31 October, 2015

Wewe ni mtumiaji wa vilevi? haya ni mambo ya muhimu unayopaswa kufahamu kuhusiana na Vilevi


“Haiuzwi kwa wenye umri chini ya miaka 18, kunywa kistaarabu” ujumbe huu unapatikana katika matangazo yote ya vilevi, na nadhani hilo linatambulika kwamba pombe si ya vijana chini ya miaka 18. Unywaji wa pombe ni kawaida kwa watu wengi lakini unakunywa kistaarabu? Sina mpango wa kukufundisha kunywa pombe wala kukushawishi uanze kunywa Pombe wote tunajua madhara yanayoletwa kwa unywaji wa pombe wa kupindukia. Leo tuongelee upande wa pili wa shilingi, faida za unywaji wa pombe kwa wastani. Narudi unywaji wa pombe kwa wastani.
Magonjwa ya Moyo.
Utafiti kutoka  Harvard University  Marekani, umegundua unywaji wa pombe kwa kiasi cha wastani kinasaidia mzunguko mzuri wa damu,hii inasaidia kuzia matatizo ya moyo na magonjwa ya kiharusi na kupooza (stroke)
Urefusha Maisha
Utafiti uliofanywa na Catholic University  huko Campobasso, waligundua kuwa kunywa chupa chini ya 4 au 2 kwa siku kwa mwanamme au mwanamke,  kwa asilimia  18 inaongeza muda wa kuishi kama  ililipotiwa na Reuters. Dr. Giovanni de Gaetano  wa Catholic University  pia alisema sio mbaya kama unaweza kunywa pombe kidogo wakati wa kula. Makala nyingine iliyoandikwa na Mediterranean diet, kuwa mvinyo (wine) ni kinywaji safii wakati wa chakula cha mchana na cha jioni. Lakini usinywe tu pombe wakati wote.
Inasaidia kuamsha Hisia za Mapenzi
Kama ilivyo Red Wine inasaidia kupunguza kasi ya magonjwa ya moyo, Mwaka 2009 jarida lililotambulika kama Sexual Medicine, liliandika kwa utafiti waliofanya  asilimia 25 – 30 wanywaji wa pombe hawapati matatizo ya kushindwa kushiriki tendo. Mkuu wa utafiti , Kew-Kim Chew Mtaalamu wa magonjwa ya mlipuko kutoka University of West Australia alifanya utafiti kwa wanaume  1,770 wa Australia,  Chew aliwashauri pia wanaume hao wasitumie pombe kupitiliza sababu bado wanafanya utafiti juu ya swala hilo kwa kina zaidi.

Pombe huamsha Akili
Utafiti uliohusisha watu zaidi ya 365,000 toka mwaka 1997 iliripotiwa na jarida la Neuropsychiatric Disease and Treatment watu wanaokunywa kwa wastani wanauwezo wa kuzuia ugonjwa wa Alzheimer na magonjwa mengine ya akili. Kiwango kidogo cha pombe kinafanya seli za ubongo ziwe hai (fit/active) alisema Edward J. Neafsey, Ph.D mwandishi wa Science Daily. alisema pia hawashauri watu wasiokunywa pombe waanza kunywa pombe. Na akasema kama wale wanaokunywa wanakunywa kwa wastani basi itawasaidia.
Husaidia Tatizo La Mawe kwenye Kibofu
Kwa wanywaji wa wastani kuna uwezekano wa kupunguza uwezekano wa kupata  tatizo la mawe kwenye kibofu huo ni  utafiti uliofanywa na University of East Anglia, watafiti walisema faida zinaonekana kwa wale wanywaji wa kawaida na sio waywaji wa pombe kupinduki  sababu unywaji wa pombe kupitiliza huleta matatizo ya kiafya
Ugonjwa wa Sukari
Tafiti zilizofanywa uholanzi,  watu wenye afya wanao kunywa glass moja au mbili kwa siku wanapunguza uwezekano wa kupata aina ya pili ya kisukari ukiachilia mbali wale wasiokunywa hata kidogo, wale wanaokunywa kidogo wana afya zaidi, walisema watafiti hao kupitia Reuters.
Angalizo kujua faida hizi za pombe haina maana kama hujaanza kunywa pombe uanze sasa na kama wewe unatumia kilevi basi kunywa kwa kiwango kidogo sababu ni faida kwa afya yako kuliko unywaji wa kupindukia. Kunywa kistaarabu.

Wanaume waliowahi kufaidi mwili wa Kim Kardashian kabla hajaolewa na Kanye West


Kimberly Noel Kardashian, maarufu kama Kim Kardashian , mke wa Rapa maarufu Marekani    Kanye West pia ni mama wa mtoto wao North West, couple maaarufu sana  duniani kote. Kanye West na Kim walifunga ndoa mei 24 mwaka 2014 huko fort di Belvedere Florence mjini  Italia. Kim na Kanye ni moja kati ya couple zinazoongelewa sana duniani kote.

Kim alianza kufahamika sana miaka ya 2007 baada ya kuonekana kwa video yake akifanya mapenzi na mpenzi wake wa zamani Ray J, baada ya umaarufu huo yeye na familia yake ilianza kuonekana kwenye kipindi cha television kilichoitwa keeping up with the Kardashian kipindi ambacho kimeingiza dollar milioni 53 hadi mwaka huu 2015.
Kabla ya Kanye West, Kim Alishaolewa mara mbili, na huu ni mtililiko wa mahusiano yake.
2000 – 2004 Kim aliolewa na producer wa muziki Damon Thomas

2006 Kim alitoka na Ray J Norwood Mdogo wa Brandy Norwood, Ray J ndie aliesambaza picha na video za utupu akiwa na Kim.

2006 Hiyo hiyo Kim aliachana na Ray na kutoka na Nick Lachey  ambae ni mcheza filamu mwanamuziki,mwandishi,mtunzi na producer

2006 mwishoni hadi mwanzo wa 2007 Kim  alitoka na Nick Cannon Kabla hajamuoa Mariah Carey ambae ni mama wa watoto wake mapacha.

2007 Kim alitoka na Reggie Bush Staa wa NFL (National Football League) Julai 2009 wakagombana na kupatana septemba 2009 na waliachana mwanzoni mwaka 2010

2010,Juni  hadi  septemba mwaka huo huo, alitoka na Mchezaji Miles Austin

2010 Kim alitoka na model Gabriel Aubry ambae alikuwa ameachana na mcheza filamu maarufu Halle Berry.

2010, Disemba kim alitoka na Staa wa NBA Kris Humphries, Kris alimchumbia Kim Mei 2011,wakaoana mwezi wa 8 mwaka huo  2011, na wakaachana Oktoba 31, 2011 moja kati ya ndoa zilizodumu muda mfupi zaidi katika historia

Rihanna apata dili la bilioni 54 kutoka kampuni ya simu ya Samsung

rihanna
Rnb staa Rihanna ambaye kwa sasa yupo kwenye matayarisho ya mwisho ya kutoa album yake mpya ya ANTI amepata dili kubwa la kampuni ya Simu ya Samsung.
Rihanna ametia wino dili lenye thamani ya dola milioni 25 ambayo ni kama bilioni 54 za Tanzania ili Samsung wapate nafasi ya kudhamini Album yake na ziara atakazofanya Rihanna katika kutangaza album hio.
Jay Z na meneja wa Rihanna ‘Jay Brown’ walikuwa na mchango mkubwa kwenye kufanikisha dili hilo.
Rihanna atatumika kupromote biashara za Samsung kama Galaxy na mashabiki watatuma video za show za Rihanna kwenye App ya Samsung ya Milk Music App.
Hii sio mara ya kwanza Samsung kufanya kazi na Roc Nation, awali walidhamini album ya Jay Z ‘Magna Carta.. Holy Grail’ na waliisambaza kupitia simu za Galaxy.

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...