Robyn Rihanna Fenty maarufu kama Rihanna ni mwimbaji, mtunzi wa nyimbo na fashion designer anaejulikana duniani kwa nyimbo nyingi kali kama Diamonds, Four Five Seconds aliomshirikisha Kanye West na Bitch better have my money, akiwa na miaka 27 tu Rihanna alishawahi
kutajwa kama
msanii mwenye ushawishi mkubwa duniani na pia kwa kipindi
alichokuepo katika muziki ameweza kuweka ramani ya jina lake katika
entertainment industry na kukubalika na mashabiki wa kila aina duniani.
Wiki hii headlines zinazomhusu Rihanna ni
kuhusiana na yeye kupumzika kidogo kufanya muziki ili aweke nguvu na
akili yake kwenye biashara ya mitindo kwa kuanza na line yake ya
accessories itakayo kuwa inauza vitu mbali mbali kama hereni, mikufu,
pete na vitu vengine kama hivyo.
Mwezi uliyopita, Rihanna kupitia kampuni yake ya Roraj Trade LLC alisajili baadhi ya hati miliki ya bidhaa zake ikiwemo brand yake mpya $CHOOL KIlls, jina lilosajiliwa na kupwea hati miliki pamoja na alama ya biashara tarehe 11 May mwka huu jijini New York
chini ya kipengele cha Nguo na bidhaa za ngozi (Leather products and
Clothing products). Brand hii mpya itakua inatengeneza vitu vingi baadhi
vikiwa mapochi na badaae nguo.
Rihanna amesema
bado anaupenda muziki na hii haimanishi ana acha kabisa kufanya
biashara ya muziki ila kwa kipindi hiki atakua amejikita zaidi kwenye
biashara hii ya mitindo na sio muziki, ataendelea kutoa singles na
albums ila sio kwa ukasi tuliouzoea kwani anapenda pia kuwekeza kwenye
vitu vingine vya kumuingizia kipato hasa wakati huu ambao jina lake
limekua kubwa ndani ya nchi na kimataifa na anahitaji kujitangaza kwa
namna tofauti kwenye biashara tofauti anazopenda kuzifanya.
No comments:
Post a Comment