Showing posts with label Politics. Show all posts
Showing posts with label Politics. Show all posts

13 October, 2016

Uchaguzi Marekani 2016: Trump 'alipapasa wanawake kama pweza'



Wanawake wawili wameambia gazeti la New York Times kwamba mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump aliwashika kimapenzi bila idhini yao.

Mwanamke mmoja amesema mgombea huyo alimshika matiti na kujaribu kuingia mkono wake chini ya sketi yake wakiwa kwenye ndege miongo mitatu iliyopita.

Wa pili anasema Bw Trump alimpiga busu bila yeye kutaka katika jumba la Trump Towers mwaka 2005.
Maafisa wa kampeni wa Trump wamesema "makala hii yote ni hadithi ya kubuni".

Gazeti la New York Times limeanzisha kampeni "ya uongo, na iliyoratibiwa kumharibia jina kabisa", taarifa ya maafisa wa Trump imesema.

Jessica Leeds, 74, kutoka Manhattan, ameambia gazeti hilo kwamba alikuwa ameketi karibu na Bw Trump sehemu ya abiria wa hadhi ya juu kwenye ndege wakielekea New York pale alipoinua sehemu ya kupumzishia mkono kitini na akaanza kumshika.

Mwanamke huyo alikuwa na umri wa miaka 38 wakati huo.
"Alikuwa kama pweza .... mikono yake ilinishika kila pahali," anasema. "Ulikuwa ni unyanyasaji."

Rachel Crooks alikuwa mpokezi wa wageni katika kampuni ya kuuza ardhi ya nyumba katika jumba la Trump Tower, wakati huo akiwa na miaka 22.
Anasema alipigwa busu la lazima na Bw Trump nje ya lifti ya jengo hilo.
"Ilikuwa vibaya sana," Bi Crooks ameambia New York Times.
"Niliudhika sana kwamba alidhani nilikuwa sina maana kiasi kwamba angefanya hivyo (bila hiari yangu)."

Wawili hao hata hivyo hawakuripoti visa hivyo kwa maafisa wa serikali.
Hata hivyo, wanasema waliwaambia marafiki na jamaa zao yaliyojiri.Trump Tower in Manhattan
Bi Leeds anasema alikasirika sana na alitatizika kimawazo baada ya Bw Trump kumgusa.

Anasema mara moja aliondoka eneo la abiria wa hadhi na kwenda kuketi eneo la abiria wa kawaida.Maafisa wa kampeni wa Clinton wamesema simulizi hizo za kuogofya kwenye New York Times zinatilia mkazo "kila kitu ambacho tunajua kuhusu jinsi Donald Trump huwachukulia wanawake".

Kumshika makalio'

Hayo yakijiri, Mindy McGillivray naye ameambia gazeti la Palm Beach Post kwamba akiwa na miaka 23 , Bw Trump alimshika makalio katika kilabu chake cha Mar-a-Lago club jimbo la Florida mwaka 2003.

Anasema alikuwa amesimama karibu na mchumba wake wa wakati huo Melania Knauss.

Bi McGillivray, ambaye kwa sasa ana miaka 36, anasema hakuripoti kisa hicho kwa polisi.

Lakini mwenzake, mpiga picha Ken Davidoff, aliambia gazeti hilo kwamba mwanamke huyo alimwita kando siku hiyo na kumwambia: "Donald amenishika makalio sasa hivi".

Maafisa wa Trump wanasema madai ya Bi McGillivray hayana ukweli wowote.
Wanawake wote watatu wamesema wanaunga mkono Bi Clinton.

Ijumaa wiki jana, video iliyopigwa mwaka 2005 ilitokea na kumuonyesha Bw Trump akinena maneno ya kuwadhalilisha wanawake na kuongea kuhusu kuwapapasa wanawake.

Aliomba radhi kuhusu matamshi hayo, lakini akasema yalikuwa mazungumzo ya mzaha faraghani.
Viongozi wengi wakuu wa Republican, akiwemo Spika Paul Ryan, wameshutumu matamshi hayo. Bw Ryan alisema hatamtetea tena Bw Trump.



CHANZO: BBC

08 July, 2016

Uingereza itakuwa na Waziri Mkuu mwanamke

May
Uingereza itakuwa na Waziri Mkuu mwanamke, ambaye atachukua majukumu kufikia mwezi Oktoba.

Hii ni baada ya wabunge wa chama tawala cha Conservative kuwateua wagombea wawili waliokuwa wanaongoza kukabiliana kuamua nani atakuwa kiongozi mpya.

Waziri wa mambo ya ndani Theresa May, ndiye anayepigiwa upatu sana kumrithi David Cameron kama kiongozi wa chama na waziri mkuu.
Waziri wa kawi Andrea Leadsom, ndiye mwanamke huyo mwingine.
Waziri wa Haki Michael Gove, aliyekuwa mmoja wa waliopigia debe Uingereza kujitoa Muungano wa Ulaya, alimaliza wa tatu kwenye kura ya akaondolewa.Gove
Matokeo kamili yanatarajiwa mwezi Septemba.
Kinyang’anyiro cha sasa cha kuchagua kiongozi mpya kilianza baada ya Bw Cameron kuamua kung’atuka.
Hii ni baada ya upande wake, uliotaka Uingereza isalie EU, kushindwa kwenye kura ya maoni mwezi uliopita.

15 March, 2016

Mahakamaa yatupilia mbali Pingamizi La Stephen Wassira

Mahakamaa Kuu Kanda ya Mwanza, imetupilia mbali maombi ya baadhi ya wapigakura wa Jimbo la Bunda Mjini ya kuruhusiwa kukata rufaa kupinga uamuzi wa Makahama Kuu wa kufuta shauri lao la kupinga matokeo ya uchaguzi.

Maombi hayo yaliwasilishwa na Magambo Masato na wenzake wanne wanaompigania Stephen Wassira, wakiiomba mahakama hiyo kuwaruhusu kukata rufaa Mahakama ya Rufani baada ya kutoridhiswa na uamuzi ya kupinga matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana yaliyompa ushindi Ester Bulaya (Chadema), dhidi ya Stephen Wasira (CCM).

Jaji anayesikiliza shauri hilo namba 25 la mwaka 2016, Rose Ebrahim alisema jana kuwa anakubaliana na pingamizi lililowekwa na wajibu maombi kuwa hayana mashiko kisheria.

Pingamizi hilo lilowasilishwa na Wakili Mfawidhi wa Serikali, Paschael Marungu alidai aliyesaini hati ya maombi siyo aliyethibitisha kwani hilo ni kosa la kisheria.

Wakili Marungu alidai hati hiyo ilisaniwa na Wakili Denis Kahangwa na kuthibitishwa na Wakili Constantine Mutalemwa kwamba hilo ni kosa kisheria, hivyo kuiomba mahakama kutupilia mbali.

Akitoa uamuzi juu ya pingamizi hilo, Jaji Ebrahim alisema anakubaliana na pingamizi hilo kwani, makosa yaliyofanywa hayarekebishiki.

“Haya maombi nayatupilia mbali hayana miguu ya kusimamia, ni kosa kubwa hati kusainiwa na mtu mwingine halafu ikathibitishwa na mwingine, hakuna namna ya kurekebisha, lazima sheria ifuatwe na taratibu zake,” alisema.

Awali, Magambo na wenzake walifungua kesi Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza kupinga ushindi wa Bulaya, lakini ilitupiliwa mbali kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya sheria.
Katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana, Bulaya alipata kura 29,973 na Wasira wa CCM aliambulia 19,123 ikiwapo tofauti ya kura 10,000.
Hata hivyo, Wasira alilalamikia matokeo hayo akidai uchaguzi ulitawaliwa na udanganyifu. 
 
CHANZO: MPEKUZI HURU

14 March, 2016

Mrithi wa Dk. Slaa Chadema apatikana ni Dk.Vicent Mashinji

Tayari Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamemtangaza Katibu Mkuu wao mpya ambaye atakitumikia chama hicho kikuu na kikubwa cha upinzani nchini, Katibu huyo si mwingine ni Dkt. Vicent Mashinje  ambaye anashika mikoba ya aliyekuwa akishika nafasi hiyo awali kabla ya kuachia ngazi, Dk. Wilbroad Slaa.
Chadema ambao wapo Mkoani Mwanza katika mkutano wao mkuu, usiku huu wameweza kulitangaza jina hilo. Awali wanachama na kada mbalimbali walikuwa na hamu ya kutaka kujua ni nani atashika wadhifa huo mkubwa kabisa ndani ya chama huku kila mmojja kutokuwa na jibu sahihi awali kabla ya Mwenyekiti wa chama hichi usiku huu, Freeman Mbowe, kuweka wazi jina hilo.
Mjue kwa ufupi hapa Katibu Mkuu Mpya wa Chadema: Ni miongoni mwa vijana wenye kuleta mageuzi katika nyanja mbalimbali ni msomi wa kiwango cha juu, kabila lake ni MSUKUMA wa Sengerema.

CV ya Katibu Mkuu Dr. Vincent B. Mashinji
Professional experience
Clinical Advisor & TB/HIV lead
UMSOM-IHV
July 2008 – Present
ART Program Doctor/IMA team lead
IMA Worldhealth
August 2006 – June 2008 (1 year 10 months)
Medical Officer/Anaesthesiology
Regency Medical Centre
October 2005 – August 2006 (10 months)
Medical Officer
Muhimbili National Hospital
August 2003 – October 2005 (2 years 2 months)
Research Assistant
Freelance
November 2002 – August 2003 (9 months)
Intern Docor
Muhimbili National Hospital
September 2001 – October 2002 (1 year 1 month)
Education history
Open University of Tanzania
PhD
August 2010 – Present
AMREF/UCLA Anderson School
MDI Certificate
April 2010 – April 2010
Blekinge Institute of Technology
MBA
September 2007 – March 2010 (2 years 6 months)
UMSOM-IHV
IPEP Certificate
May 2008 – May 2008
Evin School of Management
Certificate in CSR
October 2005 – October 2005
Muhimbili University College of Health Sciences
MMed/Anaesthesiology
September 2003 – April 2005 (1 year 7 months)
Muhimbili University College of Health Sciences
Certificate in Research Methodology
September 2004 – September 2004
Makerere University
MBChB
October 1995 – July 2001 (5 years 9 months)
Mzumbe High School
ACSEE
July 1992 – June 1994 (1 year 11 months)
St. Pius X Seminary, Makoko
GCSEE
January 1988 – October 1991 (3 years 9 months)
Iligamba Primary School
Leaving Certificate/Primary School
Januar1981October1987(6years9months)
 

SOURCE: MJENGWA BLOG

08 February, 2016

Jaji Lubuva amuonya Lowassa

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), Jaji Damian Lubuva amewataka wanasiasa walioshindwa kwenye Uchaguzi Mkuu waache kujitangaza kuwa walishinda, akisema wanapotosha wananchi.
Kauli hiyo ya Jaji Lubuva imekuja siku chache baada ya aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa kudai kuwa kama si matokeo kuchakachuliwa, alikuwa na nafasi kubwa ya kushinda kwa sababu wananchi walishaichoka CCM na wakawa wanataka mabadiliko.
Lowassa alisema hayo katika mahojiano maalum na waandishi wa habari ofisini kwake, akisema yeye na Ukawa walishinda kwa kishindo isipokuwa matokeo yalivurugwa makusudi ili CCM iendelee kubaki madarakani.
Jana, akiwa kwenye mkutano wa tathmini kati ya NEC na asasi za kiraia kuhusu utoaji elimu kwa mpigakura uliofanyika Dodoma, Jaji Lubuva alisema uchaguzi umeshapita na kilichobaki sasa ni kufanya kazi tu.
Bila ya kutaja jina la mwanasiasa huyo, Jaji Lubuva alisema kama kuna mtu alishindwa katika uchaguzi uliopita, ajipange kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao mwaka 2020.
“Hata wananchi wanawashangaa kwa kuwa wao ndio walioamua ni nani anafaa kuwaongoza,” alisema Jaji Lubuva.
Alisema kuwa NEC ilikuwa inapokea matokeo ya uchaguzi kutoka majimboni na kuyasoma kama yalivyotumwa na katika hilo hakuna wakala hata mmoja wa chama ambaye aliyapinga matokeo hayo. “Sasa nashangaa kuna baadhi ya wagombea wanaotaka Tume ifukuzwe kazi eti tu kwa sababu wao hawakushinda. Naomba ifahamike kwamba katika kila uchaguzi duniani kuna kushinda na kushindwa.
"Sasa kama kila atakayeshindwa atataka tume ifukuzwe kazi hapatakuwa na tume ya uchaguzi kwa sababu kila atakayekuwa anashindwa atakuwa anataka tume ifukuzwe kazi,” alisema Jaji Lubuva.

23 January, 2016

Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imetangaza tarehe ya marudio ya uchaguzi

Zec
Uchaguzi huo sasa utafanyika Jumapili tarehe 20 Machi.
Tangazo hilo limefanywa na mwenyekiti wa ZEC Jecha Salim Jecha.
Bw Jecha amesema tarehe hiyo iliamuliwa na tume baada ya mkutano hapo jana.
"Uchaguzi huo utahusisha uchaguzi wa Rais, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani na hakutakuwa na uteuzi mpya wa wagombea wala mikutano ya kampeni," amesema Bw Jecha.
"Wagombea wote walioteuliwa hapo awali wataendelea kuwa wagombea katika uchaguzi huu."iongozi wa chama hicho walisusia maadhimisho ya Siku ya Mapinduzi wiki iliyopita.
Chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilikuwa tayari kimewashauri wanachama wake visiwani wajiandae kwa marudio ya uchaguzi, tangazo lililoshutumiwa vikali na viongozi wa CUF.

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...