16 April, 2016

Mfahamu R.KELLY na maisha yake ya Muziki kiujumla

Leo nitamzungumzia mfalme wa R&B ambaye anaishi mpaka leo na muziki wako unazidi kuwa mtamu mithili ya divai iliyo chachushwa. Kwa majina kamili ya huyu mfalme anajulikana kama Robert Sylvester Kelly a.k.a R.Kelly. Jina lake sio geni miongoni mwa wapenzi wa burudani ya muziki hasa ile yakubembelezana.

R.Kelly alizaliwa mnamo January 8 mwaka 1967 huko Chicago, Illinois akiwa ni mtoto wa tatu kuzaliwa kati ya watoto wanne kwenye familia yao. Alilelewa na mzazi mmoja tuu ambae ni mama(Joann) yake na mama yake alifariki kwa saratani mnamo mwaka 1993. Hakuzaliwa kaitika mazingira ya utajiri ila alikulia kwenye maisha ya umasikini ambayo mama yake alipambana nayo ili tuu aweze kuimudu familia yake. R.Kelly alinukuliwa katika jarida moja lililo andika Biography yake mnamo mwaka 2012 akisema
“When my mother wasn’t around, the women ran a little freer. … As I crept up in age… I found myself more curious and sometimes aroused, and I was ashamed of being aroused.”


 Safari yake ya muziki ikaanza
R.Kelly alijiunga na shule moja ya muziki huko nchini Marekeni iliyojulikana kama Kenwood Academy High School mnamo mwaka 1980 ila hakumaliza kutokana na yeye mwenyewe kusema alikua akipata ugumu katika masomo yake nakufanya hesabu kila siku, hivyo akaamua kuacha shule nakuanza kufanya muziki mara baada ya mwalimu wake wa muziki kutambua kipaji chake pale alipomwambia R.Kelly aimbe wimbo wa Nguli wa muziki Stevie Wonder uliojulikana kwa jina la “Ribbon in the Sky” kwenye tamasha la vipaji lililofanyika katika shule aliokua akisoma. Wakati alikua akihojiwa katika interview moja R.Kelly alinukuliwa akisema “That night it was like Spiderman being bit,”
 Ikawa kwanzia hapo akawa akipiga piano katika vituo vya mabasi, na viunga mabali mbali katika mtaa aliokua akiishi. Na mwishowe alifanikiwa kuanzisha kundi la muziki akiwa na rafiki yake Marc McWilliams na hatimae wakatengeneza kibao chao cha kwanza kilicho julikana kwa jina la 'Why You Wanna Play With Me?' ambacho kilifanyika katika Studio moja iliyokwenda kwa jina la Tavdash Records mnamo mwaka 1989.

Mnamo mwaka 1991, R.Kelly na mwenzake walipata shavu lakuingia makataba na Record studio moja iliyojulika kwa jina la Jive Records na hapo ndipo mnamo mwaka 1992 na ilikua na nyimbo kama vile
She's Got That Vibe' na kile cha Dedicated'. Mwaka uliofuatia Nguli huyo aliamua kuondoka katika kundi hilo nakuanza muziki kama msanii wakujitegemea yaani solo artist. Na hapo  

Solo Career
Maisha ya Nguli huyo yalizidi kusonga na safari hii aliweza kutoa album yake akiwa kama solo Artist iliyo kwenda kwa jina la 12 PLAY, ambayo ilikua na vibao kama vile “Bump N’ Grind,” “Sex Me,” na “I Like the Crotch On You,” ambapo ilikaa kwenye chart za r&b kwa muda wa week 9.
Aliendelea na kazi zake za muziki na baadae alianza kazi yaku saka vipaji vya muziki na alifanikiwa kuwapata watu kama vile Aaliyah na Changing Faces. Baadae alifanikiwa kufanya Remix ya wimbo wa Janet Jackson uliojulikana kama Any Time, Any Place' mnamo mwaka 1994 na ule wa Marehemu Michael Jackson uliojulikana kama 'You Are Not Alone' Album yake ya pili iliendelea kufanya vizuri na aliendelea kutoa vibao vikali kama vile 'You Remind Me of Something' na  'Down Low'. Baadae mkali wa basketball na star wa film Space Jam, Michael Jordan, akamuomba R.kelly Kumuandikia kibao kwa ajili ya film hiyo na matokeo ya kibao hicho ni 'I Believe I Can Fly' kibao ambacho kilizidi kumuweka juu zaidi. Album iliyofuatai aliuza zaidi ya nakala milion nane na kama utakua unakumbuka alimshirikisha Celine Dion kwenye kibao cha 'I'm Your Angel'

Baadae alitoa album iliyokwenda kwa jina la TP-2.com mnamo mwaka 2000 na alimsha Mkali wa hi-hope kutoka Rock Nation Jay-Z kwenye wimbo wa 'Fiesta' na ule mwingine wa 'Guilty 'Til Proven Innocent' ambao ulikuja kuachiliwa kwenye ay-Z's Dynasty album. Walifanya kazi ya kuipromote album hiyo dunia nzima katika Tour waliyoiita "The Best of Both Worlds". Album hiyo haikufanya vizuri kutokana na matatizo mbali mbali yaliyokuwa kwenye baadhi ya nyimbo zilizokuako katika album hiyo na hapo ndipo R.Kelly alipoamua kuifanyia kazi tena kwa mara ya pili na kuipatia jina la "Chocolate Factory" na album hiyo iliingizwa tena sokoni na ilifanikiwa kuuza kopi zaidi ya milioni tatu.

R.Kely alitoa albu yake nyingine iliyokwenda kwa jina la  TP-3: Reloaded mnamo mwaka 2005 na ndani ya album hiyo kulikua na vibao kama vile 'Trapped In The Closet'.Mnamo mwaka 2007 mkali huyo alitoa Album nyingine iliyokwenda kwa jina la Double Up ingawaje album hiyo ilikua teyari imevija mitandaoni kabla ya kuchiliwa rasmi. Double Up ilikua na vibao alivyo mshirikisha Mkali Usher.
Aliendelea kutoa vibao vingi na mnamo mwaka 2010, Nguli huyo alipata nafasi yakuandika ngoma ya' Sign of victory' ambacho kilitumika kwenye ufunguzi wa michuano ya Kombe la dunia Africa kusini.

Maisha binafsi.
Ilisadikika kwamba mkali huyo aliingia kwenye ndoa na mkali wa R&B marehemu Aaliyah kipindi mwanadada huyo akiwa na umri wa miaka 15. Jambo ambalo wakali hao wote wawili walikanusha jambo hilo. R.Kelly ana watoto watatu aliozaa na mcheza show Andrea Lee walio oana mnamo mwaka 1996.

 Mnamo mwaka 2002, mtando mmoja huko chicao ulikuja na taarifa zilizotajwa kua wawili hao walikua wanapanga kutemana baada yakutoke uvumi kua R.Kelly alijiingiza katika ngono na mtoto wa miaka 14

 na jambo hilo liliweka picha mbaya miongoni mwa mashabiki wake wengi kua alikua akijihusisha kufanya mapenzi na watoto wadogo, jambo ambalo halijapata kuthibituka mpaka leo.

Basi mpaka hapo nmefikia mwisho wa makala hii iliyokua ikimzungumzia MFALME WA R&B anaeishi, hapa namaanisha R.Kelly. tafadhali ungana nami tena week ijayo ambapo nitakuja kumzungumzia tena mkali mwingine ambae sintomtaja kwa jina leo hii mpaka hapo juma lijalo. UBARIKIWE TENA NA TENA 

Unaweza kununua DVD ya mkali hyo hapo chini kama inavyo oneka kumbuka unaponunua kitu mtandoni kutokana na tangazo unaloliona lolote hapa mtokambali basi na mimi nitakua nimepewa kitu kidogo kutokana na mauzo hayo na hivyo utakua umenisaidia


Video Mpya ya Raymond wa WCB- Kwetu

Kutoka WCB, Raymond anatuletea Video ya wimbo wake unakwenda kwa Jina la "Kwetu" ambapo audio ya wimbo huu teyari ilikwisha tambulishwa kwene hapo awali na kupokelewa vyema. Video imetengenezwa na Godfather Production Kutoka huko kwa mzee Madiba( Africa ya Kusini)
Chukua time yako kuenjoy Video hii ya mwanetu hapo chini Kwa kubonyeza PLAY!Click Here!

15 April, 2016

New music: Godzilla ft Mwasiti ‘First Class’ (+Audio)

kutoka kwa rapper mkali wa bongo flava King zila, akiwa kamsha mwanadada Mwasiti wanatuletea ‘First Class’ enjoy good Music mwanangu

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...