wanaonekana kama wachezaji wa ziada katika mipango ya meneja mpya wa Manchester United, Jose Mourinho (Daily Record), Villareal nao wamejiunga na Everton katika mbio za kumwania kiungo Juan Mata wa United (Daily Express).

BlindMeneja wa Manchester City Pep Guardiola anataka kumsajili beki wa Atletico Madrid, Lucas Hernandez, 20, kwa pauni milioni 20 (Sun), mshambuliaji kutoka Colombia, Marlon Moreno, 19, atasaini mkataba wa miaka mitano kwenda Man City, lakini atakwenda Deportivo La Coruna kwa mkopo msimu ujao (Daily Mirror), mwenyekiti wa West Ham, David Gill amesema klabu yake haitosikiliza dau lolote chini ya pauni milioni 50 kumtaka kiungo kutoka Ufaransa, Dimitri Payet, 29 (BBC Radio 5 Live).

PayetLazio wako tayari kumwacha Filipe Anderson, 23, kuondoka, huku Chelsea wakimtaka kiungo huyo (Gazzetta World), Chelsea pia wanataka kumsajili kiungo wa Barcelona, Arda Turan, 29, ambaye pia ananyatiwa na Arsenal (Sport), Chelsea vilevile wanajiandaa kutoa pauni milioni 34 kumsajili kiungo wa Sporting Lisbon, Joao Mario 23 (A Bola).

GotzeLiverpool wamejitoa katika kutaka kumsajili kiungo wa Bayern Munich Mario Gotze, 24, huku Tottenham na Borussia Dortmund wakiendelea kumtaka (Liverpool Echo), kipa wa zamani wa Arsenal, Alex Manninger, 39, anafanya mazoezi na Liverpool akiwa na matumaini ya kupata mkataba (Sun), beki Martin Skirtel, 31, anatarajiwa kuwasili Istanbul kukamilisha uhamisho wake wa pauni milioni 5.5 kutoka Liverpool kwenda Fernabahce (Daily Mirror).

SissokoEverton wamepanda dau la pauni milioni 25.5 kumtaka beki wa Juventus Daniel Rugani, 21 (Calcio Mercato), Christian Benteke, 25, hakaribii kuondoka Liverpool na kwenda Crystal Palace, kwa mujibu wa wakala wake (Evening Standard), Inter Milan wameweka bei ya pauni milioni 43, kwa klabu inayomtaka mshambuliaji wake Mauro Icardi, 23, ambaye anasakwa pia na Tottenham (AS), Newcastle watafikiria kumuuza kiungo Moussa Sissoko, 26, kwa timu itakayokuwa tayari kulipa pauni milioni 35 (Independent).

SOURCE: BBC

Video: Country Boy – AAh Wap

Rapper Country Boy ametoa video yake mpya ya wimbo wa ‘AAh Wapi‘, video hii imefanyika katika studio za Wanene ikiwa ndio video ya kwanza kutoka. Video imeongozwa na Khalfani Khalmandro.

11 July, 2016

Hizi ndizo kazi ambazo muda sii mrefu zitachukuliwa na Teknolojia.

Katika ulimwengu wa leo swala la teknolojia limekuwa likonekana kukua kwa kasi kubwa mno kiasi kwamba kila unapojigusa ama unachogusa ndani yake kuna zao la teknology. Tumeona mengi yatokanayo na teknology mfano mzuri ni kurahisishwa kwa njia za mawasiliano, usafiri nk

  Kutokana na hilo, kazi nyingi zimezidi kuchukuliwa na teknolojia, kazi ambayo ilikua ikifanywa na watu watano basi kazi hiyo itafanywa na mtu mmoja tu!. na hizi ndizo kazi ambazo ziko hatarini kumezwa na technology.

1.Personal Assistants and Secretaries Hivi kuna haja ya kuliongelea hili?
laaa hasha! we kama huku tafadhali jiongeze maana muda sii mrefu utakosa kibarua aisee.

2.CashiersJobs that will soon be taken over by technology Kama ulikua umezoea kwenda super-market ama mgahawani na kumtafuta mhudumua kwa ajili ya kulipia manunuzi yako, iko siku hutoweza kuwaona watu hao na badala yake utakutana na mitambo maalumu kwa ajili ya kazi hiyo ambapo utalazimika kuweka bidhaa hizo katika mitambo hiyo kisha ukalipia na kupewa risi na kuondoka nyumbani.

3.Computer Operators.
 Jobs that will soon be taken over by technology IT imekuwa kubwa mno na nyanja hii tunaitazamia kuleta mapinduzi makubwa mno katika duru mbali mbali mfano Biashara, Afya nk, lakini kwa upande wa pili inaweza ikapia kazi za watu wengine ambao wako katika nyanja hiyo hiyo ya IT hapa namaanisha  Computer operators. Itafika pahala kama wewe ni Computer operator hutopigiwa simu kwamba uje urekebishe computer zetu ama uje utusaidie tatizo la computer zetu ama kazi katika computer yetu, Mwenye tatizo ataingia GOOGLE na YOUTUBE kisha ataangalia tutorials kazi imekwisha.

4.Data Entry ClerksJobs that will soon be taken over by technology Katika biashara, shughuli kampuni mbali mbali na katika uandishi(hasa magazetini na medias kwa jumla), Kutunza kumbukumbu na takwimu ni jambo la Muhimu na lakwaida mno. Wapo watu maalumu kwa ajili ya kazi hiyo ila kutokana na kurahisishwa kwa Technology, watu hao wataanza kukosa kazi hizo maana iko mifumo ambayo imetengenezwa teyari kwa ajili ya kazi hiyo ambayo inafanya kazi hiyo kwa haraka na kwa ufanisi zaidi(automated data entry systems). Kama wewe ni miongoni mwa watu walioko katika kazi hizi tafadhali jiongengeze.

5.Call ReceptionistsJobs that will soon be taken over by technologyAutomated services are fast replacing humans at companies both large and small – so much so that getting a real live person on the line when you place a call to a company can come as something of a shock. This trend shows no sign of slowing down, so if you’re one of these, get on a job search.

HIZO NI BAADHI TUU YA KAZI AMBAZO MUDA MFUPI UJAO ZITAMEZWA NA TECHNOLOGY, HIVYO BASI HUNA BUDI KUKUBALINA NA HALI HII NA KUANZA KUKIMBIZANA NA TECHNOLOGY.

video mpya ya Nikki Mbishi Ft Becka Title ‘Kwa Nini Mimi’

Hii Video mpya ya Nikki Mbishi ‘Kwa Nini Mimi’ aliyomshirikisha Becka Title. Video imeongozwa na Mecky Kaloka. Chukua time yako kuitizama kisha kumbuka kuwashirikisha wana kitaa na kuusambaza upendo.

Young Thug ana amini hakuna kitu kiitwacho Jinsia.

Young Thug  Rapper huyo kutoka pande za states amekua akisema  na kufanya vitu ambavyo vimekuwa ni vituko na kuwavutia watu wengi hasa mashabiki wake kote ulimwenguni bila kujali jinsia na mapenzi, ameendelea kutisha kitaa na mavazi yake ambayo mengi ni ya kike ila yeye hajali hilo kabisa.

  Kwenye utengenezaji wa tangazo la  Calvin Klein kampuni maarufu ya mitindo, Thug amesema haamini kama kuna Jinsia.
“In my world of course you could be a gangsta with a dress or you could be a gangsta with baggy pants. I feel like it’s no such thing as gender.”
 Na hii ndio video ya Tangazo hilo.

Shamrashamra zazidi kunoga huko ureno


Kundi kubwa la mashabiki wa Ureno limeendelea kusheherekea bada ya timu yao ya taifa kuifunga Ufaransa katika michuano ya Euro 2016 mjini Paris.
Ureno imeshinda 1-0 katika muda wa nyongeza na kuwaacha mashabiki wa Ufaransa katika hali ya simanzi ndani ya dimba la Stade de France huku mitaa ya Lisbon ikirindima kwa shangwe kubwa.

Ureno illicheka karibia mda wote bila huduma ya nyota wake Cristiano Ronaldo aliyeumia na kutolewa nje dakika 25 ya mchezo huo na baadaye kurejea na kulinyanyua kombe hilo.

Amesema kombe hilo ni kwa ajili ya Wareno wote pamoja na wote wanaioshabikia timu hiyo mjini Paris.
Hii ni mara ya kwanza kwa Ureno kushinda taji kubwa kama hilo.

Video: Gnako Feat Nikki wa Pili – Laini

Kutoka Weusi, Rapper mwenye uwezso mkubwa katika muziki Gnako(mnako) katuletea Video mpya aliyo mshirikisha rapper Nikk wa Pilli, video hiyo inakwenda kwa jina la Lain na imeongozwa na director Freeman Richard. Chukua time yako kuitizama video hiyo hapa.

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...