
Jana kwenye hoteli ya Hyatt Regency kampuni ya Huawei inayouza na
kuzalisha “simu zenye akili”a.k.a SmartPhone ilizindua toleo jipya la
simu zake kwenye P Series. Baada ya watu mbalimbali kufurahia P7, hivi
sasa ni wakati wa kutumia P8. Hizi hapa ni sababu za kutosha kabisa
zitakazo kufanya uimiliki simu hii ya Huawei P8.
Battery:
Ukizungumzia matatizo ya Smartphone hili ni moja wapo, huwezi kuniambia
niache kusikiliza music na kuchat kwa pamoja kisa battery. Kila mtu
anaitaji kufanya vitu mbalimbali kwa wakati mmoja kwenye smartphone
yake. Director of Sales and Marketing Samson Majwala amesema kwamba
battery ya Huawei P8 inauwezo wa kukuwezesha kufanya yote na kukaa kwa
siku nzima na chaji. Battery lake halitoki kwenye simu na lina uwezi
mkubwa wa Li-Po 2680 mAh
Camera:
Smartphone bila camera kali bado haijawa smart, Huawei P8 inakuja na
camera yenye mega pixel 13 (4160 x 3120 pixels) zaidi ya hapo camera
hiyo ina uwezo wa Autofocus, optical image stabilization, dual-LED (dual
tone) flash. Haijaishia hapo, bali ukiwa unapiga picha uweza kufanya
Geo-tagging, touch focus, face/smile detection, panorama na HDR.
Vipi camera ya selfie, hapo unakutana na camera yenye uwezo wa 8 mega
pixel na 1080p. So Huawei P8 inakupa uwezo wa kurekodi video ya High
Definition ya 1080p@30fps.
Umbo:
Samson Majwala anaendelea kusema kwamba mara nyingi tuvaa nguo ambayo
imetu-fit vizuri na hatutaki mizigo mingi kwenye mifuko yetu.
Ukiizungumzia Huawei P8 ni nyembamba na bado ni ngumu hata ukiiweka
mfukoni sio rahisi kukusumbua. Ina vipimo vya 144.9 x 72.1 x 6.4 mm.
Uzito wake ni 144 g (5.08 oz) na nyembamba kwa 6.4mm
Sim Card
Huawei inakupa machaguo mawili kwenye swala la simcard. Zipo Huawei P8 zenye line moja na nyingine zina line mbili.
Operating System
Kama kawaida Huawei huwa inatumia O.S ya Android, lakini Huawei P8 sio
tu kutumia Android bali inatumia Android mpya kabisa ambayo ni version
5.0.2 (Lollipop).
Speed
Hakuna anetaka kufungua camera na kuisubili sana kufunguka au kufanya
kitu chochote kwenye simu yako na ikawa slow. Huawei P8 imezingatia hilo
kwa kuipa uwezo wa Quad-core 2 GHz Cortex-A53 & quad-core 1.5 GHz
Cortex-A53. Pia Ram ya Huawei P8 ni 3GB ambayo ni RAM inayozidi hata
baadhi ya laptop.
Memory
Mfano kama picha inapigwa na camera ya 13 mega pixel basi lazima
inahitajika memory ya kutosha kuhifadhia picha,video na mafaili mengine.
Huawei P8 inaweza kuwa na memory ya 16GB au 64GB na pia kwa speed yake
unaweza kuongeza memory card hadi yenye 128GB na simu ikabaki kwenye
ubora wake.

Mr Samson Majwala (Huawei Director of Sales & Marketing) na Peter Zhang Huawei Country Manager
Network
Huawei P8 imepewa uwezo mkubwa wa kudaka network ya mtandao wako wa
simu. Mr Majwala anasema kuna wakati simu inavyobadilisha mnara,
inawezekana kuwepo na delay kidogo. Lakini simu hii inauwezo wa kudaka
haraka network na sio rahisi kupiga simu na isiunganishwe na mtandao.
Pia inawezo wa haraka wa kudaka WiFi. Smartphone hii a.k.a simu yenye
akili inauwezo wa kuchagua WiFi ambayo ina nguvu sana kwa wakati huo.
Ziada
Vitu vya ziada ni kwamba ukiwa unataka ku-screenshot kwenye Huawei P8
basi kazi ni rahisi sana. Una doubletap screen na utakua umesha
screenshot.
Director’s mode : Kwenye Huawei P8 unaweza kurekodi
video kwenye angle 3 na ukawa una mix hizo video wakati unarekodi kama
dirrector na mwisho siku ukapata video iliyokua mixed vizuri kama na
director.
Huawei P8 ni ngumu imetengenzwa kwa design nzuri ya kuvuti ikiwa na cover la chuma ngumu kulinda simu yako vizuri.
Unaipataje?
Huawei P8 lazima itakua kwenye maduka muhimu ya kuuzia simu. Ukitaka
yenye line mbili ni Tsh 1,200,000 na ukitaka yenye line moja ni Tsh
1,100,000