Showing posts with label Education. Show all posts
Showing posts with label Education. Show all posts

21 October, 2016

Matumaini mapya 66,000 waliotoswa Bodi Mikopo

KUNA matumaini mapya kwa wanafunzi 66,500 waliokosa mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo ulioanza mwezi huu.
Rais wa Daruso, Erasmi Leon, akizungumza na waandishi wa habari nje
 ya jengo la Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi
 jijini Dar es Salaam jana.
 Matumaini hayo yanakuja baada ya kupatikana kwa habari kwamba Kamati ya Bunge ya  Maendeleo na Huduma za Jamii imeweka kwenye ratiba yake ya shughuli za kamati, suala la mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.

Maelezo ya mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo, Zitto Kabwe aliyotoa jana kupitia mtandao mmoja wa kijamii ilisema "kamati itashughulia suala hilo kuanzia Jumatatu, kwa mujibu wa ratiba niliyoona." 

"Natumai tutapata jawabu la wanafunzi walikosa mikopo."

 Bodi ya Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu (HESLB) ilitangaza juzi kuwa itatoa mikopo kwa wanafunzi 21,500 tu kwa mwaka 2017/2017 hivyo kuacha 'vilio' kwa maelfu ya wanafunzi wanaotakiwa kusomea shahada katika vyuo mbalimbali nchini.

 Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru alisema juzi kuwa kati ya wanafunzi 88,000 walioomba mikopo hiyo, wanatarajia kutoa fedha hizo kwa 21,500 tu ambao "wamekidhi vigezo".

Kutokana na takwimu hizo, ni dhahiri wazazi ama walezi wa wanafunzi 66,500 watalazimika kuingia mifukoni kulipia gharama za elimu hiyo kwa watoto wao.

Aidha, mpaka sasa HESLB imetoa majina ya wanafunzi 3,966 ambao ni wanufaika wa kwanza wa mkopo kwa mwaka huu wa masomo.

Mwaka wa masomo uliopita bodi ilitoa Sh. bilioni 459 kwa wanafunzi 122,486, kati yao 53,618 wakiwa ni wa mwaka wa kwanza na 68,916 ni waliokuwa wakiendelea na masomo yao.

Taarifa ya Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo),
ilisema zaidi kuwa "wajibu wa serikali yoyote duniani ni kuhakikisha
kuwa watu wake wanapata elimu.


"Serikali inayoshindwa kusomesha watu wake haina haki ya kutawala." Kamati ya Bunge ya Maendeleo na Huduma za Jamii ipo chini ya uenyekiti wa Peter Serukamba ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CCM).

VIGEZO VIPYA
Akizungumza na gazeti hili juzi, Badru alisema wanafunzi watakaopata mikopo hiyo ni wale waliokizi matakwa ya vigezo vipya vya mikopo vilivyotangazwa na serikali hivi karibuni.

Alisema wameanza kutoa mikopo kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wanaoendelea tangu juzi.

Alisema HESLB inatoa mikopo hiyo kulingana na kalenda za vyuo husika, na kwamba kwa juzi walitoa kwa vyuo vikuu vilivyokwisha fungua kama vile Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Alisema hali ya kifedha katika HESLB ni nzuri na wanafunzi wapatao 21,500 wanatarajia kunufaika na mikopo.

“Siyo kila mwanafunzi aliyedahiliwa anaweza kupata mkopo, wengine wamedahiliwa lakini wanauwezo wa kujisomesha, hivyo tutatumia vigezo mbalimbali katika kutoka mikopo,” alisema Badru.

Mbali na UDSM, Badru alisema vyuo vingine ambavyo kwa awamu ya kwanzavimepata fedha ni pamoja na Chuo Kikuu cha Ruaha (Ruco), Chuo Kikuu ChaMtakatifu Agustino (Saut), Chuo Kikuu cha Mzumbe (Muse), Chuo Kikuu cha Ardhi, Taaisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom).

Hata hivyo, Ofisa Mikopo wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino
Tanzania (SAUT), Mwanza, Wilfred Medadi alisema hadi kufikia juzi walikuwa hawajapokea fedha zozote kutoka HESLB.


Alisema Jumanne chuo kilipokea fedha za ada za wanafunzi wa mwaka wa pili na wa tatu za mwaka jana, na kwamba taarifa za wanafunzi wanaoendelea na masomo bado hazijarudishwa chuoni hapo kutoka HESLB.

CHANZO: Nipashe

28 September, 2016

Chuo Kikuu cha Oxford chaongoza ubora wa vyuo vikuu duniani

CHUO kikongwe zaidi katika ulimwengu wa nchi zinazozungumza Kiingereza na kilichotoa viongozi mashuhuri nchini Uingereza cha Oxford, kwa mara ya kwanza kimeongoza katika orodha ya vyuo vikuu duniani, lakini Makamu Mkuu wa chuo hicho ameonya kwamba Brexit inaweza kuharibu mategemeo yake ya muda mrefu.
 
Chuo hicho cha Oxford kimepiku chuo kilichokuwa kikiongoza orodha hiyo kwa miaka mitano iliyopita, cha California Institute of Technology,  ambacho kimeshika nafasi ya pili. Pia orodha hiyo imeshuhudia vyuo vikuu vya China vikipanda kwa haraka zaidi katika orodha hiyo ya vyuo vikuu bora duniani. 

Oxford, walikosoma mawaziri wakuu wane kati ya sita waliopita wa nchi hiyo, kimepiku chuo cha Marekani baada ya bajeti yake ya utafiti kuongezeka kufikia paundi bilioni 1.4 ($1.83bn), wakati matokeo ya utafiti wake ukiongezeka, anasema Phil Baty, mhariri wa orodha hiyo. 

Lakini Baty anasema kujitoa kwa Uingereza kutoka katika Jumuiya ya Ulaya “ni hatari kubwa kwa mafanikio yetu” kwa kufanya kuwa vigumu zaidi kuwavutia wanataaluma wa juu zaidi na kuwaweka katika miradi ya utafiti. 

Brexit inahatari ya kuwaondoa wanafunzi, wafanyakazi na fedha, Makamu Mkuu wa Oxford, Profesa Louise Richardson, aliiambia redio ya BBC. 

Richardson alisema kuwa vyuo vikuu vingine vimeongeza jitihada zake katika kuchukua asilimia 17 ya wafanyakazi wake ambao ni wananchi wa Jumuiya ya Ulaya, na ambao hadhi yao katika Uingereza haiwezi kuhakikiwa baada ya kura ya Juni 23. 

“Vipo vyuo vikuu vingi duniani ambavyo vitafurahi kuwa nao na vimekuwa vikijaribu kuwafuata ili kuwachukua na kuwauliza kama wanaweza kujiunga na vyuo vyao badala ya kuendelea kubaki,” alisema.
Serikali pia imeshindwa kutoa uhakika kama itafidia kiasi cha paundi milioni 67 kwa mwaka ambazo chuo hicho kimekuwa kikipokea kutoka kwa Baraza la Utafiti la Ulaya ambazo hutumika kufanya kazi za utafiti, alisema. 

“Kusema ukweli, tuna wasiwasi juu ya hilo.”
Wakati Oxford, University of Cambridge na London’s Imperial College vya Uingereza vikiwa ndani ya vyuo kumi bora duniani pamoja na chuo kikuu cha ETH Zurich, orodha hiyo imetawaliwa na vyuo vikuu vya kutoka nchini Marekani. 

Chuo Kikuu cha Stanford cha Marekani kimeshika nafasi ya tatu, wakati Massachusetts Institute of Technology, MIT kikishika nafasi ya tano, Havard nafasi ya sita, Princeton saba na Chuo Kikuu cha California, Berkeley na Chuo Kikuu cha Chicago vikifungana katika nafasi ya kumi. Vyote hivi vinatokea nchini Marekani. 

Cambridge cha Uingereza kimeshika nafasi ya nne, wakati Imperial College kikiwa cha nane na ETH Zurich nafasi ya 9.

Chuo Kikuu cha St. Andrews cha Scotland na Chuo Kikuu cha Sheffield vimeporomoka kutoka vyuo vikuu 100 bora duniani. 

Katika Ulaya, nchi za Ujerumani na Uholanzi zimeshika nafasi ya tatu na nne, ambapo Ujerumani ina vyo vipatavyo 41 katika vyo vikuu 200 bora na Uholanzi ikiwa na vyuo vikuu 13 katika orodha hiyo. 

Nchi za Ulaya Kusini kama Hispania na Italia hazijafanya vizuri kutokana na uhaba wa fedha na matatizo katika kuwapata wafanyakazi bora, Baty alisema.

Kwa upana zaidi, orodha inaonyesha taasisi katika bara ya Asia zimepiga hatua, kukiwa na vyuo viwili kutoka barani humo – Chinese University of Hong Kong na Korea Advanced Intitute of Science and Technology – vikiwa ndani ya vyuo 100 bora na vingine vinne vikiingia katika vyuo bora 200. 


Peking University kimepanda hadi nafasi ya 29 kutoka 42, na Tsinghua kikishika nafasi ya 35, kutoka nafasi ya 47 ya mwaka 2015. 

Vyuo vya Asia vinapanda, alisema Baty, wakati serikali ya China ikiingiza mabilioni ya dola katika vyuo vyake wakati huo huo, nchi za magharibi zikikabiliwa na uhaba ya bajeti. 

 Source: RAIA MWEMA

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...