Costa, 24, amejiunga na Bayern
kwa dau la pauni milioni 21 kwa mujibu wa klabu yake hiyo ya Ukraine na
amesaini mkataba wa miaka mitano kuitumikia klabuya Bayern.
“Ndoto zangu zimetimia leo”, amesema Costa ambaye amerejea kwao na kikosi cha Brazil akitokea kwenye
michuano ya Copa America.
Usajili huo utaongeza tetesi za kiungo wa timu hiyo Bastian Schwensteiger kujiunga na Manchester United.
Guardiola ambaye amekiongoza
kikosi cha Bayern kutwaa taji la 25 la Bundesliga msimu uliopita,
anamachaguo mengi ya viungo akianza na Frank Ribery na Mhispania Thiago
Acantara, Xabi Alonso na Javi Martinez, hiyo inamaanisha Schweinsteiger,
30, atakuwa na nafasi ndogo ya kucheza kwenye kikosi hicho.
Kiungo huyo wa kimataifa wa
Ujerumani, amecheza mechi 20 tu za ligi msimu wa 2014-2015 ambazo ni
mechi chache kwake tangu ajiunge na Bayern mwaka 2002.
Costa alifunga magoli 29 kwenye michezo 149 ya ligi ambayo alicheza akiwa Shakhtar ambapo ameshinda mataji mara tano.
“Douglas Costa atakuwa ni
mchezaji mzuri kwenye timu yetu”, alisema mkurigenzi wa michezo wa
Bayern Mathias Sammer, “Ana uwezo wa ufundi, nguvu hasa mguu wa kushoto,
yuko shapu na anakasi”.
No comments:
Post a Comment