Showing posts with label Documentaries. Show all posts
Showing posts with label Documentaries. Show all posts

02 June, 2016

Lucky Dube, Mkali wa Raggea ambaye aliwahi kuishi.

 

Ninapo litaja jina la Lucky Dube ni wazi kwamba utakua unafahamu moja kwa moja namzungumzia nani. Ni moja kati ya wana harakati walio tetea haki za wanadamu hasa watu weusi walio kuwa wakibaguliwa na kuonewa kila siku kupitia sanaa ya Muziki. Kupigania Uhuru wa Africa kutoka mikononi mwa makaburu. Leo nitakupatia Historia kamili ya Mkali Huyo ikiwa ni pamoja na Historia ya maisha yake tangu kuzaliwa, safari yake ya Muziki, harakati za kupambana na Ubaguzi ulimwenguni....

Maisha yake ya Awali.

Jina lake kamili ni Lucky Philip Dude, na alizaliwa mnamo 3 August 1994 huko nchini Africa ya kusini katika eneo ambalo kwa sasa linajulikana kama Mpumalanga, awali eneo hilo lilijulikana kama Eemelo. Wazazi wake walitengana kabla ya Luck Dube Kuzaliwa, hivyo Lucky alilelewa na mama yake. Mama yake alimuita jina la LUCKY baada ya kuteseka muda mrefu bila kupata ujauzito hivyo akampatia mwanae huyo jina la LUCK(Bahati).

Akiwa na ndugu zake Thand na Patricky, Dube alikua akiishi na Bibi yake ambae ni mzaa mama kipindi chote cha udogo wake wakati mama yake akiwa kazini. Moja kati ya interview aliyo fanyiwa mnamo mwaka 1999, alieleza kwamba bibi yake ndie Kipenzsi chake, ambae alipigania yeye kuwa yeye leo hii.

safari yake ya muziki ikaanza.

Akiwa bado mdogo, Lucky alikua akifanya kazi kama gardener ila alipo kuwa mkubwa aligundua kuwa kazi ile haikuwa ya kumpatia kipato ambacho kingewezsa kutosha kuilisha familia yake, na ndipo akaamua kuanza shule ambapo shuleni huko alijinga na Kwaya na kuanza kuimba katika kwaya.

Wakati akiwa shuleni huko pia alikutana na marafiki zake ambao kwa pamoja waliamua kuunda kundi lao la muziki ambalo waliliita skyway Band. Akiwa na umri wa miaka 18, alijiunga na Band ya Binamu zake iliyo julikana kwa jina la The Love Brothers ambalo lilikua likipiga muziki aina ya Zulu Pop music wakati huo wakifanya kazi katika machimbo ya Dhahabu huko Midrand wakiwa kama walinzi na wapishi wa eneo lile.  

Kundi lile lilipata deal la kusign katika Record label ya "Teal Record Company" na hapo walipewa nafasi ya kurekodi ngoma zao ingawaje Lucky yeye bado alikua bado yupo shule ila alikua akiingia studio kipindi alipo pata likizo. Walifanikiwa kutoa Album yao ya kwanza iliyopewa jina la "Lucky Dube and the supersoul". Na ikumbukwe kwamba wakati ule ule ndio mda ambao Luck Dube alianza kujifunza Kiingereza.

Lucky ana hamia kwenye Reggea.

Kipindi Album yake ya Tano ikitoka(Mbaqunga), Dave Saga ambaye badae alikuja kuwa sound Engineer wa lucky Dube alimshauri Luck Dube kuacha zile Element alizo toka nazo kule kwenye band aliyo kuwako na Kuanza kurekodi Album zake zote zilizo fuata kwa Jina la Lucky Dube. Wakati huo Dube aligundua kwamba mashabiki wake walikua wakionyesha muitikio pale alipo kuwa akiimba nyimbo za rege katika matamasha yake. Ambapo alikua akivutiwa sana na Wasanii kama vile Peter Tosh pamoja na Jimmy Cliff wote walikua wakicheza rege. Aliona kwamba zile socio-political messages zilizo kuwa zsikkimbwa katika Jamaican Rege zingefaa kabisa katika jamii ya kibaguzi aliyo kuwa akiishi yeye Lucky Dube.

Aliamua kuazisha aina nyingine ya muziki(Rege) na alifanikiwa kutoa album iliyopewa jina la Rasters Never Die na album hiyo haikuuza sana kama ilivyo tarajiwa kwani iliuza kopi 4000 ukilinganisha na ile ya Mbaqunga iliyo ulaza Kopi 30,000. Album hiyo ilifungiwa mnamo mwaka 1985 enzi za Ubaguzi kutokana na mashairi ya Nyimbo za Album(hasa katika ule wimbo ulio julikana kwa jina la "War and Crime") hiyo kuchoma vikali serekali ya Makaburu walio kuwa wakiongoza Africa Kusini kwa kipindi kile.

Ingawaje hakukata tamaa ila aliendelea kutengeza ngoma za rege na baadae aliachilia Album ya pili iliyo pewa jina la "Think About the Childrean", album iliyo vunja Rekodi ya mauzo na kumfanya Lucy Dube kuwa mwana muziki maarufu wa Rege Africa na Ulimwenguni kote.

Biashara na mafanikio katika muziki.

Lucky Dube aliendelea kutoa album kali zilizo uza kwa wingi, na mno mwaka 1989 alifanikiwa kushinda Tuzo Nne(4) tuzo zilizo julikana kwa jina La "OKTV awards" kupitia wimbo wake wa Prisoner na baadae tena kuchukua tena tuzo nyingine kupitia Cuptured life mwaka ulio fuatia na baadae kuchukua tena tuzo mbili kupitia ngoma yake ya House of Exile. Album yake ya Victims iliuzsa zaidi ya kopi milion moja ulimwenguni kote na mnamo mwaka 1995 alipata dili la kurekodi akiwa na Motown Records.

Mnamo mwaka 1996 aliachia Albu yake iliyo mfanya kuwa juu zaidi album iliyo pewa jina la "Serius Reggae Busness", Album iliyo mfanya kujulikana kama Mwanamuziki aliyefanya mauzo Mengi ya Juu na msanii bora wa kimataifa. Album zake zote tatu zilizo fuatia zilifanikiwa kuchukua tuzo Huko Bondeni kwa Mzee Madiba.

Kifo na Mauti.

Mnamo tarehe 18,October-2007, Lucky Dube ali uawa kwa  kupigwa Risasi akiwa njiani kuwapeleka wanawe wawili kwa mjomba wao. Taarifa zilizo toka kuhusiana na Kifo chake ni kwamba,, majambazi walikuwa wakitaka kumpora gari lake hilo la Kifari aina ya Chrysler 300C. Watu watano walikamatwa kwa kuhusishwa na kifo cha Dube na watatu kati yao walipatikana na hatia na Kuhukumiwa Kifungo cha maisha Gerezani.


Na huo ndio mwisho wa Makala yangu kwa leo tafadhali nitaomba unipatie maoni amba ushauri wako kupitia anwani yangu ya mtokambali2015@gmail.com ama namba yangu +255767322193(WhatsApp only).Pia nitoe shukrani zangu kwa WIKIPEDIA kwa kufanikisha kuandika Makala hii. 

Together As One ndio Ngoma ninayo Kuacha nayo Enjoy!

25 May, 2016

Abert Mangwea Mkali wa Free-style aliye ondoka na Kipaji chake.

Hakika hujafa hujaumbika, na Mwanadamu ni uvumbi na atarudi mavumbini, Kifo na mauti havitokwepeka kwa mwanadamu/ama kiumbe chochote chenye Uhai hapa ulimwenguni.

Ikiwa week hii ni week ya kumkumbuka mkali Albert Mangea(a.k.a Mimi), yapo meengi yamepita tangu kuondoka kwake, na hasa katika game hili la Muziki wa Bongo Flava, wapo wasanii wapya pia katika game hili na muziki huu umekua na kukua kweli kweli na natamani mkali huyu ange kuwako katika enzi hizi, sipati picha.

Historia yake Kwa ufupi..

Alizaliwa na jina la Albert Keneth Mangwair mnamo tar. 16 Novemba, 1982, Mbeya, Tanzania. Kiasili, ni mtu wa Ruvuma, yaani, ni Mngoni. Lakini alizaliw mjini Mbeya na akiwa na umri wa miaka 5, familia yake ilihamia mjini Morogoro kikazi na hatimaye kuanza masomo ya msingi hukohuko mjini Morogoro hadi darasa la 5 na kupata uhamisho wa kwenda Dodoma ambapo aliweza kujiunga na shule ya msingi ya Mlimwa. Kisha baadaye shule ya Sekondari ya Mazengo na Chuo cha Ufundi cha Mazengo.

Katika ngazi ya familia, yeye ni mtoto wa mwisho (kwa baba akiwa mtoto wa 10) - na (kwa mama akiwa mtoto wa 6). Albert alifariki dunia mnamo tar. 28 Mei katika mwaka wa 2013 kwa hicho kinachoaminiwa kwamba alizidisha kipimo cha dawa za kulevya huko nchini Afrika Kusini. Ngwair aliacha mtoto mmoja.

Kazi na Muziki..

Ngwair alikuwa akiishi jijini Dar es Salaam, Tanzania ambako alikokutana na mtayarishaji mahiri wa mziki P. Funk Majani na kuanza kufanya naye kazi. Hiyo ilikuwa ni mwaka 2003 ambapo alitoa kibao cha kwanza kiitwacho 'Ghetto Langu,' wimbo uliompatia umaarufu mkubwa sana.

Mangwair pia aliwahi kushinda tuzo ya Kilimanjaro Music Awards kama mwana Hip Hop Bora wa mwaka 2005. Mwaka wa 2007 akatokea kwa wimbo wa kimya kimya akiwa na wana chemba. Katika Kimya Kimya anapagawisha.Zipo nyimbo nyingi ambazo Mangwea alitisha nazo kama Vile Gheto langu, Mikasi, CNN, she got gwan, Dakika moja, Mungu Nisamehe, na pia alipata colabo zilizo hit kama ile ya May Baby yake Quick Raka, na nyingine kibao.

Kifo na mauti...

Albert Mangwair alifariki tarehe 28/5/2013 akiwa huko Afrika ya Kusini. Taarifa zinasema alifariki baada ya kutumia madawa ya kulevya lakini kuna utata kuhusu kilichosababisha kifo cha marehemu, licha ya baadhi ya mitandao mbali mbali kuandika chanzo cha kifo cha mkali huyu ila baadae iligundulika kwamba alilewa kupindukia ilhali hakua amekula.(Rest in peace Mangwea).

 Pengo la mangwea katika Bongo Flava/Jamii...

Hakika itachukua Muda mrefu kwa pengo lake kuzibika ama hata Pengo lake kutozibika daima maana kipaji chake na mtazamo wake ulikuwa ni wa hali ya juu mno. Mashairi yake yaliburudisha, Kuelimisha jamii. Mchango wako utakumbukwa na wengi wakubwa ama wadogo, Muziki wa bongo Flava utakukumbuka kwa mchango wako mkubwa uliokua ukiutoa ili mradi tuu uone muziki huo ukisonga mbele na kukua.

Tizama Moja kati ya Video ambayo mimi naipenda kutoka kwa Mkali huyu wa free style( Kimya kimya)


Utakumbukwa na wana kibao, washkaji zako wakina J-Moe, Wana Chemba, T.I.D, Bongo Records na wengine kibao ambao walikuepo kipindi ukiwa china na hata kipindi ukiwa nazo(Marafiki wa dam dam). Mashabiki zako Tutakukumbuka kwa ngoma zako za kinyamwezi na Flow zenye mautam na zaidi ya yote tutazikumbuka zile shows zako.

Naamini ngoma zako zikipigwa club yeyote bado mzuka utakua ule ule daima.

 PUMZIKA KWA AMAN MANGWEA, MBELE YAKO NYUMA YAKO.

21 May, 2016

Ladha ya Muziki wa Dance Tanzania Inazidi kupotea.

 

Ni wazi kwamba miaka ya nyuma MUZIKII huu ulitamba sana na kila mahali ulipokua ukikatiza basi sikio lako haikosi kusikia muziki huu ila miaka hii yakizazi kipya MUZIKI WA DANCE umeonekana ukipotea licha ya BENDI tofauti tofauti kuendelea kurudishia uhai muziki huu.


    MARA nyingi nimekuwa nikijiuliza maswali mengi yasiyo na majibu pale ninapowasikia watu ambao naamini hasa ni mashabiki wa muziki wa dansi wakilalamika juu ya kupotea kwa muziki huo, licha ya kuwepo kwa bendi ambazo zinajinadi kupiga aina hiyo ya muziki hivi sasa.

   Pengine wafuatialiji hasa wa muziki huu wanaweza kutambua ukweli wa jambo hili hasa kwa kulinganisha zama hizi na zile za Dar International, Moro Jazz, Cuban Marimba Bend ,Kimulimuli JKT, Tabora Jazz, Nyanyembe Jazz na nyingine nyingi ambapo wanamuziki mahiri kama Marijani Rajabu, Mbaraka Mwinshehe, Juma Ubao,Salum Abdalah, walitamba na kuufanya muziki wa Tanzania kujulikana kimataifa.

Za Kale Ni Dhahabu by Msondo Ngoma Music Band
   Jambo la kujiuliza hapa ni kwa nini muziki wetu wakati huo ulikuwa unakubalika na jamii yote licha ya kuwa kulikuwa na upinzani mkali kutoka kwa muziki wa Zaire (sasa DRC Congo) ambayo nayo wakati huo ilikuwa na wanamuziki vigogo kama Tabu Ley, Luambo Lwanzo Makiadi (Franco) , Abeti Maskini, Mbilia Mbel, Mpongo Love, n.k.

 Ukweli wa hili utaujua ukigundua kuwa wanamuziki wa Tanzania kipindi hicho walikuwa hawapendi kuiga kutoka kwa wageni badala yake walisimama imara kupiga na kuulinda muziki wao, ndiyo maana ilikuwa vigumu kutekwa kimuziki na wageni.

 Ukirudi nyuma kidogo miaka ya 80 na 90 kulikuwa na msururu wa bendi za muziki huo hapa nchini ambapo licha ya wingi wake, zilisimama imara na kuendelea kutangaza muziki huu kimataifa zaidi ya ilivyokuwa mwanzo.


   Hakuna asiyefahamu ubora wa Bendi za Vijana Jazz wakati huo ikiwa na Hemed Maneti , Super Matimila chini ya gwiji la muziki Dk Remmy Ongara, DDC Mlimani Park ya Cosmas Chidumule, Juwata Jazz ya TX Moshi William, Tancut Almasi ya Kasaloo Kyanga na Kyanga Songa, Bima Lee ya kina Jerry Nashon ‘Dudumizi’ n.k, bendi ambazo kila moja ilipiga muziki wa dansi wa Tanzania kwa mtindo wa wake lakini bado ukawa juu kuliko ule wa kutoka nje.




Lengo letu hapa si kuzitaja bendi hizo lakini kiukweli nyingi kati ya hizo zilikuwa hazifanyi hata matangazo ya barabarani, lakini wapenzi wake walikuwa wanajua mahali ambapo zilikuwa zinafanya maonyesho na kwenda kufurahia burudani ya muziki halisi wa dansi ambao leo haupo tena.

Iko wapi leo Njata Njata , au ni wapi iliko Mwenge Jazz ‘Paselepaa’, Bantu Group ‘Kasimbagu’, Tancut Almas ‘Kinyekinye kisonzo’ ni wazi ukikumbuka haya kama ulikuwa mpenzi wa kweli wa burudani wakati huo lazima chozi litakutoka hasa ukiiona Sikinde ya sasa iliyobaki jina tu, huku ikishuhudiwa muziki wake kumezwa na aina ya muziki kutoka Congo DRC.

Kwa sasa asilimia kubwa muziki wa Tanzania imemezwa na muziki wa Kikongo, kwani kila bendi hivi sasa baada ya wimbo kuisha kinachofuata ni rap ambazo zinachukua nafasi kubwa huku zikiwa hazina ujumbe wowote zaidi ya kusifia watu

Hii ni tofauti na siku za nyuma ambapo mbali na kupata wimbo wenye mashairi mazuri yenye mafunzo kilichokuwa kinafuta baada ya wimbo kumalizika ni kuachia ufundi wa wapiga vyombo kumalizia burudani na kuwafanya mashabiki walioshiba ujumbe vichwani mwao kujimwaga ukumbini kuserebuka.

Hakika hii ilikuwa maana halisi ya dansi. Hebu tuambizane ukweli ni nani ama ni bendi ipi leo inafanya haya niende ukumbi gani ambapo sitakutana na makelele ya rapu za kumsifia mfanyabiashara fulani wa magari ambaye hana anachokijua katika muziki zaidi ya kumwaga hela ukumbini ah ah! Kazi kwli kweli!


Hakika miaka hiyo ilikuwa ya ukweli kwa dansi la Tanzania kwani mbali na ubora wa bendi na wanamuziki waliokuwa hodari wa utunzi na upigaji vyombo wakati huo pia kulikuwa na Mashindano ya kutafuta bendi bora Tanzania yaliyojulikana kama (MASHIBBOTA), mashindano ambayo kwa kiasi fulani yalikuwa nguzo ya muziki huo ambayo kwa sasa yamebaki historia.



09 May, 2016

Josee Chemelion ni nani?


Who Is Dr Jose Chameleone Moja kati ya Wana muziki nguli katika ulimwengu  wa Burudani ya Muziki kwa upande wa Africa mashariki na Africa kwa Ujumla ni Josee Chemelion.

Jina lake kamili anajulikana kama Joseph Mayanja na alizaliwa mnamo mwaka 1979 Huko nchini Uganda. Josee Chamelion alianza kazi za sanaa mnamo mika ya 1990 nakuendelea wakati akiwa sekondary na alianza kama Mc na Dj kwenye Night clubs..

Baadae alijiunga na Ogopa Djs nchini kenya na Ngoma yake ya kwanza kufanya ilikuwa ikijulikana kama "BAGEYA" mabayo alimsha Mkali mwingine kutoka kenye anaekwenda kwa jina la Red-son.
Aina ya muziki anayoimba Josee ni muunganiko wa ladha za muziki aina zouk, Rumba, na ragga na muziki kidogo kutoka pale Uganda kidogo.

Mpaka ilipo fika mwaka 2013 Chamelion alikuwa teyari ana album zipatazo 12 na album hizo ni Bageya-2000, “Mama Mia” - 2001, “Njo Karibu”- 2002, “The Golden Voice”- 2003, “Mambo Bado”-2004  “Kipepo” - 2005, "shida za dunia"-2006, "sivyo ndivyo"-2007, "Bayunga"-2009, "Vumilia"-2010, "Valu valu"-2012, Badilisha-2013.

Ni Raisi wa Ugandan Music label inayojulikana kwa jina la "Leone Island" ambayo ndani yake kuna wasanii kama Mosses Radio, Wheezle, AK 47 na wakali wengine wengi.

Ni member katika kundi la wasanii nchini Uganda ambalo wasanii hao hutumia majina yao na umaarufu wako kupinga na kupambana na umasikini pamoja na HIV/AIDS,

Tuzo alizo wahi kutwaa ni kama ifuatavyo:-

  • Beffta Awards UK – Best International Act
  • 2003 Pearl of Africa Music Awards (PAM Awards) – Artiste of the Year, Best Male Artist, Best Contemporary Artist & Song of the Year ("Mama Mia")
  • 2004 Pearl of Africa Music Awards (PAM Awards) – Artiste of the Year & Song of the Year ("Jamila")
  • 2005 Pearl of Africa Music Awards (PAM Awards) – Best Afro Beat Artiste/Group & Best Afro Beat Single ("Kipepeo")
  • 2004 Tanzania Music Awards – Best East African Album ("Bei Kali")
  • 2005 Tanzania Music Awards – Best East African Album ("Jamila")
  • 2006 Pearl of Africa Music Awards (PAM Awards) – Best Afro Beat Artiste/Group
  • 2006 Kisima Music Awards – Best Ugandan Song (Mama Rhoda) & Best Ugandan Music Video (Mama Rhoda)
  • 2007 Kisima Music Awards – Best Ugandan Song (Sivyo Ndiviyo with Professor Jay)
  • 2011 Ugandan Radio Dotcom Music Awards – Artiste of The Year
  • 2013 [Kilimanjaro Music Awards] – Best East African Song "Valu Valu"
  • 2014 [Kilimanjaro Music Awards] – Best East African Song "Tubonge"
  • 2014 HiPipo Music Awards – Song of the Year "Badilisha"
  • 2014 HiPipo Music Awards – Best Male ZOUK Song "Badilisha"
  • 2015 AFRIMA Awards - Africa Song Writer of the year 2015

Enjoy video mpya kutoka kwa  Josee Chemelion inayokwenda kwa jina la Agatako.

Hayo ni machache tuu kuhusu nguli huyu wa muziki Africa, Je una maoni gani kuhusu Blog hii? tafadhali nitumie maoni yao katika cooment box na mimi nitayafanyia kazi.

03 May, 2016

Huyu ndiye Gerald Levert

Nafahamu fika vijana wengi wanaotamba huku mitandaoni ni wale waliozaliwa miaka ya 90 nakuendelea, na naku-hakikishia ni Asilimia chache sana ya vijana walio katika kundi hili wano mfahamu huyu jamaa aliye julikana kwa jina la Gerald Levert ila kama wewe ni wale walio zaliwa miaka ya 80 basi haswaaa utakua na mimi sanjari.( ha ha haaa natania tuu bhana) but any way Jokes aside now tuje kwenye Mada yetu ya leo.

Linapo tajwa jina la wimbo Cassanova ama Baby Hold On to Me, basi hutoacha kumskia Gerald Levert hapo kati amakundi zima la O’Jays. Huyu jamaa alizaliwa mnamo July 13, 1966 huko Canton katika jimbo la Ohio nchini Marakani.Alikua ni mwana muziki na muigizaji. Na ali-zaliwa katika familia ya muziki ambapo mdogo wake Sean Levert ndie aliye husika katika kuundwa kwa kundi Lililo julikana kwa jina la LeVert.
Akiwa High school mnamo mika ya 1984, ndipo alipa amua kujiingiza moja kwa moja kwenye mziki ambapo aliungana na Mdogo wake Sean Levert akiwa na rafiki yake Marc Gordon na kuunda kundi la muziki walilolipatia jina la R&B trio LeVer.
Kundi hilo lilifanikiwa kuingia  studio nakurekodi album saba ambazo me mimi naziita "five scoring gold/platinum success" na Album hizo ni kama vile “I Get Hot” (1985), “Bloodline” (1986), “The Big Throwdown” (1987), “Just Coolin” (1988), “Rope A Dope Style” (1990), “For Real Tho” (1993) “The Whole Scenario (1997) pamoja na ngoma kali kama vile  “(Pop, Pop, Pop, Pop) Goes My Mind”, “Casanova”, “My Forever Love”, “Just Coolin” (featuring Heavy D), “Baby I’m Ready” and “ABC-123″ In 1991 the Group hit again with “Livin For The City”

Mnao mwaka 1991 Gerald aliondoka katika kundi hilo na kuamua kufanya kazi zake akiwa kama  solo artist na alifanikiwa kutengeneza album ambayo ilichukua namba moja katika chart za Bilbord album hiyo ilijulikana kwa jina la Private Line, na mwaka ulio fuatia aliachilia hit nyingine alomshirikisha baba yake na wimbo huo ulijulikana kwa jina la 'Baby Hold On to Me'. Gerald aliendelea kutoa album nyingi mpaka alipo fikia miaka ya 1990s na mwanzoni mwa miaka ya  2000s ambapo alipata collabo ya wimbo kama vile “Thinkin’ About It ulio achililiwa 1998 Funny”, “Mr. Too Damn Good to You”, “U Got That Love”, and a remake of R. Kelly’s 
“ I Believe I Can Fly”,

Gerald aliandika, kuproduce na kufanya kazi na wasanii kama vile Barry White, Stephanie Mills, Anita Baker, Eugene Wilde, Teddy Pendergrass, James Ingram, Freddie Jackson, Chuckii Booker, The Winans, Troop and The O’Jays. Na aliwahi kuonekana katika movies kama vile “Just Don’t Do It” pamoja na ile ya Always and Forever” zote hizo zilikua chini ya mkali Jamie Foxx.

Mnamo November 10, 2006, Gerald alikutwa akiwa amekufa kitandani mwake ambapoa aliyegundua kifo chake alikua ni binamu yake ambaye alikwenda kumuamsha. Kwa mara ya kwanza ili riptiwa kuwa kilicho muua nguli huyo ni matatizo ya moyo(heart attack) lakini taarifa kamili ya kifo chake ilitoka mwaka 2007 mwezi February ikieleza kua Gerald Aliji-overdoze na madawa. Na mwishoni ikafahamika kuwa ni sumu ya dawa hizo ili zidi kwenye damu. Alifariki na maika 40 tuu na aliacha mke na watoto watatu.

Aliacha albu yake ilokwenda kwa jina la “In My Songs” ikiwa bado jikoni iliyo achiliwa mwaka 2007 chini ya familia yake. Pamoja na Manaement iliyo kuwa ikimsimamia.

                 Tizama moja ya kazi zake huyu jamaaakiwa na kundi la LSG.


Kwa kifupi hiyo ni historia ya nguli huyo wa muziki aliye wahi kuishi ila teyari keshatangulia mbele za haki ambako mimi na wewe tutakwenda siku moja (R.I.P).

Unaweza kujipatia makala hii na makala zetu moja kwa moja kwenye simu yako kila ifikapo week-end Bure kabisa. Unacho takiwa kukifanya ni kujaza Fomu unayo iona hapo chini...

PITIA NA HIZI:-

>> Oliver Mtukudzi picha Halisi ya Muziki wa Kiafrica.
>> unalifahamu-kundi-la-ub40? 
>> Wafahamu madancer Albir Rojas na Sara Lopez wakali wa 'Kizomba dance'



Jiunge na watu 3000 walio chagua MTOKAMBALI ili kupata Makala zinazo chapishwa Hapa hapa MTOKAMBALI na kuja kwako moja kwa moja kupitia Emai yako kila week-End BURE!!

* indicates required

27 April, 2016

Oliver Mtukudzi picha Halisi ya Muziki wa Kiafrica.


Linapotajwa jina la wimbo wa "Neria" basi kila mmoja wetu atakua na mawazo mawili tofauti ambayo yote humuongelea Nguli wa muziki wa Kiafrica na sio mwingine ni Oliver Mtukudzi kutoka kule Zimbabwe kwa mbabe Robert Mugabe.
Jina la utani huwa wanamuita "TUKU" ambapo jina hilo limetokana na jina Mtukudzi hivyo akaamua kufupisha jina lake hilo na kupata hiyo a..ka. amezaliwa mnamo 22 Septemba 1952 mjini Highfield, Harare) ni mwanamuziki wa Kizimbabwe. Oliver ni miongoni mwa wanamuziki walio maarufu kwa muda mrefu sana katika nchi hiyo ya Zimbabwe. Na alianza shughuli za muziki kunako miaka ya 1977 pale alipojiunga na bendi ya Wagon Wheels, ambayo pia alikuwemo na mwanamuziki wa zamani Bw. Thomas Mapfumo.

   Nyimbo ya kwanza ilikuwa "Dzandimomotera" iliyoheshimika sana, na hapo ndipo Tuku alipotoa albamu yake ya kwanza, nayo pia ilileta mafanikio makubwa kabisa. Mtukudzi nae pia ni mmoja wa wanakundi la Mahube, kundi la muziki la nchi za Afrika ya Kusini.

Oliver pia ni baba wa watoto watano na wajukuu wawili, wawili hao pia ni wanamuziki. Ana dada zake wanne na kaka mmoja ambaye tayari amekwisha fariki. Anafurahia kuogelea katika bwawa lake la kuogelea (swimming pool) ambalo lina umbo la gitaa. Oliver ametoa zaidi ya albamu 40 na amepata kushinda tuzo nyingi mno na hata zingine hawezi kuzikumbuka.
   
Filamu alizoshiriki:
  • Jit (mwong. Michael Raeburn , 1990)
  • Neria (mwong. Goodwin Mawuru, imetungwa na Tsitsi Dangarembga, 1993). Mtukudzi ndiyo alikuwa nyota wa filamu na yeye ndiye aliotengeneza nyimbo ya filamu.
  • Shanda (mwong. John na Louise Riber, 2002, rev. 2004)
 Tuzo alizowahi kushiriki na kushinda.
  • Tuzo ya KORA kwa ajili ya matayarisho mazuri ya nyimbo yake ya Ndakuwara mnamo mwaka wa 2002
  • Tuzo ya National Arts Merit (NAMA) mnamo mwaka wa 2002 na 2004 kama kundi bora la muziki/ mwanamuziki bora wa kiume
  • Tuzo ya KORA kama mwanamuziki bora wa kiume wa Africa na tuzo ya Lifetime Achievement mnamo mwezi Agosti wa mwaka wa 2003
  • Tuzo ya Reel kama lugha bora ya Kiafrica mnamo wamaka wa 2003
  • An honorary degree from the University of Zimbabwe in Desemba 2003
  • Tuzo za M-Net Best kama nyimbo bora ya filamu mnamo 1992, kwa ajili ya filamu ya Neria.

Tafadhali pitia na Hizi zifuatazo.
 1.Wafahamu madancer Albir Rojas na Sara Lopez wakali wa 'Kizomba dance'
 2. Sababu tano ni kwa nini Bongo flava ya Awali ilikuwa bora kuliko ya bongo 








24 April, 2016

Wafahamu madancer Albir Rojas na Sara Lopez wakali wa 'Kizomba dance'

Well! well! well!.. Leo nmepanda hapa MTOKAMBALI kivingine kabisa japo bado niko kule kule kwenye Burudani na Leo nitawapatia angalao Biography ya wakali hawa wa dance ulimwenguni. Linapotajwa jina la 'Kizomba' basi kila mmoja haachi kumfkiria Albir Rojas  na Sara Lopez maana wakali hawa ndio wenye KIZOMBA DANCE.

Nianze na Albir Rojas:-
Ni  dancer, choreographer, actor na ni professor.
 Alizaliwa mnamo 25th mwezi October 1979 huko PANAMA na mama yeke kumpatia jina la Albir ambalo hakutaka mwanae kuchakachua jina hilo kamwe, na mama yake aliamua hivyo sababu kuna siku mama yake huyo alikwenda nchini India nakumkuta mama mmoja akimwita mwanae wa kiume "Albir" kisha akamuuliza mama huyo wa kihindi jina hilo lina maana gani? basi mama yule wa kihindi akajibu "BRAVE" na ndipo mama yake dancer huyu akaamua kumpatia jina hilo.

Wakati akiwa mdogo wa umri mika 12, mama yake alikua akimfundisha dancing japokua wakati huo jamaa huyu alikua havutiwi na dancing na badala yake alikua akivutiwa na Video games na akaendelea na video games pamoja na dancing mpaka akiwa na umri wa miaka 14 wakati alipokuwa High school.
Akiwa high  school alialikwa kushiriki kwenye choreography na hapo ndipo Albir akaamua kuikubali DANCING na kuanza kuifanyia kazi. Akiwa na umri wa mika 16, alijiunnga na darasa ladance katika funky dance school na huko alikua akijifunza mambo mengi kuhusiana na choreography.
 Albir alimaliza high school akiwa na umri wa miaka 18 na lifanikiwa kutoka na Bachelor of Commerce degree (Accounting).

Baada ya kumaliza masomo yake alipata kazi akiwa kama accountant na huku alikua pia akisoma masomo yake ya shahada ya uzamivu katika maswala hayo hayo ya biashara. Albir alikua akiutesa mwili wake kwa kazi mno maana hasubuhi alikua akienda kazini na jioni alikua akihudhuria darasani na usiku alikua akifanya mazoezi ya dance jambo ambalo mwili wake kuna muda uluonekana kuchoka.
Licha ya hivyo jamaa huyo hakukata tamaa na aliamua kuacha kazi ofisini na kuamua Kuifanya sanaa kwa ujumla kipindi chote cha cha maisha yake.

Albir alikua katika dancing mwaka hadi mwaka na aliwahi kuonekana katika kazi kama Grease, the King and I, Fame, West Side Story na Fantastics, kote huko alikua kama Actor na dancer.
Aliamua kwenda  Madrid kwa ajili ya masomo yahusuyo Communication, Advertising, Film making and Sound Technician na alimaliza na akamua kuishi Madrid tangu mwaka 2001 mpaka leo.

Albir amekua akifundisha dancing styles kama cuban salsa, salsa in line, bachata dominicana, bachata madrid, hip hop, popping, KIZOMBA, TARRAXINHA, SEMBA and ballroom dances ambazo yeye ni MASTER wa Style hizo.
Albir anapenda anachokifanya na hua anapenda kushirikisha feelings zake kwa watu wapenda dancing mfano Mimi ( ha ha ha haa).

Nije kwa bibie Sara López:-
AlbirRojas2Mwana dada huyu ni mzaliwa  Madrid, Spain na alizaliwa mnamo mwaka 1986. Alianza dancing akiwa na umri mdogo wa miaka 5 na alitumia miaka 7 kujifunza dance katika ballet, contemporary dance, modern dance, hiphop. na akiwa na umri wa miaka 16 alinza na Latin dances, Salsa, Bachata pamoja na Kizomba.

Akiwa na umri wa mika 18 tuu, akawa amemaliza elimu yake ya  Sekondary na akaamua kwenda Madrid kwa ajili ya kujifunza classical ballet. Huko alikaa kwa muda wa mika mitatu zaidi akiwa akijifunza tena Latin rhythms.
Alipata dancing partner wake wa kwanza nchini humo aliyejulikana kama Ronald Jara ambaye alionekana nae katika mashindano ya dancing Madrid in Africadançar (Lisbon Ureno) mnamo mwaka 2012.
na baadae akatambulishwa kwa Mkali Albir ambaye walionekana kufanya kazi kwa pamoja hadi mwaka 2014 walipo achana.

Ikumbukwe kuwa Dancers hawa hawakuwahi kuwa wapenzi kamwe licha ya watu wengi ulimwenguni kufahamu kuwa walikua wapenzi. Nikupatie angalao video moja ya wakali hawa wakifanya vitu vyao katika KIZOMBA.

Mpaka hapo sina la ziada nikutakie siku njema na tukutane tena Juma lijalo hapa hapa MTOKAMBALI,







Mtokambali |

22 April, 2016

ELIMU YA TANZANIA YENYE MFUMO WAKIKOLONI



 Mara nyingi ukimkuta mzazi mtaani akiwa na mwanae hupenda sana kumhusia maswala ya elimu. Ni jambo jema kwa mzazi kumuasa mwanae juu ya elimu ya dunia hii maana hata vitabu vitakatifu vilivyo andika maneno ya Mwenyezi Mungu yanasema Mkamate sana elimu usimwache aende zake kwa  maana ndie mkombozi wa maisha yako. Haya yote ni mwanzo ama utangulizi wa mada yetu ya leo ambayo nimekwisha itambulisha kwako wewe mdau wangu.
    Tanzania ni moja ya nchi zilizowahi kutawaliwa na waingereza enzi zile za ukoloni na hivyo kuifanya kuwa nchi hii kuwa moja kati ya nchi za jumuia ya madola(common wealth). Kiuhalisia nchi hizi huchukua mfumo wa kiuongozi pamoja na mifumo yakielimu kutoka kwa waingereza. Tanzania ni moja kati ya nchi zinazochukua mfumo huo wa elimu kutoka kwa waingereza tangu miaka ya nyuma ambapo Tanzania ikijulikana kama Tanganyika.
Ni elimu ambayo kwa lugha yakigeni inaitwa formal education na wala sii ile ambayo wazee wetu waliipatia chini ya miti yaani informal eduction.

     Elimu ya Tanzania imekua ikionekana kuyumba kutokana na kuingiliwa na wazimu siasa ambapo kipindi cha miaka ya nyuma, elimu hii ilionekana yenye thamani na iliyodhamiria kuijenga jamii nakubadili ama kukuza uchumi wa nchi yetu kwani elimu hiyo ilijikita katika maendeleo ya jamii kwa ujumla wake. Tizama masomo yaliyo pata kufundishwa kipindi cha nyuma katika shule za msingi na hata ufundishaji wake ni tofauti na wa sasa. Watoto wa Mjini wanasema wamechakachua, yawezekana hayo yanasababishwa na utandawazi lakini bado elimu hii ya sasa hapa kwetu ni taabu tupu kulinganishwa na hapo awali.
 Elimu ya mwanzoni ilikua ikimjengea kijana mazingira yakuweza kujiajiri nakujikomboa mwenyewe katika umaskini na taabu lakini hii ya sasa imekua ni tofauti kwani kwa asilimia kubwa imekuwa ikimjengea mwanafunzi mazingira yukuajiriwa ofisi jambo ambalo limekua ngumu na tatizo kuu hapa nchini mwetu na vijana wengi hubaki bila ajira na kurudi nyuma kimaendeleo binafsi na hata maendeleo ya jamii kwa ujumla.
 
  Vijana wengi ambao hawana ajira wamezidi kuongezeka mitaani ni sababu ya msingi mibovu ya elimu yetu hapa nchini. Kijana anasoma mpaka anahitimu lakini mwisho wa siku anabaki pale pale akiranda randa mitaani na bahasha yenye vyeti kibao akitafuta kazi maofisini. Elimu iliyowahi kutolewa miaka ya nyuma ilikua ikimjenga kijana katika mazingira ambayo pindi kijana atakapokua amehitimu masomo yake unakuta teyari kijana huyo anaweza kufanya kitu pasipo kuajiriwa ofisini nikimaanisha kujiajiri.

    Kiukweli mfumo huu wa elimu tulio nao ni mbovu na naweza kusema umepitwa na wakati kwani ni wazi kwamba unamjenga kijana katika mazingira yakutegemea kuajiriwa maofisini kitu ambacho hakitakiwi.
Kwa upande wa sekondari nako ni majanga matupu kwani vijana wengi hapo ndipo ndoto zao huzima mazima. Kwa elimu yetu ni kwamba mwanafunzi akiwa shule ya msingi masomo yake yote kutoa kiingereza hufundishwa kwa Kiswahili lakini pindi anapofikia kuingia sekondari mfumo wa masomo unabadilika na masomo yote kutoa somo lakiswahili ambalo huendeshwa kwa kiswahi na mengine yote ni kiingereza kitupu. Halii hii inakua kigezo kikubwa kinachomfanya mwanafunzi kushindwa kuendena na mfumo huo nakushindwa kufanya vyema katika masomo hayo. Jambo hili linamfanya mwanafunzi kuishia kukariri pasipo kuelewa ni nini anachokifanya.
 
    Kwa upande mwingine Gharama za elimu hii ni ghali kiasi kwamba wapo baadhi ya watoto wetu kushindwa kuendelea na masomo yao. Jambo hili limekua kama chambo chakuvulia kura katika majukwaa ya siasa. Wanasiasa wengi wamekua wakitamba majukwaani kwamba endapo wakiingia madarakani watatoa elimu hii bure, jambo ambalo kiukweli wananchi wanashawishika kuwapigia kura lakini mwisho wa siku hali inabaki pale pale. Siasa za nchi hii ndio zimeharibu kabisa mfumo wa elimu yetu kiasi kwamba haifai tena katika nchi hii.

Wito wangu kwa serekali na wadau mbali mbali wa elimu hapa nchini ni wakae pamoja na kutafuta suluhisho kamili ambalo litaokoa elimu yetu na kuondoa tatizo hili la ajira kwa vijana. Vijana wapewe elimu wajiajiri na sio kungojea kupata kazi maofisini kitu ambacho hata kwenye nchi zilizoendelea Hakipo



123ContactForm | Report abuse

MISITU YETU TANZANIA TUNAFAIDIKAJE NAYO?

 
Kwanza napenda kuchukua fursa hii kumshukuru sana Mwenyezi Mungu, muumba wa mbingu na dunia na vyote vilivyomo tukiwamo sisi wanadamu, kwa mema mengi mno anayonitendea na hasa kwa kutujalia uhai hadi leo hii.
Kwa vyovyote vile bila ya Mwenyezi Mungu kutuwezesha na kututia nguvu sisi wenyewe hatuwezi, bali hali ilivyo ya kimazingira na kimaumbile tutakwama tu, hata hao wanaokwenda angani na kufanya wanayoyafanya huko si kwa uwezo wao tu, bali pia ni kwa mapenzi yake Mola

Nipende kuchua nafasi hii kukukaribisha katika makala yetu leo . Leo nitapenda kuzungumzia swala hili la Rasilimali ya Misitu tuliyojaliwa na Mwenyezi Mungu.
Katika hali ya kawaida ni kwamba Misitu tulionayo inatosha kukidhi mahitaji yetu sote tuliopo karibu na Misitu katika mambo ya uhifadhi wa wanyama pori, kupata vyanzo vya maji, upatikanaji wa mbao kwa ajili ya ujenzi na hata kupatikana kwa kuni kwa ajili ya kupikia kwa wale wengi wetu tunayotumia nishati hii ya kuni.
 Misitu ya asili ni matokeo ya kazi nzuri iliyofanywa na Mwenyezi Mungu tangu alipouumba ulimwengu, ikiwamo sayari hii tunayoishi sisi wanadamu. Kwa maneno mengine, misitu au maliasili zote tulizonazo ikiwa ni pamoja na madini, wanyamapori, samaki na viumbe wengine waishio baharini, ardhi (kwa maana ya udongo), maji (kwa maana ya vijito, mito, maziwa, mabwawa, bahari na ardhioevu), nishati mafuta na gesi asilia ni zawadi tuliyopewa na Mwenyezi Mungu.
   Kwa bahati nzuri Tanzania Bara imebahatika kuwa na eneo kubwa lenye misitu ya asili pamoja na mapori mazuri yenye utajiri mkubwa wa wanyamapori. Kwa takwimu za mwaka 1998 (ambazo sasa zimeboreshwa na matokeo ya mradi wa kitaifa wa kupima na kutathmini misitu ya asili), Tanzania ilikuwa na eneo la misitu ya asili la takribani hekta milioni 33.5.

Kati ya hizo, hekta milioni 13 ni eneo la misitu lililohifadhiwa kisheria (misitu ya hifadhi ya Serikali Kuu (Central Government Forest Reserves) takribani misitu 600 na misitu 200 ikimilikiwa na Serikali za Mitaa (Local Authority Forest Reserves) chini ya halmashauri za wilaya); na zaidi ya hekta milioni 20 ya misitu ya asili bado haijahifadhiwa na kusimamiwa kisheria.

Kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita, vijiji vichache vimeweza kutenga sehemu ya misitu katika vijiji vyao na kuitangaza kuwa misitu ya hifadhi ya vijiji yenye jumla ya hekta zaidi ya milioni saba. Hatua hiyo ni ya kupongezwa maana vijiji husika sasa vina nguvu ya kisheria kusimamia na kutumia misitu husika ipasavyo na hatimaye kunufaika na usimamizi huo, kwa kuongozwa na Sheria ya Misitu na kanuni zake.
Vilevile, vijiji vinayo fursa ya kujiwekea sheria ndogo ndogo kwa lengo la kuimarisha zaidi utekelezaji wa shughuli za kulinda msitu kwa faida yao na Taifa kwa jumla. Pamoja na mafanikio hayo, bado sehemu kubwa ya misitu ya asili ambayo haijahifadhiwa kisheria inapatikana katika maeneo ya vijiji na haitumiki ipasavyo kuviletea vijiji maendeleo endelevu.

Miaka zaidi ya 20 Serikali imekuwa ikitekeleza mpango wa Usimamizi Shirikishi wa Kutunza na Kuendeleza Misitu nchini (Participatory Forest Management-PFM). Dhana ya Ushirikishwaji ni mbinu ya uongozi inayowezesha kupata mchango wa mawazo na ushiriki mzuri kutoka kwa wadau mbalimbali, hasa katika utekelezaji wa shughuli za kujiletea maendeleo endelevu kwa kutumia rasilimali za asili tulizonazo.

Ushirikishwaji husaidia watu kubadilishana mawazo na kufahamu vizuri nini kinaendelea au kinatekelezwa kwa faida yao. Hivyo kwa kuwashirikisha wanavijiji katika masuala yanayohusu maendeleo yao vijijini ni suala muhimu sana na huondoa lawama, pia huongeza motisha wakati wa kutekeleza jambo lililoamuliwa.

Isitoshe, ni wajibu wa kila mdau kuhakikisha kuwa anawajibika ipasavyo katika kutoa mawazo na kufikia uamuzi sahihi ili lengo na madhumuni ya mipango ya maendeleo katika sehemu yao iweze kufanikiwa. Ili wanakijiji au jamii katika ujumla wake waweze kufanya hivyo, ni lazima waelimishwe vya kutosha na kuwajengea uwezo (capacity) wa kusimamia na kutumia kwa misingi endelevu rasilimali na fursa zilizopo ikiwamo misitu ya asili.

Swali lililopo ni je tunafaidika vyema na hizi faida zitokanazo na misitu tulio nayo?
Zipo faida nyingi zitokanazo na Misitu hii tuliyo nayo na faida hizo na kama vile kutumika katika maswala ya ufugaji wa nyuki, hifadhi za wanyama, upatikanaji wa nishati ya kuni na upatikanaji wa mbao ambazo tunatumia katiaka maswala ya ujenzi na maendeleo hapa nchini.
Ni ukweli ulio wazi na usiopingika ya kwamba rasilimali hii haitufaidishi ipasavyo na nathibitisha ukweli huu kwa kutumia mfano mdogo tuu wa upungufu wa MADAWATI mashuleni mwetu hasa zile za msingi. Kimsingi tusingetarajia kuona fedheha na aibu hii kubwa inayotukumba  sisi leo hii Hapa nchini Kwetu. Kuna wakati nilikua natazama taarifa ya habari nikaona habari inayo onyesha watu wa Jamhuri ya watu wa SWITZILAND wakitoa msaada wa MADAWATI katiaka shule Fulani ya msingi huko Dar-es-salaam. Jamani hivi ni kweli tumekosa miti yakuweza kutupatia hayo madawati ambayo watoto wetu wanalizimika kukaa kwenye sakafu na juu ya mawe wakati wakiwa madarasani waifundishwa?
  Huo ni mfano mdogo tuu unaonyesha ni jinsi gani bado rasilimali za misitu hapa nchini hatufaidiki nazo ipasavyo.
Maoni yangu na mapendekezo yangu ni haya juu ya swala la ukosefu wa madawati mashuleni.
Kwa sasa zipa shule nyingi za UFUNDI hapa Tanzania ambazo zinamilikiwa na serekali na baadhi ya nyingine zinamilikiwa na taasisi binafsi na point ni kwamba Kuna baadhi ya misitu mikubwa ambayo imekomaa na ambayo inaweza kutupatia mbao kwa ajili ya kutengeneza madawati yakutosha.
Kwa nini serekali isivune miti hiyo kwa mujibu washeria na ki sha kutumia ile sera ya “KATA MTI PANDA MITI  ili kurudisha miti ambayo imevunwa kwa ajili yakutengeneza madawati?
    Inawezekana kabisa kufanya hivyo na kisha mbao kupatikana ambapo mbao hizo zitipelekwa katika vyuo vya ufundi ambapo wanafunzi wanaojifunza ufundi seremala watatengeneza madawati hayo kama sehemu ya  somo  lao darasani. Ni matumaini yangu kila mkoa vyuo hivi vya ufundi vinapatikana na jambo hili linaweza kufanikiwa kwa kiasi Fulani.
Serekali Kwa kupitia wataalamu wa mambo ya misitu waandae miche yakutosha kwa ajili yakupanda sehem zitakazokua zimevunwa miti hiyo.
 Kwakufanya hivyo tutaondoa aibu na tatizo hili la ukosefu wa madawati Katika shule zetu.
 Yasije yakawa yale yaPenye miti mingi hapana wajenzi.”
  Nichukue nafasi hii kukushukuru wewe ulie chukua nafasi na muda wako kupitia makala zetu. Tafadhali ungana nami tena katika makala zetu zinazotoka kila Mwisho wa wiki.
  
      MAKALA HII IMEANDIKWA NA:-
              Francis Mawere



Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...