25 December, 2015

RONALDO APATA MAPOKEZI BABKUBWA NBA

Mshambuliaji Cristiano Ronaldo wa miamba ya soka ya nchini Hispania Real Madrid ametumia fursa ya mapumziko ya sikukuu za krismasi kutembelea nchini Marekani ambapo alitokea katika mechi ya mpira wa kikapu nchini humo NBA Kati ya Miami Heat na Detroit Pistons.
Star 1
Cristiano Ronaldo ambaye ndiye mwanasoka tajiri zaidi hivi sasa alipokelewa kwa mapokezi mazuri huku akikabidhiwa jezi ya Miami Heat iliyokuwa imechapishwa jina lake mgongoni, sanjari na namba 7 kuonesha heshima kubwa aliyonayo staa huyo raia wa Ureno.
Star 2
Ronaldo alikabidhiwa jezi hiyo pamoja na kushiriki utani na stori pamoja na mchezaji wa kikapu wa NBA mwingereza Luol Deng ambaye alifunga points 9 katika dakika 33 alizocheza Jumanne hii na baadae kushiriki stori na Cristiano.
Star 3
Katika mechi hiyo Miami walipoteza kwa taabu kwa points 93 kwa 92 katika mchezo uliokua mkali na wakuvutia, huku mashabiki wakifurahia uwepo wa staa huyo wa soka na mshindi wa Ballon d’Or mara 3.
Star 6
Baadaye Cristiano Ronaldo kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika kumshukuru Luol Deng mwingereza ambaye pia ni shabiki wa kutupwa wa Arsenal, pamoja na kuishukuru klabu ya Miami kwa ukarimu wao.
Star 7
Cristiano bado yuko nchini Marekani akijipumzisha kwa ajili ya Christmas kwani bado Ana muda wa kutosha kabla ya kurudi Hispania kwa ajili ya muendelezo wa ligi kuu nchini humo pamoja na michuano mingine.
Star 4
Star 5

MBWANA SAMATTA ATUA UBELGIJI KUKAMILISHA USAJILI

Samatta-JPN 6
Taarifa kutoka nchini Ubelgiji zinasema kwamba, mchezaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga kwenye klabu ya TP Mazembe ya nchini Congo DR Mbwana Samatta muda wowote anaweza kujiunga na klabu ya Genk inayoshiriki ligi kuu nchini Ubelgiji (Belgian Pro League).
Kwa muda mrefu sana kulikuwa na harakati za Mbwana Samatta kujiunga na vilabu vya Ulaya, klabu ya Genk ya Ubelgiji kwa asilimia nyingi ipo kwenye dakika za mwisho kukamilisha deal la kumsajili Mbwana Samatta kutoka TP Mazembe.
Genk ipo nafasi ya sita (6) kwenye msimamo wa ligi kuu ya soka nchini Ubelgiji ikiwa imecheza michezo 20 na kufanikiwa kukusanya jumla ya pointi 28 hadi sasa.
Moise Katumbi ambaye alikuwa anaonekana kama kikwazo yupo Ubelgiji na jana alikuwa anafanya mazungumzo na timu ya Genk na kufikia makubaliano ambapo na yeye pia amekubali kumruhusu Mbwana Samatta.
Dirisha dogo la usajili kwa vilabu vya Ulaya litakapofunguliwa mwezi January Samatta atatua Belgium kujiunga na klabu hiyo.
Samatta amebakiza mkataba wa miezi minne pekee kuendelea kusalia kwenye klabu yake ya TP Mazembe ambayo msimu huu ameisaidia kutwaa kombe la klabu bingwa Afrika.

Miss Colombia atoa ya moyoni kuhusu kuporwa ushindi wa Miss Universe

post-feature-image
Baada ya shindano la Miss Universe lililofanyika Jumapili iliyopita (Dec 20) kukumbwa na dosari ya MC kukosea kumtaja mshindi, Miss Colombia ambaye alitangazwa mshindi na dakika chache baadaye kupigwa na butwaa baada ya MC Steve Harvey kurudi na kutangaza kuwa alipewa ushindi kimakosa, hatimaye mrembo huyo ametoa ya moyoni na kumpongeza mshindi wa mwaka huu Miss Ufilipino.

Kupitia Instagram yake Miss Colombia , Ariadna Gutierrez aliandika ujumbe mrefu wa kugusa kuhusu kilichotokea, akieleza kuwa sasa moyo wake umetulia na maisha lazima yaendelee. Pia akagusia kwamba huko mbele ya safari itakuja kufahamika kwanini mambo yalitokea vile yalivyotokea, na akamaliza kwa kuwapongeza Wafilipino kwa kupata Miss Universe mpya Pia Alonzo Wurtzbach .
After the storm comes the calm. I want to thank each and everyone of you who have sent messages of support and strength. Every one of you has become an incredible human being in my book and I am the most fortunate and thankful for having the support not only from one country but from the whole entire world. Your destiny is written for you. And my destiny was this. I was able to bring happiness to my country after becoming Miss Universe for only a couple of minutes... Today because of that COLOMBIA and the LATIN COMMUNITY are being talked about in every corner of the world. I also want to congratulate the Philippines for their new Miss Universe 🙏🏼. The happiness that you must be feeling must be incredible. Life continues and in the future we will find out why things happen the way they happen. Thank you all for your LOVE SUPPORT and KINDNESS. ❤️
A photo posted by Ariadna Gutierrez Arevalo (@gutierrezary) on
Huu ndio ujumbe wake: "After the storm comes the calm. I want to thank each and everyone of you who have sent messages of support and strength. Every one of you has become an incredible human being in my book and I am the most fortunate and thankful for having the support not only from one country but from the whole entire world. Your destiny is written for you. And my destiny was this. I was able to bring happiness to my country after becoming Miss Universe for only a couple of minutes... Today because of that COLOMBIA and the LATIN COMMUNITY are being talked about in every corner of the world. I also want to congratulate the Philippines for their new Miss Universe ����. The happiness that you must be feeling must be incredible. Life continues and in the future we will find out why things happen the way they happen. Thank you all for your LOVE SUPPORT and KINDNESS. ❤️"
post-feature-imageJeshi la Polisi mkoani Arusha linawashikilia watu wanne wakiwemo mke wa marehemu dereva na mtunza bustani kwa tuhuma za mauaji ya aliekuwa mkuu wa kitengo cha ulinzi na usalama wa shirika la hifadhi za Tanapa Emili Kisamo aliyeuwawa kwa kukatwa shingo na kutelekezwa ndani ya gari lake Nissan Mazda No T 435 CSY eneo la Lemala jijini Arusha tarehe kumi na nane ya mwezi huu.

Kamanda Polisi mkoa wa Arusha Lebaratus Sabas amesema baada ya tukio hilo jeshi la polisi lilifanya uchunguzi na kuwakamata watu hao lakini mtunza bustani Ismail Swalehe amekiri kufanya mauajki hayo kwa tamaa ya fedha kiasi cha shilingi milioni tano na kati ya hizo milioni nne zimepatikana zikiwa zimefukiwa chini nje ya nyumba ya marehemu na kudai alimkata shingo kwa panga akiwa sebuleni  anakunywa uji ili aweze kuelekea kazini.

Kamanda Sabas amesema uchunguzi wa jeshi la polisi pia umegundua panga moja liliokuwa na damu ambalo lilikutwa kwenye stoo ya nyumba ya marehemu vitu vingine ni taulo nne kitambaa cha mezani suruali ya mtuhumiwa ambazo zilifichwa kwenye migomba karibu na banda la kuku nyumbani kwa marehemu ambazo zinadaiwa ndiyo zilizo tumika kupigia deki baada ya kuuwawa.

Mwalimu jela kwa ‘kufuga’ wanafunzi watoro

post-feature-imageMahakama ya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga imemhukumu mwalimu wa Shule ya Msingi Nonwe, Raphael Matima kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ya Sh600,000 ili afiche wanafunzi watoro.


Hakimu Mkazi Mfawidhi, Robert Oguda alitoa hukumu hiyo jana baada ya Mahakama kuridhishwa na ushahidi uliotolewana upande wa mashtaka.
Alisema mshtakiwa huyo aliomba fedha hizo kwa wazazi wa wanafunzi watatu wa shule hiyo iliyopo katika Halmashauri ya Ushetu.
Awali, Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wilayani Kahama, Kelvin Murusulu alidai kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo kinyume cha Sheria ya Elimu.
Murusulu alimuomba hakimu wa mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa huyo kwa kuwa kuomba na kupokea rushwa kwa wazazi wa watoto hao ni kosa na anadidimiza elimu. Alidai licha ya taasisi yake kuweka mtego wa kumkamata, mshtakiwa huyo anapaswa kutumikia kifungo kikubwa.
Hakimu Oguda alimhukumu kifungo hicho cha miaka mitano ili iwe fundisho kwa walimu wengine wenye tabia kama hiyo.

Wakati huohuo, Ofisa Utumishi wa Halmashauri ya Ushetu, Focus Kahendaguza amekutwa na kesi ya kujibu kwenye tuhuma zinazomkabili za kutumia madaraka vibaya ikiwamo kugushi nyaraka na kujipatia fedha zaidi ya Sh4,000,000 kinyume cha sheria.
Mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo na Takukuru wilayani Kahama. Murusulu alidai kuwa mshtakiwa huyo alitumia madaraka vibaya akiwa mtumishi halali ya Serikali na kujipatia kesi hicho cha fedha.
Madai mengine yanayomkabili ni pamoja na kutosambaza viti kwa watendaji wa vijiji wakati huo ikiwa halmashauri ya wilaya ya Kahama kabla ya kugawanywa . Hakimu Oguda aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 19, mwakani mshtakiwa huyo atakapoanza kuwasilisha utetezi wake.
-Mwananchi

Diddy kampatia $1 Million kwa ajili Christmas?

French MontanaOK. Maybe I am missing something here but Diddy kampatia raper French Montana kiasi cha dola milioni moja kwa ajili ya Christmas? Diddy is the boss of bosses. I am just trying to figure this out. Now look at the picture. Screen Shot 2015-12-24 at 7.09.05 PMScreen Shot 2015-12-24 at 7.09.19 PM

Adele ataka collabo na Beyonce.

adele-new-song-19oct15
Mwimbaji mwenye mauzo makubwa zaidi kwenye muziki wa pop kwa sasa duniani Adele amefanyiwa mahojiano na jarida la Time na kuweka wazi kuwa alikuwa na mpongo mkubwa wa kufanya kazi na Beyonce kwenye album yake mpya ya 25.
Adele anasema aliongea na watu wa Beyonce na walipanaga kuendelea maongezi ila haikukamilika na album ilibidi itoke. Adele pia amekata kusema nani alifanya mpaka collabo hio ishindikane ila amesema bado mipango ipo.

HIS AND HERS STYLE::DIAMOND PLATNUMZ AND ZARI THE BOSS LADY

This is a second time tuna wa feature Diamond na Zari they love to dress up na kupiga zile picha za pamoja .Wakiwa ni kati ya celeb couple inapondwa sana Africa Mashariki.12345971_446821785521649_1348586846_n
Wote wakiwa Uganda juzi kati walitinga ki tofauti kidogo Diamond na kanzu yake na kilemba kwa ndani akatupia Jeans 12345716_1391246594516450_371140711_n
Wakati zari akitinga zake Dera jekundu na Kilemba hii picha ya kilemba na Miwani imemtoa very stylish
12394101_1734033823495348_1418197722_n
spotted na sandals zao12328347_804207009725239_54977596_n
Second look ni ile wakiwa wanashoot video ya utanipenda love how zari alivaa the Fur coat and her shoe game was on point ,Diamond ina all black and hints of white
12346127_678307882310865_944754594_n
lets call this a Dinner date look ,Dai in a black Tuxedo and Zari akitinga a black dress with Gold
z
In All white na hii kwenye ile video ya Utanipenda,12317872_1043721542317687_1257778618_n
Black outfit and pop of silver and white,Zari in a cut out black dress with silve shoes ,mmh the shoe though,Daimond in all black but akamilizia na Adidas sneakers zenye Silver na nyeupe.
Which look is ur favourite???wapi walitokelezea zaidi????

20 December, 2015

Shoo ya Diamond Platnumz kwenye Born2Win Concert nchini Uganda

msanii Diamond Platinum alitumbuiza kwenye tamsasha kubwa ‘Born 2 Win Concert’ jijIni Kampala, Uganda. Mbali na Diamond msanii Patoranking naye alitumbuiza kwenye tamasha hilo.

Hizi ni baadhi ya picha za Diamond akitumbuiza kwenye tamasha hilo.Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...