22 April, 2016

ELIMU YA TANZANIA YENYE MFUMO WAKIKOLONI



 Mara nyingi ukimkuta mzazi mtaani akiwa na mwanae hupenda sana kumhusia maswala ya elimu. Ni jambo jema kwa mzazi kumuasa mwanae juu ya elimu ya dunia hii maana hata vitabu vitakatifu vilivyo andika maneno ya Mwenyezi Mungu yanasema Mkamate sana elimu usimwache aende zake kwa  maana ndie mkombozi wa maisha yako. Haya yote ni mwanzo ama utangulizi wa mada yetu ya leo ambayo nimekwisha itambulisha kwako wewe mdau wangu.
    Tanzania ni moja ya nchi zilizowahi kutawaliwa na waingereza enzi zile za ukoloni na hivyo kuifanya kuwa nchi hii kuwa moja kati ya nchi za jumuia ya madola(common wealth). Kiuhalisia nchi hizi huchukua mfumo wa kiuongozi pamoja na mifumo yakielimu kutoka kwa waingereza. Tanzania ni moja kati ya nchi zinazochukua mfumo huo wa elimu kutoka kwa waingereza tangu miaka ya nyuma ambapo Tanzania ikijulikana kama Tanganyika.
Ni elimu ambayo kwa lugha yakigeni inaitwa formal education na wala sii ile ambayo wazee wetu waliipatia chini ya miti yaani informal eduction.

     Elimu ya Tanzania imekua ikionekana kuyumba kutokana na kuingiliwa na wazimu siasa ambapo kipindi cha miaka ya nyuma, elimu hii ilionekana yenye thamani na iliyodhamiria kuijenga jamii nakubadili ama kukuza uchumi wa nchi yetu kwani elimu hiyo ilijikita katika maendeleo ya jamii kwa ujumla wake. Tizama masomo yaliyo pata kufundishwa kipindi cha nyuma katika shule za msingi na hata ufundishaji wake ni tofauti na wa sasa. Watoto wa Mjini wanasema wamechakachua, yawezekana hayo yanasababishwa na utandawazi lakini bado elimu hii ya sasa hapa kwetu ni taabu tupu kulinganishwa na hapo awali.
 Elimu ya mwanzoni ilikua ikimjengea kijana mazingira yakuweza kujiajiri nakujikomboa mwenyewe katika umaskini na taabu lakini hii ya sasa imekua ni tofauti kwani kwa asilimia kubwa imekuwa ikimjengea mwanafunzi mazingira yukuajiriwa ofisi jambo ambalo limekua ngumu na tatizo kuu hapa nchini mwetu na vijana wengi hubaki bila ajira na kurudi nyuma kimaendeleo binafsi na hata maendeleo ya jamii kwa ujumla.
 
  Vijana wengi ambao hawana ajira wamezidi kuongezeka mitaani ni sababu ya msingi mibovu ya elimu yetu hapa nchini. Kijana anasoma mpaka anahitimu lakini mwisho wa siku anabaki pale pale akiranda randa mitaani na bahasha yenye vyeti kibao akitafuta kazi maofisini. Elimu iliyowahi kutolewa miaka ya nyuma ilikua ikimjenga kijana katika mazingira ambayo pindi kijana atakapokua amehitimu masomo yake unakuta teyari kijana huyo anaweza kufanya kitu pasipo kuajiriwa ofisini nikimaanisha kujiajiri.

    Kiukweli mfumo huu wa elimu tulio nao ni mbovu na naweza kusema umepitwa na wakati kwani ni wazi kwamba unamjenga kijana katika mazingira yakutegemea kuajiriwa maofisini kitu ambacho hakitakiwi.
Kwa upande wa sekondari nako ni majanga matupu kwani vijana wengi hapo ndipo ndoto zao huzima mazima. Kwa elimu yetu ni kwamba mwanafunzi akiwa shule ya msingi masomo yake yote kutoa kiingereza hufundishwa kwa Kiswahili lakini pindi anapofikia kuingia sekondari mfumo wa masomo unabadilika na masomo yote kutoa somo lakiswahili ambalo huendeshwa kwa kiswahi na mengine yote ni kiingereza kitupu. Halii hii inakua kigezo kikubwa kinachomfanya mwanafunzi kushindwa kuendena na mfumo huo nakushindwa kufanya vyema katika masomo hayo. Jambo hili linamfanya mwanafunzi kuishia kukariri pasipo kuelewa ni nini anachokifanya.
 
    Kwa upande mwingine Gharama za elimu hii ni ghali kiasi kwamba wapo baadhi ya watoto wetu kushindwa kuendelea na masomo yao. Jambo hili limekua kama chambo chakuvulia kura katika majukwaa ya siasa. Wanasiasa wengi wamekua wakitamba majukwaani kwamba endapo wakiingia madarakani watatoa elimu hii bure, jambo ambalo kiukweli wananchi wanashawishika kuwapigia kura lakini mwisho wa siku hali inabaki pale pale. Siasa za nchi hii ndio zimeharibu kabisa mfumo wa elimu yetu kiasi kwamba haifai tena katika nchi hii.

Wito wangu kwa serekali na wadau mbali mbali wa elimu hapa nchini ni wakae pamoja na kutafuta suluhisho kamili ambalo litaokoa elimu yetu na kuondoa tatizo hili la ajira kwa vijana. Vijana wapewe elimu wajiajiri na sio kungojea kupata kazi maofisini kitu ambacho hata kwenye nchi zilizoendelea Hakipo



123ContactForm | Report abuse

MISITU YETU TANZANIA TUNAFAIDIKAJE NAYO?

 
Kwanza napenda kuchukua fursa hii kumshukuru sana Mwenyezi Mungu, muumba wa mbingu na dunia na vyote vilivyomo tukiwamo sisi wanadamu, kwa mema mengi mno anayonitendea na hasa kwa kutujalia uhai hadi leo hii.
Kwa vyovyote vile bila ya Mwenyezi Mungu kutuwezesha na kututia nguvu sisi wenyewe hatuwezi, bali hali ilivyo ya kimazingira na kimaumbile tutakwama tu, hata hao wanaokwenda angani na kufanya wanayoyafanya huko si kwa uwezo wao tu, bali pia ni kwa mapenzi yake Mola

Nipende kuchua nafasi hii kukukaribisha katika makala yetu leo . Leo nitapenda kuzungumzia swala hili la Rasilimali ya Misitu tuliyojaliwa na Mwenyezi Mungu.
Katika hali ya kawaida ni kwamba Misitu tulionayo inatosha kukidhi mahitaji yetu sote tuliopo karibu na Misitu katika mambo ya uhifadhi wa wanyama pori, kupata vyanzo vya maji, upatikanaji wa mbao kwa ajili ya ujenzi na hata kupatikana kwa kuni kwa ajili ya kupikia kwa wale wengi wetu tunayotumia nishati hii ya kuni.
 Misitu ya asili ni matokeo ya kazi nzuri iliyofanywa na Mwenyezi Mungu tangu alipouumba ulimwengu, ikiwamo sayari hii tunayoishi sisi wanadamu. Kwa maneno mengine, misitu au maliasili zote tulizonazo ikiwa ni pamoja na madini, wanyamapori, samaki na viumbe wengine waishio baharini, ardhi (kwa maana ya udongo), maji (kwa maana ya vijito, mito, maziwa, mabwawa, bahari na ardhioevu), nishati mafuta na gesi asilia ni zawadi tuliyopewa na Mwenyezi Mungu.
   Kwa bahati nzuri Tanzania Bara imebahatika kuwa na eneo kubwa lenye misitu ya asili pamoja na mapori mazuri yenye utajiri mkubwa wa wanyamapori. Kwa takwimu za mwaka 1998 (ambazo sasa zimeboreshwa na matokeo ya mradi wa kitaifa wa kupima na kutathmini misitu ya asili), Tanzania ilikuwa na eneo la misitu ya asili la takribani hekta milioni 33.5.

Kati ya hizo, hekta milioni 13 ni eneo la misitu lililohifadhiwa kisheria (misitu ya hifadhi ya Serikali Kuu (Central Government Forest Reserves) takribani misitu 600 na misitu 200 ikimilikiwa na Serikali za Mitaa (Local Authority Forest Reserves) chini ya halmashauri za wilaya); na zaidi ya hekta milioni 20 ya misitu ya asili bado haijahifadhiwa na kusimamiwa kisheria.

Kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita, vijiji vichache vimeweza kutenga sehemu ya misitu katika vijiji vyao na kuitangaza kuwa misitu ya hifadhi ya vijiji yenye jumla ya hekta zaidi ya milioni saba. Hatua hiyo ni ya kupongezwa maana vijiji husika sasa vina nguvu ya kisheria kusimamia na kutumia misitu husika ipasavyo na hatimaye kunufaika na usimamizi huo, kwa kuongozwa na Sheria ya Misitu na kanuni zake.
Vilevile, vijiji vinayo fursa ya kujiwekea sheria ndogo ndogo kwa lengo la kuimarisha zaidi utekelezaji wa shughuli za kulinda msitu kwa faida yao na Taifa kwa jumla. Pamoja na mafanikio hayo, bado sehemu kubwa ya misitu ya asili ambayo haijahifadhiwa kisheria inapatikana katika maeneo ya vijiji na haitumiki ipasavyo kuviletea vijiji maendeleo endelevu.

Miaka zaidi ya 20 Serikali imekuwa ikitekeleza mpango wa Usimamizi Shirikishi wa Kutunza na Kuendeleza Misitu nchini (Participatory Forest Management-PFM). Dhana ya Ushirikishwaji ni mbinu ya uongozi inayowezesha kupata mchango wa mawazo na ushiriki mzuri kutoka kwa wadau mbalimbali, hasa katika utekelezaji wa shughuli za kujiletea maendeleo endelevu kwa kutumia rasilimali za asili tulizonazo.

Ushirikishwaji husaidia watu kubadilishana mawazo na kufahamu vizuri nini kinaendelea au kinatekelezwa kwa faida yao. Hivyo kwa kuwashirikisha wanavijiji katika masuala yanayohusu maendeleo yao vijijini ni suala muhimu sana na huondoa lawama, pia huongeza motisha wakati wa kutekeleza jambo lililoamuliwa.

Isitoshe, ni wajibu wa kila mdau kuhakikisha kuwa anawajibika ipasavyo katika kutoa mawazo na kufikia uamuzi sahihi ili lengo na madhumuni ya mipango ya maendeleo katika sehemu yao iweze kufanikiwa. Ili wanakijiji au jamii katika ujumla wake waweze kufanya hivyo, ni lazima waelimishwe vya kutosha na kuwajengea uwezo (capacity) wa kusimamia na kutumia kwa misingi endelevu rasilimali na fursa zilizopo ikiwamo misitu ya asili.

Swali lililopo ni je tunafaidika vyema na hizi faida zitokanazo na misitu tulio nayo?
Zipo faida nyingi zitokanazo na Misitu hii tuliyo nayo na faida hizo na kama vile kutumika katika maswala ya ufugaji wa nyuki, hifadhi za wanyama, upatikanaji wa nishati ya kuni na upatikanaji wa mbao ambazo tunatumia katiaka maswala ya ujenzi na maendeleo hapa nchini.
Ni ukweli ulio wazi na usiopingika ya kwamba rasilimali hii haitufaidishi ipasavyo na nathibitisha ukweli huu kwa kutumia mfano mdogo tuu wa upungufu wa MADAWATI mashuleni mwetu hasa zile za msingi. Kimsingi tusingetarajia kuona fedheha na aibu hii kubwa inayotukumba  sisi leo hii Hapa nchini Kwetu. Kuna wakati nilikua natazama taarifa ya habari nikaona habari inayo onyesha watu wa Jamhuri ya watu wa SWITZILAND wakitoa msaada wa MADAWATI katiaka shule Fulani ya msingi huko Dar-es-salaam. Jamani hivi ni kweli tumekosa miti yakuweza kutupatia hayo madawati ambayo watoto wetu wanalizimika kukaa kwenye sakafu na juu ya mawe wakati wakiwa madarasani waifundishwa?
  Huo ni mfano mdogo tuu unaonyesha ni jinsi gani bado rasilimali za misitu hapa nchini hatufaidiki nazo ipasavyo.
Maoni yangu na mapendekezo yangu ni haya juu ya swala la ukosefu wa madawati mashuleni.
Kwa sasa zipa shule nyingi za UFUNDI hapa Tanzania ambazo zinamilikiwa na serekali na baadhi ya nyingine zinamilikiwa na taasisi binafsi na point ni kwamba Kuna baadhi ya misitu mikubwa ambayo imekomaa na ambayo inaweza kutupatia mbao kwa ajili ya kutengeneza madawati yakutosha.
Kwa nini serekali isivune miti hiyo kwa mujibu washeria na ki sha kutumia ile sera ya “KATA MTI PANDA MITI  ili kurudisha miti ambayo imevunwa kwa ajili yakutengeneza madawati?
    Inawezekana kabisa kufanya hivyo na kisha mbao kupatikana ambapo mbao hizo zitipelekwa katika vyuo vya ufundi ambapo wanafunzi wanaojifunza ufundi seremala watatengeneza madawati hayo kama sehemu ya  somo  lao darasani. Ni matumaini yangu kila mkoa vyuo hivi vya ufundi vinapatikana na jambo hili linaweza kufanikiwa kwa kiasi Fulani.
Serekali Kwa kupitia wataalamu wa mambo ya misitu waandae miche yakutosha kwa ajili yakupanda sehem zitakazokua zimevunwa miti hiyo.
 Kwakufanya hivyo tutaondoa aibu na tatizo hili la ukosefu wa madawati Katika shule zetu.
 Yasije yakawa yale yaPenye miti mingi hapana wajenzi.”
  Nichukue nafasi hii kukushukuru wewe ulie chukua nafasi na muda wako kupitia makala zetu. Tafadhali ungana nami tena katika makala zetu zinazotoka kila Mwisho wa wiki.
  
      MAKALA HII IMEANDIKWA NA:-
              Francis Mawere



19 April, 2016

Things men should stop saying before sex

post-feature-image
Pleasing women has always been very tricky, even before Lord Maurice Egerton built a castle in Njoro for Lady Victoria, who was never pleased and likened it to nyumba ya kuku or mbwa! Indeed, with women, all you have to do is press the wrong button and they will be gone. Just like that! 
Matters get even trickier in the bedroom where being nervous can get men sweating profusely, mumbling incoherently for madam to turn on the lights, yet she prefers giza totoro.


Here are 10 things men should avoid telling a woman before hitting the sack:
1. I will rarua you 
When you start roaring how you will shred her into small pieces, she imagines you are endowed like a horse where it matters. But just shut up. She will compliment you if need be or you surpass her expectations.
2. I will set it on fire
No woman loves being left feeling sore after it’s over. Don’t tell her a zima moto will be needed only for you to light up half your kiberiti that is blown off even before she starts panting.
3. Are you wet
Can’t you check Men check the oil gauge of their cars, but for that, they have to ask! Yet it is part of pre-match warm up. ‘Are you wet’ is a retarded question that should be reserved for umbrella hawkers.

4. This is what you have been begging for
Why do some men make it sound like one is so desperate to indulge in ‘field events’ The whole sheet-wrinkling session is a two-way traffic.  Besides, if you really didn’t want her, how did you end up throbbing at the temples in eager anticipation

5. Does your ex know you are here
Talking about an ex, whether yours or the woman’s, is a big no-no and turn off. The only time one should talk about an ex (file) is 10 years after they’re dead, or if they owe you loads of dough. Whether the ex knows you’re the new ‘Sheriff in her town’ is  neither here nor in Suguta Valley.
6. Where do you want me to touch
Use experience, bloody moron! And if you’re a first-timer, does it mean you ploughed through high school without gaining any knowledge from movies
7. Can I unleash a ‘silencer’
Unleashing a ‘silencer’ or a thunderous ‘bazooka’, specially if you are used to each other, is part of that silly laughter being comfortable with each other brings. If you really need to fart, please go ahead, but keep in mind that nobody wants to anticipate the stench of half-cooked beans and other decaying plant proteins you have been eating.
8. Did you bring rubber
Dear men, over 50 years after independence and you still have to ask whether we carried ‘Rubber Johnny’ Just sheath your kuni!  9. Don’t tell my girlfriend
 Women are naturally jealous. So, if your chick’s best pal decides you have to kuta vitu, then never mention another woman. It is common sense, stupid!
10. Baby, I’m broke
Not unless you are saying that to a ‘night nurse’ hoping to get a discount, don’t talk about money matters in the bedroom. It not only makes you sound weak, but could also see you lose her, especially if it’s the first time Miss Babes is unleashing Venus for you. Women love men who have their lives in order. Man up!

New Music: Walter Chilambo X Raymond 'KWETU' (Cover)

Walter Chilambo X RaymondWalter Chilambo aliyekuwa mshindi wa shindano lakusaka vipaji Bongo star search mwaka 2014, katuletea ngoma ya KWETU ambayo ni cover Kutoka kwa Rymond wa Wasafi Classic ambayo ngoma hiyo imeonekana kufanya vyema katika vituo mbali mbali vya Redio na Television. Ninayo Cover hiyo hapa, chkua time yako kuisikiliza na Kumbuka kushare na wana.
Download ngoma hiyo >>HAPA<<

Sababu tano ni kwa nini Bongo flava ya Awali ilikuwa bora kuliko ya bongo Flava ya Sasa

Leo nmepanda tena hapa Mtokambali nikiwa upande mmoja na upande huo siyo mwingine bali ni ule upande wa ile bongo flava ya P-FUNK MAJANI, MWIKA MWAMBA, MJ na wakali wote waliowahi kukipia vyema katika game hii ya Bongo flava kipindi cha nyuma.Yawezekana kwa namna moja ama nyingine ukajiuliza ni kwa nini nmeamua upande hou angali Bongo flava ya sasa inaonekana kufanya vyema!

Ngoja nikupe sababu ni kwa nini nasema hivyo:-
1.Vipaji halisia vilikua huku.
Ifahamike kua sjasema wasanii wa sasa hawana vipaji laa hasha, ninaposema vipaji vya kweli vilikua kipindi cha nyuma namaanisha kuwa ubunifu wa hali ya juu ulionekana zaidi kuliko sasa, ukitaka kujua ukweli juu ya hili chukua ngoma Moja ya Bongo Flava iliyotengenezwa miaka ya 2000-2005 na uchukue ngoma ya sasa ilofanywa kuanzia 2010-016 utatambua ni kwa nini nmeitaja sababu hii.

2.Hamasa ya kweli
Kama wewe ni mpenzi wa burudani ya muziki hapa nyumbani kuanzia miaka ya 1998-2007 utakua unafahamu nachotaka kukielezea hapa, Hamasa ya kweli ilipatikana katika muziki huu sababu nyimbo zilizokua zikitungwa wakati huo zilikua zimejaa ujumbe na mafunzo tele kwa jamii na hivyo watu weengi walihamasika vilivyo (mimi ni mmoja wa hao tulio hamasika). Chukulia nyimbo kama ELIMU DUNIA, aloimba Daz-Baba, au ile ya NDIO MZEE aliyoimba Prof J na ngoma nyiingi amabazo zilikimbiza wakati ule utaona ni jinsi tulivyo pata darasa huru.

3.Production ya kweli.
Hapa nitazungumzia studio zilizokua zikitumika kurekodi ngoma hizo mfano Bongo Records, Mj, na 41 records. Hakika maproducer waliokua wakifanya kazi katika studio hizo walikua na vipaji vya hali ya juu kiasi kwamba ilikua ni vugumu msanii kukubaliwa kuingia studio moja kwa moja nakurekod bila kusota kweli na kuiva kweli kweli. Midundo (Kicks na snare)  vilikua hatari na unique. Mkono wa Producer kama Majani ulikua umebarikiwa kweli kweli na ilikua huwezi kufananisha mkono wa Majani na Mkono wa producer yeyote yule, kila mmoja alikua na ladha yake. Lakini bongo flava ya leo ni mwendo wa kukopi na kupaste tuu hakuna ubunifu.

4.Ushirikiano ulikuwako.
Jiulize ni kwa nini mwanzoni kulikuwako na makundi meengi ya muziki na yalifanya poa mno ila kwa sasa makundi hayo siku hizi hayapo na kama yakijitokeza baada ya muda mchache utasikia kundi hilo limevunjika? huu ni ushahidi tosha kua ushirikiano kwenye game la bongo flava ya sasa hakuna kabisa na ndio maana utamu wa muziki huo unazidi kupotea.

5.Muziki ulijulikana kama kipaji na sio biashara.
Hapa ndipo utabisha na kuniambia UTANDAWAZI umechangia muziki wa sasa kuonekana biashara, Kama ndio hivyo jiulize ni kwa nini kuku wa kienyeji anauzwa ghali kuliko wa kisasa? Jibu utakalokuwa nalo utaniachia kwenye comment hapo chini ila kwa sasa acha nikuambie kuwa wasanii wa hapo nyuma walifanya muziki for funy na sio kwa ajili ya biashara licha ya kuonekana wakikazana na kuuza album kwa wahindi nakujipatia kipato kidogo ila wao waliwekeza nguvu kubwa kaktika kukuza vipaji vyao maana waliamini kizuri kitajiuza na kibaya kitajitembeza.

Basi hizo ni sababu Tano(5) ni kwa nini bongo flava ya Mwazo ni bora kuliko hii ya sasa. Tukutane tena panapo majaliwa Hapa hapa MTOKAMBALI.

Ningependa uniachie maoni yako hapo chini kwenye comment box na kama una jambo lakunieleza kuhusiana na makala hii ama una swali lolote kuhusiana na makala hii niulize nitakujibu mara moja kwa kadri niwezavyo.
Tangazo

18 April, 2016

New Video: Mad Ice ‘Delilah’


Ni miongoni mwa wasanii waliofanya na wanazidi kufanya poa sana katika game hil. Licha ya Mad-Ice kukaa nje ya Bongo lakini bado ana wafuasi/mashabiki wengi hapa bongo jambo ambalo bado muziki wake unakubalika. Na safari hii katuletea video yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Delilah’ Enjoy na washirikishe washkaji kitaa.



Furaha ya kweli inaletwa na wewe mwenyewe.

Well well well! Karibu tena MTOKAMBALI, imekua kitambo sasa tangu nmeondoka hapa Mtokambali na leo nmerudi tena na nmekuja kukupatia kile ulichokikosa kutoka kwangu. Kwanza nipende kumshukuru Mwenyezi Mungu aliye hai kwa kunifanya kuiona tena siku hii nikiwa na Afya na Amani Moyoni mwangu, sii kwa akili zangu ama kwa ujanja wangu kufikia hapa nilipo ila ni kwa NEEMA tuu. Nikushukuru ewe mpenzi msomaji wa blog hii kwa kuzidi kutupatia ushirikiano wako.

Leo nmekuja na somo hili linalohusu FURAHA! hivyo nikukaribishe mpenzi msomaji kuwa nami katika somo hili na kabla ya yote nikupatie mwongozo mzima wa somo hili:
Baada ya somo hili utajifunza vitu vifuatavyo:-
1. Maana kamili ya Furaha
2.Mambo yanayokuzuia kutopata Furaha maishani mwako
3.Nini kifanyike ili kurejesha Furaha iliyo potea.

Maana kamili ya Furaha
Furaha kamili ni amani ya Moyo wako. Unajua wanadamu wengi tunashindwa kuelewa maana kamili ya neno Furaha, na matokeo yake tunaposhindwa kuipata Furaha hiyo tunaishia kutafuta furaha hiyo pasipo kuipata popote kumbe dawa ya tatito hiyo tunayo Mioyoni mwetu.

Kuna tofauti kubwa kati ya RAHA na FURAHA, raha ni Tukizo la mwili kutoka kwenye taabu na ifahamike kua raha hudumu kwa muda mchache angali Furaha hudumu Daima. Raha hutokana na Furaha.

Wacha nikupatie story kidogo juu ya Maisha yangu ya hapo awali. Kipindi nikiwa natoka utotoni na kuelekea huku ujanani nilipata tabu mno kuelewa ni FURAHA ya maisha yangu na kiukweli ilinichukua muda mwingi kupata jibu kamili juu ya swala hilo. Niliamini yakua nikiwa napenda raha za ulimwengu huu basi hapo nitakua nmemaliza kila kitu. Kwa kweli mwisho wa siku nilijipata katika hali mbaya sana nafsini mwangu hali ambayo nilikua napata msongo mkubwa wa mawazo, sikua na amani kwa kweli maana vile vyote nilivyo tamani kufanya ili kupata Furaha ya kweli nilikua nikivikosa kutokana na hali ya Umasikini niliokuwa nao. Niliumia na Ujana vilivyo na mwishowe nilivyo tafuta amani ya moyo wangu ndipo maisha yangu yakawa na FURAHA mpaka leo licha ya matatizo niliyo nayo bado nina Furaha moyoni mwangu.

Kwa maana hiyo basi tuanalie mambo ambayo yana kuzuia kupata Furaha maishani mwako
Yapo mambo mengi ambayo kwa namna moja ama nyingine yanakuzuia kupata Furaha ya kweli maishani mwako na mbo hayo yanaweza kuwa yanasababishwa na WEWE mwenyewe ama MAZINGIRA yanayo kuzunguka na mabo hayo ni kama yafuatayo.

1.Kukosa amani moyoni mwako.
Jambo hili limekua likitesa wanadamu tulio wengi hasa vijana, na hii inatokana na mambo mengi mfano Umasikini/ufukara, mapenzi, unyonyaji na hata rushwa na kutokumjua MUNGU. Unapokua na amani kwenye moyo wako, ni wazi kwamba hata akili hufunguka nakufanya mambo makubwa zaidi ya kimaendeleo na kiuchumi na hivyo maisha kuwa Murua kabisa na unapokosa amani hiyo ni wazi kua akili huvurugika nakuishia pabaya katika maendeleo yako kiuchumi na kiimani. Na mwishoni unakosa Furaha ya kweli maisha yako.

2.Kutokumjua Mungu.
Rafiki yangu kama mpaka leo Huamini kuwa Mungu yupo na kuamini kuwa yeye ndiye kila kitu katika kazi za mikono yako na maisha yako kwa ujumla basi umekwisha potea mazima. Unajua hakuna jambo zuri kama kumjua Mungu hapa duniani, Unaweza kuwa na Mali nyingi mno hapa dunia lakini bila Kumjua Mungu ni bure kabisa, utakosa mambo mengi ya muhimu mno kuliko mali ulizo nazo na Furaha ya kweli utaisikia kwa wegine huko barabarani.

3.Imani za kishirikina.
Asikufiche mtu hapa duniani hakuna watu wanaoteseka kama washirikina. Wamekua wakitabasamu katika nyuso zao wakati wakiwa kwenye makutano ya watu wengi lakini mioyoni mwao hawana amani kabisa. We mwenyewe unajiuliza iko wapi Furaha? Hivyo basi, unapokua unaamini katika mambo hayo hakika utakua umeipoteza FURAHA YA KWELI maishani mwako.

4.Wivu na husda usio na Tija.
Kuna watu huwa hawapendagi kuona mtu amepata kitu jamani katika ulimwengu huuu wa Mnyezi Mungu, wamekua wakiteseka mioyoni mwao kila kukicha kwamba "kwa nini Fulani kapata hichi?". We jiulize mtu kama huyo atakua na Furaha kweli?

5.Dhiki na changamoto za masha.
Dhiki imekua miongoni mwa changamoto za kimaisha na wengi inawapata taabu kweli kweli hapa duniani. Maandiko ya Mnyezi Mungu yanasema "Ulimwengu mna dhiki lakini jipeni Moyo". Hakuna haja yakufikiri kila siku juu ya taabu na mateso tuliyo nayo.

Hayo ni baadhi ya Mambo ambayo hutufanya wanadamu kuikosa furaha ya kweli na sasa tupate kutizama nini kifanyike ili kuirejesha Furaha iliyopotea;-

Ukiweza kutambua sababu kuu ni kwa nini unakosa furaha ya kweli basi itakua ni rahisi kutatua tatizo lako mazima. Mpende Mungu, Jiamini, Tafuta kuwa na amani ya kweli moyoni mwako, acha mambo yakishirikina, punguza wivu na Husda, Mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe, Jifunze kusamehe, shukuru kwa kila jambo.
Kwa kufanya mambo hayo yote basi utakua umejitengenezea FURAHA YA KWELI maishani mwako.

Basi ndugu zanu nimefikia mwisho wa somo langu, na nikushukuru wewe ulipendezwa na somo hili na kuamua kulipitia mwambo mwisho "Ubarikiwe Tena na Tena" nikuache na neno la Mungu kutoka katiaka kitabu kile cha Wafilipi sura ya 4 mstari wa 4 hadi ule wa 5 ambao unasema "Furahini katika Bwana tena nasema Furahini, Upole wenu na ujulikane na watu wote, Bwana yu karibu" 
Aksanteni na tukutane tena katika somo jingine hapa hapaMTOKAMBALI.



Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...