21 May, 2016
Ladha ya Muziki wa Dance Tanzania Inazidi kupotea.
Hakuna asiyefahamu ubora wa Bendi za Vijana Jazz wakati huo ikiwa na Hemed Maneti , Super Matimila chini ya gwiji la muziki Dk Remmy Ongara, DDC Mlimani Park ya Cosmas Chidumule, Juwata Jazz ya TX Moshi William, Tancut Almasi ya Kasaloo Kyanga na Kyanga Songa, Bima Lee ya kina Jerry Nashon ‘Dudumizi’ n.k, bendi ambazo kila moja ilipiga muziki wa dansi wa Tanzania kwa mtindo wa wake lakini bado ukawa juu kuliko ule wa kutoka nje.
Lengo letu hapa si kuzitaja bendi hizo lakini kiukweli nyingi kati ya hizo zilikuwa hazifanyi hata matangazo ya barabarani, lakini wapenzi wake walikuwa wanajua mahali ambapo zilikuwa zinafanya maonyesho na kwenda kufurahia burudani ya muziki halisi wa dansi ambao leo haupo tena.
New Video Mayunga ft Akon ‘Please don’t go away’
Mtanzania mwenzetu Mayunga aliye Tuwakilisha vyema katika shindano la Trace Music star na kuibuka mshindi katika shindano hilo, Leo may 21 katuletea Video ya nyimbo yake aliyo achilia siku mbili tatu zilizo pita inayo kwenda kwa jina la ‘Please Don’t go away’. Ambapo kamshirikisha mkali Kutoka Huko Senegal (Akon).
20 May, 2016
New Movie: Money Monster
In the real-time, high stakes thriller Money Monster, George Clooney and Julia Roberts star as financial TV host Lee Gates and his producer Patty, who are put in an explosive situation when an irate investor who has lost everything (Jack O’Connell) forcefully takes over their studio. During a tense standoff broadcast to millions on live TV, Lee and Patty must work furiously against the clock to unravel the mystery behind a conspiracy at the heart of today's fast-paced, high-tech global markets.
Watch The Trailer.
Video: Alikiba – Aje
Huu umeonekana ni mwaka wa mafanikio kwa msanii Alikiba, na hii imekuja baada ya Yeye jana kuingia mkataba na kampuni kubwa ya Sony ambapo sasa atakua chini ya kampuni hiyo akiwa pamoja na Chriss Brown na wakali wengine wa kimataifa ambao wako chini la Sony.
18 May, 2016
New AUDIO: Papaa Masai Ft. Yamoto Band - Mtoto Wa Kariakoo | Download
Papaa Masai ni miongoni mwa wale wasanii waliokuja kwa kasi katika muziki huu wa kizazi kipya ambapo ngoma iliyo mleta katika masikio ya wengi ilikua ni Ng'ari Ng'ari na Baadae akaja na Ngoma ya Mapenzi Upele ila Baada ya Hapo alikaa kimya kwa muda mrefu . Leo katuletea ngoma mpya Inayokwenda kwa Jina la Mtoto Wa Kariakoo akiwa amewashirikisa Yamoto Band.
Bofya HAPA kuupata wimbo Huo.
Japo utaumia lakini Utajifunza.
Wakati mwingine inatokea hali ya sisi kujichukulia kwamba na watu walio shindwa na kukata tamaa, ila hakuna ukweli juu ya jambo hili. Ni lazima tupitia mchakato mzima wa maisha ili tuweze kuishi maisha yanayo stahili. Na mchakato huu huja pale tunapo jaribu kufanya vitu mbali mbali kwa wakati tofauti tofauti, na Huo ndio ukweli wa maisha. Ni lazima tupige mawazo hasi katika maisha .
Labda hii inatokana na sisi kutotambua ni maana ya Neno "Kushindwa" kwa sababu ndani yake hakueleweki. Lakini wacha nikuambie kitu kimoja, Kila jambo nililo fanikiwa nilifanikiwa kupitia Kushindwa lakini sikukata tamaa.
Failure isn’t fatal, but failure to change might be” – John Wooden
Ninacho zungumzia mimi ni kwamba, yatupasa kuchukulia neno "Kusindwa" kama darasa la kujifunzia. Lichukulie neno 'Kushindwa' na kulileuza kuwa 'Kujifunza'. Najua ni Ngumu kufanya hivyo ila ndio njia nzuri ya kufanikiwa, inaumiza ila mafanikio yako ndiko yaliko.
“Success is most often achieved by those who don’t know that failure is inevitable.” – Coco Chanel
Subiri kidogo nikupe kitu hapa..
Nilimuuliza Girlfriend wangu ni nini maana ya Kushindwa, na akanijibu kwa kifupi "Ni kufika mwisho" ndio ni kufika mwisho ndipo nilipo chukua Computer yangu na kutafuta maana halisi ya kushindwa. Nikapata kama ifutavyo. Niliandika What really is “failing”?
Unaona hii? A wekness in a character! Kushindwa(maungufu/weakness) kunaweza kuimarishwa kwa kufanya zaidi(Practice enough). Kushindwa siyo njia ya kufikia tamati ya maisha, Kushindwa ni jambo zuri mno katika maisha maana utapata akili mpya ya na kuzidi kupambana.
“Only those who dare to fail greatly can ever achieve greatly.” – Robert F. Kennedy
Hapa nimekuwekea mambo machache ambayo mara nyingi huwa tuna "shindwa" lakini tukiweka nguvu na akili zetu huwa tuna fanikiwa kweli kweli:-
1.Utashindwa katika urafiki.
Marafiki milele? laa hasha. Itafika kipindi rafiki ulio nao utawaona wamebadilika yaani wamekua tofauti na ulivyo tegemea. Inauma kwa kweli lakini ni jambo ambalo tunapaswa kulipitia kama wanadamu, wapo marafiki zako watakudanganya, wengine watakukimbia katika matatizo uliyo nayo na wengine watakuambia majukumu yamezidi hivyo hawana muda na wewe na maambo mengi ilimradi wakutenge ( Doh!) lakini unapaswa kujifunza jambo katika hili. Chagua marafiki sahihi na wa kweli, ambao hata ukianguka popote mbali na wao watakutafuta na kukuokota. Achana na marafiki wote unao ona ni wanafiki(Najua ina umiza ila yakupasa kufanya hivyo). Usiogope maana baada ya hili utakua muwazi na huru daima na mwisho wa siku utashinda.
“The phoenix must burn to emerge.” – Janet Fitch
2.Utashindwa Kufanya maamuzi Makubwa.
Nikiwa mwenye umri wa mika 20 na kitu hivi mpaka sasa nashindwa kueleza ni maamuzi magumu mangapi nimekwisha kushindwa kuyachukua. Hapana itakuwa ni Hatari kwa mimi kuyataja hapa yote. Nitaangalia machache kwa ajili yako. Lakini point ni kwamba hasa pale unapokuwa una ukosa mwongozo wa mtu fulani muhimu katika maisha yako, unakuwa unafanya maamuzi ya ajabua mabayo mwishoni unakuja kuyajutia. Pointi moja ya kweli ni kwamba utakua umeshindwa kuiruhusu hali hii ikutokee katika maisha yako na kama hali ni hiyo, basi iwe ni njia yenye maumivu makubwa katika kuelekea kwenye mafanikio yako.
Tafuta mtu wa kukusaidia, soma mambo mengi yahusuyo maisha(Tumia internet yako vizuri). Hali hii hutokea wengi mno hasa vija ambao wengi wetu ndio tunaanza maisha. Jaribu kuchanganua jambo hili kwa kina.
“I’ve failed over and over and over again in my life and that is why I succeed.” – Michael Jordan
3.Utashindwa kuwekeza kwa ajili ya badae.
"Unaishi mara moja tuu" is the mantra of most 20-somethings, hii inaonekana ni nzuri si ndiyo? Muda baada ya muda utafahamu ni nini ambacho uatkifanya kwa undani peke yako. Kumbuka, kama unataka kuwa na familia na kuitunza, basi mahusiano na wapenzi wengi siyo suluhisho. Na ndivyo ianatakiwa kuwa katika malengo yako ya muda mrefu. Utajifunza kuwa mtu wa maono ya mbali.
“Failure should be our teacher, not our undertaker. Failure is delay, not defeat. It is a temporary detour, not a dead end. Failure is something we can avoid only by saying nothing, doing nothing, and being nothing.” – Denis Waitley
4.Utashindwa kuendeleza Muonekano wako(Personal style).
Jamii, familia na marafiki vimetusafisha akili zetu kwa ujumla wake. Pale ambapo tuana mambo na kujaribu kuyabadili, basi tunakua tukijaribu kubadili muonekano wetu.Easier said than done but why not learn about self development? (Jifunze katika hili).
“When you take risks you learn that there will be times when you succeed and there will be times when you fail, and both are equally important.” – Ellen DeGeneres
5.Utashindwa Kupangilia na kumiliki pesa zako.
Wengi walio katika umri wa miaka ya 20 hadi ishirini na ushehe, hawanaga plan yeyote ya kuaminika, na wengi unakuta wako vyuoni wakifanya masomo yao(Wrong Degrees) na wengine wakiwa wamekaa tuu wakingojea Elimu kubadili maisha yao. Ni lazima tutafute njia mbadala kuondokana na hii hali. Na ndivyo ilivyo kwa Pesa. Huwezi ukaijua pesa ilivyo mpaka ufahamu Lugha ya pesa. Chakufanya hapo ni kununua vile vitu vya muhimu, kuwekeza katika jambo moja tuu ambalo baade litakuja kukupa uhuru wa maendeleo. Usihangaike kununua vitu ambavyo utanunua leo na kutumika leo na kesho itakavyo fika utajikuta huna.
“I have not failed. I’ve just found 10,000 ways that won’t work.” – Thomas A. Edison
Yapo mengi utakayo shindwa kufanya katika maisha ila kama utapambana kwa nguvu zako zote na akili zako zote, hakika utaweza kuyashinda, Japo utakua umeumia ila utakua umeupata Ushi.
Subscribe to:
Posts (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...