Chelsea wametoa dau la pauni
milioni 6 kumtaka kipa Asmir Begovic, 28, kuziba nafasi ya Petr Cech, 33
aliyehamia Arsenal (Telegraph).
Tottenham huenda wakamtoa Emmanuel Adebayor, 31 kwenda Aston Villa kubadilishana na Christian Benteke, 24 (Daily Mirror).
West Ham huenda wakamtaka
mshambuliaji wa Liverpool Fabio Borini, 24, lakini Liverpool huenda
wakamtumia kumwania Benteke (Independent).
Meneja wa Liverpool Brendan
Rodgers anakaribia kukamilisha usajili wa wachezaji watatu, Nathaniel
Clyne, 24, kutoka Southampton, Bobby Adekanye, 16 kutoka Barcelona na
Ludwig Augustinsson, 21 kutoka FC Copenhagen (Daily Star).
Manchester City wanafikiria kumchukua beki kutoka Brazil Fabinho, 21 anayechezea Monaco (Daily Mail).
Baada ya kumkosa Bastian
Scheinsteiger Manchester United watajaribu kumsajili kiungo wa
Southampton Morgan Schneiderlin, 25 (Daily Express).
Douglas Costa wa Shakhtar Donestk amesema Bayern Munich wanamtaka (Guardian).
Arsenal wameacha kumfuatilia kiungo wa Juventus Arturo Vidal, 28 (Telegraph).
Badala yake Arsene Wenger angependa kumchukua kiungo wa Sporting William Carvahlo, 23 (London Evening Standard).
Everton wanamfikiria beki wa
kulia wa Leeds United Sam Ryram, 21, wakati Manchester United
wakifikiria kumchukua Seamus Coleman 26 (Daily Express).
Meneja mpya wa West Ham Slaven
Blic ametakiwa kumaliza katika nafasi nane za juu na atafukuzwa kazi
bila fidia kama klabu hiyo itashuka daraja (Sun).
West Ham wanajaribu kumsajili
beki wa kati kutoka Tunisia Aymen Abdennour, 25 kutoka Monaco na Alex
Song, 27 kutoka Barcelona (Daily Mail).
Meneja wa manchester United
Louis van Gaal amemuambia kipa David De Gea, anayesakwa na Real Madrid,
kuripoti kambini siku ya Jumatatu (Daily Star). Kiungo kutoka Uturuki
Arda Turan, 28, anajiandaa kuondoka Atletico Madrid na atatangaza
anakwenda wapi siku chache zijazo, kwa mujibu wa wakala wake. Mchezaji
huyo anatakiwa na Barcelona, Paris St-Germain na Manchester United
(NTVSpor).
West Brom wanataka kuvunja
rekodi yao ya usajili kwa kumchukua Charlie Austin, 25 anayeuzwa kwa
pauni milioni 15 (Birmingham Mail).
Barcelona wametoa dau la euro
milioni 80 na nyongeza nyingine milioni 10 kumtaka Paul Pogba. Chelsea
wametoa euro milioni 50 pamoja na Oscar, huku Manchester City wakitoa
euro milioni 100 (Sport).
Juventus wangependa kumuuza
Pogba kwenda Barcelona kwa sababu Pogba ataendelea kuichezea klabu yake
kwa kuwa Barca wana kikwazo cha kusajili hadi msimu ujao (Sport).
Arsenal watawapa napoli pauni
milioni 9 kutaka kumsajili Faouzi Ghoulam, 24 wiki hii. Mchezaji huyo
pia anatazamwa na Chelsea na Manchester City, lakini Arsenal wana nafasi
kubwa ya kumchukua (Metro).
Manchester United wametoa euro milioni 40 kumtaka Sergio Ramos wa Real Madrid (Sky Sports).
Chelsea wanajiandaa kupanda dau
kumtaka beki wa Everton John Stones anayethamanishwa kwa pauni milioni
20 (Daily Express) na AC Milan wanataka kumchukua kiungo wa Tottenham
Erik Lamela wakishindwa kumsajili Axel Witsel (Mediaset).
No comments:
Post a Comment