Kwa muji wa ripoti hiyo, Man
United imetoa ofa hiyo kwa Muller kwa ajili ya kumsajili na kumpa
mkataba wa miaka mitano kuitumikia klabu hiyo ya Old Trafford. Mashetani
wekundu wameweka kitita hicho cha Euro milioni 160 ikiwa ni ada ya
uhamisho pamoja na mshahara wa mchezaji huyo.
Christian Falk ametoa taarifa
hiyo kufuatia mahojiano aliyofanya na Muller kwa ajili ya gazeti la
udaku linaloitwa ‘Bild’ ambapo gazeti hilo linasema kuwa Man United
imependekeza dili hilo kwa Muller ambaye mwaka jana alitwaa kombe la
dunia akiwa na timu yake ya taifa ya Ujerumani.
Taarifa hizo za Manchester United
kupeleka ofa hiyo kwa ajili ya kumnasa Muller kutasababisha baadhi ya
mashabiki waamini kuwa klabu hiyo inaweza ikamnyakua mchezaji huyo
mwenye umri wa miaka 25.
Kuondoka kwa Radamel Falcao na
tetesi za Robin van Persie kutaka kutimka ndani ya kikosi hicho,
kutapelekea Wayne Rooney kuwa mshambuliaji pekee ambaye anatazamwa na
Manchester United kuelekea msimu ujao.
Sasa je,Manchester wangependa
kumsajili Muller? Ndiyo wanataka. Lakini je, wataweza? Ni kitu ambacho
kinaoinekana kwa sasa kinaonekana kuwa kigumui.
No comments:
Post a Comment