04 April, 2015
Arsenal yaichapa Liverpool
Ligi kuu ya Uingereza jioni ya leo imeendelea katika viwanja tofauti nchini humo huku Arsenal ‘The Gunners’ wakiwafumua Liverpool kwa jumla ya mabao 4-1 na kufanya ndoto wa Majogoo hao wa jiji la Landon kuzidi kupoteza matumaini ya kushiriki klabu bingwa Ulaya mwakani.
Arsenal ndio walianza kupata bao
kupitia kwa Hector Bellerin kunako dakika ya 37 kabla ya Ozil kucheka na
nyavu dakika ya 40 baada ya kuachia shuti kali lililotokana na adhabu
ndogo kufatia mchezaji wa Aresenal kufanyiwa madhambi.
Dakika ya 45 Sanchez aliiandikia
The Gunners bao la tatu kabla ya Olivier Giroud kufunga kabisa idadi
ya mabao katika uwanja wa Emirates kwa kuandika bao la 4, Bao pekee la
Liverpool limefungwa na Jordan Henderson kwa mkwaju wa penati.
Katika mchezo huo Mchezaji wa
Arsenal ambao walikuwa wanatumia mfumo wa (4-2-3-1) na Timu ya Taifa ya
Ujerumani, Mesut Ozil, alifanikiwa kuibuka
Man of the Match.Kocha wa Arsenal
Mfaransa Arsene Wenger aliwatumia Ospina, Bellerin, Mertesacker,
Koscielny, Monreal, Coquelin, Cazorla, Ramsey, Sanchez, Ozil, Giroud. huku wengine wakianza benchi kama, Gibbs, Macey, Rosicky, Walcott, Welbeck, Gabriel, na Flamini.
Kikosi cha Liverpool kikiwa chini ya Brendan Rodgers ambacho kilitumia mfumo wa
3-4-2-1 kilikuwa ni Mignolet, Can 5, Toure, Sakho, Henderson, Allen,
Lucas, Moreno, Markovic, Coutinho, Sterling huku Sturridge, Borini,
Brannagan, Johnson, Jones, Lovren, Manquillo wakianzia benchi.
Kuatia matokeo hayo sasa Aresenal inakuwa imeishusha
Manchestar City katika nafasi ya pili ikiwa na alama 63 mele kwa pointi 2
huku wakiendelea kusoma namba za Chelsea wanaoongoza kwa alama 67.Rapa Kendrick Lamar ametoa video mpya iliyofanyika mitaa ya kwao “King Kunta”,itazame hapa
Rapa Kendrick Lamar ametoa video mpya ya “King Kunta” iliyotayarishwa na director X iliyofanyika kwenye mitaa aliyozaliwa ya Compton. Album yake mpya To Pimp a Butterfly bado ipo namba moja kwenye chati za Billboard 200 ambayo mpaka sasa imeuza kopi 447,000.
Video,Hatua kubwa aliyopiga Kendrick Lamar kwenye mapenzi.
Rapa Kendrick Lamar amedhibitisha kuwa amemvalisha pete ya uchumba
mpenzi wake wa muda mrefu Whitney Alford. Kendrick na Whitney walisoma
wote shule ya sekondari na ni marafiki wa muda mrefu.
Hii ndio interview ya Kendrick lamar kwenye kipindi Power 105.1 “The Breakfast Club” jana.
YANGA YATINGA 16 BORA>>>>>>>
Maabingwa wa zamani wa ligi kuu
ya Tanzania bara, ambao ni wawakirishi pekee wa Tanzania katika michuano
ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, Dar es Salaam Young Africans, leo
wamefanikiwa kusonga mbele katika hatua ya 16 bora ya michuano hiyo
licha ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya FC Platinum.
Yanga ambao walikuwa na faida ya
bao 5 ambazo walizipata katika mchezo wa kwanza uliopigwa Jijini Dar Es
Salaam wiki mbili zilizopita, leo walijikuta wakifungwa na wenyeji hao
kupitia kwa W. Musona kunako dakika ya 30 kipindi cha kwanza kwa shuti
kali akiunganisha krosi safi kutoka upande wa kushoto.
Katika mchezo huo Platinum
walikuwa wakishambuia kwa wingi lango la Yanga huku Watanzania hao
wakifanya mashambulizi ya Kushitukiza, ambapo dakika ya 4 Platinum
Walipata bao lakini muamuzi akalikataa kwasababu tayari mchezaji alikuwa
amekwisha otea.
Dakika ya 12 Kipa wa Yanga Ally
Mustafa Bartez aliisaidia Yanga baada ya kuokoa mchomo uliopigwa langoni
huku mshambuliaji wa Platinum akiwa na kipa lakini kipa huyo akapangua
na kufanya Yanga waanze upya kujipanga.
Mshambuliaji wa Yanga Mrisho
Halfani Ngassa alikosa bao kunako dakika ya 22 baada ya ‘kukunjuka,
kupiga Tik-Tak ambayo haikuzaa matunda kufatia kichwa cha Amis Tambwe
aliyeunganisha mpira wa kona uliopigwa na Simon Msuva.
Hadi muamuzi anapuliza kipenga
cha mwisho kuashiria kipindi cha kwanza kimemalizika Yanga walikuwa
Nyuma kwa bao 1-0 lililofungwa na Musona.
Kipindi cha pili kilianza kwa
kasi ambapo kocha wa Yanga Hans Van Pluijm aliamua kumtoa beki Said Juma
Allly na nafasi yake akaingia mkongwe Calvin Yondani ili kuhakikisha
Platinum hawapati bao linguine na kuwaweka Yanga katika wakati mgumu.
Dakika ya 53 Mrisho Ngassa
anakosa bao la wazi baada ya kupenyezewa pasi na Kiungo Haruna Niyonzima
lakini Uncle akawa kwenye kizingiti cha mabeki wa Platinum ambao
waliokoa mpira huo.
Simon Msuva kunako dakika ya 55
aliwakosesha Yanga bao baada ya kuwaadaa mabeki wa Platinum na kuachia
shuti kali ambalo pia halilkuleta madhara na kugeuka mboga kwa kipa wa
Platinum.
Ili kuhakikisha labda wanapata
angalau bao la ugenini hata moja Kocha Hans Van Pluijm aliamua
kumpumzisha Msuva na nafasi yake kuchukuliwa na Dan Mrwanda kunako
dakika ya 89.
Baada ya dakika 4 za nyongeza
Mrisho ngasa alipewa kadi ya Njano kwa kumchezea vibaya mchezaji wa
Platinum ikiwa ni pamoja na kupinga maamuzi ya Refa.
Hadi dakika ya mwisho Yanga
wanauwa wamefanikiwa kusonga mbele kwa jumla ya mabao 5 kwa 2 kwani
mchezo wa awali matokeo ilikuwa 5 kwa Yanga na 1 kwa Platinum.
Garissa:Redio 2 zafungwa Somalia.
Mamlaka nchini Somalia imevifunga
vituo viwili vya redio nchini humo baada ya kutangaza habari za
wapiganaji wa Al-shabaab kuhusu shambulio la chuo kikuu nchini Kenya.
Kituo cha redio cha Sky FM na kile cha Shebelle vilifungwa huku mtangazaji na mkurugenzi wakikamatwa.Vikosi vya usalama nchini Somali vimekuwa vikiwakamata wanahabari ambao hufanya mahojiano na wapiganaji wa Al-shabaab ama kutangaza habari zao.
Wanaotaka kujifunza muungano, waje Tanzania
Rashid Yussuf Mchenga
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni muungano wa mfano duniani. Ni dola mbili huru zilizoungana na kuunda nchi moja yenye serikali mbili.
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni muungano wa mfano duniani. Ni dola mbili huru zilizoungana na kuunda nchi moja yenye serikali mbili.
Tanganyika ilipata uhuru wake Desemba 9/1961 na ikapata kiti chake katika Umoja wa Mataifa Desemba 14, 1961. Namba ya kiti hicho ni ‘GA resolution 1667 (XVI).’ Zanzibar nayo ikapata uhuru wake Desemba 10, 1963 na ikapata kiti chake katika Umoja wa Mataifa Desemba 16, 1963; namba ya kiti hicho ni ‘GA resolution 1975 (XIII).’
Ilipofika Aprili 26, 1964, mataifa hayo mawili huru yaliungana na hapo ndipo ilipozaliwa nchi iliyojulikana kwa jina la Tanzania.
Novemba 2, 1964 kupitia Wizara wa Mambo ya Nchi za Nje ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, iliuandikia barua Umoja wa Mataifa na kutaka Zanzibar na Tanganyika ziondoshwe katika orodha ya mataifa na iingizwe nchi inayojulikana kwa jina la Tanzania.
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni sawa na muungano wa Siria na Misri walioungana mwaka 1958 na ni sawa na muungano wa Yemen ya Kaskazini na Yemen ya Kusini walioungana mwaka 1990. Kwa bahati mbaya muungano wa Siria na Misri ulivunjwa mwaka 1961 (ulidumu kwa miaka 3).
Jinsi ya Kuishi Maisha Yenye Furaha
“Nitakuwa na furaha nikifunga ndoa na kupata watoto.”
“Nitakuwa na furaha nikimiliki nyumba yangu mwenyewe.”
“Nitakuwa na furaha nikipata kazi.”
“Nitakuwa na furaha nikiwa na . . .”
JE, UMEWAHI kuhisi
hivyo? Je, ulipopata kile ulichokuwa unatamani, furaha yako ilidumu, au
ilianza kupungua? Kwa kweli, kufikia lengo au kupata kitu tulichotamani
kunaweza kutufanya tuwe na furaha, lakini furaha hiyo huenda isidumu.
Furaha ya kudumu haitegemei tu mafanikio au vitu tulivyo navyo. Badala
yake, furaha ya kweli inategemea mambo mengi kama tu jinsi mtu
anavyohitaji kufanya mambo mbalimbali ili awe na afya nzuri.
Mahitaji yetu
yanatofautiana. Kinachokufurahisha wewe huenda kisimfurahishe mwingine.
Kwa kuongezea, tunabadilika tunapoendelea kukua. Ingawa hivyo,
uthibitisho unaonyesha kwamba kuna mambo ambayo huhusianishwa na furaha.
Kwa mfano, furaha ya kweli inahusiana na kuridhika, kutowaonea wivu
wengine, kuwapenda watu, na kutokata tamaa. Acheni tuchunguze mambo
hayo.
1. KURIDHIKA
Mwanamume mmoja
mwenye hekima alisema hivi: “Pesa ni ulinzi.” Hata hivyo, aliongezea
kusema hivi: “Anayependa fedha hatatosheka na fedha, wala anayependa
mali hatatosheka na mapato. Hilo pia ni ubatili.” (Mhubiri 5:10; 7:12)
Alimaanisha nini? Ingawa ni kweli tunahitaji pesa ili kuishi, tunapaswa
kuepuka pupa, kwa sababu hatuwezi kutosheleza tamaa hiyo!
Mfalme Sulemani wa Israeli la kale, aliyesema maneno hayo, alifanya
utafiti ili kuthibitisha ikiwa kuishi maisha ya anasa kunaleta furaha ya
kweli. Aliandika hivi: “Sikuyanyima macho yangu chochote ambacho
yaliomba. Sikuunyima moyo wangu shangwe ya aina yoyote.”—Mhubiri 1:13; 2:10.
Baada ya
kujikusanyia utajiri, Sulemani alijenga majumba makubwa, alitengeneza
mabwawa ya kuogelea na bustani maridadi, na alikuwa na wafanyakazi
wengi. Alipata kila kitu alichotaka. Alijifunza nini? Mambo hayo
yalimletea furaha kwa kiasi fulani, lakini si kwa muda mrefu. Aliandika
hivi: “Na, tazama! kila kitu kilikuwa ubatili na kufuatilia upepo, wala
hapakuwa na lolote lenye faida.” Hata aliyachukia maisha! (Mhubiri 2:11, 17, 18) Kwa kweli, Sulemani alitambua kwamba maisha ya kujistarehesha tu hayaleti furaha ya kudumu. *
Je, utafiti wa
kisasa unakubaliana na jambo hilo? Makala moja kwenye Jarida la Masomo
ya Jinsi ya Kuwa na Furaha (la Kiingereza) inaeleza hivi: “Mara baada ya
mtu kutosheleza mahitaji yake ya msingi, vitu vingine atakavyozidi
kupata havitamwongezea furaha.” Kwa kweli, utafiti unaonyesha kwamba
ikiwa mtu anaamua kufuatilia maisha ya anasa na kupuuza viwango vya
maadili na vya kiroho, anaweza kupoteza furaha.
KANUNI YA BIBLIA: “Namna yenu ya maisha iwe bila upendo wa pesa, huku mkiridhika na vitu vya sasa.”—Waebrania 13:5.
2. EPUKA KUWAONEA WIVU WENGINE
Kamusi moja
inafafanua wivu kuwa “uchungu au kinyongo kinachotokana na kutambua
kwamba mwingine ana kitu ambacho huna, na pia tamaa ya kutaka kuwa na
kitu hicho.” Kama tu uvimbe hatari unaoenea haraka, kuwaonea wivu
wengine kunaweza kutawala maisha ya mtu na kumfanya akose furaha. Mtu
huanzaje kuwaonea wivu wengine? Tunawezaje kutambua kama tuna tatizo
hilo? Na tunawezaje kukabiliana nalo?
Kulingana na kitabu Encyclopedia of Social Psychology watu
huwa na mwelekeo wa kuwaonea wivu watu ambao wanalingana nao, huenda
katika umri, uzoefu, au malezi. Kwa mfano, si rahisi kwa mfanyabiashara
kumwonea wivu mwigizaji maarufu. Lakini huenda akamwonea wivu
mfanyabiashara mwenzake mwenye mafanikio kuliko yeye.
Mfano: Maofisa
fulani katika utawala wa zamani wa Uajemi, hawakumwonea wivu mfalme,
badala yake walimwonea wivu Danieli ofisa mwenzao. Kwa sababu ya wivu
wao hata walifanya mpango wa kumwua Danieli! Hata hivyo mpango huo
haukufanikiwa. (Danieli 6:1-24) Kitabu Encyclopedia of Social Psychology kinaendelea
kusema hivi: “Ni muhimu tutambue kwamba wivu unaweza kutufanya tutake
kuwadhuru wengine. Ndiyo maana kuna visa vingi vya ukatili katika
historia ya wanadamu ambavyo vimesababishwa na kuwaonea wivu wengine.” *
3. WAPENDE WATU
Kitabu Social Psychology kinasema:
“Ikiwa watu wana uhusiano mzuri miongoni mwao, jambo hilo linaweza
kuwafanya wafurahie maisha hata kuliko furaha inayopatikana kwa kuwa na
kazi, mshahara mnono, kukubaliwa katika jamii, au kuwa na afya nzuri.”
Kwa ufupi, ili wanadamu wawe na furaha ya kweli, wanahitaji kupenda na
kupendwa. Mwandikaji mmoja wa Biblia alisema hivi: “Ikiwa . . . sina
upendo, mimi si kitu.”—1 Wakorintho 13:2.
Sisi sote tuna
nafasi ya kusitawisha upendo. Kwa mfano, Vanessa alikuwa na baba mkatili
na mlevi kupindukia. Alipokuwa na umri wa miaka 14, alitoroka nyumbani
na hakuwa na makazi maalumu, na hata alimwomba Mungu amsaidie. Kisha,
inaonekana kwamba Mungu alimsaidia kwa sababu alianza kuishi na familia
iliyofuata kanuni ya Biblia inayosema “upendo ni wenye ustahimilivu na
wenye fadhili.” (1 Wakorintho 13:4)
Kuishi na familia hiyo na kujifunza Biblia, kulimsaidia Vanessa kupona
kihisia na kiakili. Alisema hivi: “Nilianza kufaulu masomoni na alama
zangu zikawa bora.”
Vanessa bado anakumbuka mambo yaliyompata zamani. Hata hivyo, sasa ana ndoa yenye furaha na ni mama wa wasichana wawili.
KANUNI YA BIBLIA: “Jivikeni upendo, kwa maana huo ni kifungo kikamilifu cha muungano.”—Wakolosai 3:14.
Lil Wayne kuhusu album mpya na mpenzi wake mpya.
Rapa Lil Wayne amesema yupo tayari kutoa album yake mpya ya “Free Weezy Album” mwezi wa nne mwaka huu 2015.
Lil Wayne anasema album itatoka kama solo projet yake mwenyewe ikiwa ni ya pili baada ya Sorry 4 Tha Wait iliyotoka January baada yakushindwa kutoa Tha Carter 5.
Wayne ambaye ni Bosi wa kundi la Young Money, amemuweka wazi mpenzi wake mpya, Christina Milian, ambaye ni mmoja wa wanachama wa kundi hilo analoliongoza. Baada ya kuweka wazi habari hiyo, Wayne kupitia mtandao wa Twitter, aliandika, “Samahani kwa kusubiri muda mrefu kujua nini kinaendelea, kwa sasa hakuna tena maswali nikiwa na Christina, huyu ni mpenzi wangu.”
Kumbe Habida aliwahi kubakwa? ilikuaje? na anaichukuliaje sasa hivi?
Tulilijua kwa ukubwa jina la Habida baada
ya kutoa hit single ya kesho zaidi ya miaka mitano iliyopita akiwa ni
mwimbaji kutokea Kenya.
Kwenye interview na show ya Mambo Mseto ya
Radio Citizen Kenya, kwa mara ya kwanza Habida amefungua kinywa chake na
kukiri aliwahi kubakwa akiwa mdogo.
Radio Citizen Kenya, kwa mara ya kwanza Habida amefungua kinywa chake na
kukiri aliwahi kubakwa akiwa mdogo.
Ilitokeajie???? >>>>>> ‘Nilikua
bikra wakati huo na huyo Mwanaume alikua akisema wewe nitakupata tu,
sasa siku moja ilitokea nikawa nimetoka na marafiki zangu, nikalewa na
wakati nataka kwenda nyumbani huyu Mwanaume akasema atanipeleka nyumbani
lakini hakunifikisha, ndio akanibaka‘
bikra wakati huo na huyo Mwanaume alikua akisema wewe nitakupata tu,
sasa siku moja ilitokea nikawa nimetoka na marafiki zangu, nikalewa na
wakati nataka kwenda nyumbani huyu Mwanaume akasema atanipeleka nyumbani
lakini hakunifikisha, ndio akanibaka‘
Kwenye sentensi nyingine, Habida amesema
anataka kuwaonyesha Wanawake wengine kwamba hata kama ukibakwa
haimaanishi ndio umefeli maisha, anataka kutumia kilichomtokea kuonyesha
Wanawake wengine kwamba hata kama kuna kitu kilitokea hakikuharibu
maisha yake, yuko hapa na ameendelea na maisha, single yake mpya inaitwa
Keep on walking.
anataka kuwaonyesha Wanawake wengine kwamba hata kama ukibakwa
haimaanishi ndio umefeli maisha, anataka kutumia kilichomtokea kuonyesha
Wanawake wengine kwamba hata kama kuna kitu kilitokea hakikuharibu
maisha yake, yuko hapa na ameendelea na maisha, single yake mpya inaitwa
Keep on walking.
WANAMWITA LULU MICHAEL UMRI WAKE NA UREMBO WAKE NI SHIIIIIDA
Inasemekana ndio kwanza atatimiza miaka 20 soon lakini ukimwangalia
kwenye picha uzuri wake na urembo ni shida kwa umri wake je unafikiri
ingekuwa vizuri kuwa mke au andelee tu kuwa pambo na watu wazidi
Reginald Mengi amefunga ndoa na Jacqueline Ntuyabaliwe, picha ziko hapa
Mtandao wa Bongo5.com umepata nafasi ya kupokea pichaz Exclusive kutoka kwenye harusi hii ambayo imefungwa kwenye ardhi ya nchi ya Mauritius kwenye mwisho wa mwezi March 2015.
Hii ndoa pia ilishuhudiwa na watoto wao wawili mapacha kama wanavyoonekana kwenye picha pamoja na marafiki wengine wa familia pamoja na ndugu ambao idadi yao inafikia 50.
Ndoa imefungwa miezi minne baada ya Reginald Mengi kumchumbia Jacky Dubai kwenye siku ya kuzaliwa ya mrembo huyu December 2014.
EPL LEO KUENDELEA............
ARSENAL wapo katika kibarua kingine kizito leo kwa kuikaribisha Liverpool uwanja wa Emirates.
Miamba hiyo ya soka nchini England inachuana mapema saa 8:45 mchana.
RATIBA NZIMA YA LIGI KUU ENGLAND EPL LEO JUMAMOSI
Miamba hiyo ya soka nchini England inachuana mapema saa 8:45 mchana.
RATIBA NZIMA YA LIGI KUU ENGLAND EPL LEO JUMAMOSI
Moroco yashinda kesi CAS.
KIONGOZI wa juu wa Shirikisho
la soka nchini Morocco, Nour Eldin Boushehati ameweka wazi kuwa taifa
lake liko tayari kuwa mwenyeji wa fainali za mataifa ya Africa, Afcon
2017.
Mahakama ya juu ya rufani ya
FIFA ya masuala ya mpira (CAS) alhamisi ya wiki hii iliitangaza Morocco
kuwa huru kutoka katika kifungo cha CAF na kusema wanaweza kushiriki
fainali za Afcon 2017 na 2019.
Boushehati sasa anajiamni kuwa wako tayari kuhodhi michuano hiyo kwa miaka miwili mfululizo.
“Tuko yatari kuwa wenyeji wa
michuano ijayo ya Afcon kama serikali itatupa ruksa, tuko tayari,
tunaisikiliza serikali. Wakituruhusu tutakuwa tayari kuwa wenyeji,”
Amesema Boushehati.
Morocco walitakiwa kuwa wenyeji
wa fainali za Afcon mwaka huu 2015 lakini walichomoa dakika za mwisho
wakihofia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.
Guinea ya Ikweta ilikubali kuwa mwenyeji wa fainali hizo muda mfupi baada ya kuombwa na CAF.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...