Maradhi ya zinaa yanayosambazwa miongoni mwa wapenzi wanaume wa jinsia moja inatamausha.
Haya ni kwa mjibu wa shirika la afya ya umma nchini Uingereza.Takwimu za mwaka 2014 zinanonesha kuwa
asilimia 46 ni maambukizi ya
kaswende, ilihali asilimia 32 ni maambukizi ya kisonono, huku maambukizi
ya maradhi ya "chlamydia" ikiwa kwa asilimia 26.
Ripoti hiyo inasema kuwa kumekuwa na viwango vya juu vya visa ya kufanya
ngono bila ya kutumia mipira ya kondomu, hali iliyozidisha kusambaa
zaidi kwa maambukizi ya virusi vya HIV miongoni mwa wanaume hao.
Sasa idara hiyo ya afya ya umma inapendekeza upimaji wa mara kwa mara wa maradhi ya zinaa.
Kote nchini Uingereza kwa ujumla, idadi ya maambukizi ya maradhi ya
zinaa imepungua kwa asilimia 0 nukta 3 tofauti na mwaka uliotangulia na
kufanya idadi ya walioambukizwa maradhi hayo hadi 439,243 ya visa vipya.
Kuna tofauti ya sura ya wanaume waliofanya ngono na wanaume
wenzao:Mambukizi ya ugonjwa wa kaswende yalipanda kutoka 2,375 hadi
3,477. Kisonono kiliongezeka kutoka watu 13,629 hadi 18,029
Waliopatikana na maradhi ya "chlamydia" waliongezeka kutoka 9,118 hadi
11,468 Ugonjwa wa viungo vya uzazi nao uliongezeka kwa asilimia 10
kutoka watu 3,156 hadi 3,456.
Idara ya afya ya umma nchini Uingereza inaongeza kuwa watu wote walio na
nguvu ya kufanya ngono walio chini ya umri wa miaka 25 wanafaa kupimwa
mara kwa mara kila mwaka hasa wanapowabadilisha wapenzi wa ngono.
Usisumbuke Mawerenewz.blogspot.com ndio mtandao wako wakipekee unaokupa habari za BURUDANI,MICHEZO, SIASA, na HABARI MBALIMBALI ZA KIMATAIFA pamoja na KITAIFA Endelea kutembelea MTOKA MBALI pia nifuate twitter>>>@mawere3, facebook>>>Mawere Mtoka Mbali, Instagram>>>mawere_mtoka_mbali,
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment