08 July, 2016

Faida 9 za kula mboga za Spinach kwa mama mjamzito

Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu mwilini na madini mbali mbali ambayo huhitajika na Mwili. Mboga za Spinach ni moja kati ya mboga maarufu mno katika jamii zetu na hizi ndizo faida zake kwa wanawake wajawazoto:-
 1. Huzuia mtoto kuzaliwa na matatizo kama mgongo wazi na mdomo na pua kuwa na uwazi uliongana( mdomo sungura)
2. Hupunguza uwezekano wa mtoto kuzajiwa njiti yaani kuzaliwa kabla hajafikisha mienzi 8 tumboni kwa mama. kutokana na kutokuwa na madini ya chuma ya kutosha mama anaweza pata tatizo ili ila kwa sababu spinach ina madini ya chuma ya kutosha yaani folic basi huweza kuzuia shida hii.
3. Huzuia kupata tatizo la upungufu wa damu  hii ni kutokana na spinach kuwa na madini ya folic na chuma yanayoongeza damu mwilini.
4. Husaidia katika utengenazi wa mapafu ya mtoto. inakemikali inayoitwa beta-carotene ambayo hubadilishwa kuwa vitamini A hii ndiyo hutumika kwa ajili ya uundaji wa mapafu ya mtoto.
5. Hutibu tatizo la haja kubwa kuwa ngumu kwa kuwa spinach ina nyuzi nyuzi kiitaamu huitwa fiber ambazo hulainisha choo na kupunguza maumivu.
6. hupunguza maumivu kwa kutumia chemicali yake inayoitwa glyco-lipid ambayo huzuia maumivu katika sehemu za miguu na misuli.
7.  Huwastanisha msukumo wa damu mwilini kwa kutumia kemikali yake inayoitwa nitrate.
8. Huweka kinga ya mwili wa mama mjamzito imara kwa spinach ina vitamin C  hivyo hutapata yale maradhi ya lazima kwa mama mjamzito.
9. Huwezesha utengenezaji  bora kwa mifupa ya mtoto kwa sababu spinach ina madini ya kalishamu ambayo hujenga mifupa ya mama na mtoto.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...