14 May, 2016

Download Music: Ben Pol - Moyo Mashine

 

Ni mfululizo wa wasanii wa bongo flava kuachalia new hits song zao, na baada ya kutoa Video ya wimbo huu, "Moyo Mashine" hii ndio Audio ya Moyo Mashine kutoka kwa mkali huyu wa muziki aina ya R&B BenPol.

13 May, 2016

Sema naye, mwambie ukweli usimwogope.

Habari gani mpendwa msomaji wa Mtokambali? week-end ndiyo hiyoo imekwisha fika na kama ilivyo ada lazima tabasabu litawale kwa baadhi ya wafanyakazi ambao hawakupata muda wa kupumzika kwa takribani siku tano.

Leo nmepanda hapa MTOKAMBALI nikiwa na swala moja tuu ambalo mara nyingi hunitawala katika fikra zangu na hata kuyaona kwa macho yangu na jambo hilo ni "Uoga katika kumwambia mtu Ukweli ama la Moyoni"

Kuna wale vijana wenzangu mtaani huwa naonaga wakiitwa Madomo zege na Wengine niliwahi kusikia wakiitwa nyoka Kibisa(Yaani hawana sumu), nashindwa kutambua hali hii maana nakuawa na maswali mengi kichwani juu ya jambo hili yakwamba Je ni uoga wa kumwambia mtu? je ni Aibu ya kumwambia mtu kitu? ama je ni nini hasa kinachomfanya mtu kuwa katika hali hiyo?(Embu tuongee kidogo hapa)

 Leo acha nikuambie ndugu yangu...

Nafahumu kwamba moyo wa mtu siyo wa chuma bali ni nyama, na kila mwanadamu ana haki ya kupendwa na hata kupenda pia.. ila linapo kuja swala la Mapenzi moyo huo huo hujeuka sega la asali ama kujeuka chungu kama shubiri na ndivyo mapenzi yalivyo.

Ila kwa kuwa tumeumbiwa kupenda, hatupaswi kuunyima moyo kile unacho stahili, sasa je ni kwa nini uogope kuuupatia moyo kile unacho kipenda? Je hufahamu kwamba faraja na furaha huja kutoka moyoni?

Kuna wale vijana wenzangu ambao humpenda mtu kwa dhati kabisa na hata kudhamiria kuwa na mtu fulani katika maisha yake ila anaogopa kumwambia mtu yule. Na hii nimeiona hasa kwa Vijana wa kiume, mara nyingi wamekuwa wakitamani kuwa na wachumba wazuri wenye hadhi flani ila wamekuwa wakijikuta katika wakati mgumu pale wanapo taka kufunguka.

 Utakuta mtu ana maswali meengi katika moyo wake kwamba je atanionaje? je si atanitukana? je si atanikataaa?

Kakuambia nani kwamba yule unaye mtaka takufanyia hayo unayowaza? Ndiyo yawezekana ukaambiwa hayo maana kuna watu wengine huwa na hulka ya kujiskia kwamba wao ni bora zaidi ila kabla hujafikia huko na wewe jiulize je ukimwambia na akakubali utajiskiaje?(Aibu ama furaha?)

Na ndiyo maana leo hii nakupa mambo kadhaa ya kufanya ili kuondokana na hiyo hali na mwishoni kupata kile ulicho kitamani katika maisha yako.

1.Acha kuwa na maswali mengi yasiyokuwa na majibu 

Yale maswali ya Atanionaje, hatanitukan? hatani fanyeje tafadhali yawekwe pembeni. Acha nikuambie tuu ukweli mpenzi msomaji, hakuna jambo linalo umiza katika ulimwengu wa leo kama Mapenzi. Mapenzi upofu, mapenzi ukichaa mapenzi uchizi. Ukitaka kumla bata uache kumchunguza.

2.Funguka mbele ya macho yake (say it to his/her face)

Kipekee mimi huwa napenda mtu ambaye huniambia hisia zake mbele ya uso wangu kuliko yule anaye tumia njia kama simu ama njia nyingine ile. Watu wengi pia hupenda hivyo, na kwa maana hiyo basi huna budi kutenga muda wako na kukutana na mtu ambye unampenda ila unaogopa na kisha mwambie.

3.Jiamini.

Kitika mapenzi bwana hakuna mambo ya uoga, wewe kuwa jasiri na kujiamini kisha mfute na kumwambia ukweli juu ya moyo wako, mweleze na yeye atakusikiliza bila hiyana.

4.Kuwa muwazi.

Unajua ni bora kuwa muwazi wakati wote maana watu watujua namna ya kukusaidia kuliko kuficha ficha mambo na mwisho wa siku unaumia moyo wako bure pasipo kuwa na msaada.

5.Usi sikilize ya watu we fanya yako.

Japo unapaswa wakati mwingine kusikiliza watu wana sema nini, ila wakati mwingine hupaswi kuyasikiliza maana ya mwanadamu ni mengi na mengine ni yakuvunja moyo. Nafahamu kuna vijana wengine kazi yao ni kuvunja vijana wengine moyo hachelewi kukuambia yule mwanamke ni Malaya, mhuni ama nini. Kwa namna hiyo basi jiepushe na hali hiyo.


Kwa kusema hayo nimalizie kwa kusema "Usione sooo sema nae, mwambie ukweli. Tukutane tena hapa hapa Mtokambali nyumba ya maajabu na visa, mtaa wa burudani na hamasa kwa vijana.

Kanuni 9 za mafanikio kutoka kwa Steve Jobs

  http://allaboutstevejobs.com/index/index.jpg

Steve Jobs ni moja kati ya watu walio wahi kuwa Maarufu katika ulimwengu wa teknologia na Amekuwa mfano wa kuigwa na kazi zake zimekuwa changanoto katika ulimwengu wa Sayansi. Watu wengi wamekuwa wakihamasika kupitia speech zake alizokuwa akitoa katika mikutano mbali mbali ya kibiashara na hata katika teknologia Alifariki mnamo mwaka 2011 akiwa na umri wa mika 56 Soma zaidi kuhusu maisha yake kwa ujumla >> Mfahamu Steve Jobs mwanzilishi wa kampuni ya Apple

 Mimi nimekuwa mmoja kati ya watu ambao wamekuwa wakihamasika kutokana na speech za Job na ndio maana mpaka leo nzaidi kumfuatilia maana nafahamu sinto weza kukosa kitu kutoka kwake, namaanisha "ukitaka kunukia basi kaa karibu na Waridi"

   Basi leo acha nikupe mambo tisa ya kujifunza kutoka kwa Steve Jobs

1.Follow your heart(Futa nafsi yako.)

Embu kuwa na maono juu ya kile unacho kiamini kwamba unakiweza, weka malengo yako ambayo yatakufikisha kule uliko tamani kufika siku zote za maisha yako, fanya mwenyewe ili kuyaona machungu ya kazi yako pasipo kuingiliwa na mtu yeyote. Amini kama unaweza. Kumbuka mafanikio hayaji kwa kukata tamaa bali huja kwa kuongeza nia na ghadhabu katika kazi zako.

Almost everything–all external expectations, all pride, all fear of embarrassment or failure–these things just fall away in the face of death, leaving only what is truly important. Remembering that you are going to die is the best way I know to avoid the trap of thinking you have something to lose. You are already naked. There is no reason not to follow your heart.

2.Trust yourself(Jiamini peke yako)

Tunapo kuja katika kipengele hichi ni lazima mtu ajikubali kwanza kwamba anaweza kusimama yeye kama yeye katika Vission(maono yake) na zaidi ya yote aweze kusimama katika kutimiza ndito zake kwa vitendo, hivyo swala la kujiamini la muhimu sana. Umeamua kufanya biashara na kuacha kazi ofisini usiogope we fanya biashara maana kile ulicho kitaka katika maisha yako yote kitakuwa katika hiyo biashara endapo tuu utaamua kufanya hivyo. Njia nzuri ya mtu kujifunza ni kufanya makosa na kisha kujifunza kutokana na makosa..

 You can’t connect the dots looking forward; you can only connect them looking backwards. So you have to trust that the dots will somehow connect in your future. You have to trust in something — your gut, destiny, life, karma, whatever. This approach has never let me down, and it has made all the difference in my life.

3.Love what you Do(Penda kile unacho kifanya.)

Mafanikio siku zote huja kwa kupenda kile unacho kifanya, naamini kabisa endapo utapenda kile unacho kifanya kwa moyo wako na akili zako basi chance ya wewe kufanikiwa ni kubwa kuliko yule ambae anafanya kitu ambacho moyo wake hauridhiki. Ngoja nikupe mfano hai( Mimi nilipo hitimu chuo cha mafunzo ya Utabibu, niliamua kuti kujihusisha na mambo ya hosipitalini pamoja na Madawa na badala yake niliamua kuwa Blogger.... mmh maajabu eeh!) hii yote ilisababishwa na mimi kuamini kwamba mafanikio yangu yatakuja katika kile nachopenda kukifanya(Blogging). 

Your work is going to fill a large part of your life, and the only way to be truly satisfied is to do what you believe is great work. And the only way to do great work is to love what you do.

 4.Go for a home run

Kitika maisha yako yote kamwe usizarau ubora. Ubora ni zaidi kuliko kiasi. Fanya kazi zko kwa bidii na hakikisha unazalisha mazao yenye Ubora na siyo tuu bora mazo. Umeamua kufanya kitu basi hakikisha umekitendea haki. Jambo hili litakuletea mafanikio makubwa katika maisha yako.

Be a yardstick of quality. Some people aren’t used to an environment where excellence is expected. One home run is much better than two doubles.

5.Fanya uchaguzi kwa makini(Pick carefully)

Kuwa bize, fanya mambo yako, futa yale mambo ambayo ni ya msingi tuu achana na hayo menine, muda wako mwingi uwe ni wakujifunza mambo ya maendeleo tuu, epuka vitu vinavyo kusabisha kupoteza muda mfano kuangalia Tv kwa muda mrefu, Kufuatilia habari za udaku, kupoteza muda mwingi kwenye social medias ukitafuta new updates n.k. 

People think focus means saying yes to the thing you’ve got to focus on. It means saying no to the hundred other good ideas that there are. You have to pick carefully.

6.Work hard to make it simple.

Kuna nguvu yakutengeneza kile unacho kiamini kwamba ndicho utakacho kifaya katika maisha yako. Fanya kazi kwa bidii na mwisho wa siku utasimama mbele ya umati wa watu na kuzungumza kitu chenye sura na mtazamo chanya wa kazi yako. Pangilia magumu yako yote katika kazi zako na kisha yatendee kazi na kuyatatua na mwisho wa siku kila kitu kitakaa katika mstari wake kama inayo takiwa kuwa.

Design is not just what it looks like and feels like. Design is how it works. Simple can be harder than complex. You have to work hard to get your thinking clean to make it simple.

7.Iba/iga/chukua idea kubwa( Steal great ideas).

Unajua wakati mwingine kama kitu kimekupendeza na kinaendana na wewe, siyo mbaya ukakichukua na kukifanyia kazi kikamilifu. Jifunze Mengi kutika kwa watu wenye fikra kubwa , fanya mengi ya kuiga kutoka kwao na mwishoni na wewe utaweza kubadilisha idea zile zikawa mafanikio yako na ikawa ni rahisi kwako wewe kuwa pahala ulipotamani kuwa katika maisha yako yote.

We have always been shameless about stealing great ideas.

 8.Lengo lako lisiwe ni Kutengeneza hela kwanza (Your goal isn’t to make money).

Usiweke pesa mbele bali tumia muda wako kutengeneza na kukuza jina pamoja na kazi zako. Watu watakuja kuiga ujuzi na kukuukiza maswali na kujifunza kutoka kwako na mwisho wa siku pesa zitakuaja tuu(Kizuri cha jiuza na kibaya chajitembeza, na pesa huja baada ya mafanikio).

Apple’s goal isn’t to make money. Our goal is to design and develop and bring to market good products. We trust as a consequence of that, people will like them, and as another consequence, we’ll make some money.

9.Usipoteze Tumaini(Don’t lose faith)

Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, bayana yasiyo onekana. Unapokua ukifanya kazi zako, kuna muda uanatamani kukata tamaa na kupoteza tumaini.. lakini hupaswi kuiruhusu hali hivyo iwepo katiaka kazi zako. Kumbuka pale unapokuwa ukikata tamaa, ndipo mafanikio yako huwepo ama huwa karibu. Jiulize na kujitazama ulikotoka na hapo ulipo.

Sometimes life hits you in the head with a brick. Don’t lose faith.


Kwa leo nimetia nanga na meli iko ufwekweni, ni matumaini yangu umejifunza kitu katika post hii,ningeomba unachie maoni ama ushauri hapo chini kama utakuwa nayo, basi tukutane tena panapo majaliwa ya Mwenyezi Mungu.

12 May, 2016

New Video: Ben-Pol "moyo mashine"

Kwa muda mrefu sasa Ben-Pol amekuwa akizidi kutamba katika game la Muziki wa r&b hapa nyumbani na Africa mashariki kwa ujumla wake, na leo katuletea Video mpya inayo kwenda kwa jina la Moyo Mashine aloifanya huko Bondeni kwa Mzee Mandela.

Download Music: Alikiba Ft. M.I - Aje

 
 Alikikiba leo katuletea single yake mpya inayokwenda kwa jina la "AJE" akimshirikisha vyema Rapper M.I kutika kule Nigeria.

11 May, 2016

Acha kuogopa maisha, Thubutu kufanya...

“Kuzaliwa Masikini Sio Kosa Lako, ila Kufa Masikini ni Kosa Lako Kubwa Sana”Msingi wa kufanikiwa ni kuthubutu kufanya jambo fulani kwa mfano kufungua miradi, kufanya biashara, kusoma kwa bidii na mambo mengine kibao.


Ngoja nikuulize tena, maana najua utakua ushaulizwa hili swali mara nying, Hivii unatamani kuishi au uwe kama nani ? wengi wetu mtasema natamani kuishi maisha mazuri na bora.


Hii iko hivi unapozungumza na watu wote duniani kila mtu atakwambia kuwa anataka kuwa na maisha mazuri ,huenda na ni vigumu kwa mtu wa kawaida kusema anataka maisha yake yawe ya shida kila siku. Huyo atakua ana lake.Wewe una stashahada una shahada na elimu nyingine nyingi, sijui umeahudhulia workshop kama ishirini, ila ndugu yangu bado utaendelea kuchapwa bakora na maisha kama hautakuwa makini na kuthubutu kufanya mambo unayotamani kufanya.


 Kusoma sana ama kidogo kuwa na marafiki waliofanikiwa ama wasiofanikiwa,kwenda nje ya nchi ama au kuzaliwa katika familia masikini au tajiri bado sio tiketi ya kukufanya uwe na maisha bora .


Kuna watu kwa mfano unaweza kuona anakata tamaa eti kisa amezaliwa katika familia maskini kitu ambacho sio sahihi.Bill Gates alisema “Kuzaliwa Masikini Sio Kosa Lako, ila Kufa Masikini ni Kosa Lako Kubwa Sana”


Yaani anamaanisha duniani kuna fursa nyingi sana ambazo unaweza kuzitumia na kuwa na maisha unayoyataka.


Kuwa na maisha bora ni kufanya kazi kwa bidii na  kwa malengo zaidi usiishi tuu ilimradi siku zinaenda mbele. Kwa chochote unachokifanya kifanye kwa kutafakari na kuangalia faida na hasara yake.

Yapo mambo mengi ambayo yameweza kuzungumzwa ambayo yanaweza kukusababishia wewe kusonga mbele kimaisha lakini hata ukisoma mambo mengi yanayohusu mambo ya kimaisha bila kuthubutu kufanya kitu unachotaka kufanya ni kazi bure.


 Inabidi kuwatathimini watu ambao wanakuzunguka, kuanzia marafiki, majirani, na hata baadhi ya ndugu.Kuna wengine hata ukimwangalia sura yake tu anaonekana wazi kuwa hana furaha unapomwambia kuwa mambo yako yanakwenda vizuri kwa sababu watu wengi wanapenda kusikia kuwa unaishi maisha ya shida ndio wengi walivyo na wakijua hivyo ndio unaongeza uoga wa kuthubutu kufanya kazi. Sijui kwa nini hii inatokea, lakini achana na hao wewe kazana kubuni miradi mingi ili uwe na maendeleo bora maana wao kukasirika haikuzuii kufanya mambo yako.


Mafanikio yako yanatokana na akili yako ulionayo maana wengine wamekuwa wakisema kuwa ugumu wa maisha ndio kipimo chako cha akili yako.


Katika jamii tunakoishi utakua ushasikia watu wanalalamika kuwa maisha ni magumu,na hawajui wafanyaje lakini nikwambie kuwa kipimo cha maisha unacho hapo wewe mwenyewe na akili yako. Kama unajua kusoma na kuandika ni tosha kabisa kwa wewe kujiendeleza.


Kwaiyo jamani ni vizuri ukakaa na kutathimini unatamani maisha yako yaweje au unataka kuishi vipi  au maisha yako yakae katika level gani ya kimaisha hapa duniani? Kipimo cha maisha ambayo unataka  kuishi unacho wewe mwenyewe pia uoga wako ndo umaskini wako yawezekana hapo ulipo kaa una wasiwasi ,una uoga ,unawaza una tathimini wakati nguvu unazo, sababu unazo, elimu unayo vifaa pia unavyo. Ila… kwa kumalizia Kitu kimoja tu unahitaji ndugu yangu. “JITUME”.


Ukitaka kuelewa hii angalia wiki nzima iliyopita kama umefanya kitu ambacho kinaendana na mambo ambayo unataka kufaninikiwa maishani mwako. Kama kipo Good… kama hakipo, basi anza kujituma leo… yaani leo namaanisha anza kupanga mikakati, kama serikali inavyoweka mipango na mikakati ya miradi yake kwa wananchi na wewe kaa chini tengeneza mikakati ya maisha yako.


Kumbuka Unapanga mikakati ya maisha YAKO! Sio ya jirani yako ambae anakusema sema kila siku au mlie kosana nae juzi.


PITIA NA HIZI PIA

   >>> Tuzungumze yanayo tusibu na Kupata suluhisho.

  >>>  Viashiria 6 ni kwa nini unatakiwa kubadili Maisha yako Leo.  

 >>>    Furaha ya kweli inaletwa na wewe mwenyewe.


09 May, 2016

Josee Chemelion ni nani?


Who Is Dr Jose Chameleone Moja kati ya Wana muziki nguli katika ulimwengu  wa Burudani ya Muziki kwa upande wa Africa mashariki na Africa kwa Ujumla ni Josee Chemelion.

Jina lake kamili anajulikana kama Joseph Mayanja na alizaliwa mnamo mwaka 1979 Huko nchini Uganda. Josee Chamelion alianza kazi za sanaa mnamo mika ya 1990 nakuendelea wakati akiwa sekondary na alianza kama Mc na Dj kwenye Night clubs..

Baadae alijiunga na Ogopa Djs nchini kenya na Ngoma yake ya kwanza kufanya ilikuwa ikijulikana kama "BAGEYA" mabayo alimsha Mkali mwingine kutoka kenye anaekwenda kwa jina la Red-son.
Aina ya muziki anayoimba Josee ni muunganiko wa ladha za muziki aina zouk, Rumba, na ragga na muziki kidogo kutoka pale Uganda kidogo.

Mpaka ilipo fika mwaka 2013 Chamelion alikuwa teyari ana album zipatazo 12 na album hizo ni Bageya-2000, “Mama Mia” - 2001, “Njo Karibu”- 2002, “The Golden Voice”- 2003, “Mambo Bado”-2004  “Kipepo” - 2005, "shida za dunia"-2006, "sivyo ndivyo"-2007, "Bayunga"-2009, "Vumilia"-2010, "Valu valu"-2012, Badilisha-2013.

Ni Raisi wa Ugandan Music label inayojulikana kwa jina la "Leone Island" ambayo ndani yake kuna wasanii kama Mosses Radio, Wheezle, AK 47 na wakali wengine wengi.

Ni member katika kundi la wasanii nchini Uganda ambalo wasanii hao hutumia majina yao na umaarufu wako kupinga na kupambana na umasikini pamoja na HIV/AIDS,

Tuzo alizo wahi kutwaa ni kama ifuatavyo:-

  • Beffta Awards UK – Best International Act
  • 2003 Pearl of Africa Music Awards (PAM Awards) – Artiste of the Year, Best Male Artist, Best Contemporary Artist & Song of the Year ("Mama Mia")
  • 2004 Pearl of Africa Music Awards (PAM Awards) – Artiste of the Year & Song of the Year ("Jamila")
  • 2005 Pearl of Africa Music Awards (PAM Awards) – Best Afro Beat Artiste/Group & Best Afro Beat Single ("Kipepeo")
  • 2004 Tanzania Music Awards – Best East African Album ("Bei Kali")
  • 2005 Tanzania Music Awards – Best East African Album ("Jamila")
  • 2006 Pearl of Africa Music Awards (PAM Awards) – Best Afro Beat Artiste/Group
  • 2006 Kisima Music Awards – Best Ugandan Song (Mama Rhoda) & Best Ugandan Music Video (Mama Rhoda)
  • 2007 Kisima Music Awards – Best Ugandan Song (Sivyo Ndiviyo with Professor Jay)
  • 2011 Ugandan Radio Dotcom Music Awards – Artiste of The Year
  • 2013 [Kilimanjaro Music Awards] – Best East African Song "Valu Valu"
  • 2014 [Kilimanjaro Music Awards] – Best East African Song "Tubonge"
  • 2014 HiPipo Music Awards – Song of the Year "Badilisha"
  • 2014 HiPipo Music Awards – Best Male ZOUK Song "Badilisha"
  • 2015 AFRIMA Awards - Africa Song Writer of the year 2015

Enjoy video mpya kutoka kwa  Josee Chemelion inayokwenda kwa jina la Agatako.

Hayo ni machache tuu kuhusu nguli huyu wa muziki Africa, Je una maoni gani kuhusu Blog hii? tafadhali nitumie maoni yao katika cooment box na mimi nitayafanyia kazi.

Maajabu ya khanga!

  Na The Bitoz

 Hakuna mwanamke ambaye hajawahi kuvaa khanga, vilevile hakuna mwanaume ambaye hajawahi kufunikwa na khanga (utotoni si ulibebwa )....Yafuatayo ni maajabu ya khanga


1/Historia

Asili ya vazi hili ni pwani ya Afrika Mashariki kama sehemu za Mombasa nchini Kenya na visiwani Zanziba. Ndio walikuwa watu wa kwanza kulivaa vazi hili na kuliheshimu.Haijajulikana ilikuwa ni miaka gani. Kwahiyo historia inaonyesha vazi la khanga limeasisiwa na watu wa pwani ya Afrika Mashariki


2/Fahari ya Mwafrika

Khanga ni fahari kwa wanawake wa kiafrika , Ni vazi ambalo limetumiwa miaka kwa miaka, kizazi kwa kizazi.....ni utambulisho wa waafrika na halichuji !!


3/Linapendwa na rika zote

Khanga ndio vazi linalopendwa na wanawake wa aina zote, vijana kwa wazee, mjini kwa vijijini ....ni mwendo wa kutupia khanga !!


4/Matumizi kibao

Khanga ni vazi lenye matumizi mengi pengine kuliko yote, linatumika kubebea watoto, kufungia ngata,kama kamba.taulo n.k


5/Khanga moko ni shida

Wanawake wakitupia khanga moko mwanaume lazima utoe jicho , khanga moko uswahilini ni balaa hadi kwenye vigodoro....mwanamke khanga!!!


6/Vazi linalosema

Khanga huwakilisha hisia za mvaaji kupitia maneno yaliyoandikwa, kuna vijembe, busara,matusi, hekima n.k

 [​IMG]

Jionee mwenyewe maajabu haya .....

[​IMG]

Mwanamke khanga Babu weeee...


[​IMG] 

Tuzungumze yanayo tusibu na Kupata suluhisho.


Mtu mmoja alipata kusema "Hasara roho, pesa makaratasi" na mimi nasema ni kweli kabisa.
Je una Amani ya moyo mwako? Je uhuru ulio nao unautumiaje? Je ukitazama ndani ya Fikra zako unaona Mafanikio yeyote? Je una imani juu ya ndoto zako? Je una mpango wowote juu ya Kuthubutu kuishi ndani ya Ndoto zako?.....

     Leo nimepanda hapa MTOKAMBALI nikiuliza maswali hayo nikiwa na maana ya kwamba maswali hayo Yamekuwa chachu ya Mafanikio ya mtu yeyote hapa Ulimwenguni,,, Huwezi niambia ya kwamba utaweza kufanikiwa katika mambo yako angali Huna Amani Moyoni mwako wala kufanikiwa wakati umeshindwa kuutumia vyema Uhuru ulio nao ama Kufanikiwa angali hujawahi kuthubutu kufanya chochote juu ya ndoto zako...

Licha ya kuishi katika nchi yenye Uhuru lakini bado kuna vijana wenzangu hawana UHURU katika maisha yao. Wamekuwa wakiishi kama watumwa, wamekuwa wakipoteza hata matumaini yakuishi.. Hii yote inasababishwa na KIFUNGO CHA FIKRA.

Acha nikuambie rafiki yangu,
Hakuna jambo la muhimu na lenye nguvu katika maisha ya mwanadamu awaye yeyote hapa ulimwenguni litakalo weza kuishinda nguvu ya Fikra.(Weka kumbu-kumbu juu ya mstari huu tafadhali).

Kile ambacho unafikiri kwa Muda mrefu ndicho kitakachotokea katika maisha yako. Fikra zako zina nguvu ya uumbaji.. na zaidi ya yote fikra zako ndizo zitakazo kupatia Uhuru wa kweli katika maisha yako na mafanikio tele utayaona. Ila pale unapokuwa mtumwa wa fikra zako, hakika utatamani kuiona Ardhi inapasuka kisha Uingie ndani yake na kupotea katika ulimwengu huuu wenye dhiki tele.

Leo nitakupatia njia ambazo zitakufanya uondokane na Utumwa wa fikra zako na kisha kupata uhuru wa Fikra zako na kufanikiwa kuishi katika baadhi ya ndoto zako. Tambua yakwamba njia hizi nitakazo kupatia, ni njia ambazo nilizitumia mimi kipindi nikiwa Utumwani na hadi Leo nathubutu kusema "NIKO HURU".

Je uko teyari? lets move-on...

       1. Jiamini unaweza
Katika maisha ya mwanadamu ni lazima kila mmoja ajiamini kwamba anaweza. Mwana harakati mmoja aliwahi kusema "Uoga wako ndio umasikini wako". Njia ya kwanza ya kutoka katika kifungo cha fikra zako ni kuamini kwamba unaweza kuleta mabadiliko yeyote katika maisha yako licha ya hali uliyo nayo. Amini kwamba utaweza kuboresha maisha yako yakawa bora zaidi kama tuu utaongeza bidii katika hilo.

       2.Ondoa Mawazo hasi katika maisha yako.
Moja ya maadui wakubwa wa Uhuru wa fikra za mwanadamu na Maisha kwa ujumla ni Fikra hasi(potofu). Fikra hasi huwa na hulka ya kukua kidogo kidogo katika maisha ya mwanadamu awaye yote yule na mwishoni huleta maafa makubwa mno na majuto yale ya mjukuu. Ili kuepuka hali hii unapaswa kuchukulia mambo kwa upande wa chanya zaidi kuliko upande wa hasi... hii itakusaidia sana katika kufikiri kwenda mbele ya mafanikio yako. Fikra hasi hupoteza matumaini siku zote hivyo yakubidi kuziepuka.

      3.Epuka kuchukulia mambo kwa ujumla 
Kuna vijana wengi huchukulia mambo kirahisi kama yalivyo na mwisho wa siku wanajikuta katika hali ngumu mno katika maisha yao. Embu jaribu kuchambua jambo moja moja kwa kina kisha ainisha ni lipi jema na ni lipi baya katika huo ujumla ulio nayo. Kumbuka unapokuwa ukichukulia mambo kwa ujumla, hutopata changamoto yeyote ile ambayo itakufanya Kufikiri kwa kina.

       4.Thubutu kufanya.
Njia nyingine ya kutoka katika utumwa na kuupata uhuru wako ni kuthubutu kufanya kile ulicho nacho katika fikra zako juu ya maendeleo yako. Natambua kila mmoja wetu hapa ana ndoto fulani kubwa katika maisha yake na kama( huna ndoto yeyote katika maisha yako jua una hali mbaya kupindukia..). Je uliwahi kujaribu kuifika hata nusu ya ndoto zako? kama jibu ni ndio basi endelea na safari maana bado kidogo utafika mpendwa na kama bado hujathubutu basi kwa nzia sasa thubutu.

     5.Acha kufanya mambo mengi kwa mawazo yako.
Mwanadamu hajakamilika siku zote na kila mwanadamu ana mapungufu yake , hivyo mapungufu yako wenda ikawa mwenzako anaweza kuyatua na wewe pia unaweza kuyatatua, hivyo utaona ni kwa namna gani utakapo kuwa ukishirikiana na wenzako katika kutimiza mambo yako utafanikiwa zaidi kuliko kufanya peke yako..
       6.Jali muda wako.
Nafahamu kwamba kwa asilimia kubwa mno vijana wengi wamekuwa wakipoteza muda wao katika mambo yasiyo na msingi na mwisho wa siku wanajikuta hawajafanya mambo yaliyo wapasa kufanya kwa wakati ule na kuanza kujuta ni kwa nini..... Embu kabla ya kupata majuto, jaribu kufanya mambo katika muda husika bila hata kupoteza sekunde moja katika Muda wako. "Majuto ni mjukuu"

Kwa kusema hayo, nammba nikwamie hapo na ni matumaini yangu kwamba nimekupatia kile unachokihitaji. Nimejfunza mengi mno katika maisha haya licha ya Umri wangu mdogo nilio nao. Likini kwa kuwa naamini katika ndoto zangu, sioni kama naumia bali nayaona maisha yangu katika Ulimwengu wa mafanikio.

Je umependa somo langu? Tafadhali niachie maoni yako hapo chini.


NINEPENDA PIA UPITIE NA HIZI:-
>>>> Viashiria 6 ni kwa nini unatakiwa kubadili Maisha yako Leo

>>>> Furaha ya kweli inaletwa na wewe mwenyewe.

>>>>  Amani ya Moyoni mwako ndio Kunawiri kwa Uso wako.


08 May, 2016

Video: Shetta - Namjua

Tizama Video mpya ya Shetta inayokwenda kwa jina la Namjua. Mi wimbo wa kwanza wa Shetta alio fanya akiwa mwenyewe baada ya kipindi kirefu akiwa anafanya ngoma na wasanii wengine. Enjoy the Good Video From Shetta - Namjua

Godzilla Ft Mwasiti - First Class

Baada ya kutoa Audio ya First-class, Godzzila akiwa Amemshirikisha mwanadada Mwasiti wametuletea tena Video ya Wimbo huo.  Enjoy the Video.

Video: Jose Chamileone Ft Dejay Pius - Agatako

Jose Chamileone kwa mara nyingine akizidi kuonyesha Ulimwengu kwamba Muziki uko kwenye Damu na ndio maana tangu ameanza Muziki hajawahi kuanguka. Mara hii kaja na Hii video inayokwenda kwa jina la "Agatako" ambayo kaimba na Dejay Pius. AGATAKO ni neno la Kinyarwanda lenye maana ya kumbu kumbu Yenye uzuri Apewayo Mpenzi kama Ishara ya mapenzi na Kukumbukana katika mapenzi yao.

Injoy the Video

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...