Showing posts with label Habari. Show all posts
Showing posts with label Habari. Show all posts

09 August, 2016

Sababu ya samaki kupungua Ziwa Tanganyika

Ziwa Tanganyika
 Utafiti mpya umebaini kupungua pakubwa kwa idadi ya samaki katika Ziwa Tanganyika, mojawapo ya  maziwa muhimu zaidi kwa uvuvi duniani, kumetokana na ongezeko la joto duniani katika karne moja iliyopita.

Ziwa Tanganyika ndilo la kale zaidi Afrika na samaki wake huwa muhimu sana kwa lishe katika mataifa yanayopakana na ziwa hilo.
Lakini idadi ya samaki imepungua sana, huku wavuvi wakiendelea kuongezeka.
Ongezeko hili la wavuvi lilidhaniwa kuwa chanzo kikubwa cha kupungua kwa idadi ya samaki.
Lakini utafiti mpya unaonesha chanzo hasa ni ongezeko la joto duniani kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.
Ziwa Tanyanyika ndilo la pili kwa ukubwa duniani miongoni mwa maziwa yenye maji yasiyo na chumvi na maji yake huwa katika mataifa manne: Burundi, Jamhuri ya KIdemokrasia ya Congo, Tanzania na Zambia.
Samaki kutoka kwa ziwa hilo hutoa asilimia 60 ya protini zitokanazo na wanyama ambazo huliwa na watu eneo hilo.
Aidha, ni eneo lenye aina nyingi ya wanyama na mimea.


Ziwa Tanganyika 

Ili kufahamu mabadiliko yanayotokea katika ziwa hilo, watafiti wamechukua sampuli za mchanga kutoka kwenye kina cha ziwa hilo.
Baada ya kufanya utathmini wa mchanga huo na visukuku, wamepata viashiria kwamba idadi ya samaki imekuwa ikishuka sambamba na ongezeko la joto duniani.

Wanasayansi wanasema katika maziwa yanayopatikana maeneo yenye joto karibu na ikweta, ongezeko la joto katika maji hupunguza kuchanganyikana kwa maji kutoka sehemu ya juu ya ziwa ambayo huwa na oksijeni pamoja na maji yenye virutubisho vingi sehemu ya chini kwenye ziwa.

Kutochanganyikana vyema kwa maji haya husababisha virutubisho vinavyofika juu kwenye ziwa kupungua, hili hupunguza ukuaji wa miani (mimea ya rangi ya kijani, kahawia au nyekundu inayoota chini ya bahari) na hili hupelekea kupungua kwa lishe ya samaki.

Ziwa Tanganyika

Watafiti waliohusika katika utafiti huo wanasema ongezeko la joto limepunguza kuchanganyikana kwa maji, kupungua kwa ukuaji wa miani pamoja na kupungua kwa maeneo ambayo viumbe waishio chini ya bahari wanaweza kuishi na kustawi.

"Wazo letu lilikuwa kuchunguza visukuku na kubaini kushuka kwa idadi ya samaki kulianza wakati gani," anasema Prof Andrew Cohen kutoka Chuo Kikuu cha Arizona.
"Iwapo hili lilifanyika kabla ya kuanza kwa uvuvi wa kiviwanda miaka ya 1950, basi ungekuwa na ushahidi mkubwa kwamba hili halitokani na ongezeko la uvuvi na hivi ndivyo tulivyobaini."

Wanasayansi hao hata hivyo hawajapuuzilia mbali athari za ongezeko la uvuvi katika miongo sita iliyopita.
Wanasema kumekuwa an ongezeko la watu tangu miaka ya 1990, hasa kutokana na wakimbizi waliotoroka mizozo na kuhamia maeneo yaliyo karibu na ziwa hilo.Ziwa Tanganyika
"Ukizingatia mtindo wa sasa wa kuendelea kugawika zaidi kwa maji kwenye ziwa, idadi ya samaki itaendelea kupungua. Watu wanaosimamia sera wanafaa kuanza kufikiria kuhusu chanzo mbadala cha mapato na lishe kwa watu wanaoishi eneo hilo."

Matokeo ya utafiti huo yamechapishwa katika jarida la kisayansi la Proceedings of the National Academy of Sciences.

CHANZO: BBC SWAHILI

14 March, 2016

Magufuli awateua wakuu 13 wapya wa mikoa ( List kamili)


Rais Magufuli amewateua wakuu 13 wapya wa mikoa miongoni mwa orodha mpya ya wakuu 26 wa mikoa iliyotangazwa jana na ikulu ya rais.
Rais John Pombe Magufuli amewahifadhi wakuu 13 waliohudumu katika serikali ya Jakaya Kikwete.
Uteuzi huo umetangazwa na katibu mkuu kiongozi, Mussa Ibrahim Iyombe.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari iliyotiwa sahihi na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, katika ikulu, Gerson Msigwa, Viongozi hao wote walioteuliwa wataapishwa katika hafla maalum itakayoandaliwa jumanne tarehe 15 Machi, 2016 saa tatu asubuhi jijini Dar es salaam.
Orodha ya wakuu wa mikoa walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
   
Afisa Mkuu wa Mkoa
Paul Makonda Dar es Salaam
Ezekiel Elias Kyunga Geita
Salum Mustafa Kijuu Kagera
Raphael Muhuga Katavi
Emmanuel Maganga Kigoma
Godfrey Zambi Lindi
Dkt. Steven Kebwe   Morogoro
Zerote Steven   Rukwa
Anna Malecela Kilango   Shinyanga
Methew Mtigumwe   Singida
Antony Mataka   Simiyu
Aggrey Mwanri   Tabora
Martine Shigela   Tanga
Jordan Mungire Rugimbana   Dodoma
Said Meck Sadick   Kilimanjaro
Magesa Mulongo   Mara
Amos Gabriel Makalla   Mbeya
John Vianey Mongella   Mwanza
Daudi Felix Ntibenda   Arusha
Amina Juma Masenza   Iringa
Joel Nkaya Bendera   Manyara
Halima Omary Dendegu   Mtwara
Dkt. Rehema Nchimbi   Njombe
Evarist Ndikilo   Pwani
Said Thabit Mwambungu  Ruvuma
Chiku Galawa   Songwe (Mkoa mpya)

01 March, 2016

Rufaa ya Babu Seya na Mwanaye Kuanza Kusikilizwa March 11 Mwaka Huu


Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika (AfCHPR) katika kikao chake kilichoanza jijini Arusha, itapitia maombi ya rufani ya mwanamuziki maarufu nchini, Nguza Viking na John Viking dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hata hivyo, taarifa iliyotolewa na mahakama hiyo jana, ilieleza kuwa kesi hiyo namba 006/2015 iliyopangwa kusikilizwa Machi 11 haitasikilizwa katika mahakama ya wazi.

Ni kesi mbili pekee kati ya 50 zitakazosikilizwa kwenye mahakama ya wazi, ikiwamo inayomhusu mwanasiasa maarufu wa Rwanda, Victoire Ingabire aliyoifungua kupinga ukiukwaji wa haki anaofanyiwa na Serikali yake.

Pia, mahakama ilieleza kuwa kikao hicho cha 40 cha kawaida kitakamilika Machi 18 na kutoa uamuzi wa mashauri manne.

Kesi ya Ingabire inayotarajiwa kuvuta hisia za watu wengi ikizingatiwa upinzani ambao amekuwa akiuonyesha dhidi ya serikali yake, itasikilizwa Machi 4.

Katika kesi hiyo, Ingabire pamoja na mambo mengine anadai haki zake kuvunjwa ambazo zinatajwa kwenye Mkataba wa Mahakama hiyo Ibara ya 7, 10 na 18 hivyo anaitaka itoe uamuzi.

Pia, Taasisi ya Action Pour la Protection des Droits de I’Homme (APDH) inaishtaki Serikali ya Ivory Coast kuvunja mkataba wa Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu Ibara ya 3 na 17 katika kesi namba 001/2014, iliyopangwa kusikilizwa Machi 3.

Mahakama hiyo inaundwa na majaji 11 kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) na inakuwa na vikao vinne kwa mwaka, kufikia Januari 31 tayari ilikuwa imepokea kesi 74 kati ya hizo 25 imetolewa uamuzi.

Maombi manne yamepelekwa  kwa uamuzi zaidi kwenye Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu.

24 February, 2016

Wagombea urais wa chama cha Republican washindania jimbo la Nevada

Trump
Wagombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani wanakabiliana kwenye uchaguzi wa mchujo katika jimbo la Nevada katika kinyang’anyiro cha nne cha kuamua mgombea wa chama hicho.
Mfanyabiashara Donald Trump, ambaye amekuwa akiongoza kwenye kura za maoni kitaifa, anaongoza pia kwenye kura za maoni jimbo hilo, na anatarajia kupata ushindi wa tatu mtawalia baada ya kushinda New Hampshire na South Carolina.
Nevada, ambalo ni jimbo lisilo na mbabe na lenye watu wengi wa asili ya Amerika Kusini, ni muhimu sana katika uchaguzi.
Upigaji kura kwa sasa unaendelea na kuna foleni ndefu vituoni.
Kura ya maoni ya karibuni CNN/ORC imeonesha Trump ana uungwaji mkono 45% akifuatwa na Seneta Marco Rubio 19% naye Seneta Ted Cruz akiwa na 17%.
Ingawa Nevada ina wajumbe wachache, inatarajiwa kuwa mtihani kwa Trump kutokana na matamshi yake dhidi ya wahamiaji ikizingatiwa kwamba ina watu wengi wa asili ya Amerika Kusini.
Hillary Clinton alishinda kwenye jimbo hilo katika chama cha Democratic Jumamosi.
Alimshinda mpinzani wake Bernie Sanders kwa kumpita kwa asilimia tano na wagombea hao wawili sasa wanaangazia jimbo la South Carolina lenye watu wengi weusi.
Uchaguzi wa mchujo wa chama cha Republican katika jimbo la South Carolina utafanyika Jumamosi.
Uchaguzi wa mchujo hutumiwa kuchagua wagombea wa vyama viwili vikuu kwenye uchaguzi mkuu wa urais ambao utafanyika mwezi Novemba

 SOURCE: BBC

20 February, 2016

Marekani yashambulia kambi ya IS Libya

Maafisa wa Marekani wamethibitisha kuwa ni ndege za Marekani zilizofanya mashambulio huko Libya wakiwalenga wanamgambo wa IS. Hata hivyo shambulio hilo la karibu na mji wa Sabratha,lililonuiwa kumlenga hasa mpiganaji mmoja wa Tunisia limeripotiwa kuwauwa watu 30 .
Mpiganaji huyo wa Tunisia anasemekana ndiye aliyefanya shambulio la mwaka jana katika kumbukumbu za Bardo na hoteli ya ufuoni mwa bahari ya Sousse huko Tunisia ambako watu zaidi ya 10 waliuawa.
Mashambulio hayo yalilenga kambi moja ya wapiganaji wa Islamic State na kumuua kiongozi mmoja mwenye itikadi kali ,maafisa wa Marekani wamesema. Noureddine Chouchane anahusishwa na mashambulio mawili nchini Tunisia mwaka uliopita ,ikiwemo shambulio lililowaua raia 30 wa Uingereza.
Kundi la IS limekuwa likifanya oparesheni zake nchini Libya kwa kipindi cha mwaka mmoja na Marekani inakadiria kwamba lina hadi wapiganaji 6,000 nchini humo.Libya inasalia katika machafuko ya wenyewe kwa wenyewe miaka minne baada ya kupinduliwa kwa aliyekuwa kiongozi wake Muammar Gaddafi,na inapiganiwa na makundi tofauti ikiwemo kundi la IS.

17 February, 2016

Marekani na Cuba zimetiliana tena saini makubaliano ya kurejesha tena safari za ndege za abiria baina ya nchi hizo mbili


Marekani na Cuba zimetiliana tena saini makubaliano ya kurejesha tena safari za ndege za abiria baina ya nchi hizo mbili kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka hamsini iliyopita.
Utiwaji wa saini ya makubaliano hayo ulikuwa ni baina ya waziri wa usafiri wa Marekani , Anthony Foxx na mwenziwe kutoka Cuba Adel Izquierdo Rodriguez, mjini Havana makubaliano hayo yatashuhudia safari lufufu za kila uchao baina ya mataifa hayo yaliyokuwa mahasimu hapo awali.
Matarajio ya kuanza kwa safari hizo ni baada ya mwezi mmoja,ingawa mpaka sasa kisheria ni Marufuku kwa raia wa Marekani kuitembelea Cuba kama mtalii.
Ki diplomasia uhusiano wa nchi mbili hizo ilianza kurejea zaidi ya takribani mwaka mmoja uliopita .Mwandishi wa BBC aliyeko mjini Havana ameelezea juu ya makubaliano hayo ya hivi karibuni kwamba yamekuja baada ya ikulu ya Marekani kutafakari uwezekano wa safari za kiserikari za rais wa Cuba nchini Marekani.

13 February, 2016

Naibu Rais wa Kenya William Ruto amepata ushindi Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC)

Ruto
Naibu Rais wa Kenya William Ruto amepata ushindi muhimu kwenye kesi yake inayosikizwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) baada ya majaji wa rufaa kukubali rufaa yake ya kupinga kutumiwa kwa ushahidi wa mashahidi waliojiondoa.
Hii ina maana kwamba ushahidi ulioandikishwa awali na upande wa mashtaka hauwezi kutumiwa dhidi ya Bw Ruto na mwanahabari Joshua Sang.
Uamuzi huo ni pigo kubwa kwa upande wa mashtaka unaoongozwa na Fatou Bensouda.
Upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi sita waliokuwa wanahusisha Bw Ruto na ghasia za baada ya uchaguzi za mwaka 2007-08, vilivyosababisha vifo vya watu 1,200, walioondoa ushahidi wao.
Upande wa mashtaka unasema walitishiwa au wakahongwa.
Majaji wa rufaa wamebatilisha uamuzi wa awali wa majaji uliosema upande wa mashtaka unaweza kutumia ushahidi uliowasilisha na mashahidi hao kabla yao kubadili nia.
"Ushahidi ulioandikisha awali uliwasilishwa bila washtakiwa kupewa fursa ya kuwahoji na kuwauliza maswali mashahidi hao,” amesema jaji wa mahakama ya rufaa Piotr Hofmanski.
Bw Sang amefurahia uamuzi huo na kusema maombi yake yamejibiwa.

11 February, 2016

Mgombea wa urais Ugand Mbabazi aahidi kurejesha mabaki ya aliyekuwa rais wa nchini hiyo Idi Amin Dada


Mgombea wa urais katika uchaguzi mkuu ujao nchini Uganda ameahidi kurejesha nyumbani mabaki ya aliyekuwa rais wa nchini hiyo Idi Amin Dada na kuujengea makavazi.
Aliyekuwa waziri mkuu wa Uganda Amama Mbabazi,alisema endapo atachaguliwa kuwa rais azimio lake la kwanza itakuwa kuwapatanisha waganda wa kila tabaka na kabila.
Kwa madhumuni hayo anapanga kuwaleta pamoja watu anaohisi kuwa wanaomuunga mkono Idi Amin wale waliomuunga mkono Milton Obote na wale wanaomuunga mkono rasi wa sasa Yoweri Kaguta Museveni.
Viongozi hao watatu ndio waliochangia kwa njia moja au nyengine mwelekeo wa kisiasa wa Uganda.
Marehemu Idi Amin Dada aliiongoza Uganda kwa miaka minane kati ya mwaka wa 1971 hadi 1979 utawala ambao ulishuhudia mauaji ya wapinzani wake wengi.
Vilevile anatuhumiwa kwa kuwatimua wahindi wote nchini Uganda kabla ya kupinduliwa na Milton Obote.
Marehemu Idi Amin aliaga dunia akiwa uhamishoni nchini Saudi Arabia.
Rais Yoweri Museveni, anatarajiwa kuchaguliwa tena kuongoza taifa hilo la Afrika Mashariki kwa hatamu ya tano.

10 February, 2016

Donald Trump na Bernie Sanders wamepata ushindi katika mchujo wa jimbo la New Hampshire.

Trump
Seneta wa Vermont Bernie Sanders, aliyemshinda Hillary Clinton, amesema ushindi wake unaonesha watu wanataka “mabadiliko kamili”.
Bw Trump na Seneta Sanders wote wawili wamekuwa wakiwataka watu wapige kura dhidi ya watu ambao tayari wamekuwa kwenye mfumo wa utawala.
Maafisa wa jimbo walikadiria kwamba watu wengi wangejitokeza kushiriki kura za mchujo huo wa New Hampshire.
Gavana wa Ohio John Kasich alimaliza wa pili katika chama cha Republican, mbele ya gavana wa Florida Jeb Bush, Texas Seneta Ted Cruz na Seneta wa Florida Marco Rubio wote ambao wanang’ang’ania nafasi ya tatu.
Bi Clinton tayari amempongeza Bw Sanders, lakini akasema ataendelea kupigania kira kura kwenye kinyang’anyiro hicho cha kumtafuta mgombea urais wa chama cha Democratic.
Mchujo huo wa New Hampshire umewapa washindi nguvu mpya wanapoelekea kwa michujo ijayo South Carolina na Nevada.Trump
Ushindi wa Trump New Hampshire ndio wa kwanza mfanyabiashara huyo kutoka New York, ambaye hajawahi kuwania wadhifa wowote wa siasa, na ambaye amekuwa akiongoza kwenye kura za maoni.
Akitangaza ushindi wake, bilionea huyo amempongeza mshindi wa Democratic Bw Sanders lakini akamshambulia akisema “anataka kuuza taifa letu, jameni!”
Baada ya asilimia 50 ya kura kuhesabiwa, Seneta Sanders anaongoza kwa zaidi ya asilimia 10 ya kura dhidi ya Clinton.
Aliongoza kwenye kura za maoni New Hampshire kwa miezi kadha, na ilitarajiwa kwamba angeshinda, lakini bado ni ufanisi mkubwa.
Wengi wanaamini huenda ushindi wake umechangiwa na hali kwamba anatoka jimbo jirani la Vermont.Sanders
"Kile watu hapa wamesema ni kwamba ukizingatia mgogoro wa kiuchumi unaokabili nchi yetu kwa sasa, muda umepita kwa watu wale wale, ambao wamekuwa kwenye mfumo wa siasa na uchumi,” Bw Sanders alisema akiwahutubia wafuasi wake kwenye hotuba ya ushindi baadaye Jumanne.
Mgombea huyo mwenye umri wa miaka 74 ameahidi kumaliza pengo kati ya matajiri na maskini, kutoa elimu ya vyuo vikuu bila malipo na ‘kuvunja’ benki kubwa kubwa

09 February, 2016

Ripoti ya Umoja wa Mataifa inasema maelfu ya raia wa Syria waliowekwa kizuizini wamekuwa wakifa kinyama


Maafisa wa Umoja wa mataifa waliofanya uchunguzi huo wanasema raia wa Syria ambao wamekuwa wakiunga mkono waasi au kuipinga serikali wamekuwa wakikamatwa hapo hapo.
Wakati huo huo Wakati Majeshi Syria yakiendelea na mapambano katika mji wa Allepo, Uturuki imesema kipaumbele chake cha kwanza ni kuwapa misaada wale waliokimbia makazi yao kutokana na vita.
Naibu Waziri Mkuu Numan Kurtulmus amesema raia wa Syria wapatao elfu sabini na saba wanapatiwa msaada na Uturuki katika kambi katika eneo la mpakani.mepangwa katika siku za usoni katika maeneo yaliyoathirika kwenye eneo hili, idadi kubwa ya wakimbizi wapatao laki sita, wanaweza kukusanyika katika eneo la mpaka wa Uturuki na Syria. kama leo karibu watu elfu sabini na saba wamepatiwa makazi kwenye kambi zilizojengwa mpakani mwa Uturuki na shirika lisilo la kiserikali la AFAD. kama unavyojua tumewachukua waarabu elfu tano na wasirya wenye asili ya Uturuki nchini Uturuki wiki iliyopita."
Naye Waziri wa mpito wa Syria Hussein Bakri ameelezea kusikitishwa na kutokana na hali ilivyo"Haya ni mashambulizi ya mabomu yasiyo ya kawaida. Yamesababisha watu zaidi ya sabini elfu kukimbia makazi yao katika mji wa Alleppo kwa ujumla, na hasa eneo la kaskazini.Kama hali itaendelea kama hivi sasa, itasababisha watu zaidi laki nne kutoka Jimbo la Allepo na mji wa Allepo pekee kukimbia makazi yao. Ni wazi kabisa Urusi imedhamiria kuuzunguka na mji wa Allepo, kama ilivyotokea katika maeneo mengine ya Syria..

CHANZO=(BBC )

08 February, 2016

Mamilioni ya watu wenye asili ya China, duniani kote wanasheherekea mwaka mpya wa ki China .


Baruti nyingi zilirushwa angani mjini Beijing ikiwa ni ishara ya kusheherekea siku ya kwanza ya mwaka mpya wa nyani,Nyani wakiwa ni miongoni mwa wanyama kumi na mbili wanaotumiwa kati ya alama za kichina katika masuala ya utabiri.
Nako mjini Yokohama nchini Japan, wao wanasheherekea siku kuu hii kwa kuhesabu muda huku wakicheza ngoma ya asili ya kucheza na simba.
Maadhimisho ya sherehe hizi za mwaka mpya zinajumuisha watu kula pamoja,kufanya usafi na familia kuwa pamoja huku wakirusha fashi fashi angani.

07 February, 2016

Tetemeko kubwa la ardhi limekumba Taiwan Kusini,


Tetemeko hilo la kipimo cha Ritcher 6.4 lilitokea karibu na mji wa Tainan.
Zaidi ya watu 200 wameokolewa kutoka kwa jengo hilo, ingawa waokoaji wangali wanajaribu kuwafikia watu wengine ambao inadhaniwa wangali wamekwama katika mabaki ya jengo hilo.
Tetemeko hilo liligonga usiku wa manane wakati watu wengi walikuwa wamelala.
Kumetokea matetemeko mengine madogo matano mda mfupi baada ya tetemeko hilo kuu.
Idara ya kusimamia maswala ya chini ya radhi inasema kuwa tetemeko hilo lilitokea sehemu ya juu pekee, hali ambayo husababisha madhara makubwa zaidi.

06 February, 2016

Magari 2 yakamatwa yakihusishwa na wizi ofisi ya Kamishna Mkuu TRA

Sirro
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna Simon Sirro.
Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kukamata magari mawili yakihusishwa na wizi katika ofisi ya kamshina mkuu wa TRA huku yakiwa na vifaa vilivyoibiwa katika ofisi hiyo vikiwa ni pamoja na komputa, na TV.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kamanda Simon Sirro amesema kutokana na oparasheni kali iliyokuwa ikiendeshwa na jeshi ilifanikiwa kuwatia nguvuni watuhumiwa wanne wakiwa na vifaa vilivyoibiwa.
Aidha kamanda huyo wa kanda maalum ya Dar es Salaam amesema katika oparesheni hiyo pia jeshi la polisi lilifanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi milioni 150 mali ya Bw Ahmed Huwel mkazi wa Msasani.
Katika hatua nyingine Kamanda Sirro ametangaza kusitishwa kwa muda kwa shughuli za ulinzi shirikishi katika vituo vya polisi kutokana na vikundi hivyo kualamikiwa na wananchi kwa kutokuwa na tija katika jamii.

05 February, 2016

Kakatika kwa umeme mara kwa mara ni kutokana na uchakavu wa miundo mbinu


Serikali  imesema tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara nchini linatokana na uchakavu na kuzidiwa kwa vituo vya kupoza umeme na miundombinu ya usafirishaji na usambazaji nishati hiyo.
Katika kukabiliana na tatizo hilo Tanesco inachukua hatua za kujenga mifumo ya njia kubwa za umeme wa msongo wa kilovoti 400 (Iringa- Dodoma-Singida-Shinyanga), gridi ya Kaskazini Mashariki (Dar es Salaam, Chalinze,Tanga –Arusha), ya Kaskazini Magharibi (Geita- Kagera –Katavi- Kigoma- Rukwa na Mbeya) na Makambako- Songea wa kilovoti 220.
Kauli hiyo ilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani wakati akijibu swali la Mbunge wa Magu, Boniventure Kiswaga (CCM). 
Kiswaga alitaka kufahamu serikali imejipangaje kukabiliana na tatizo la kukatika katika kwa umeme.
Pia mbunge huyo alitaka kufahamu, Je serikali itakamilisha lini kupeleka umeme katika vijiji vya jimbo hilo ikizingatiwa mpaka sasa ni asilimia 20 tu ya vijiji ndiyo vina umeme. 
Kalemani akijibu swali hilo, alisema tatizo la kukatika kwa umeme linatokana na uchakavu na kuzidiwa kwa miundombinu ya kupoza umeme pamoja na matukio ya kulipuka kwa transfoma yanayosababishwa na radi hasa kipindi cha mvua pamoja na wizi wa mafuta ya transfoma unaofanywa na wananchi wasio waaminifu.
Alisema Tanesco inakamilisha upanuzi wa usambazaji wa umeme katika majiji makubwa ya Arusha, Dar es Salaam, na Mwanza ambapo kazi hizo zitahusisha ujenzi wa njia mpya za umeme na kupanua vituo vya kupoza umeme.

“Kukamilika kwa kituo cha kupoza umeme cha KIA mkoani Kilimanjaro kumeimarisha upatikanaji wa umeme maeneo ya Mirerani na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA),” alisema Kalemani.

Pia vituo vya kupoza umeme katika jiji la Dar es Salaam vya Gongo la Mboto, Kipawa, Mbagala, na Kurasini vitaunganishwa kwa njia ya sakiti mzunguko kutoka Ubungo na Kinyerezi kuanzia Machi mwaka huu.

04 February, 2016

Makamanda wa juu wa wanamgambo wa Islamic State wameingia nchini Libya


Makamanda wa juu wa wanamgambo wa Islamic State wameingia nchini Libya miezi ya karibuni wakitokea Iraq na Syria,Afisa wa maswala ya intelijensia nchini Libya ameeleza.
Afisa huyo ameliambia Shirika la utangazaji la uingereza  BBC kuwa wapiganaji wa kigeni wameingia mjini Sirte.
Wawakilishi kutoka nchi 23,wakiwemo wa kutoka Marekani na Uingereza wamekutana Rome siku ya jumanne kujadili tishio la wanamgambo wa IS nchini Libya.
Hali ya kutokubaliana kwa serikali hasimu nchini humo imesababisha jitihada za kupambana na IS kugonga mwamba.
IS iliudhibiti mji wa Sirte mwaka jana.mji huo ulikuwa makazi ya aliyekuwa Kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi.
Kundi la IS linaaminika kuungwa mkono na wale waliokuwa watawala wa utawala uliopita.
Lakini Ismail Shukri, mkuu wa idara ya intelijensia mjini Misrata, ameiambia BBC kumekuwa na wapiganaji wengi wa kigeni miezi ya karibuni.
Wengi wa wapiganaji wa IS ni wageni kwa asilimia 70. Wengi wao ni raia wa Tunisia,wakifuatiwa na Misri, raia wa Sudan na wachache kutoka Algeria.
Pia Raia wa Iraq na Syria, raia wengi wa Iraq wanatoka kwenye jeshi la Saddam Hussein.
Shukri amesema makamanda wa IS wamekimbilia Libya,kutokana na matukio ya mashambulizi ya anga nchini Iraq na Syria.
Mamlaka mjini Misrata zimesema zinajiandaa kupambana na IS mjini Sirte.

02 February, 2016

Seneta wa Texas Ted Cruz amemshinda Trump mchujo wa Iowa

Trumpeneta wa Texas Ted Cruz ameshinda mchujo wa uchaguzi wa mgombea wa uchaguzi wa Republican katika jimbo la Iowa, Marekani.
Huo ndio mchujo wa kwanza katika uchaguzi wa urais wa 2016 ambao utafanyika baadaye mwezi Novemba.
Mfanyabiashara Donald Trump alikuwa akiongoza kwenye kura za maoni kabla ya kura kupigwa lakini sasa dalili zinaonyesha kwamba atakuwa wa pili.
Seneta wa Florida Marco Rubio anaonekana kufanya vyema kuliko ilivyotarajiwa, na huenda akamaliza nambari tatu.
Kura za mchujo wa chama cha Democratic bado zinahesabiwa.
Asilimia 85 ya kura ambazo zimehesabiwa zinaonyesha pengo kati ya Hillary Clinton na mshoshialisti wa chama cha Democratic Bernie Sanders ni 1% pekee.
Akizungumza baada ya matokeo kujulikana, Marco Rubio amempongeza Bw Cruz na kusema ndiye mgombea ambaye anaweza kuunganisha chama cha Republican ambacho kimegawanyika.CruzWagombea wawili wamejiondoa kinyang’anyironi.
Duru za karibu na mgombea wa Democratic Martin O'Malley, aliyekuwa gavana Maryland, zimeambia BBC kwamba atasitisha kampeni yake, na kufanya ushindani mkali sasa kuwa kati ya wagombea wawili.
Upande wa Republican, gavana wa zamani wa Arkansas Mike Huckabee ameandika kwenye Twitter kwamba atasitisha kampeni yake.

01 February, 2016

Muungano wa Afrika AU hautatuma kikosi cha walinda amani hadi pale serikali ya rais Burundi


Msemaji wa Muungano wa Afrika AU, amesema kuwa umoja huo hautatuma majeshi ya kulinda amani nchini humo hadi pale watakapopokea mwaliko kutoka kwa taifa hilo la kanda ya Afrika Mashariki.
Kauli hiyo ni kinyume na pendekezo la awali la umoja huo ambao uliibua taharuki kuhusu uhalali wake na wajibu wake wa kulinda maisha ya wananchi.
Mjumbe maalum wa umoja huo kanda ya maziwa makuu Ibrahima Fall, anasema kuwa haijawahi kuwa nia ya AU kutuma walinda amani, bila ya idhini ya taifa husika.
Mkutano wa viongozi na marais wa Afrika huko Ethiopia ulishindwa kupitisha mswada uliohitajika ilikuwatuma wanajeshi wapatao 5000 kulinda amani nchini Burundi kufuatia mauaji ya mamia ya wapinzani wa rais Nkurunziza.
Machafuko nchini humo yalitibuka baada ya Nkurunziza kutangaza nia ya kuwania uchaguzi katika muhula wake wa tatu.
Wapinzani wake walisema Nkurunziza alikuwa anakiuka katiba ya taifa na kisha maandamano yakaanza kukotokea hata jaribio la mapinduzi ambayo ilizimwa na kisha rais huyo akaibuka mshindi katika uchaguzi ambao ulisusiwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa wa upinzani.
Kulikuwa na pendekezo la kutuma kikosi cha wapiganaji 5,000 wa muungano wa Afrika ilikuokoa maisha ya wapinzani wa rais huyo.
Awali rais Nkurunziza alionya kuwa majeshi yake yangewakabili vikali jeshi hilo ''Vamizi'' akisema kuwa nchi hiyo iko salama na kuwa ni vitongoji vichache tu vya Bujumbura ambavyo ni ngome ya upinzanani.
Kauli ya mwaka jana wa Nkurunziza kuamua kuwania urais kwa muhula wa tatu ilisababisha vurugu nchini humo, ambapo mamia ya watu wameuwawa na wengine wengi wakitorokea mataifa jirani.

Marekani kutowa msaada zaidi kwa Ethiopia kukabiliana na ukame

Mkulima nchini Ethiopia katika eneo la Megenta  Afar, Ethiopia, Januari,  2016.
Idara ya misaada ya maendeleo ya Marekani USAID, imetangaza kutowa dola millioni 97 ya msaada wa dharura kwa Ethiopia kusaidia kukabiliana na mzozo unaoendelea wa kibinadam, ulosababishwa na athari za mfumo wa El Nino.
Serikali ya Marekani inasaidia waethopia kukabiliana na athari za El Nino na msaada wetu wa ziada utasidia kujenga juhudi za kushugulikia hali hiyo inayoendelea, alisema mratibu wa USAID Gayle Smith, katika taarifa ilotolewa jana.
Idara ya USAID inaeleza kuwa hali ya jotojoto ilotanda katika bahari ya Pacific, imeathiri kwa kiasi kikubwa mifumo ya hali ya hewa , na  kuharibu uzalishaji wa kilimo, na kufanya maisha kuwa magumu, na kadhalika usalama wa chakula miongoni mwa watu masikini na dhaifu.
USAID inaeleza kuwa msaada huo unajumlisha zaidi ya tani elfu 176 ya chakula ambacho kitasambazwa kwa waethiopia na wakimbizi takriban millioni nne.
Katibu mkuu wa umoja mataifa Bw Ban Ki Moon, alionya jana kuwa Ethiopia inakumbwa na ukame mbaya kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 30. Alisema, kiwango cha dharura kinachokabiliwa na Ethiopia ni kikubwa mno kwa taifa moja kuweza kukabiliana nayo pekee yake.
Umoja mataifa unaeleza kwamba watu millioni 10 wanahitaji chakula huko Ethiopia, na kuongezea kuwa, idadi hiyo inaweza kuongezeka maradufu katika kipindi cha miezi 9.

29 January, 2016

Wagombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani wamemkejeli Donald Trump baada yake kususia mdahalo

Trump
Wagombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani wamemkejeli Donald Trump baada yake kususia mdahalo wa kupeperushwa runingani katika jimbo la Iowa.
Aliamua kusususia mdahalo huo wa shirika la Fox News baada ya shirika hilo kukataa kumuondoa msimamizi wa mdahalo Megyn Kelly, ambaye Bw Trump amemtuhumu kwa kuwa na mapendeleo.
Mfanyabiashara huyo tajiri badala yake aliandaa hafla ya kuchangisha pesa, za kuwasaidia wanajeshi wastaafu.
Wapiga kura jimbo la Iowa watapiga kura Jumatatu kuchagua mgombea wao katika kila chama.
Lakini kutokuwepo kwa Trump katika mdahalo huo mjini Des Moines kulijitokeza wazi, na wagombea saba wanaoshindana naye walihisi kutokuwepo kwake.
Seneta wa Texas Ted Cruz aligusia hilo kwa ucheshi dakika za kwanza za mdahalo na kuwakejeli wapinzani wake.
"Mimi ni wazimu na kila mtu katika jukwaa hili ni mjinga, mnene na asiyevutia, na Ben [Carson], wewe ni daktari mbaya wa upasuaji,” alisema, huku akijaribu kumuiga Trump, ambaye hakuwepo.
Gavana wa zamani wa Florida Jeb Bush pia alimchokoza mfanyabiashara huyo tajiri kutoka New York, ambaye amekuwa akimshambulia Bw Bush midahalo ya awali.
"Kwa kiasi fulani namkosa Donald Trump; alikuwa mwanasesere wa dubu kwangu,” alisema huku akitabasamu.
Mengine makuu yaliyojitokeza:
  • Seneta wa Florida Marco Rubio alitetea msimamo wake wa awali wa kufunga misikiti ambayo inatumiwa kueneza itikadi kali
  • Pia aliahidi kuvunja mkataba wa nyuklia na Iran siku ya kwanza akiwa rais.
  • Seneta wa Texas Ted Cruz alisema: "Nitawawinda Isis [IS] popote walipo na kuwaangamiza "
  • Gavana wa New Jersey Chris Christie alisema hajui lolote kuhusu misongamano ya magari ambayo inadaiwa kusababishwa makusudi na wasaidizi wake
  • Gavana wa zamani wa Florida Jeb Bush amesema wanajeshi wa Marekani waliowahi kupigana vijani wanafaa kupata heshima zaidi kuliko wanavyopata sasa chini ya utawala wa Obama
  • Seneta wa Kentucky Paul alieleza wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa mchango wa Marekani kijeshi nchini Syria
Kwingineko mjini Des Moines wakati uo huo, Bw Trump ameongoza mkutano mkubwa wa kutoa heshima kwa wanajeshi wa Marekani waliostaafu
“Unaponyanyaswa, lazima usimame na kutetea haki zako,” amesema, akirejelea mzozo wake na Fox News.
“Lazima tusimame kidete kama watu na kutetea taifa letu iwapo tunanyanyaswa.”
Wengi katika mitandao ya kijamii walionekana kukubali kwamba mdahalo huo wa Fox News ulimkosa sana Trump.
Lakini wengine walisema kukosekana kwake kulisaidia wagombea wengine, ambao hawajakuwa wakisikika kutokana na ‘ubabe’ wa Trump, kusikika.
Uchaguzi wa Iowa Jumatatu ijayo utakwua mtihani wa kwanza kamili kwa wagombea, na mwanzo tu wa msururu wa uchaguzi wa kuwachagua wajumbe wa vyama vya Republican na Democrats.
Kinyume na uchaguzi wa kawaida wa wagombea, ambapo kura za siri hupigwa, uchaguzi wa Iowa huwa ni mkutano wa wagombea wa vyama waliosajiliwa ambao kwanza huwajadili wagombea na kisha kupiga kura zao.
   Source:BBC

27 January, 2016

Elimu dhidi ya Ebola yawaponza vijana


Watu watatu wamepelekwa hospitali kaskazini mwa Siera leone wakiwa na majeraha yaliyotokana na kupigwa risasi baada ya kulumbana na askari juu ya mambo gani wanapaswa kuzingatia ili kuepukana na Ebola.
Polisi wamesema walirusha mabomu ya machozi baada ya vijana hao kuvamia kituo chao huko mjini Barmoi,eneo ambalo mtu mmoja alikufa kutokana na Ebola wiki iliyopita.la Nchi ya Siera leone ilitangaza kuwa iko huru na ugonjwa huo kabla ya kifo hicho kutokea.
Vijana walikuwa na hasira juu ya kufungwa kwa soko katika mji mmoja nchini humo lakini utawala ulitanabahisha kwamba ulisimamisha shughuli hizo za kibiashara kuendelea sokoni ili waweze kubaini watu watatu walipotea huku wakiwa wameathirika na ugonjwa huo.

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...