Sio kila mtu anataka kua katika mahusiano kitu ambacho ni sawa kwa
asilimia 100.Lakini kuna watu ambao kila saa wanalalamika kwa kua wapo
single japokua hawajahi kujaribu kutatua naweza kusema tatizo hili. Kuna
watu inawezekana ni kweli hawajakutana na watu sahihi wa kuwa nao
lakini kunawengine huamua kuwa wa kweli kueleza ni sababu gani wapo
single.
1 . Unajibana mwenyewe na vigezo na viwango fulani
Utasikia jamaa anasema mimi nataka demu mwenye umbo zuri kama Kim
Kardashian , sasa jiulize hawa watu wako wangapi na hata kama wapo wengi
hua wana wanaume kibao wanawafukuzia. Au kwa upande wa wadada utasikia
nataka mtu mwenye gari , awe na nyumba , awe msomi , analipwa mshahara
wa kutosha kunitoa kila weekend. Watu wanaweza kukushangaza lakini
hawawezi kama utawageuzia migongo na kutowapa nafasi. Haya ni mahesabu
tu, kama ukiweka vigezo na viwango kibao vya jinsi unavyotaka mpenzi
wako aweje utabakia na watu 10 tu duniani wanaoweza kua hivyo na wewe
utakua ni mpumbavu sababu umejitengenezea mtu wa kusadikika na
unastahili kuwa single.kubali kwamba hauelewi chochote kinachoendelea
baina yako na mtu fulani na vingine vitakuja kawaida tu. Zingatia
kukutana na watu halisi , jifunze na upate kuwajua , na upime kama
unaendana nao kama watu halisi na sio watu wa kufikirika ambao hata kama
wapo inawezekana wasikutake wala kukupenda. Inauma lakini ndio ukweli
halisi.
2. Kama unataka bora inabidi na wewe uwe bora
Watu wanajipenda ambacho ni kitu cha kawaida kabisa na wanafikiria
kwamba wanaitaji mtu bora katika maisha yao lakini jiulize ili upate mtu
aliye bora haufikiri kwamba inabidi uweze kukidhi ubora wa mtu huyu
unayemtaka ? Unaposema nataka mtu mrefu , anayelipwa mshahara wa
mamilioni,anayependa watu, mwenye nyumba nzuri na gari zuri , anayeweza
kulea watoto , je ni kitu gani ambacho na wewe utakiongeza kwenye
uhusiano wako na mtu huyu? Uhusiano sio “One-way Street” kawa watasha
wanavyosemaga.Si maanishi kwamba inabidi uwe bora kabisa , hapana sema
ni muhimu kujitathmini mwenyewe na kuangalia ni kitu gani unaweza
kuchangia kama ukimpata mtu fulani. Wakati upo single una muda mwingi wa
kujifunza kuhusu wewe , sio lazima uwe bora lakini unaweza kufanya vitu
vidogovidogo kama kua msikilizaji mzuri wa maongezi , kujifunza mambo
unayopenda kufanya na kadhalika.
3. Unajipenda Sana
Ushawahi kuona watu wanaojiona kama Dhahabu , watu kama hawa hata
siku moja hawawezi kukubali kama wamekosea sehemu au wamefanya kitu
kibaya kwasababu wanajipenda sana na kujiona kwamba wao ndio bora kuliko
wengine. Kuna mda inabidi uamke usingizini na ujitambue kwamba wewe sio
bora na kwamba inabidi utoe ili upokee. kwa mfano kama wewe demu
unajijali sana na unategemea mwanaume akufukuzie , akutafute kila saa ,
aonyeshe dalili zote kwamba anakupenda wakati wewe unamwangalia tu labda
utakua hauko tayari kupenda na kujali kama watu wafanyavyo kwenye
mwanzo wa mahusiano.Sio kila saa ni kuhusu unachotaka kwani ni wakati
muafaka wa kuanza kujali na kusikiliza upande wa pili unataka nini.Watu
hua wanajua kama mtu anajisikia , kama mtu anategemea kuabudiwa na ni
kitu ambacho hakivutii kabisa.
4. Unajifungia ndani
Kuna watu wanajifungia ndani alafu wanapigia watu makelele kwamba
wapo single,sijui wanataka story kama ya cinderella. Kwa watu hawa
inabidi waamke. Kama unataka kuwa na mtu usitegemee atadondoka tu kutoka
popote.Yes, unaweza hotea lakini ukweli ni kwamba upo katika hatihati
ya kuishi peke yako maisha yako yote.Najua kutoka na kujichanganya ni
vigumu hasa kwa wale watu ambao hawapo “Comfortable” jinsi
walivyo.Kutoswa inaogopesha na inauma.Lakini unajua kitu gani hakiumi?
ni kujua kwamba umejaribu na umeweka juhudi zako zote . Kuamini kitu
unachotaka ni muhimu na kukitafuta pia.Toka nje, kutana na watu , sio
tu bar bali hata kwenye vitu mbalimbali kama movies hivi au swimming
kutokana na “hobby” yako. Kama vyote umeshindwa na bado unataka
kujifungia ndani basi fanya hata “online dating” , siku hizi kuna app ya
simu inaitwa tinder ina watoto kibao wazuri wa kibongo.
5. Haujielewi unataka nini
Hii ni muhimu sana , kama upo tayari kuwa serious katika mahusiano
basi uwe tayari kuwa serious. Kama ukikutana na mtu akaanza kusema
maneno kaka ” Sitafuti kitu serious kwa muda huu” au “Sijielewi bado
ninataka nini” basi usijidanganye na kusema ” Sawa tu , ngoja tuone
mambo yataendaje” kwani utaishia pabaya na mwisho wake kutofanikisha
malengo yako.
6. Sio mvumilivu na unakata tamaa kirahisi
labda ushajiweka mara kibao kwa wadau au umekuwa na dates mbaya
nyingi au haujajibiwa message zako. Kwa sababu fulani fulani watu
wengine hnyoosha mikono juu na kusema “Yamenishinda, hamna haja” ,
lakini ukweli ni kwamba sio kila mtu utakayekutana naye inabidi awe bora
tena ni jambo la kheri umefikiria hivyo. kwahiyo fanya kila majaribio
kama sehemu ya kupata ujuzi zaidi.