Showing posts with label Africa. Show all posts
Showing posts with label Africa. Show all posts
09 May, 2016
07 March, 2016
Maridhiano nchini Burundi ni Muhimu
Mamia ya watu wameuawa kutokana na vurugu hizo huku maelfu wakilazimika kuikimbia nchi yao na kukimbilia nchi jirani.
Rais Pierre Nkurunziza Katika mazungumzo hayo na kiongozi huyu wa Kiroho,muda mwingi alionekana ni mwenye furaha na tabasamu mbele ya ambapo undani wa mazungumzo hayo ilikuwa ni kuhimiza ushiriki wa pande zote ili kuhakikisha kuwa amani ya kweli inafikiwa nchini humo.
Askofu Just Welby amesema kuwa suala la maridhiano nchini Burundi linahitaji watu kujitoa muhanga.
Hata hivyo amesisitiza hatua za msingi za kuzingatiwa ili kuweza kufikiwa kwa amani ya kweli nchini Burundi.
Taifa la Burundi lililopata Uhuru wake 1962 na kupitia katika vipindi mbalimbali vya machafuko limejikuta katika upotevu wa hali ya amani katika kipindi kingine kufuatia uamuzi wa Rais wa taifa hilo Pierre Nkurunziza kuamua kuwania muhula mwingine hatua inayopingwa na upinzani nchini humo.
02 March, 2016
Bi Odinga: Nilikosea, Olduvai Gorge iko Tz
Mwanawe aliyekuwa waziri mkuu wa
Kenya, Raila Odinga, Rosemary, amekiri kuwa alikosea alipodai kuwa bonde
la Olduvai Gorge liko Kenya ilhali liko Tanzania.
''Bonde la
Oldupai ama Olduvai liko Tanzania, nimekubali kuwa nilikosea nilipokuwa
nikihutubia mkutano wa viongozi wa vijana kutoka kote duniani nikiwa New
York Marekani(International Young Leaders Assembly).''Nahisi kama ambaye nimewakosea ndugu zangu kutoka Tanzania''.
''Nia yangu ilikuwa ni kusema kuwa nilipokuwa mdogo nikienda shuleni nilifunzwa kuwa fuvu la mtu wa kale lilipatikana Olorgesaiile eneo la Kajiado.
Nisemeje ,,nawaombeni radhi Watanzania.
Olduvai Gorge iko salama wala haijanyakuliwa na kenya
'Katika ile hali ya undugu naomba kuwanyoshea mkono wa amani kwa sababu mwisho wa siku Afrika mashariki ndio kitovu cha ubinadamu'' alisema bi Odinga kupitia mtandao wake wa Instagram.
Tamko lake kuhusiana na bonde hilo la Olduvai (Oldupai) lililoko Tanzania lilihusiana na mada ya siku hiyo.
Olduvai ndiko kulikopatikana vifaa vilivyotumika na watangulizi wa binadamu yapata miaka milioni moja na laki sita iliyopita (milioni 1.6)
Bi Rosemary aliomba radhi baada ya kuzomewa na maelfu ya watu kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook Instagram na Twitter wakidai aliwapotosha hadhira yake na haswa ulimwengu kwa kusema eti Olduvai ipo Kenya.
Mbunge Zitto Kabwe alikuwa amechangia mada kwa kusema kuwa Tanzania sharti izinadi vivutio vyake vya kitalii ilikuzima dhana potovu.
Aidha alidai kuwa watu wanafikiria kuwa mlima kilimanjaro uko Kenya ilahali ukweli halisi upo Tanzania sawa na mwanamuziki nyota Diamond Platnumz ambaye ni Mtanzania.
26 February, 2016
Rais wa Misri 'auzwa' mtandaoni
Raia wa Misri wamekuwa wakimkejeli
rais wao Abdul Fattah al-Sisi mtandaoni baada yake kusema kwamba anaweza
kujiuza ili kusaidia uchumi wa taifa hilo.
"Ingeliwezekana mimi niuzwe, ningejiuza,” alisema Bw Sisi alipokuwa akihutubu kupitia runinga ya taifa.Muda mfupi baadaye, ukurasa uliundwa kwenye mtandao wa kuuza bidhaa mtandaoni wa Ebay wa “kumuuza” Bw Sisi.
Kwenye ukurasa huo, uliofunguliwa dakika chache baadaye, mwuzaji alisema akiuza “jemedari ambaye amemaliza muda wake wa kutumia” na kuweka picha ya rais huyo hapo.
Bei ilizidi $100,000 (£72,000) baada ya saa kadha. Ukurasa huo baadaye ulifutwa.
Bw Sisi alikuwa pia amependekeza Wamisri watoe “pauni 10 ($1.2; £0.9) kwa Misri kupitia ujumbe wa simu” kusaidia kupunguza mzigo wa kiuchumi unaokumba taifa hilo.
Alisema hayo alipokuwa akizindua mpango wa ukuaji wa kiuchumi wa 2030.
Alikejeliwa pia kwenye Twitter huku watu wakifanyia mzaha tamko lake. Kwa muda, kitambulisha mada #Ebay kilivuma sana kwenye Twitter nchini humo.
Matatizo yanayokabili Misri kwa sasa ni pamoja na kupungua kwa uwezekaji kutoka nje pamoja na kupungua kwa watalii.
Kiwango cha mfumkko nchini humo kimepanda sawa na ukosefu wa ajira.
Hivi vimetokana na miaka kadha ya machafuko.
Bw Sisi ameapa kuendelea kujenga nchi hiyo “hadi mwisho wa maisha yangu au muhula wangu” na kuwahimiza Wamisri wamsikize yeye pekee iwapo wanaipenda Misri kwa dhati.
"Msiwasikize wengine, nisikizeni mimi,” amewahimiza.
23 February, 2016
Mugabe aadhimisha miaka 92 yakuzaliwa
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, amekata keki kubwa na kuzima mishumaa kusherekea siku yake ya kuzaliwa. Kiongozi huyo mkongwe muanzilishi wa taifa hilo lililoko Afrika ya Kusini ameadhimisha miaka 92 ya kuzaliwa kwake. Keki hiyo ilikabidhiwa bwana Mugambe katika sherehe iliyoandaliwa na wafanyikazi wake asubuhi ya leo.
Maandishi ya keki hiyo yalikuwa ‘ siku njema ya kuzaliwa Gushungo’ Gushungo ni jina lake la ukoo.
Sherehe hiyo iiyoandaliwa kwenye ikulu ya rais ilihudhuriwa na majenerali wa kijeshi na wageni wengine mashuhuri walioalikwa.
Siku ya kuzaliwa kwake ilikuwa hapo jana na amepanga sherehe nyengine itakayo gharimu takriban dola milioni moja $1m huko Masvingo , Kusini mwa mkoa wa Zimbabwe, ripoti zinasema.
22 February, 2016
Besigye apinga matokeo ya uchaguzi Uganda
Mmoja wa wapinzani wakuu katika
uchaguzi mkuu uliomalizika hivi punde nchini Uganda, Dkt Kizza Besigye,
amekatalia mbali matokeo ya uchaguzi huo, uliofanyika siku ya Alhamisi.
Bw
Besigye ambaye amekuwa akizuiliwa nyumbani kwake tangu siku ya Ijumaa
amesema kuwa raia nchini Uganda wameshuhudia ulaghai mkubwa mno wa
uchaguzi mkuu, kuwahi kufanyika katika taifa hilo la mashariki mwa
Afrika. Kanali huyo mstaafu ameelezea uchaguzi huo kama usio halali na kuwa ni mapinduzi ya kijeshi. Rais wa muda mrefu Yoweri Kaguta Museveni,
alitangazwa mshindi. Rais Museveni ameiongoza Uganda kwa muhula wa tano mtawalia.Rais Museveni ambaye amekuwa mamlakani kwa miaka thelathini sasa, alipata zaidi ya asilimia 61 ya kura huku Besigye akijipatia asilimia 35 ya kura. Wachunguzi wa kimataifa wanasema kuwa uchaguzi huo uliandaliwa katika mazingara ya hofu na kudhalalishwa.
16 February, 2016
Busu lililovunja Record Barani Africa.
Mbunge mmoja nchini Zimbabwe
Joseph Chinotimba ameingia katika kumbukumbu za Afrika baada ya
kumbusu mke wake Vimbai kwa muda mrefu zaidi kuwahi kunakiliwa barani
Afrika.
Mbunge huyo na mkewe walizoa tuzo hilo baada ya kupigana busu kwa dakika 10 na sekunde 17.Rekodi hiyo iliwekwa katika hafla moja iliyopigiwa upatu na kunadiwa kuwa ''Mashindano ya busu refu zaidi kuwahi barani Afrika''
Hafla hiyo ilipangwa na kuandaliwa kwa ushirikiano na waandalizi wa Daftari la rekodi barani Afrika.
Hafla hiyo iliandaliwa katika mji mkuu wa Harare kama sehemu ya kuadhimisha sikukuu ya wapendanao iliyoadhimishwa jumapili.
15 February, 2016
Wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wamepiga kura
Wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya
Kati wamepiga kura kumchagua rais mpya katika uchaguzi unaorudiwa baina
ya waliokuwa mawaziri wakuu, Faustin Touadera na Anicet Dologuele.
Pia watachagua wabunge baada ya uchaguzi uliofanywa mwezi Disemba mwaka jana kubatilishwa kutokana na kasoro zilizojitokeza.Mwandishi wa BBC Abdourahmane Dia kutoka Bangui anasema mara hii, wananchi hawakuwa na hamasa kubwa ya kupiga kura, ingawa maafisa wa tume ya uchaguzi wanasema upigaji kura umefanyika vizuri.
Wapiga kura wanachagua rais wao na wabunge wao katika uchaguzi ambao unatarajiwa kumaliza mapigano ya zaidi miaka mitatu baina ya jamii za nchi hiyo.
Hakuna matukio makubwa yaliyoshuhudiwa, lakini vituo vya kupigia kura vilionekana vikiwa na wapiga kura wachache, ikilinganishwa na uchaguzi uliofanyika mara ya kwanza, hayo ni kwa mujibu wa mwandishi wa BBC ambae yuko katika mji mkuu wa Bangui.
Tatizo la mipango na ukosefu wa baadhi ya vifaa umetawala uchaguzi huo kama walivyoeleza baadhi ya wapiga kura.
"nimeshindwa kupiga kura kwa sababu jina langu halipo katika daftari la kupiga kura. Na mara ya mwisho niliweza kupiga kura, lakini leo wamekataa. Inaumiza, ni uonevu kwa sababu mimi ni raia pia."
"nimeshindwa kuona jina langu na mara ya mwisho nimepiga kura hapa. Nimeangalia kila sehemu lakini sijaona jina langu. Sijui nitafanya nini sasa."
Hata hivyo, maafisa wa tume ya uchaguzi wamesema kwamba hatua mpya zimechukuliwa ili kuepusha mapungufu hayo.
Marudio ya uchaguzi huo yanafanyika mwezi mmoja na nusu baada ya mchuano wa mara ya kwanza ambapo wagombea thelathini waliingia kwenye kinyang'anyiro cha urais.
Wagombea wote wawili Anicet Dologuele, ambae amebobea katika maswala ya benk na Faustin Touadera, ambae ni mhadhiri wa chuo kikuu, wote wanasimamia umoja wa kitaifa, usalama, na uchumi.
Hata hivyo, atakaeibuka kidedea, atatakiwa haraka sana, atatue tatizo la makundi yenye kumiliki silaha ambayo bado yana nguvu katika maeneo mbali mbali ya nchi licha ya kuwepo kwa vikosi vya kulinda amani elfu kumi na moja vya Umoja wa Mataifa.
13 February, 2016
Naibu Rais wa Kenya William Ruto amepata ushindi Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC)
Naibu Rais wa Kenya William Ruto
amepata ushindi muhimu kwenye kesi yake inayosikizwa katika Mahakama ya
Kimataifa ya Uhalifu (ICC) baada ya majaji wa rufaa kukubali rufaa yake
ya kupinga kutumiwa kwa ushahidi wa mashahidi waliojiondoa.
Hii
ina maana kwamba ushahidi ulioandikishwa awali na upande wa mashtaka
hauwezi kutumiwa dhidi ya Bw Ruto na mwanahabari Joshua Sang.Uamuzi huo ni pigo kubwa kwa upande wa mashtaka unaoongozwa na Fatou Bensouda.
Upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi sita waliokuwa wanahusisha Bw Ruto na ghasia za baada ya uchaguzi za mwaka 2007-08, vilivyosababisha vifo vya watu 1,200, walioondoa ushahidi wao.
Upande wa mashtaka unasema walitishiwa au wakahongwa.
Majaji wa rufaa wamebatilisha uamuzi wa awali wa majaji uliosema upande wa mashtaka unaweza kutumia ushahidi uliowasilisha na mashahidi hao kabla yao kubadili nia.
"Ushahidi ulioandikisha awali uliwasilishwa bila washtakiwa kupewa fursa ya kuwahoji na kuwauliza maswali mashahidi hao,” amesema jaji wa mahakama ya rufaa Piotr Hofmanski.
Bw Sang amefurahia uamuzi huo na kusema maombi yake yamejibiwa.
22 January, 2016
Bomu lalipuka katika mgahawa Somalia
Bomu lililotegwa ndani ya gari
limelipuka nje ya mgahawa mmoja uliopo katika ufukwe wa bahari katika
mji mkuu wa Somalia Mogadishu,kulingana na maafisa wa polisi.
Walioshuhudia
wamemwelezea mwandishi wa BBC Ibrahim Aden kwamba gari hilo lililojaa
vilipuzi liligonga mgahawa huo maarufu wa Lido Beach kabla ya watu
watano kujitokeza na kuanza kufyatua risasi.Haijulikani iwapo kumekuwa na majeruhi.
Hakuna kundi lililokiri kutekeleza shambulizi hilo,lakini kundi la Alshabaab ndilo linaloshukiwa kwa kutekeleza mashambulizi mengine kama hayo hapo awali.
Mgahawa wa Lido Beach uliopo pembezoni mwa Mogadishu,huwavutia maelfu ya vijana wa Somalia wanaojifurahisha.
Migahawa kadhaa imefunguliwa katika ufukwe huo katika miaka ya hivi karibuni.
Afisa mkuu wa polisi katika eneo hilo Meja Abdiqadir Ali amekiambia chombo cha habari cha reuters kwamba shambulio hilo lilitokea katika lango la mgahawa huo.
Amesema kuwa uchunguzi unaendelea.
CHANZO:BBC
Subscribe to:
Posts (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...

-
Mshambuliaji huyo wa umri wa miaka 26 ambaye amekuwa akichezea klabu ya Corinthians ya Ugiriki amechezea taifa lake mechi 27 na kuwafungi...
-
Brit Awads 2016 zimefanyika huko London ambapo mwanamuziki Adele ameondoka na tuzo nyingi zaidi katika nomination alizo kuwepo. Hizi hapa...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...