Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi (TRA) Bw. Richard Kayombo
Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikiwa kukamata bidhaa za magendo kwenye
maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Bahari ya Hindi, Ziwa Victoria na
mipakani.
Taarifa
hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi (TRA)
Bw. Richard Kayombo wakati akifanya mahojiano na Mwandishi wa Idara ya
Habari (MAELEZO) ofisini kwake Jijini Dar es Salaam kuhusu juhudi za
operesheni ya kutokomeza bidhaa za magendo nchini.
Bw.
Kayombo ameeleza kuwa, mkoani Lindi TRA imefanikiwa kukamata mashua
katika bandari ya Lindi ambayo ilisheheni bidhaa za magendo zenye
thamani ya shilingi 159,361,046.
Ameongeza
kuwa katika operesheni hiyo, TRA imefanikiwa kukusanya kodi ya jumla ya
shilingi 10,500,678 kutoka katika bidhaa zilizokuwa katika nyaraka za
forodha (manifest) ambapo pia inategemea kukusanya kodi ya shilingi
19,529,500 kutoka katika bidhaa ambazo zilikuwa katika nyaraka za
forodha lakini thamani yake ilikuwa chini ya bei halisi.
Akitaja
bidhaa hizo za magendo zilizokamatwa katika mashua hiyo ni mifuko 3,725
ya sukari yenye thamani ya shilingi 127,070,562, betri katoni 50, mchele
mifuko 3,087, mafuta ya kula madumu 80, majokofu manne ya mtumba,
baiskeli 4 za mitumba pamoja na katoni 20 za hamira.
“Mashua
hiyo ilikamatwa katika bandari ya Lindi tarehe1 Februari, 2016 baada ya
wasamaria wema kutoa taarifa ya kuwepo bidhaa za magendo ndani ya mashua
hiyo ambapo upakuaji wa shehena hiyo ulianza mara moja.’’Alisema
Kayombo.
Ameongeza
kuwa, Jijini Dar es Salaam, TRA kwa kushirikiana na kikosi cha doria
cha Jeshi la Wanamaji wameweza kukamata Jahazi lenye jina la ‘Takbiri’
lenye usajili wa namba Z-875 likiwa limesheheni lita 19,700 za dizeli
ambapo thamani yake bado haijapatikana kwakuwa imepelekwa kwa Mkemia
Mkuu wa Serikali kwa ajili ya Uchunguzi zaidi.
Aidha,
majahazi mengine matatu yamekamatwa katika eneo la Kigombe mkoani Tanga
ambayo yalikuwa na bidhaa za magendo yenye thamani ya shilingi 99, 682,
273, 48 ambapo ndani kulikuwa na magunia ya sukari, mchele, mafuta ya
kula, matairi ya magari, nyavu za kuzuia mbu, jokofu, jiko la umeme,
rangi za kupuliza, betri na biskuti.
Majahazi hayo yalitaifishwa baada ya wahusika kujitosa ndani ya maji na kutoroka.
TRA kwa
kushirikiana na Jeshi la Polisi inafanya doria saa 24 kila siku katika
maeneo yote yaliyoshamiri upitishaji wa bidhaa za magendo pia imeunda
Kanda Maalum katika maeneo ya Mbweni, Msasani, Kunduchi pamoja na
Kigamboni.