Official AUDIO | Engine - I miss u[Make Me Sing RMX] | Download
27 February, 2016
GIANNI INFANTINO RAIS MPYA WA FIFA
Raia wa Switzerland Gianni Infantino amechukua mahala pake Sepp Blatter kama rais wa shirikisho la soka duniani Fifa.
Katibu huyo mkuu wa Fifa alipata
kura 115 katika raundi ya pili ikiwa ni kura 27 zaidi ya mpinzani wake
wa karibu Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa.
Mwanamfalme Ali bin al-Hussein alikuwa wa tatu akiwa na kura nne huku Jerome Champagne akishindwa kupata hata kura moja.Tokyo Sexwale alijiondoa kabla ya kura kuanza kupigwa mjini Zurich.
Raundi ya kwanza ya upigaji kura ilishindwa kum’baini mshindi wa moja kwa moja.
Wingi wowote wa kura[zaidi ya aslimia 50] katika raundi ya pili ya uchaguzi huo ulikuwa unaweza kumwezesha mgombea kutangazwa mshindi katika raundi ya pili.
Infantino ni wakili mwenye umri wa miaka 45 kutoka eneo la Brig jimbo la Valais nchini Switzerland ,ikiwa ni eneo lililopo chini ya maili sita kutoka nyumbani kwa Blatter.
Blatter ambaye aliliongoza shirikisho hilo tangu mwaka 1998 alijiondoa mwaka uliopita kabla ya kupigwa marufuku katika shughuli zozote za kandanda kwa kipindi cha miaka sita.
Baada ya kutangazwa mshindi, Infantino aliwaambia wajumbe waliopiga kura kwamba hakuweza kujielezea kutokana na hisia alizokuwa nazo.
Lakini aliwaambia wajumbe kwamba ”kwa pamoja wataweza kuirudisha sura ya Fifa na heshima ya Fifa”.
Chanzo: BBC Swahili
26 February, 2016
Rais wa Misri 'auzwa' mtandaoni
Raia wa Misri wamekuwa wakimkejeli
rais wao Abdul Fattah al-Sisi mtandaoni baada yake kusema kwamba anaweza
kujiuza ili kusaidia uchumi wa taifa hilo.
"Ingeliwezekana mimi niuzwe, ningejiuza,” alisema Bw Sisi alipokuwa akihutubu kupitia runinga ya taifa.Muda mfupi baadaye, ukurasa uliundwa kwenye mtandao wa kuuza bidhaa mtandaoni wa Ebay wa “kumuuza” Bw Sisi.
Kwenye ukurasa huo, uliofunguliwa dakika chache baadaye, mwuzaji alisema akiuza “jemedari ambaye amemaliza muda wake wa kutumia” na kuweka picha ya rais huyo hapo.
Bei ilizidi $100,000 (£72,000) baada ya saa kadha. Ukurasa huo baadaye ulifutwa.
Bw Sisi alikuwa pia amependekeza Wamisri watoe “pauni 10 ($1.2; £0.9) kwa Misri kupitia ujumbe wa simu” kusaidia kupunguza mzigo wa kiuchumi unaokumba taifa hilo.
Alisema hayo alipokuwa akizindua mpango wa ukuaji wa kiuchumi wa 2030.
Alikejeliwa pia kwenye Twitter huku watu wakifanyia mzaha tamko lake. Kwa muda, kitambulisha mada #Ebay kilivuma sana kwenye Twitter nchini humo.
Matatizo yanayokabili Misri kwa sasa ni pamoja na kupungua kwa uwezekaji kutoka nje pamoja na kupungua kwa watalii.
Kiwango cha mfumkko nchini humo kimepanda sawa na ukosefu wa ajira.
Hivi vimetokana na miaka kadha ya machafuko.
Bw Sisi ameapa kuendelea kujenga nchi hiyo “hadi mwisho wa maisha yangu au muhula wangu” na kuwahimiza Wamisri wamsikize yeye pekee iwapo wanaipenda Misri kwa dhati.
"Msiwasikize wengine, nisikizeni mimi,” amewahimiza.
Man United yaichapa Midtjylland Europa
Mechi za Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya Uefa Europa Ligi imeendelea tena usiku wa Alhamisi kwa michezo mbali mbali .
Baadhi
ya matokeo ya mechi hizo Manchester United imevuna ushindi mnono wa
mabao 5-1 dhidi ya Midtjylland , Liverpool wakiwa nyumbani dhidi ya Fc
Ausbarg imechomoza na ushindi wa bao 1-0, Loco motiv Moscow na
Fenerbahçe zimefungana bao 1-1.Mechi nyingine Schalke 04 imechapwa na Shakt Donsk, Rapid Vienna imechapwa na Valencia bao 4-0, Lazio imeichapa Galatasaray bao 3-1, Tottenham imeshinda dhidi ya Fiorentina bao 1-0, Bayer Levkusen imeibugiza Sporting ba0 3-1, Ath Bilbao imetoka sare na Marseille bao 1-1.
PICHA
Subscribe to:
Posts (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...