15 September, 2016

Audio Mpya: Kila siku Maneno - Tosha Bonie

Tosha Bonie Ni msanii Chipukizi Kutokea Pande Za Moshi na Hii ndio kazi yake ya Kwanza. Tumpatie support Basi Kijana wetu aweze songa Mbele. Bofya DOWNLOAD hapo chini Kuupakua wimbo huo.

14 September, 2016

Ceferin achaguliwa kuwa Rais mpya wa Uefa

Alexander Ceferin
Rais wa chama cha soka cha Slovenia Alexander Ceferin amechaguliwa kuwa Rais mpya wa shirikisho la soka barani ulaya (UEFA)
Ceferin anachukua nafasi iliyowachwa wazi na Michel Platini ambaye alifungiwa na FIFA kwa miaka minane Baada ya kukutwa na kosa la kupokea mlungula wa £1.3mil.
Rais huyu mpya amemshinda Michael Van Praag Rais wa chama cha mpira cha Uholanzi katika kura iliyopigwa Leo jijini Athens.
Ceferin atashika kiti hicho cha uraisi mpaka mwaka 2019

New Audio Download: Chemical Ft Centano- am Sorry Mama

Image result for chemical sorry mama photos Burudika na ngoma kutoka kwa mwana dada Chemical, ngoma inakwenda kwa jina la am Sorry Mama. Bonyeza DOWNLOAD hapo chini kuupakua wimbo huo.

Paralimpiki: Mkenya Samwel Kimani ashinda dhahabu 1500m

Samwel Kimani alikuwa pia ameshinda dhahabu mita 5000 kitengo T11
Mwanariadha mlemavu kutoka Kenya Samwel Mushai Kimani ameshindia Kenya dhahabu nyingine baada ya kuibuka mshindi wa mbio za wanaume mita 1,500 kitengo T11 Paralimpiki.
Kimani aliandikisha muda wa 4:03.25, muda bora zaidi msimu huu.
Mbrazil Odair Santos alimaliza wa pili.

Mbio hizo hata hivyo hazikuwa za kasi kama za kitengo T13 ambapo wanariadha wanne waliomaliza wa kwanza waliandikisha muda bora kushinda wa mshindi wa mbio za Olimpiki mita 1,500.

Katika mbio za kitengo T13, raia wa Algeria Abdellatif Baka alishinda na kuandikisha rekodi ya dunia ya 3:48.29. Mshindi wa dhahabu Olimpiki Matthew Centrowitz alitumia muda wa 3:50.00.

Kimani alikuwa ameishindia Kenya dhahabu ya kwanza katika michezo ya Olimpiki ya walemavu ya Rio 2016 kwa ushindi katika mbio za mita 5,000 kitengo T11 (wanariadha wasioona wakisaidiwa na waelekezi).
Odair Santos alishinda fedha katika mbio hizo naye Erick Sang wa Kenya akatwaa shaba.
Kenya ilishinda dhahabu mbili Paralimpiki za London, na kubeba medali sita kwa jumla.

Ligi ya Mabingwa: Barcelona 7-0 Celtic

Celtic hawakuweza kumdhibiti Messi
Celtic walipokezwa kichapo kibaya zaidi katika mashindano ya Ulaya Jumanne usiku baada ya kuchapwa mabao 7-0 na Barcelona uwanjani Camp Nou.
Mshambuliaji Lionel Messi, raia wa Argentina, alifunga 'hat-trick' yake ya sita katika mechi hiyo ya kundi C.
Alianza kwa kufunga bao la mapema

Mchezaji wa Celtic Moussa Dembele alishindwa kufunga penalti kabla ya Messi kufunga la pili.
Kipindi cha pili, Neymar alifunga kupitia frikiki, Andres Iniesta akafunga la nne, Messi akaongeza la tano naye Suarez akakamilisha ushindi kwa mabao ya sita na saba.Neymar baada ya kufunga bao la tatu Camp NouKatika misimu miwili ambayo wamekuwa pamoja Nou Camp, Messi, Neymar na Luis Suarez wamefunga mabao 253 na kusaidia ufungaji wa mabao 120.Andres Iniesta alifunga baada ya kuingia kama nguvu mpya

13 September, 2016

12 September, 2016

KILIMANJARO QUEENS WAANZA VIZURI MICHUANO YA CECAFA

capture
capture
 Timu ya soka ya Tanzania Bara ya wanawake, Kilimanjaro Queens imeanza Michuano ya Kombe la CECAFA kwa kishindo baada ya kuichapa Rwanda mabao 3-, mchezo uliofanyika Uwanja wa Njeru, mjini Jinja, Uganda.
Kilimanjaro Queens walipata mabao yao kupitia kwa Amina Ally pamoja na Asha Rashid aliyefunga mabao mawili.
Rwanda kwa upande wao, walipata mabao yao kupitia kwa Ibangarrye Anne Marrie pamoja na Stumai Abdallah ambaye alijifunga.
Michuano hiyo inashirikisha timu nane ambazo ni wenyeji Uganda, Kenya, Ethiopia, Rwanda, Burundi, Zanzibar, Sudani Kusini na Tanzania Bara.
Timu hiyo iko chini ya kocha mkuu Sebastian Nkoma katika mashindano hayo ya kwanza kufanyika ukanda huu yakihusisha timu za wanawake.

Ushahidi: Jaden Smith hajafa

Jaden Smith and Sarah Snyder hold hands whilst out in New York

Featuring: Jaden Smith, Sarah Snyder
Where: Manhattan, New York, United States
When: 12 Sep 2016
Credit: TNYF/WENN.com Ingawaje mitandao inalazimisha kwamba nyota huyu kinda kutoka marekani amefariki, lakini taarifa hizo hazina ukweli wowote.
 Taarifa hizi zilianza kuzagaaa mitandaoni kwamba nyota huyu kajitoa uhai wake. Taarifa hizi zilipata Nguvu pale ambapo Jaden aliacha kupost chochote katika account za social media anazo miliki.
 Na good news ni kwamba jamaa kaonekana mtaani kiroho safi akiwa na Bibie Sara kama picha zifuatazo zinavyo onyesha.Jaden Smith and Sarah Snyder hold hands whilst out in New York

Featuring: Jaden Smith, Sarah Snyder
Where: Manhattan, New York, United States
When: 12 Sep 2016
Credit: TNYF/WENN.comJaden Smith and Sarah Snyder hold hands whilst out in New York

Featuring: Jaden Smith, Sarah Snyder
Where: Manhattan, New York, United States
When: 12 Sep 2016
Credit: TNYF/WENN.comJaden Smith and Sarah Snyder hold hands whilst out in New York

Featuring: Jaden Smith, Sarah Snyder
Where: Manhattan, New York, United States
When: 12 Sep 2016
Credit: TNYF/WENN.com

Young Thug: Kutakua na maharusi wawili kwenye Harusi yangu.

Young Thug Rappper asiye ishiwa na vituko kutokea pande za Marekani Young Thug ambaye hivi karibuni alibadili jina na kujiita Jeffrey amenukuliwa akisema kutakua na Maharusi wawili kwenye Harusi yangu “There will be two brides at the wedding.” Hayo aliyasema kwenye Interview  aliyo fanya na Billbord.

VIDEO: Barnaba ‘Lover Boy’

Tizama Video mpya ya Barnaba inayokwenda kwa jina la  ‘Lover Boy’ Pia unaweza Kudownload Audio yake kwa kubonyeza DOWNLOAD hapo chini.

SHILOLE: Jina langu ni Fursa ya mafanikio.

 
Mwanamuziki na Muigizaji Zuenna Muhamed maarufu kama Shilole "SHISHI BABY" amesema Usanii ni mlango wakupitia ili kufuata mafanikio yalipo, huku akiahidi kuifanyia kazi kila nafasi itakayo katiza mbele yake. Akizungumza hivi karibuni, Shilole alisema ukiwa msanii unafahamiana na watu wengi wanao fanya mambo mbali mbali, hivyo ni nafasi yakufahamu mambo mengi pia.

 Shilole alisema tangu muziki hajawahi kukatishwa tamaa wala kufikiria kufanya hivyo licha yakua na mashabiki wa aina mbali mbali wanao kubali kazi zake. Alisema 
" Watu wengi wanatafuta nafasi yakufahamiana na watu wengi ili wapanue uwigo wa uelewa kati yaon na kufanikisha ndoto zao, sasa kwa nini mimi nimepata nafasi hiyo bado mimi nishangae, naifanyia kazi kila Fursa nitakayoiona mbele yangu"
Shilole aliwataka wasanii wakike na wakiume kuwekeza kipindi ambacho wana nguvu ili iwe msaada Baadae. 
"Wasanii hatuna kiinua mgongozaidi yakukikuza kile kidogo tunacho pata, hakuna njia nyingine zaidi ya Biashara, wasichana tupunguze mashindano ya mavazi tandae kiinua mgongo, Vivyo hivyo wavulana wapunguze Bata wajiandalie kiinua mgongo"

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...