De Gea mwenye miaka 24 wiki hii ameonekana mjini Madrid na kuongeza uvumi zaidi kuwa anaondoka Old Trafford na kutua Bernabeu.
Kipa
huyo amesisitiza kwamba yupo Madrid kupumzika wakati huu wa likizo,
lakini anawindwa na Real Madrid ambayo mara chache sana hushindwa
kumnunua mchezaji wanayemtaka.
De Gea alijiunga na United kutokea Atletico mwaka 2011, ambapo alianza maisha yake ya soka kwa paudi milioni 18.9.
Mwaka mmoja kabla ya kuondoka Atletico, aliisaidia timu hiyo kushinda ubingwa wa Europa.
Tomas Ujfalusi ambaye alikuwa
moja ya sehemu ya safu ya ulinzi ya De Gea katika msimu huo anasema
kipa huyo anapendwa na kuheshimika kwa mashabiki wa Atletico.
Lakini anaamini atachukiwa sana kama atajiunga na Real Madrid kwasababu ataonekana kama ameisaliti Atletico.
Hali hii imemtoka Petr Cech ambaye amejiunga na Arsenal kutokea Chelsea.
Cech ameitumikia Chelsea kwa
miaka 10 ya mafanikio na alijenga heshima kubwa kwa mashabiki wa
Chelsea, lakini kitendo cha kujiunga na wapinzani wa klabu hiyo ya
darajani, kimewachukiza mno na kutishiwa kuuawa.
Usisumbuke Mawerenewz.blogspot.com ndio mtandao wako wakipekee unaokupa habari za BURUDANI,MICHEZO, SIASA, na HABARI MBALIMBALI ZA KIMATAIFA pamoja na KITAIFA Endelea kutembelea MTOKA MBALI pia nifuate twitter>>>@mawere3, facebook>>>Mawere Mtoka Mbali, Instagram>>>mawere_mtoka_mbali,
No comments:
Post a Comment