23 January, 2016

NEW: JUMA NATURE & CANNIBAL – KIDA LUSO ( MUSIC AUDIO)

Mkongwe wa muziki nchini Tanzania maarufu kama Juma Nature ambaye anatokea kundi la wanaume Halisi, mwenye miondoko yake ya ki-Cartoon, kwenye tasnia ya muziki wa Hip Hop Tz ameachia wimbo mpya unaoitwa ‘Kida luso’ akiwa na Cannibal. Take your time to Enjoy with us the good music here

ratiba ya ligi kuu uingereza leo january 23, 2016

Image result for ratiba ya ligi kuu uingereza leo january 2, 2016
Saturday 23 January

Norwich 12:45 Liverpool

Crystal Palace 15:00 Tottenham

Leicester 15:00 Stoke

Manchester United 15:00 Southampton

Sunderland 15:00 Bournemouth

Watford 15:00 Newcastle

West Bromwich 15:00 Aston Villa

West Ham 17:30 Manchester City

Je PEP GUADIOLA atakwenda MANCHESTER UNITED ?

Guardiola- man u
Manchester United wamekanusha kwamba walikutana na boss wa Bayern Munich Pep Guardiola kuhusu uwezekano wa kuchukua mikoba ya bosi sasa Louis van Gaal, baada ya soka Ufaransa kusema kuwa mkutano ulifanyika jana mjini Paris, lakini United wamesisitiza kuwa hadithi hizo sio za kweli.
Guardiola, 45, ataondoka Bayern Munich mwisho wa msimu huu huku akisema kuwa anataka kufundisha soka nchini England.
Manchester City ndio wanaopewa kipaumbele kumnasa Mhispania huyo, lakini Chelsea na Manchester United wao pia wamekuwa wakihusishwa pamoja na kutaka kupata huduma ya bosi huyo.
Bayern Munich wapo katika kambi ya mafunzo mjini Doha katika mapumziko ya baridi huku ligi kuu nchini Ujerumani ikitarajiwa kurudi tena wikend hii ambapo Bayern Munich watacheza mchezo wao dhidi ya Hamburg siku ya Ijumaa.
Guardiola, ambaye mkataba wake na Bayern unafikia tamati katika majira ya joto, hapo awali alisema ana nia ya kufundisha soka nchini England, hali iliyosababisha presha kubwa kwa makocha wa timu za City na United ambao timu zao hazina muelekeo mzuri sana katika ligi.
Tayari Pep Guadiola amewaomba radhi makocha nchini England kama kauli zake za kutamka kutaka kufundisha soka nchini England zimesababisha presha miongoni mwao.

CHAN: Tunisia yatoka sare na Nigeria

Tunisia
Mechi za mkumbo wa pili Kundi C katika michuano ya kombe la taifa bingwa Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani zimemalizika kwa klabu zote kutoshana nguvu.
Nigeria walitangulia kwa kutoka sare ya 1-1 na Tunisia mjini Kigali.
Bao la Nigeria lilitingwa wavuni na Elvis Chikatara dakika ya 51.
Tunisia walihakikisha wanaondoka na alama moja baada ya kusawazisha kupitia Ahmed Akaichi dakika ya 69. Akaichi alikuwa ametumbukiza mpira kimiani kwa kichwa dakika ya kwanza lakini alikuwa ameotea.
Kwenye mechi ya pili, Issa Moussa alifungia Niger bao la kwanza nao Guinea wakapata lao kupitia Alseny Camara.
Ammadou Issa, aliyekuwa ameingia uwanjani kama nguvu mpya, aliweka Niger kifua mbele dakika ya 49.
Aboubacar Bangoura hata hivyo alikomboa bao hilo na mambo yakasalia hivyo hadi kipenga cha mwisho kilipopulizwa.
Kwa sasa Nigeria wanaongoza kundi hilo na alama nne, Tunisia na Guinea wakifuata wakiwa na alama mbili kila mmoja, nao Niger inavuta mkia ikiwa na alama moja pekee.
Mechi za mwisho Kundi C zitachezwa Jumanne wiki ijayo ambapo Nigeria watacheza dhidi ya Guinea nao Tunisia wacheze dhidi ya Niger.

Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imetangaza tarehe ya marudio ya uchaguzi

Zec
Uchaguzi huo sasa utafanyika Jumapili tarehe 20 Machi.
Tangazo hilo limefanywa na mwenyekiti wa ZEC Jecha Salim Jecha.
Bw Jecha amesema tarehe hiyo iliamuliwa na tume baada ya mkutano hapo jana.
"Uchaguzi huo utahusisha uchaguzi wa Rais, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani na hakutakuwa na uteuzi mpya wa wagombea wala mikutano ya kampeni," amesema Bw Jecha.
"Wagombea wote walioteuliwa hapo awali wataendelea kuwa wagombea katika uchaguzi huu."iongozi wa chama hicho walisusia maadhimisho ya Siku ya Mapinduzi wiki iliyopita.
Chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilikuwa tayari kimewashauri wanachama wake visiwani wajiandae kwa marudio ya uchaguzi, tangazo lililoshutumiwa vikali na viongozi wa CUF.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi Ya Januari 23


22 January, 2016

Kama ulikosa U Heard ya leo..Zari kaamua kujibu kwa wanaomsema mitandaoni kuhusu mtoto sio wa Diamond


Wiki hii inaisha huku kukiwa na stori kubwa zilizoanzia kwenye mitandao ya kijamii, majibizano yaliyofanya mpaka ishu ya watu kutaka DNA ya mtoto wa Diamond Platnumz na Zari iwekwe wazi ili ijulikane kama kweli ni mtoto wake.
Diamond alijibu hii ishu kwenye exclusive interview, na pia Soudy Brown kaamua kumtafuta Zari kusikia pia anachukuliaje hizo story za mitandaoni.
ZARI II
Zari kasema kachoshwa na maneno kuhusu mtoto wao Tiffah, kwanza hawahusu chochote kwa hiyo hata kama ni mtoto wa Diamond au sio wake, wanaozungumzia DNA hawamhusu chochote.
Kingine Zari amesema wana mtoto huyo mmoja lakini yuko tayari hata kuwa na watoto watatu na Diamond.
Soudy BrownMakorokocho‘ na Zari utawasikia kwenye hii U Heard niliyorekodi na kukusogezea sauti yake hapa, bonyeza play uipate

Tyga Addresses Rumors Of Texting An Underage Girl & Dating A Transgender Actress (VIDEO)

tygaCalifornia rapper Tyga has been caught in numerous rumors over the last year. There was the transgender actress Mia Isabella claiming she was once in a relationship with Tyga, and 14-year-old singer Molly O’Malia accused Tyga of making her “uncomfortable” by texting her.
The creator of the recently released Rawwest N*gga Alive mixtape stopped by Streetz 94.5, and he was asked about all the tabloid stories surrounding him. Tyga first addressed the O’Malia situation.
“That girl that said she was 14 – I feel like when you’re on social media, a lot of people are models, singers, artists trying to get discovered,” said Tyga. “It was like, ‘Damn, you can’t talk to a person or give a person a break. That’s what I thought was kind of crazy. It was nothing to hide. That’s why I put the texts out to let people know.”
Host Jazzy McBee then asked Tyga about the stories he was dating Isabella. Again, the Young Money affiliate fought back against the accusations.
“I didn’t even know at one point. I’m like, ‘Damn, you’re making this sh*t up.’ Somebody really got something against me up top somewhere,” suggested Tyga.
He added, “You just brush the sh*t off. It’s a new story every day. At the end of the day, I’m living my life, and the people around me know what’s real and know how I move.”

JINSI YA KUISHI NA MWANAUME/MKE MWENYE GUBU.

how to deal with nagging spouse 8020fashions 3
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumbani haitoshi, au akichelewa kurudi mke wake humsingizia John kuwa ana wanawake wengine huko nje ndio kisa cha kuchelewa kurudi nyumbani, hata John akitoka na marafiki pia ni tatizo kubwa.
John anasema muda mwingine anatamani hata aanze kumpiga mke wake kwakuwa mambo anayolalamika au anayoyasema si ya kweli. Mke wake anashindwa kuuliza maswali kwanza bali anaanza kulalamika na kumsingizia vitu vingi.
John anasema alianza pole pole kufanya vitu mke wake alivyokua akimsingizia kwani alianza kuchelewa kurudi nyumbani ili asikutane na mke wake, na baadaye akapata mwanamke mwingine na kuanza kunywa pombe.
John anasema matendo aliyoyafanya yalifanya ndoa yake izidi kuharibika na mke wake ndio alizidisha gubu.
Hili jambo hutokea sana kati ya wanandoa na sio mwanamke tu anayekua hivo, hata wanaume nao, Gubu, malamiko lazima itatokea katika mahusiano, inategemea tu ni jinsi gani mnaweza kuihandle na kuzuia matatizo makubwa zaidi.
how to deal with nagging spouse 8020fashions
JINSI YA KUISHI NA MWANAUME AU MKE MWENYE GUBU sio rahisi lakina inawezekana,
  • Kwanza kabisa unatakiwa uwe msikivu, hili tatizo linaanza pale mwanaume/mke akiwa na malalamiko lakini mwenzako hawi msikivu. Hii itapelekea mwenzako kuona kuwa huna time naye na hujali vitu anavyokwambia, na hivyo huyo mtu ataanza kulalamika na kufiria sababu zingine kabisa za kwanini humsikilizi kama vile kuwa na mpenzi mwingine nje ya mahusiano yenu.
how to deal with nagging spouse 8020fashions 4
  • Jaribu kuwa muelewa, kama mambo yameshakuwa mabaya kati yenu jaribu kuwa muelewa, acha kujibu malalamiko ya mwenzako kwa kufoka au kwa vurugu. Jaribu kufikiria ni kitu gani kinachomfanya mwenzako awe hivo na kuongea nae.
  • Kwa wanawake mpunguze dharau, hasira na malalamiko yasiyo na mbele wala nyuma kwa waume zenu, na msizue matatizo yalipita. Focus katika tatizo lililopo ili muweze kulisolve.
  • Kwa wanaume, mnatakiwa kuwasikiliza wake zenu, sikiliza malalamiko waliyokuwa nayo, myaongelee na kuyasolve matatizo.

Young couple has breakfast at italian café
Wanandoa wakishindwa kutatua matatizo kama haya, chuki inakua kati yao na ndoa inazidi kuwa chungu, na matumaini ya kusolve matatizo kati yao yanakuwa hamna tena, na hii inaweza kuwa mwisho wa mahusiano yao.
Wewe je, unaishi na mwanaume au mwanamke mwenye gubu? Unawezaje kuishi nae, au unafanya nini ili kuweza kumhandle na kuepuka matatizo kati yenu?

Davido asaini mkataba na label ya Sony Music

Davido amekuwa msanii wa kwanza Afrika kusaini na label ya Sony music global.
Davido signs new deal with Sony Music.

Japo bado hajatangaza zaidi kuhusiana na mkataba huo lakini kupitia Instagram aliandika,
“To all those that doubted me!! it’s a done deal! 1st african artist to sign a global record deal !! my story is just starting!! my mother is smiling in heaven right now!! sony music entertainment !! owo ti wole.” 
Davido ameungana na wasanii wengine ambao wapo chini ya lebel hiyo ikiwemo Future, Travis Scott,  Carrie Underwood, kundi la Fifth Harmony na wengine.

New Video: AY – Zigo Remix Feat. Diamond Platnumz [Official Music Video]

aytzAY ameachia video mpya ya Remix ya wimbo wake Zigo aliomshirikisha Diamond Platnumz, Video imetengenezwa chini ya Studio Space Pictures.

Yanga yaizamisha Majimaji

Yanga 4
Amis Tambwe ameibuka shujaa kwenye mchezo wa Yanga vs Majimaji baada ya kutupia kambani goli tatu (hat-trick) wakati Yanga ikiibuka na ushindi wa bao 5-0 na kupaa tena hadi kileleni mwa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.
Yanga walianza kupata bao lao la kwanza kupitia kwa Thabani Kamusoko ambaye alipachika bao hilo dakika ya nne kipindi cha kwanza kwa kutumia makosa yaliyofanywa na golikipa wa Majimaji FC David Burhani aliyesogea mbele na kuliacha lango lake wazi.
Yanga 1
Bao hilo lilidumu hadi dakika zote za kipindi cha kwanza kinamalizika Yanga wakiwa mbele kwa bao 1-0 dhidi ya Majimaji.
Donald Ngoma alipachika bao la pili dakika ya 50 kipindi cha pili na kuiweka Yanga mbele kwa bao mbili mwanzoni mwa kipindi cha pili.
Yanga
Gharika ya magoli ilianza baada ya Majimaji kuruhusu bao la pili, kwani Amis Tambwe ndiyo ukawa muda wake wa kutafuta (hat-trick) nyingne kwenye ligi ya msimu huu. Dakika ya 60 Tambwe alizama wavuni kuiandikia timu yake bao la tatu huku likiwa ni bao lake la kwanza kwenye mchezo wa leo.
Tambwe alipachika bao jingine la pili akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Deus Kaseke ambaye alimuwekea krosi Tambwe naye akaitupia kwenye nyavu. Mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Burundi alikamilisha hat-trick yake dakika ya 84 baada kupiga goli safi kufuatia beki wa Majimaji kujiangusha kwenye eneo lake la hatari na kutoa mwanya kwa Tambwe kufunga goli kwa urahisi.
Yanga 2
Mchezo wa jana ulikuwa ni wa pili kwa Kally Ongala tangu akichukue kikosi cha Majimaji akiwa kama kocha mkuu wa timu hiyo na kujikuta akiambulia kichapo cha nguvu kutoka kwa Yanga.
Mchezo wa jana ni wa pili kwa Majimaji kupoteza kwa idadi kubwa ya Magoli wakati mchezo wao wa kwanza kupoteza kwa kipigo kikubwa ulikuwa ni dhidi ya Simba walipokubali kulala kwa bao sita.
Yanga 3
Kikosi cha Yanga: Deogratias Munishim Kelvin Yondani, Juma Abdul/Said Juma ‘Makapu’, Oscar Jushua, Vicent Bossou, Salum Telela, Simon Msuva/issoufou Boubcar, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma/Paul Nonga, Amis Tambwe na Deusi Kaseke.
Kikosi cha Majimaji: david Burhani, Alex Kondo, Bahati Yusuph, Mpoki Mwakinyuke, Sadiq Gwaza, Lulanga Mapunda/Kened Kipepe, Peter Mapunda/Hassan Hamisi, Paul Mahona/Gogfrey Taita, Marcel Bonaventura, Sixmund Mwakasega na Frank Sekule.
Matokeo ya mechi nyingine zilizopigwa jana kwenye viwanja tofauti na uwanja wa taifa ni kama ifuatavyo:
Mwadui FC 2-1 Kagera Sugar
Mtibwa Sugar 0-0 African Sports

Bomu lalipuka katika mgahawa Somalia


Bomu lililotegwa ndani ya gari limelipuka nje ya mgahawa mmoja uliopo katika ufukwe wa bahari katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu,kulingana na maafisa wa polisi.
Walioshuhudia wamemwelezea mwandishi wa BBC Ibrahim Aden kwamba gari hilo lililojaa vilipuzi liligonga mgahawa huo maarufu wa Lido Beach kabla ya watu watano kujitokeza na kuanza kufyatua risasi.
Haijulikani iwapo kumekuwa na majeruhi.
Hakuna kundi lililokiri kutekeleza shambulizi hilo,lakini kundi la Alshabaab ndilo linaloshukiwa kwa kutekeleza mashambulizi mengine kama hayo hapo awali.
Mgahawa wa Lido Beach uliopo pembezoni mwa Mogadishu,huwavutia maelfu ya vijana wa Somalia wanaojifurahisha.
Migahawa kadhaa imefunguliwa katika ufukwe huo katika miaka ya hivi karibuni.
Afisa mkuu wa polisi katika eneo hilo Meja Abdiqadir Ali amekiambia chombo cha habari cha reuters kwamba shambulio hilo lilitokea katika lango la mgahawa huo.
Amesema kuwa uchunguzi unaendelea.
  CHANZO:BBC

Asilimia 65.67 wamefeli katika somo la Kiingereza mtihani darasa la nne


Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), limetangaza matokeo ya mitihani ya kujipima ya darasa la nne huku matokeo hayo yakionyesha wanafunzi wengi wamefeli katika somo la Kiingereza kwa asilimia 65.67 katika mitihani hiyo iliyofanyika mwishoni 2015.

Akitangaza matokeo hayo jana Jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt. Charles Msonde amesema juhudi za makusudi zinahitajika katika kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzia ili kuboresha kiwango cha ufaulu.

Jumla ya wanafunzi 869,057 kati ya wanafunzi 977,886 sawa na asilimia 88.87 waliofanya upimaji wamepata alama katika madaraja ya A,B,C,na D. Wanafunzi 108,829 sawa na asilimia11.13 wamepata alama za ufaulu usioridhisha.

Aidha wanafunzi wamefanya vizuri zaidi katika somo la Sayansi kwa asilimia 89.44, na baraza limewataka walimu kuweka mkazo zaidi kwa wanafunzi waliofanya vibaya ili wawasaidie kuimarika na waweze kupata ufaulu mzuri.
 ==>Bofya Hapa Kuyaona Matokeo

RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI AWASILI MKOANI ARUSHA APOKELEWA NA UMATI WA WANANCHI KIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege wa KIA mkoani Kilimanjaro leo huku akiongozana na Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha Mhe.Daudi Felix Ntibenda tayari kwa hafla ya kuwatunuku kamisheni maafisa wapya wa jeshi la Wananchi waliohitimu vyema mafunzo yao katika chuo cha Jeshi Monduli Mkoani Arusha itakayofanyika Januari 23 /2016. PICHA NA IKULU 
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akishiriki kupiga ngoma za utamaduni wakati alipowasili kwenye uwa nja wa ndege wa KIA mkoani Kilimanjaro leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi waliofika kwenye uwanja wa ndege wa KIA mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya kumlaki uwanjani hapo.Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na wananchi waliofika kumlaki kwenye uwanja wa ndege wa KIA mkoani Kilimanjaro. Baadhi ya wananchi wakimpungia mikono Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa KIA mkoani Klimajaro.Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi waliofika kumlaki uwanja wa ndege wa KIA mkoani Kilimanjaro.Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ukiondoka kwenye uwanja wa ndege wa KIA kuelekea Arusha mjini.

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...