Wanasayansi wametumia picha za za setilaiti kuchunguza namna maji ya dunia yalivyohama kwa zaidi ya miaka 30.
Walibaini
kwamba kilo mita za mraba 115,000 za ardhini kwa sasa zimefunikwa
na maji na kilomita 173,000 za maji zimefunikwa sasa na ardhi.
Ongezeko
kubwa la maji limetokea katika eneo tambarare la betan , huku bahari
ya Aral eneo kubwa la maji sasa limegeuka kuwa ardhi.
wanasayansi hao wanasema kuwa maeneo ya mwambao pia yamekuwa na mabadiliko makubwa .
Utafiti
uliofanywa na taasisi ya utafiti ya Deltares ya nchini Uholanzi
umechapishwa na jarida la mabadiliko ya asili ya hali ya hewa.
Watafiti walitathmini picha za setilaiti azilizochukuliwa na kituo
cha wataalam wa masuala ya anga cha Nasa ,ambacho kimekuwa
kikichunguza dunia kwa miongo kadhaa .
Waliweza kufuatilia mabadiliko ya sehemu ya juu ya dunia inayoweza kuonekana kwenye kipimo maalum .
Waliweza
kubaini eneo pana ambalo wakati mmoja liliwahi kuwa ardhi ambalo sasa
limekuwa na maji , eneo kubwa zaidi likiwa ni lile la maeneo tambarare
yenye vilima ya Tibetambako barafu zilizoyeyuka zinasababisha maziwa
makubwa .
Kuongezeka kwa idadi ya mabwawa pia kunaongeza kiwango cha maji, na
kwa kutumia data za setilaiti , Timu hiyo ya wanasayansi iliweza
kugundua shughuli za ujenzi ambazo hazikuripotiwa awali.
Dr Fedor Baart kutoka taasisi ya Deltares anasema : "Tulianza kuangalia kwenye maeneo ambayo hayakuwekwa kwenye ramani awali.
"Tulifahamu nchini Myanmar kwamba mabwawa kadhaa yalikuwa yanajengwa,
lakini tuliweza kuona mengi . Na pia tuliweza kuona Korea kaskazini na
tukaona mabwawa yanayojengwa huko karibu tu na mpaka wa Korea Kusini."
Vile vile watafiti waliweza kubaini kwamba hata maeneo makubwa ya maji yamebadilika kuwa ardhi sasa
Mabadiliko haya makubwa yalionekana katika bahari ya Aral Sea katika Asia ya kati.
Yale
yaliyowahi wakati mmoja kuwa maziwa makubwa duniani kwa sasa karibu
yanakauka kabisa baada ya wahandisi kuelekeza maji katika shughuli za
kilimo cha umwagiliaji.
CHANZO: BBC