29 June, 2015

Wema Sepetu Amtaja Mtu Anayemzuia Kupata Mimba


.Ishu ya  Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu kutopata ujauzito imeshazungumzwa mara kadhaa na hata yeye mwenyewe alishawahi kujitokeza na kuizungumzia lakini safari hii amelizungumzia kwa njia tofauti. Wema ambaye pia ni muigizaji wa filamu, awali alisema sababu kubwa ya kutopata ujauzito ni
masuala ya kiafya lakini safari hii ametoa kauli tata ambayo inahusiana na imani za nguvu za giza.Wema ambaye alifunguka hayo hivi karibuni, anadai kuwa yawezekana marehemu Steven Kanumba anahusika kwenye suala hilo.
“Unajua hili suala la mtoto linanisumbua sana yaani na linaniuma kwa sababu napenda watoto sana na pia napenda kuitwa mama, nimehangaika sana katika kuhakikisha nafanikiwa katika hili lakini ndiyo hivyo imeshindikana.
“Serious! Ilifika kipindi yaani nilikuwa nachukia nilipokuwa nikiziona siku zangu, nilikuwa sipendi kukutana na hiyo hali kwa sababu naumia sana lakini ndiyo hivyo baada ya kuhangaika sana inabidi nimwachie Mungu tu. Nahisi kukata tamaa lakini bado sijakata tamaa.

“Watu wananiambia mimi bado mdogo kwa hiyo sitakiwi kuwa na wasiwasi sana ila muda unakwenda, sasa nina miaka 27. Niliwahi kupata mimba mwaka 2008, aliyenipa alikuwa marehemu Kanumba, lakini baadaye ilitoka na aliposikia hivyo (Kanumba) alikasirika kwa kweli.

“Lakini baadaye ikawa kawaida, hata nilipokuja kuachana naye, bado alikuwa rafiki yangu na tulikuwa tunaongea vizuri na kupigiana simu kama kawaida ila alikuwa ananiambia ‘unajua una deni, nakudai watoto wangu na nitafanya juu chini ili unilipe’.

“Basi ikawa kawaida yake kuniambia hivyo, wiki chache kabla ya kufariki aliniomba tuonane lakini haikuwezekana kutokana na ratiba zetu kutofautiana.

“Kuna muda huwa nafikiri au mizimu yake inahusika katika hii ishu! (anacheka sana).

“Unajua ile mimba ya Kanumba hata mimi sikuwa tayari kupata mtoto wakati ule, niliona ndiyo kwanza naingia kwenye mapenzi halafu ndiyo nimetoka kuwa miss tu, sasa itakuwaje, lakini huwezi jua labda pengine kwenye ‘abortion’ walivuruga baadhi ya vitu ndiyo maana mpaka leo imekuwa hivi.”
Usisumbuke Mawerenewz.blogspot.com ndio mtandao wako wakipekee unaokupa habari za BURUDANI,MICHEZO, SIASA, na HABARI MBALIMBALI ZA KIMATAIFA pamoja na KITAIFA Endelea kutembelea MTOKA MBALI pia nifuate twitter>>>@mawere3, facebook>>>Mawere Mtoka Mbali, Instagram>>>mawere_mtoka_mbali,

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...