
Mshambuliaji wa klabu ya Psg Zlatan Ibrahimovic amefungiwa mechi 4
huko katika ligi ya Ufaransa kwa kosa la kuponda uendeshwaji wa ligi
hiyo.
Tukio hilo lilitokea baada ya Psg kupokea kipigo cha 3-2 kutoka kwa
Bordeaux mwezi uliopita ambapo msweden huyo alinaswa na kamera
akizungumza lugha chafu juu ya waamuzi wa mechi hiyo na huku akiitusi
nchi hiyo kwa madai ya kushindwa kuendesha soka.
Hata hivyo Ibrahimovic aliomba msamaha baada ya kufanya hivyo lakini
chama cha cha soka nchini humo kimeamua kimfungie ili iwe fundisho.
Kutokana na adhabu hiyo ,sasa Zlatan atakosa mechi za ligi dhidi ya Nice,Lille,Metz na Nantes
Hili ni pigo kubwa kwa klabu ya Psg kumkosa mshambuliaji huyo ambaye
alifunga hat trick katika mechi ya juzi dhidi ya St Etienne katika kombe
la Coup de France.
Psg ipo kileleni mwa ligi kuu nchini Ufaransa kwa tofauti ya pointi 1
na wanaoshika nafasi ya pili Lyon,huku wakiwa wamebakisha mechi 7
kumaliza ligi hiyo msimu huu.
Aidha Zlatan Ibrahimovic,33, atakosa mechi ya kwanza ya robo fainali
ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Barcelona wiki ijayo kufuatia kadi
nyekundu aliyoipata katika mechi ya pili ya hatua 16 bora dhidi ya
Chelsea
Mawerenewz.blogpot.com ndio mtandao wako wakipekee
unaokupa habari za BURUDANI,MICHEZO,SIASA, na HABARI MBALIMBALI ZA KIMATAIFA
pamoja na KITAIFA
Endelea kutembelea MTOKA MBALI pia nifuate twitter>>>@mawere3,
facebook>>>Francis mawere the jr, Instagram>>>Zawadi_mawere.
AKSANTE.