Radamel Falcao amesaini mkataba
wa kujiunga na klabu ya Chelsea na ataungana na timu yake mpya kwenye
ziara ya kujiandaa na msimu ujao (pre-season) huko bara la America ya
Kaskazini hii ni kwa muji wa ripoti.
Mjomba pamoja na baba yake Falcao wamethibitisha kwamba, mkataba umeshasainiwa kati ya mshambuliaji huyo na klabu ya Chelsea.
Kwa mujibu wa gazeti la The
Guardian, Chelsea wamekubaliana na Monaco kumsajili Falcao kwa mkopo wa
mwaka mmoja lakini mkataba huo unakipengele cha kumsajili moja kwa moja
msimu ujao.
Chelsea bado hawajatangaza rasmi
kumsajili Falcao lakini walikuwa na mazungumzo na wakala wa mchezaji
huyo, Jorge Mendez kwa takribani wiki tatu ili kuhakikisha wanamsajili
Falcao licha ya kwamba mshahara wake unagharimu kiasi cha pauni 265,000
kwa wiki.
The Guardian limeripoti kuwa,
mabingwa hao wa ligi ya England wakotayari kumlipa Falcao kitita cha
pauni 180,000 kwa wiki na pauni milioni 4 kama ada ya uhamisho.
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho
amesema atamsaidia Falcao kurudia makali yake ya zamani baada ya kuwa na
msimu mbovu alipokuwa Manchester United kufuatia jeraha la goti la
mudamrefu.
No comments:
Post a Comment