18 July, 2015

MAKALA : MUZIKI WETU BONGO.

Katika maisha ya kawaida Muziki umekua sehemu kubwa mno kutokana na kwamba muziki ni njia mojawapo inayotumika katika maswala ya uelimishaji, burudani, na hata uamasishaji katika jamii zetu.
Leo nimemona niandike makala hii na ikufikie wewe msomaji wangu na makala hii inauzungumzia MUZIKI WETU HAPA BONGO.

    Miaka ya nyuma kuanzia miaka ya 2000 hadi 2005 na 2006 muziki wetu wabongo(BONGO FLEVA) ulianza kuonekana ukilipa na kukua kwa kasi kiasi ambacho liliongezeka kundi kubwa la wasanii wa muziki huo wengi wao wakiufanya muziki huo kwa makundi au kama msanii mojamoja yaani SOLO ARTIST.

Image result for wakali kwanza
MAKAMUA NA Q JAY
Yalikuwapo makundi makubwa kama vile TMK WANAUME, ambao kwa sasa kundi hilo limevunjikia mbali, WAKALI KWANZA, ambao nao hatufaham walipotelea wapi, EAST COST TEAM, kundi ambalo lilisheheni wakali kama vile AY, KING CRAIZY GK, FA na wakali kibao ambao nao hatufahamu walipoishia. 

     Hayo ni baadhi ya makundi makubwa yaliyotikasa mno katika muziki huu wa BONGO FLEVA, Kuna wasanii waliotisha mika hiyo na hadi leo wengi wetu hatufahamu walipo na wanafanya nini kwa sasa baadhi yao tumekuwa tukiwaona katika mitandao yetu yakijamii na mara tuu wanapo ulizwa VIPI MBONA HATUKUONI KATIKA GAME  TENA? majibu ya swali hili Kutoka kwa wana WAPOTEVU hawa ni majibu yanayo tukosesha raha au kutufanya sisi kuwaona kama wamepoteza moja kwa moja VIPAJI vyao HADIMU ambovyo sisi wadau tume vikosa kwa muda mrefu, moja ya majibu wanayo tupatia ni NAJIANDAA NA PROJECT MPYA SO MASHABIKI WANGU MKAE TAYARI KWA UJIO WANGU MPYA, Mimi nadhani huambizana kwa maana kila msinii kati yao anapohojiwa mahali popote kwa muda tofauti huja na jibu moja.

   Tuyaache hayo ya WANA WAPOTEVU hawa, kazi yetu sisi ni kuwangoja kwa hamu na shauku kubwa na tuje kwenye swala letu moja kwa moja.

             Ni kwa nini Muziki wetu hautambuliki kimataifa?
Kila mmoja wetu hujiuliza swali hili na ni matumaini yangu yakwamba swali hili huleta shida na utata katika upatikanaji wa majibu yake.

   Jibu ni kwamba muziki wetu ni uleeee waku kopi na kupest, na hii inaonekana wazi kwa kila mmoja wetu hapa BONGO. Kuanzia utayarishaji hadi usambazaji wake umekua ni wakuiga tuu na sio tulio buni sisi. Tujiulize ni kwa nini wenzetu UGANDA muziki wao una kua kila siku na wanapata kujulikana Karibu ulimwengu mzima ilhali nchi yao kiuchumi bado ipo chini? Je wao ni bora kuliko sisi? laa hasha, ni Aina pekee waliyo ibuni na kuitumia wao kama wao na hadi leo hii wana wika. Huu ni ukweli na wa weza bisha lakini kiuhalisia ndivyo mambo yalivyo.

  Leo hii huwezi kumlinganisha mwana muziki wa Bongo na wa UG, kiuchumi na hata kimuziki kwani wenzetu wanajua wanacho kifanya katika game ya muziki hasa katika kanda hii ya Afrika Mashariki.

  Wabongo tumekuwa tuki iga na wala  sio kubuni kilicho chetu. Mfano mzuri na kwamba Kipindi Suma lee  aliporudi katika game baada yakipindi kirefu kukaa kimya alikuja na Ngoma ya HAKUNAGA ngoma yenye mahadhi ya KWAITO na alitisha sana katika vituo mbali mbali vya redio na TV za hapa BONGO na katika kumbi mbali mbali za starehe

 Chakushangaza baada ya muda mfupi watu waliiga staili ile ya KWAITO jambo ambalo kila mwana muziki alijaribu kufanya KWAITO. Wazi mpaka hapo? Tukumbuke yakwamba KWAITO sio MUZIKI WETU  huu ni muziki wa AFRICA KUSINI kuleee kwa mzee madiba.
    
Mziki wetu Sasa umehamia Nigeria?
Ni ukweli usio pingika yakwamba wasanii wetu wa hapa nyumbani wamekua wakiiga muziki wa NIGERIA ambao kwa sasa watoto wa uswahilini wanasema ni HABARI YA MJINI. Utaskia ngoma ya hapa nyumbani na utashindwa kutofautisha Kati yao na sisi WABONGO.

  Huku ni kuwatukuza Na kuwapa wenzetu MAUJIKO na kwa hakika kwa halii hii tuta fail kama tunavyozidi kufail kwenye nyanja nyingine za kimaendeleo hapa kwetu.

Tuu ache UJINGA HUU na tutengeneze kile kilicho chetu na tukifanye kwa nguvu zetu zote na akili zetu zote na Mabadiliko haya yaanzie Huko kwa MAPRODUCER hadi WASANII.
 Wenye misemo yoa walisema "MTAKA CHA UVUNGUNI SHARTI AINAME" na "NGUO YAKUAZIMA HASITIRI MAUMBILE"

Je Diamondi ndio msanii mwakilishi wa Tanzania Kimataifa?
Siwezi sema moja kwa moja NDIO kwani mimi binafsi Bado naona wapo wasanii kibao na MALEGENDARY wanaofanya vizuri Kimataifa akiwepo AY na wenzake ambao walianza Kuitambulisha Tanzania kimataifa hata kapla ya DIAMOND kujulikana

   Ni kwamba mwenzetu Kaokota DODO chini ya MUAROBAINI. Ni jambo la faraja kuona kijana wetu anafanya poa nyumbani na ugenini na hii inatokana na Jitihada anazozifanya ili azidi kung'ara mthili ya nyota angani.
  
Tufanye nini ili na sisi tutoke?
     Hapa ndo penyewe. Chakufanya ni kila msanii kujituma na kuacha kukopi vya watu, ebu kila msanii ajaribu kutoka kwa staili ya kipekee kama wenzetu wanavyofanya. Na sisi WADAU tuache ushabiki usio na tija na tuungane kuwapa shime vijana wetu kwani mziki NI BIASHARA na wengi wetu ndipo FARAJA ZETU HUPATIKANA.Niliyo yasema ni machache mno hayo ni baadhi tuu yapo mengi yanayo husu muziki wetu hapa BONGO.


 Kipekee nipende kukushukuru wewe uliechukua mda wako wa thamani kusoma makala hii na ni imani yangu umepata picha angalau wapi muziki wetu unapokwenda. kwa maoni au ushauri tafadhali wasiliana nami kupitia namba 0767322193 au tembelea ukrasa wangu wa facebook MAWERE MTOKA MBALI na twitter @mawere3.

Knocking On My Door!! – (Video) D’banj

dbanj2
Ni siku chache tuu zimepita toka D’banj aachie wimbo wake wa Knocking on my door na sasa video ya wimbo huo imetoka. Director wa video hii ni Moe Musa na D’banj mwenyewe.
Kwa sasa D’banj yupo Durban South Africa kwa ajili ya tuzo za MTV Africa Music Awards 2015.
Nimekusogezea video wa wimbo huo hapa chini, bonyeza play kuitazama.

Balmain celebrates Siblings' love in new theme shoot

Bella and Gigi Hadid...Kyle and Kendall JennerJoan and Erica Smalls

 Armando and Fernando...

Nay wa Mitego: Nina Maana Yangu Kutumia Damu Kwenye Video Zangu

Akizungumza na Clouds E ya Clouds TV, Nay amesema bado kuna video zinakuja zitakazokuwa na damu.
“Hii ni video ya pili naifanya hivi na kutakuwa na video nyingine ya tatu ambayo itakuwa na vitu kama hivyo,” alisema. “Hii ni kama sign yangu, kwahiyo nimepokea maoni mengi kuhusu kufanana kwa hii video lakini yote ni kwaajili ya damu na damu ni kama nilivyosema hii ni sign yangu,” aliongeza.

Pia Nay alieleza sababu iliyofanya wimbo wake na Diamond, Mapenzi au Pesa kufeli.

“Ndio haujafanya vizuri lakini tukumbuke wimbo Mapenzi au Pesa ni wimbo ambao umekosa video. Kwenye muziki wetu wa siku hizi watu wanataka video haraka, ukichelewa kufanya video wimbo unakuwa unapungua kasi siku hadi siku. Tumeshaona hili kwenye nyimbo nyingi sana za wasanii wetu, ukichelewa kutoa video, wimbo unakufa haraka sana, yaani unakuwa unapungua nguvu siku hadi siku.”

Nimempata Mwanaume Wa Ndoto Zangu, Alinikuta Nikiwa Kwenye Maumivu ya Mapenzi – Linah

Akizungumza na Bongo5 leo, Linah amesema mwanaume aliye naye kwa sasa ni mwanaume aliyekuja kumuokoa akiwa katika wakati mgumu wa kimapenzi.

“Kiukweli malengo yetu ni ndoa na wala haitachukua muda mrefu. Mungu akijalia mwakani,” amesema Linah. “Sasa hivi nataka ndoa mambo ya kuzini sitaki. Mimi sidhani kama ndoa ina ugumu wowote. Nataka sasa hivi kuwa wa halali kwa mtu mmoja na baadaye tupate watoto. Kwa jinsi tulivyoongea kazi ni kazi na mapenzi ni mapenzi, kwahiyo nafasi yangu ya kazi itakuwa pale pale. Na ninafikiri huyu ni mtu sahihi kwangu, ninafikiri ni mtu ambaye anaweza akawa mume wangu ndio maana nimekimbilia ndoa,” ameongeza.

“Amekuja kwangu kama mtu anayenipenda, ameona jinsi ninavyoumia kimapenzi. Kwahiyo huyu amekuja kama mtu mwenye nia, ni aina ya mwanaume ambaye nilikuwa namtafuta kwa muda mrefu na hatimaye amefika, sasa hivi nafurahi.”

Ubunge CCM Kama Urais

wabunge+pixWANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanaowania kibali cha chama hicho ili wagombee ubunge, wamejitokeza kwa wingi katika baadhi ya majimbo na kufanya mchakato huo kuwa na mvuto wa aina yake, unaofanana na ule wa urais.

Jana ikiwa siku ya pili tu tangu kufunguliwa kwa pazia la uchukuaji fomu za kuwania ubunge katika majimbo mbalimbali nchini, idadi ya wanachama waliochukua fomu katika baadhi ya majimbo, imekuwa kubwa na kuelekea kulingana na wawania urais katika chama hicho, ambao walifikia 42. Jimbo jipya la Mbagala ndilo lilitia fora kwa kuwa na wasaka ubunge 17, waliolipa Sh laki moja na kuchukua fomu ya kuomba wanaCCM wapendekeze mmoja wao kuwania nafasi hiyo katika jimbo hilo.
Kwa mujibu wa Katibu Muenezi wa Wilaya ya Temeke, Rutami Masunu, mpaka jana siku ya pili ya utoaji fomu, waliojitokeza katika Jimbo hilo jipya ni wanachama hao 17.
Alitaja baadhi ya aliowakumbuka kuwa ni pamoja na Peter Nyalali, Richard Tambwe Hiza, Lucas Malegeli, Issa Mangungu, Mindi Dominck Haule, Ally Makwilo, Kivuma Msangi na wengine.
Katika Jimbo la Temeke waliojitokeza kuchukua fomu ni Mbunge wa jimbo hilo anayemaliza muda wake, Abbas Mtemvu, Hamis Salim maarufu kama Chicago, Maimuna Chicago pamoja na Joseph Mhoha.
Masunu alisema kwa upande wa Jimbo la Kigamboni waliojitokeza kuchukua fomu ni pamoja na Dk Faustine Ndugulile anayetetea nafasi yake pamoja na wanachama wengine watatu.
Kwa Wilaya ya Ilala, Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Ernest Charles aliliambia gazeti hili kuwa jumla ya waliojitokeza katika wilaya hiyo ni wanachama 26.
Aliwataja baadhi ya wanachama hao na majimbo yao kwenye mabano kuwa ni Mussa Azzan Zungu, Mrisho Gambo, Waziri Kindamba (Ilala), Zahoro Lyasuka, Bona Kalua, Apruna Jaka, Siasa Chuma na Nicholaus, Baraka Omary, Christopher Japhet, Scholastica Kevela, Simon Kambe na Tunza Kanabe (Segerea).
Kwa jimbo la Ukonga ni Meya Jerry Slaa, Anthony Kalokola, Jacob Kasema, Hamza Mshindo, Fredrick Rwegasira, Ramesh Patel, Peter Kaseleko, John Machuta, Magesa Magesa, Amos Hangaya, Thomas Masegese, Edwin Moses na Ammo Mkuno.
Taarifa kutoka majimbo mengine ya Dar es Salaam, zilieleza kuwa katika Jimbo la Kinondoni walijitokeza wagombea tisa, Ubungo sita na jimbo jipya la Kibamba 10.
*Morogoro Kusini
Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, lililopo katika Wilaya ya Morogoro Vijijini nalo lilijikuta likipata wasaka ubunge 12, akiwemo mbunge anayemaliza muda wake, Dk Lucy Nkya.
Katibu wa CCM Wilaya ya Morogoro Vijijini, Shaibu Mtawa, alitaja baadhi yao aliowakumbuka kuwa ni Upendo Konyaki, Abdallah Mohammed, Athuman Maneno, Issa Dilunga na Semeni Mwinyimvua Kingalu.
Chilonwa, Morogoro
Mkoa mwingine ambao umepata wasaka ubunge wengi katika jimbo moja ni Dodoma, katika Jimbo la Chilonwa, lililokuwa likiongozwa na Hezekiah Chibulunje, ambaye alitangaza kutogombea tena ubunge. Waliochukua fomu mpaka jana mchana walifikia wagombea 12.
Miongoni mwa waliojitokeza kuwania jimbo hilo ni Godrick Ngoli, Paschal Ndolosi, Charles Ulanga, Peter Mlugu, Amos Kusakula na Chiuti Masagasi Jimbo la Mtera, mbunge anayemaliza muda wake, Livingstone Lusinde, naye amejikuta akikabiliwa na ushindani wa makada sita, akiwemo Charles Ulanga, Essau Mzuri na Dk Charles Msendekwa.

Duka La Westgate Kufunguliwa Leo

westgate
Duka la westagate lililo mji mkuu wa Kenya Nairobi linafungua milango yake hii leo kwa umma karibu miaka miwili tangu lishambuliwe na wanamgambo wa al shabab.
Watu 67 waliuawa wakati wa makabiliano ya siku nne wakati wanamgambo hao walipowafyatulia risasi wateja.
Duka hilo linafunguliwa wiki moja baada ya rais wa Marekani Barack Obama kufanya ziara nchini kenya hatua inayoonekana kama ishara ya imani kwa usalama wa nchini Kenya.
Al Shabab wameendesha mashambulizi mengine mabaya nchini Kenya tangu litokee shambulizi la Westgate likiwemo la chuo kikuu cha Garissa ambapo watu 150 waliuawa.

Manchester United wanajiandaa kumuachia David De Gea kama mchezaji huru msimu ujao kuliko kumuuza kwasasa kwenda Real Madrid.

david-de-gea-training-in-seattleMan United wameweka masharti kwamba De Gea atauzwa Real Madrid majira haya ya kiangazi endapo miamba hiyo ya Bernabeu itakubali kuwauzia mlinzi wa kati, Sergio Ramos.
Kumbuka De Gea na Ramos wote wapo katika timu zao kujiandaa na msimu mpya.
Kocha mpya wa Real Madrid, Rafa Benitez amesema hataki tu Ramos abakie Bernabeu bali anataka kumpa kitambaa cha unahodha kufuatia Iker Casillas kuondoka.
Kwa mujibu wa The Guardian, inasemekana dili la Ramos kutua Old Trafford linaweza kukamilika kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili la Majira ya kiangazi.
United hawana presha ya kuuza wachezaji kwenda klabu kama Real Madrid kwasababu wana mkwanja wa kutosha kuweza kuwazuia wanasoka wake.

17 July, 2015

Alipokosea Lowassa, Kilichomponza Membe Na Bahati Ya Magufuli

lowassa+-px
SITAKI kudai kuwa najua kwa uhakika sababu za Kamati ya Usalama na Maadili kukata jina la Edward Ngoyai Lowassa kutoka katika orodha ya wagombea wa urais ambao majina yao yaliwasilishwa katika Kamati Kuu ya Halmashauri ya Taifa kwa ajili ya mchujo.
Lakini si vigumu sana kudodosa kwa nini kampeni ya Lowassa iliangukia pua. Lowassa alifanya makosa kadhaa ya kimkakati.
Ili kuelewa kilichomfanya Lowassa kufanya makosa hayo ya kimkakati, ni muhimu kupitia muktadha wa historia ya Lowassa kisiasa. Kuna mambo mawili ya msingi katika muktadha huu.
Kwanza, Mwalimu Nyerere alihoji usafi wa Lowassa na inadaiwa alimkataa wakati wa uhai wake asigombee urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na utajiri mkubwa usioelezeka.
Pili, Lowassa alilazimika kujiuzulu uwaziri mkuu mwaka 2008 baada kashfa ya Richmond iliyohusiana na mkakati wa Serikali wa kutafuta njia za dharura za kutatua tatizo kubwa la uhaba wa umeme.
Hicho ndio cheo chake cha mwisho kikubwa cha kisiasa. Ndoto za Lowassa, ambaye aliamini angedumu katika wadhifa huo kwa miaka 10 yote ya Kikwete na hatimaye kumrithi nafasi ya urais, zilizimika ghafla.
Watu wawili wanatajwa kuwa ni nyota wa sinema ile ya kisiasa, ya Richmond, iliyomdondosha Lowassa. Mwenyekiti wa Kamati Teule ya Bunge, Dk. Harrison Mwakyembe na Spika wa Bunge wa wakati ule, Samuel Sitta. Si ajabu basi kuwa wawili hawa wamebakia kuwa ni maadui wa kisiasa wa Lowassa.
Baada ya kustaaafu, kumekuwa na tetesi kuwa uhusiano wa Lowassa na rafiki yake wa karibu wa siku nyingi, Jakaya Kikwete umekuwa ukiyumba huenda labda kwa sababu Lowassa anaamini hakutetewa. Wapo hata wanaoamini kuwa Kikwete alikuwa nyuma ya mkakati wa kumuondoa kutokana na ‘spidi’ kali ya utendaji ya Lowassa iliyotishia kumfunika.
Katika muktadha huo, urais kwa Lowassa ungekuwa na maana mbili kubwa. Kwanza, ingekuwa ni nafasi ya kusafisha jina lake kwa sababu kwa kawaida ni matendo yetu ya mwisho ndiyo yanayojenga urithi wa namna tutakavyokumbukwa. Nafasi ya juu ya Lowassa serikalini ilikuwa ni uwaziri mkuu ambao aliuacha kwa kashfa akituhumiwa kufisidi.
Pili, kwa Lowassa hii ingekuwa nafasi ya kulipa kisasi kwa wabaya wake. Wapambe walidai hana visasi, lakini je angemteua Mwakyembe, Sitta au Paul Makonda kushika nafasi yoyote Serikalini.
Nina hakika, utawala wa Lowassa ungehitimisha au kufifisha mustakbali wa kisiasa wa wanasiasa hawa katika uongozi wa nchi hii.
Hakuna haja ya kukaza mishipi ya shingo kupinga ukweli huo kwa sababu Lowassa asingekuwa wa kwanza kufanya hivyo. Ukichunguza utagundua kuwa hata Nyerere, Mwinyi, Kikwete – wote waliwanyima fursa baadhi ya watu. Watawala wote wanafanya hivyo na si vibaya kufanya hivyo, kisiasa.
Akijua kuwa angekamilisha mawili hayo, kusafisha jina na kulipa kisasi, Lowassa aliutaka sana urais. Kuutaka sana si tatizo. lakini kuonyesha kuwa anautaka sana ilikuwa ni tatizo. Ilikuwa ni suala la ‘iwe isiwe’, ‘vyovyote iwavyo’ na ‘kwa gharama yoyote’. Ilitutisha baadhi ya watu. Na hilo lilikuwa kosa la kwanza alilolifanya.
Katika kuutaka sana urais, Lowassa kiaina alitoa ‘ultimatum’ (tishio) kwa chama chake. alinukuriwa akisema haoni uwezekano wa kushindwa na haoni mtu wa kumkata jina lake.
Hilo lilikuwa ni kosa jingine. Alikiuka msingi muhimu wa CCM ambao wenyewe wamekuwa wakiukariri mara kwa mara, ‘chama kwanza, mtu baadaye’.
Ni wazi kuwa kama angekuwa Rais, ingekuwa ngumu kwa CCM kumdhibiti. Angekuwa na nguvu kuliko chama. Haipaswi kuwa hivyo, hususan, sasa wakati ambao Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana anamikakati ya kukipa chama nguvu zaidi za kusimamia Serikali.
Lowassa akaendelea kufanya kosa jingine la kukaribisha marafiki na wapambe wenye tuhuma na tabia za kutia shaka katika kampeni yake. Miongoni mwa hao walikuwapo mawaziri wa zamani na wafanyabiashara waliotoka serikalini kwa kashfa mbalimbali.
Haikuwa hatua nzuri kwa Lowassa ambaye tayari ana doa la Richmond kujizungushia atu wenye madoa kama yeye.
Hata watu waliojitokeza hadharani kuhoji uamuzi wa Kamati Kuu, Mwenyekiti wa Jumuia ya Wanawake Sophia Simba, Mwenyekiti wa zamani wa Jumuiya ya Vijana wa CCM, Emmanuel Nchimbi na mbunge wa Afrika ya Mashariki, Adam Kimbisa, kwa maoni yangu waliongozwa na maslahi yao kuliko ya watu. Hakuna kati yao mwenye rekodi safi ya kuonyesha anasimamia maslahi ya umma. Kwangu hawa wote ni ‘opportunists’.
Kampeni ya Lowassa pia ilikuwa ya kitajiri. Pesa zilikuwa nje nje hadi ikawa ni ngumu kujua nani anamfuata Lowassa kwa sababu ya pesa na nani anaamini kwa dhati katika ubora wa urais wa Lowassa kwa ajili ya maendeleo!
Baadhi ya waandishi wa habari walineemeka mno katika kipindi hiki na ulikuwa muda mzuri kwa wenyeviti wa mikoa wa CCM kuchuma hadi wakajitoa ‘akili’ na kuonyesha wazi mapenzi yao. Hata Mwenyekiti wa Geita, anakotoka Magufuli, alikuwa kambi ya Lowassa!
Katika kuonyesha nguvu ya pesa tulishuhudia masheikh na wachungaji wenye njaa na mabodaboda waliokata tamaa wakienda kumshawishi agombee – usanii mtupu! Maandalio ya nguo na vifaa vingine vya Timu Lowassa yalikuwa makubwa mno – hata kabla hajajua kama atapita katika mchujo!
CCM kumteua Lowassa ingeweza hata kukiletea chama hicho hatari kwa sababu wapo wanaodhani mgombea huyo alikiuka si tu kanuni za maadili za chama, bali pia sheria za uchaguzi. Ikumbukwe msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi alishaonya kuhusu kuzingatia sheria ya gharama za uchaguzi inayothibiti matumizi mabaya ya fedha katika mchakato huo.
Lowassa, akijua hatari anayokabiliana nayo kutoka kwa wahafidhina ndani ya chama waliohoji maadili yake, akaamua kuja na mkakati wa kuunda ‘kundi la msukumo kutoka nje ya chama’ ili wahafidhina wafanye uamuzi kwa shinikizo. Haukuwa pia mkakati mzuri sana na kinyume na matarajio uliimarisha azma ya wahafidhina ya ‘kumkata’.
Hata hivyo, makosa ya kimkakati aliyoyafanya Lowassa yanaeleweka. Alikuwa na kazi mbili ya kuzuia na kushambulia na akatumia mkakati wa kutumia maguvu mengi kuliko akili. Hatimaye ikamgharimu.
Lakini Lowassa angefanyaje? Jibu rahisi ni kuwa angekuwa mnyenyekevu kitabia, angetengeneza timu ya watu wasafi, angefanya mambo kwa kiasi na chinichini. Wazungu wanasema, ‘ chochote kikizidi sana kinadhuru’.
membe+px
Mhe. Bernard Membe
Kilichomponza Membe…
Binafsi sikutarajia kwamba Membe angepita katika mchujo, wakati Lowassa amekatwa. Nilitarajia kuwa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ingeona busara ya kukata jina lake (Membe) ili kuvunja makundi na kuleta umoja katika chama.
Nani asiyejua kuwa Membe ndiye aliyekuwa mpinzani wa moja kwa moja wa Lowassa? Hawa ni kama Simba na Yanga.
Kotowiva kwa kwa kambi ya Lowassa na Membe hakukuja hivi hivi. Timu ya Lowassa iliamini kuwa Membe ni mtu wa karibu wa Kikwete na ndiye chaguo la Ikulu. Kwa hiyo timu ya Lowassa iliamini juhudi za Ikulu kumkata mgombea wao zililenga kumsaidia Membe.
Kutokana na ukaribu unaozungumzwa wa Kikwete na Membe, ambao ni kama mashemeji ukizingatia Membe anatoka Lindi kama mama Salma, haikuwa ngumu kwangu kutabiri kuwa Membe angeanguka katika Halmashauri Kuu ya Taifa ambayo ilijaa wapenzi wa Lowassa.
Kadhalika, haikuwa ngumu kung’amua kuwa kijana mwingine wa Kikwete, mwandishi wake hotuba wa zamani, Januari Makamba angeungana na Membe kutupwa nje ya kinyang’anyiro. Ukaribu wao na Kikwete uliwaponza wawili hawa.
Katika ‘saga’ la Lowassa, sitaacha kuhoji kuhusu misimamo ya Kingunge Ngombale Mwiru, mwanasiasa mkongwe, ambaye kabla ya matukio haya nilimweka katika kiwango cha uadilifu, umahiri na heshima cha Nyerere, Kawawa na waasisi wengine.
Kwa nini alikubali kujipaka matope na kuondoa heshima yake kwa sababu ya Lowassa? Aliahidiwa nini hadi akajitokeza hadharani kama muasi na kujaribu kuaminisha watu kuwa CCM itashinda tu kama Lowassa atakuwa mgombea? Yule si Kingunge niliyemfikiria alivyo.
magufuli
Mhe. John Magufuli
Magufuli aokota dodo…
Mwisho wa siku mwanakemia John Magufuli, aliyeendesha kampeni ‘poa’ ya bila mbwembwe, akaokota embe dodo mchangani katika Mkutano Mkuu wa CCM baada ya kuwadondosha wanawake wawili Amina Salim Ally na Asha Rose Migiro ambao aliingia nao fainali katika kinyang’anyoro hicho.
Sina hakika kama anastahili zaidi kuliko wagombea wote lakini bila shaka alikuwa chaguo bora kuliko akina mama wawili alioingea nao fainali, ukizingatia changamoto zinazolikabili taifa na changamoto ya vyama vya upinzani.
Magufuli anatoka Kanda ya Ziwa. Yeye ni mtendaji mzuri anayetaka kuona matokeo, ana uzoefu usiopungua miaka 20 serikalini. Pamoja na kuwa ni mwanasayansi, Magufuli ni mwanasiasa mahiri jambo lililothibitika kwa jinsi alivyokuwa akichangamana na watu katika Mkutano Mkuu ukumbini hapo akiomba kura.
Magufuli ana udhaifu wake pia. Hajui Kiswahili na anachanganya ‘r’ na ‘l’ katika matamshi yake. Wakati fulani anaweza kuwa dikteta. Pia Magufuli ana maamuzi ya haraka. Naamini hana uzoefu mkubwa kimataifa na labda atawahitaji wazoefu kama Amina Salim Ally, Asha Migiro na Dk. Augustine Mahiga, kumsaidia katika eneo hilo.
Hata hivyo, ukweli ni kuwa changamoto nyingi zinazokabili Taifa kwa sasa ni za ndani zaidi kuliko nje. Tunatarajia Magufuli akipitishwa kuwa rais ataimarisha mshikamano wa Taifa, atapambana na rushwa na ufisadi, ataanzisha vita dhidi ya madawa ya kulevya, ataleta nidhamu katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali na matumizi.

Wachezaji wa Bayern Munich wamepata mapokezi ya ajabu baada ya kuwasili Mjini Beijing

bayern-fans-in-china-july-2015 (1)Wachezaji wa Bayern Munich wamepata mapokezi ya ajabu baada ya kuwasili Mjini Beijing, China wiki hii.
Bayern kwasasa wapo China kujiandaa na msimu mpya na kiukweli mabingwa hao wa Bundesliga wana mashabiki kibao barani Asia.
Tazama video jinsi Thomas Muller na Manuel Neuer walivyopokelewa…..

Meneja wa Manchester United, Louis van Gaal amethibitisha kwamba bado anahitaji kusajili wachezaji wawili majira haya ya kiangazi

2A90E9D400000578-3165253-image-a-26_1437135700028
Meneja wa Manchester United,  Louis van Gaal amethibitisha kwamba bado anahitaji kusajili wachezaji wawili majira haya ya kiangazi licha ya ukweli kuwa ameshanasa saini ya wachezaji wanne mpaka sasa.
Van Gaal ametumia paundi milioni 80 kumsajili winga wa  PSV Eindhoven, Memphis Depay, beki wa kulia wa Torino, Matteo Darmian na viungo Bastian Schweinsteiger kutoka Bayern  na Morgan Schneiderlin Southampton.
Mholanzi huyo ameiambia MUTV kuwa bado ana mapengo mawili katika kikosi chake.
“Hapana, hatujamaliza usajili”. Amesema Van Gaal na kuongeza: ” Tutanunua mchezaji ambaye anaweza kuleta mchango, nadhani bado tunahitaji kuongeza wachezaji wawili katika sehemu mbili na tutafanya hivyo pale inapowezekana”.
Van Gaal  pia anamuwinda mlinzi wa kati Sergio Ramos, lakini dau la paundi milioni 40 alilotuma Real Madrid limekataliwa mara kadhaa, wakati huo inaelezwa kwamba Man United wanataka kumuuza Jonny Evans.
Van Gaal amesema kwamba Javier Hernandez “Chicharito” atakuwa sehemu ya kikosi chake.

busu ni ishara ya kuonyesha mahaba?


Utafiti mpya umegundua kwamba busu la mdomo kwa mdomo sio ishara kamili ya kuonyesha mapenzi, kinyume na dhana ya watu wengi
Aidha wanyama wa porini pia wameonekana kutojali mtindo huo.
Swali ni je busu kama ishara ya mahaba limeenea vipi kutoka kizazi kimoja hadi chengine?null
Ukitizama tendo hilo la busu la mdomo kwa mdomo kwa kina, si la kufurahisha sana, kuna kubadilishana mate, ambayo kwa wastani, yana bakteria zaidi ya milioni 80, na si wote wazuri
Lakini kwa hakika kila mtu anayeshiriki tendo hilo hukumbuka busu lake la kwanza kwa undani hata kama lilipendeza ama lilikuwa la kuaibisha, na kwa hivyo ni tendo ambalo linaendelea kuwa msingi wa kuashiria mahaba.
Katika jamii ambazo bado zimejikita katika mila na desturi, hakuna ushahidi wa chanzo cha busu kama ishara ya mahaba.
Kwa mfano katika jamii ya Mehinaku nchini brazil, wnachukulia kubusu kama kitendo cha uasinull
Kulingana na mwandishi William Jankowiak kutoka chuo kikuu cha Nevada, Las Vegas Marekani, utafiti unatofautiana na imani kwamba kubusu kunaonyesha mahaba kama dhana ya watu wengi duniani, na anasema ni ubunifu wa jamii ya wazungu unaopitishwa kutoka kwa kizazi kimoja hadi chengine.
Ushahidi wa kwamza kabisa wa mila ya kubusu ulinukuliwa kwa mara ya kwanza katika maandiko ya kihindi Vedic Sanskrit miaka 3,500 iliyopita na ilikuwa ishara ya kurithi nafsi ya mtu mwinginenull
Ushahidi wa zamani wa kubusu unatokana Hindu Vedic Sanskrit maandiko ya zaidi ya miaka 3,500 iliyopita.
Wanyama wa pori pia hutumia busu kwa ishara zingine. Sokwe hushiriki tendo hili kama ishara ya kupatikana kwa amani baada ya mvurugano

Je,mbu hutambua vipi mwili wa mwanadamu usiku?


Utafiti mpya umebaini kwamba mbu hutafuta kitu cha kula kwa kutumia vigezo vitatu,harufu,macho na joto.
Utafiti huo unasema kuwa mbu anaweza kufahamu aliko mwanadamu kupitia hewa ya kaboni ambayo watu hupumua nje.
Inasemekana mbu hunusa hewa hii kiasi cha mita 50.
Wanasayansi wamesema kwamba walimfuatilia mbu mwenye njaa, ndani ya mtaro uliofunikiwa.
Kisha waligundua kwamba mbu hao walianza kunusa nusa hewa ya kaboni, na kutema mapovu yenye matone meusi yaliowekwa na watafiti hao sakafuni.null
Imebainika kwamba wakati mbu yuko mita chache karibu na kile anacholenga, huvutiwa sana na joto.
Hii imebainisha kwamba hata hufuata joto hilo na kisha kumshambulia mwanadamu.
Huenda ukapata Malaria au ukaponea lakini utakua na vipele pale vya mbu anapokuuma.

Samsung yazindua simu nyembamba zaidi

Kampuni ya Samsung imezindua simu yake nyembamba zaidi aina ya smartphone kufikia sasa.
Simu hiyo kwa jina Galaxy A8 ina upana wa milimita 5.9 ikiwa ni wembamba wa asilimia 85 ikilinganishwa na simu ya Galaxy S6 Edge.
Licha ya wembamba huo waandisi wameweza kuiweka betri pamoja na kamera yenye uwezo wa mega pikseli 16.null
Mmoja ya wataalam aliuliza swali la muhimu wa kutengeza simu nyembamba.
Kwa sasa Samsung imetangaza kwamba simu hiyo itauzwa nchini Uchina na Singapore.
''Galaxy A8 haitauzwa nchini Uingereza'' alisema msemaji wake.
Ijapokuwa itakuwa simu nyembamba zaidi kutoka kwa mojwapo ya kampuni kubwa ,kampuni nyengine za Uchina tayari zimeanza kuuza simu kama hizo.

16 July, 2015

Victor Valdes na Kocha Louis Van Gaal hakuna amani


Ndani ya masaa 72 tu mahusiano mazuri kati ya golikipa wa Manchester United Victor Valdes na kocha wa timu hiyo Louis Van Gaal yamevunjika, tofauti kati yao ilianza wakati Valdes alipogoma kucheza kikosi cha wachezaji wa akiba.
Maswali yalianza kutawala baada ya Valdes kuenguliwa na David de Gea kujumuishwa kikosini licha ya kuhusishwa pia na story kwamba ana mpango wa kuihama klabu hiyo, katika kikosi kilichosafiri na timu kwenda Marekani kwa maandalizi ya msimu mpya.
Valdes ameachwa na timu na wengi walianza kudhani labda kaachwa sababu ya majeruhi kabla ya Van Gaal kufichua ukweli katika kikao na waandish wa habari jumatano hii Marekani.
Lakini sasa majibu kamili ya nini kimetokea kati ya wawili hao kimejulikana, Van Gaal amemuacha Valdes kwa sababu hataki kufuata falsafa zake hivyo ni mtovu wa nidhamu na hana nafasi katika kikosi chake.
“hafuati falsafa zangu, hivyo hakuna nafasi ya mtu kama huyo”>>> Van Gaal
Van Gaal anamtuhumu Valdes kwa utovu wa nidhamu baada ya kukataa kucheza mechi na kikosi cha wachezaji wa akiba akiba msimu uliopita. Kufuatia mvutano huo Valdes kuna uwezekano mkubwa wa kutoendelea kuvaa jezi ya Manchester United msimu ujao.
Valdes alijiunga na Man United january 2015 kama mchezaji huru akiwa amemaliza mkataba wake na klabu  ya FC Barcelona.

DMX afungwa jela miezi 6

DMX ameswekwa ndani leo hii na kama atabahatika  anaweza kutoka kw aajili ya hizi sikukuu zinazokuja.
Rapper huyo amewekwa ndani huko Buffalo, New York siku ya juma nne, kwa kushindwa kukubaliana na hukumu ya mahakama ya familia.

DMX amekuwa na historia ya matatizo kwenye kuhudumia mtoto na mmoja wa baby mama wake ambae anaishi maeneo y akaribu nae, mwisho wa siku ndo haya yamemkuta.

DMX amepelekwa ndani kwa hukumu ya miezi sita na hapo hapo akaingizwa ndani, County Holding Center.
It's kind of a numbers game -- DMX has been repeatedly, Dmx amekuwa akikamatwa kwa makosa mbali mbali hivi karibuni lakini hajatumikia kifungo kirefu tangu alipotumikia mwa 2011 alipofungwa kwa miezi 7

Video: Jidenna feat. Kendrick Lamar – 'Classic Man (Remix)'

Suited and booted. Jidenna hits the West Coast and connects with Kendrick Lamar in the video for his remix to “Classic Man.” While looking dapper in his tailored suits, the young OG cruises the streets of L.A. in his classic Mercedes convertible. He hits up the convenience store and scoops up two ladies before joining K-Dot at an underground party. The Compton MC gets his dance on, while Janelle Monáe, Ty Dolla $ign, and Hit-Boy make cameos.

The remix and the original song can be found on Wondaland Presents: The Eephus, which drops Aug. 14. The six-track EP also features Janelle Monáe and Jidenna’s hit “Yoga.”

IJUE VIZURI SIMU YA HUAWEI P8 KABLA HAUJAINUNUA

PPP
Jana kwenye hoteli ya Hyatt Regency kampuni ya Huawei inayouza na kuzalisha “simu zenye akili”a.k.a SmartPhone ilizindua toleo jipya la simu zake kwenye P Series. Baada ya watu mbalimbali kufurahia P7, hivi sasa ni wakati wa kutumia P8. Hizi hapa ni sababu za kutosha kabisa zitakazo kufanya uimiliki  simu hii ya Huawei P8.
Battery:
Ukizungumzia matatizo ya Smartphone hili ni moja wapo, huwezi kuniambia niache kusikiliza music na kuchat kwa pamoja kisa battery. Kila mtu anaitaji kufanya vitu mbalimbali kwa wakati mmoja kwenye smartphone yake. Director of Sales and Marketing Samson Majwala amesema kwamba battery ya Huawei P8 inauwezo wa kukuwezesha kufanya yote na kukaa kwa siku nzima na chaji. Battery lake halitoki kwenye simu na lina uwezi mkubwa wa Li-Po 2680 mAh
p5
Camera:
Smartphone bila camera kali bado haijawa smart, Huawei P8 inakuja na camera yenye mega pixel 13 (4160 x 3120 pixels) zaidi ya hapo camera hiyo ina uwezo wa Autofocus, optical image stabilization, dual-LED (dual tone) flash. Haijaishia hapo, bali ukiwa unapiga picha uweza kufanya Geo-tagging, touch focus, face/smile detection, panorama na HDR.
Vipi camera ya selfie, hapo unakutana na camera yenye uwezo wa 8 mega pixel na 1080p. So Huawei P8 inakupa uwezo wa kurekodi video ya High Definition ya 1080p@30fps.
p17
Umbo:
Samson Majwala anaendelea kusema kwamba mara nyingi tuvaa nguo ambayo imetu-fit vizuri na hatutaki mizigo mingi kwenye mifuko yetu. Ukiizungumzia Huawei P8 ni nyembamba na bado ni ngumu hata ukiiweka mfukoni sio rahisi kukusumbua. Ina vipimo vya 144.9 x 72.1 x 6.4 mm. Uzito wake ni 144 g (5.08 oz) na nyembamba kwa 6.4mm
Sim Card
Huawei inakupa machaguo mawili kwenye swala la simcard. Zipo Huawei P8 zenye line moja na nyingine zina line mbili.
Operating System
Kama kawaida Huawei huwa inatumia O.S ya Android, lakini Huawei P8 sio tu kutumia Android bali inatumia Android mpya kabisa ambayo ni version 5.0.2 (Lollipop).
p2
Speed
Hakuna anetaka kufungua camera na kuisubili sana kufunguka au kufanya kitu chochote kwenye simu yako na ikawa slow. Huawei P8 imezingatia hilo kwa kuipa uwezo wa Quad-core 2 GHz Cortex-A53 & quad-core 1.5 GHz Cortex-A53. Pia Ram ya Huawei P8 ni 3GB ambayo ni RAM inayozidi hata baadhi ya laptop.
Memory
Mfano kama picha inapigwa na camera ya 13 mega pixel basi lazima inahitajika memory ya kutosha kuhifadhia picha,video na mafaili mengine. Huawei P8 inaweza kuwa na memory ya 16GB au 64GB na pia kwa speed yake unaweza kuongeza memory card hadi yenye 128GB na simu ikabaki kwenye ubora wake.
20150715152416
Mr Samson Majwala (Huawei Director of Sales & Marketing) na Peter Zhang Huawei Country Manager
Network
Huawei P8 imepewa uwezo mkubwa wa kudaka network ya mtandao wako wa simu. Mr Majwala anasema kuna wakati simu inavyobadilisha mnara, inawezekana kuwepo na delay kidogo. Lakini simu hii inauwezo wa kudaka haraka network na sio rahisi kupiga simu na isiunganishwe na mtandao. Pia inawezo wa haraka wa kudaka WiFi. Smartphone hii a.k.a simu yenye akili inauwezo wa kuchagua WiFi ambayo ina nguvu sana kwa wakati huo.
Ziada
Vitu vya ziada ni kwamba ukiwa unataka ku-screenshot kwenye Huawei P8 basi kazi ni rahisi sana. Una doubletap screen na utakua umesha screenshot.
p1
Director’s mode : Kwenye Huawei P8 unaweza kurekodi video kwenye angle 3 na ukawa una mix hizo video wakati unarekodi kama dirrector na mwisho siku ukapata video iliyokua mixed vizuri kama na director.
Huawei P8 ni ngumu imetengenzwa kwa design nzuri ya kuvuti ikiwa na cover la chuma ngumu kulinda simu yako vizuri.
Unaipataje?
Huawei P8 lazima itakua kwenye maduka muhimu ya kuuzia simu. Ukitaka yenye line mbili ni Tsh 1,200,000 na ukitaka yenye line moja ni Tsh 1,100,000

BASTIAN SCHWEINSTEIGER AMEKULA DILI LA BEATS by DRE BAADA YA KUHAMIA MANCHESTER UNITED

cccc
Hapa shabiki wa Manchester united anaweza kuimba line ya John Makini “Brand kubwa sio kitoto”. Baada ya Bastian Schweinsteiger kuhama kutoka Bayern Munich amehamia Manchester united wahusika wa masoko wa brand ya Beats by Dre wametumia fursa ya uhamisho wake kwenye biashara yao.
Hivi sasa limetoka tangazo ambalo linamuonyesha Bastian Schweinsteigerakihama kutoka Berlin kueleka Manchester ambapo Bastian Schweinsteiger anaonekana anafungasha mizigo yake. Kwenye hiyo process Bastian Schweinsteiger anavaa headphones za Beats by Dre. So hawa jamaa wameona kwamba Manchester ni brand kubwa ina mashabiki wengi, kumhusisha mchezaji mwenye jina kubwa Bastian Schweinsteiger akihamia Manchester united ni rahisi kwa brand yao kupata wateja wapya ambao ni mshabiki wa Man United.
Sio uongo wala sio hasara, pesa walizomplipa Bastian Schweinsteiger zinaweza kurudi kwasababu tangazo lake limeshaangaliwa mara milioni 3 mbalimbali duniani. Mitandao karibia yote duniani ya michezo pamoja na shaffhdauda.co.tz wameandika habari hii. Bila shaka Beats by Dre wanapata matangazo ya bure kupitia Bastian Schweinsteiger.
Pia kuna mashabiki wa Manchester united hivi sasa wanafikiria kwenda kununua headphone hizi sio kwamba wamesikia ni nzuri bali ni kwasababu Bastian Schweinsteiger amehusika ku-promote. Mpira wa bongo lini huku. Mchezajji mkubwa akihamia most valuable club biashara sio kuuza jezi tu, mambo ndio kama haya.

15 July, 2015

Video:Nay Wa Mitego ‘Sina Muda’

nay videoWakati mashabiki wa Nay wa Mitego wakisubiri kwa hamu video ya ‘Mapenzi au Pesa’, mwenyewe tayari ameachia video ya ngoma yake nyingine mpya ya ‘Sina Muda’. 
   Itazame hapa 

14 July, 2015

KUMBE MCHEZAJI HUYU WA EPL NI DJ BAABKUBWA…

deki
Zaidi ya kuwa na kipaji kimoja mtu anaweza kuwa na kipaji kingine au passion na kitu kingine tofauti na kile kinachompatia pesa kila siku.
Swala hili limedhihilika kwa mchezaji wa Manchester city Gael Clichy. Huyu jamaa hata akisafiri lazima abebe Dj Set up ili akifika huko anapoenda kama sehemu moja wapo ya starehe yake anaanza kufanya mixing ya ngoma mbalimbali.
Akiojiwa na Manchester TV wakati wapo kwenye moja ya majiji waliyotembelea kwenye pre-season tour, Gael Clichy alisema huwa habebi vitu vingi akiwa kwenye safari lakini hawezi kuacha DJ set up zake.

2A85681B00000578-3160676-image-a-41_1436877546165
2A85680500000578-3160676-image-a-31_1436877462262 (1)2A85681300000578-3160676-image-a-32_1436877469965

Shirikisho la soka la Urusi limethibitisha kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba na kocha mkuu wa timu ya Taifa ya nchi hiyo

18E4B25E000005DC-0-image-a-2_1435161204487
Shirikisho la soka la Urusi limethibitisha kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba na  kocha mkuu wa timu ya Taifa ya nchi hiyo, Fabio Capello   baada ya kushindwa kutimiza malengo waliyojiwekea.
Katika taarifa yake, RFU wamemshukuru  Capello kwa kazi yake aliyofanya na wamemtakia kila la kheri katika maisha yake yajayo, huku naye akilishukuru Shirikisho hilo, mashabiki pamoja na wachezaji kwa kutoa ushirikiano mkubwa katika kipindi chote alichofundisha timu hiyo.
Mkataba wa Capello unatakiwa kumalizika mwaka 2018 ambapo Urusi itahodhi kombe la Dunia, lakini maamuzi yaliyochukuliwa yanalifanya Shirikisho hilo limlipe fidia ya paundi milioni 11.
Ripoti kutoka Urusi zinasema kwamba,  kocha wa CSKA Moscow, Leonid Slutsky anapewa nafasi kubwa ya kurithi mikoba ya Capello mwenye umri wa miaka 67 ambaye amekinoa  kikosi cha Urusi kwai kwa miaka mitatu.
Capello alianza kuifundisha Urusi mwaka 2012, muda mfupi baada ya kujiuzulu kuifundisha  timu ya Taifa ya England, lakini alishindwa kuwaongoza vizuri Warusi katika fainali za kombe la Dunia mwaka jana nchini Brazil na mwaka huu nchi hiyo imefanya vibaya katika mechi za kufuzu kombe la Mataifa ya Ulaya 2016.
Urusi inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa kundi G ambapo imeshinda mechi mbili tu kati ya sita ilizocheza.

Saa 72 za Lulu Ndani Ya Gold Digger Ni Hatari

Saa 72 za Lulu Ndani Ya Gold Digger Ni Hatari


UNAPOONGELEA Muigizaji wa kike mwenye mvuto na anayejua kuigiza basi msanii huyo si mwingine unamuongelea binti mwenye nyota kali Elizabeth Michael almaarufu kama Lulu, baada ya kimya cha muda mrefu kuwepo likizo Lulu kwa karudi kwa nguvu kubwa katika sinema.

Nakutonya ni zaidi ya saa 72 Lulu anasimama kuigiza huku wasanii anaoshiriki nao wakibadilishana naye akibadilisha nguo tu na kurudi katika scene nyingine baada ya kumaliza scene moja baada ya moja, bila kupumzika hata akiambiwa sasa unaweza kupumzika anasema kuwa tumalizie hiyo ya moja.

Muongozaji wa sinema hiyo Karabani anasema kuwa Lulu ni msanii wa kipekee kwani kwanza hakosei kuongea wala kuigiza nje ya script ni msanii wa kipekee Karabani anasema kuwa katika aliofanya nao kazi toka Ulaya huyu ni wa aina yake.
Baba James mmoja ya wasanii anashiriki naye katika sinema ya Gold Digger anasema Lulu yupo katika viwango vya kimataifa anajua kuigiza na anabadilika kulingana na tukio tofauti na wale wasanii wanaobebwa na wasanii wengine au script.
“Lulu ni msanii hatari sana unapocheza naye jipange na kama haujui ni utajua kwanza hana makuzi kazini yeye ni mtu wa utani lakini baada ya kazi na hawezi kuacha scene eti njaa hiyo kwake hakuna,”anasema Baba James.
Msanii huyo anasema kuwa katika filamu ya Gold Digger kulikuwa na ushindani mkubwa sana wasanii kuonyeshana uwezo, wasanii kama Dude, Isarito, Baba James, Kojack na wasanii wengine zaidi ya 200 kuifanya sinema hiyo kuwa ya kimataifa.

Video: Digna Ft. Maromboso - 'Kidodosa'

Digna from JJ Band feat Maromboso from Yamoto Band is two biggest musicians from East Africa Tanzania. Audio Produced by Shirko. Video directed by Hanscana and Khalfani, dressed by World wear Fashion, Powered by Jembe Ni Jembe.

Waziri John Pombe Magufuli-MGENI RASMI michuano ya Kombe la Kagame

images 
Waziri wa Miundombinu nchini Tanzania, John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa michuano ya Kombe la Kagame siku ya Jumamosi, Julai 18 2015 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Magufuli baada ya kufungua rasmi michuano hiyo, atashuhudia mchezo wa ufunguzi rasmi wa mashindano ya Kagame, mechi itakayowakutanisha miamba ya Afrika Mashariki timu ya Yanga dhidi ya Gor Mahia kutoka nchini Kenya.
Michuano ya Kagame inatarajiwa kuanza kutimua vumbi siku ya jumamosi kwa michezo mitatu, ukindoa mecho ya Yanga Vs Gor Mahia, mechi zingine zitakua ni kati ya APR dhidi ya Al Shandy uwanja wa Taifa saa 8 mchana, KMKM Vs Telecom saa 10 jioni uwanja wa Karume.
Kuanzia leo tutakua tunawaleta kwa ufupi timu zinazoshiriki michuano hiyo mwaka huu, na kwa kuanza tunaanza na kundi A;
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Pesa Aliyolipwa Diamond Platnumz Baada ya Video yake Kuchezwa kwenye TV ya Marekani.

D


Ni utamaduni wa kawaida kwenye nchi zilizoendelea au nchi kubwa duniani Wasanii kulipwa pesa kutokana na nyimbo zao kuchezwa kwenye TV na Radio ambapo hii imemtokea Mtanzania Diamond Platnumz baada ya wimbo wake kuchezwa kwenye TV maarufu kwa burudani, BET ya Marekani.
Tazama hii video hapa chini ujue hizo milioni alizozichukua Diamond.

Lil Wayne karushiwa chupa na Birdman night club akashtukia.. tukio lilirekodiwa kwenye hii video.

lil wayneKwa muda mrefu sasa hivi kumekuwepo na beef kati ya rapper Lil Wayne na Birdman wa Cash money na hii ni baada ya Wayne kujitoa Cash Money kwa kutoridhishwa na ishu kadhaa ikiwemo kutosikilizwa anachotaka hasa kwenye ishu ya album yake kucheleweshwa kutoka.
lil wayne 2
Picha za tukio lenyewe, Lil Wayne akishangaa kurushiwa chupa alafu kwenye hii ya kulia ndio birdman anaonekana na timu yake.
Baada ya kujitoa Cash Money, Wayne ameendelea na show zake kama kawaida ambapo weekend iliyopita alikuwepo Miami Marekani kwenye club moja ya usiku ambapo kumbe na ‘mbaya wake’ Birdman nae alikuwepo tena akimtazama Lil Wayne kwa chini wakati akiperform.
Inadaiwa Birdman alirusha kwa Lil Wayne chupa ya kinywaji alichokua anakunywa na kusababisha show kusimama kwa sekunde chache huku watu wakijiuliza chupa imetoka wapi lakini badae ndio ikaja kujulikana kwamba Birdman ndio aliirusha.
Hivi vipisi vya video vinaonyesha hiyo moment kwenye hili tukio.

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...