Showing posts with label MAKALA. Show all posts
Showing posts with label MAKALA. Show all posts

19 December, 2015

Miaka 9 ya Wayne Rooney na Man United

Nahodha wa Manchester United Wayne Rooney leo anatarajia kutimiza mechi yake ya 500 tangu alipoanza kuitumikia klabu hiyo mnamo 2004.
 
Rooney anatarajiwa kurejea dimbani leo baada ya majeruhi ya enka yaliyomuweka nje katika mechi 3 dhidi ya  West Ham, Wolfsburg na Bournemouth.
Rooney alijiunga na  United kutoka Everton mwaka 2004 kwa ada ya uhamisho ya £25.6m akiwa na miaka 18 na katika mechi yake ya kwanza tu alifunga hat trick yake ya kwanza katika ushindi wa 6-2 vs Fenerbahce.
 
Mshambuliaji huyo mpaka sasa ameshashinda makombe matano ya EPL na moja la Champions League, na tuzo kadhaa zake binafsi.

Wayne Rooney ameshacheza mechi 499 akiwa na jezi za mashetani wekundu, akishika nafasi ya 10 katika listi ya wachezaji waliocheza mechi nyingi zaidi katika historia ya klabu hiyo.


Mpaka kufikia sasa Rooney ameshafunga jumla ya magoli 237 katika mechi 499, katika magoli hayo – amefunga hat trick mara 8.
 Klabu ya Aston Villa ndio timu ambayo Rooney ameifunga magoli mengi zaidi tangu alipoanza kuitumikia United. 
Wayne Rooney amefunga magoli 11 katika mechi 24 vs Manchester City. Idadi hii inamfanya kuwa mchezaji aliyefunga magoli mengi zaidi kwenye Manchester Derby – Baba Kai pia ana rekodi ya kutoa assists 82 katika premier league tu.

12 December, 2015

Sababu 5 Kwanini Neymar Atakuwa Mwanasoka Bora Wa Dunia Miezi Kadhaa Ijayo

Kwa mara ya kwanza jukwaa la Ballon D’or litapata ugeni mpya wakati mshambuliaji wa kibrazil Neymar Dos Santos atakapoungana na wafalme wawili wa tuzo hizo ambao wameitawala tuzo hiyo zaidi ya miaka 8 – Cristiano Ronaldo na Lionel Messi – itakapofika January 2016. Kama isingekuwa siasa za soka basi mbrazil huyo angeweza kushika nafasi ya pili nyuma Lionel Messi. Lakini hii ni ‘era’ mpya ya soka.
IMG_1225.JPGKatika miaka 8 iliyopita Ballon D’or imekuwa inatawalia na Messi dhidi ya Ronaldo, lakini kadri siku zinavyozidi kwenda inaonekana mtu wa kupambana na Messi si Ronaldo tena ambaye umri unamtupa – anakaribia kutimiza miaka 31, Ni Neymar ambaye nyota yake inazidi kung’aa kila kukicha.
Pamoja na kufanya kazi kwa kushirikiana vizuri na washambuliaji wengine wa Barca, pia Neymar ameonyesha anaweza ku-control mechi kama ilivyo kwa Messi, tofauti na Ronaldo.
Wadau na wachambuzi wengi wa michezo duniani wanaamini katika kipindi kifupi kijacho Neymar atakuja kuwa mwanasoka bora zaidi duniani, mimi nikiwepo kwenye kundi hilo na hizi ndio sababu zangu.
  1. Kupafomu vyema Anapokosekana Messi 
281D9A4600000578-3060793-image-a-29_1430309883032Unapocheza pembeni ya Lionel Messi, vitu huenda kiurahisi zaidi. Wakati Messi alipoumia hivi karibuni kwa zaidi ya mwezi mmoja, wachambuzi wengi walikuwa na mashaka na uwezo wa Neymar kuziba pengo na kuisadia Barcelona kama ilivyokuwa kwa Messi. Lakini matokeo yake, Neymar akafanya vizuri zaidi katika kuisadia Barcelona kushinda kila mara na sasa wapo juu ya kilele cha msimamo wa ligi na wamefuzu raundi ya 16 bora wa UEFA Champions League. Kuziba pengo la mmoja wa wanasoka bora zaidi kuwahi kuugusa mpira sio jambo rahisi kabisa lakini kwa namna Neymar alivyohimili presha na kuifanya kazi, inaonyesha wazi dalili za world class player mwenye uwezekano wa kutwaa  Ballon d’Or hivi karibuni.
  1. Uwezo Binafsi
150606223921-neymar-champions-league-final-super-169Yes, ni kweli hivi sasa Neymar amekuwa mchezaji anayecheza kitimu zaidi kuliko ilivyokuwa zamani. Hata kuna wakati timu ikiwa inacheza vibaya, Neymar amekuwa akijitokeza na kuchukua majukumu ya timu kutumia uwezo binafsi kuiletea timu matokeo chanya. Anaweza kuchukua ‘vijiji’  kiurahisi na kuiletea madhara makubwa ngome ya timu pinzani, si rahisi kutabiri nini atafanya wakati mwingine. Ni mchezaji ambaye ni vigumu kumkaba na mbinu zake kali alizonazo miguuni na kadri anavyoendelea kucheza na kupata uzoefu, Neymar yupo njiani kuwa mwanasoka bora zaidi duniani.
3. Uwezo wa Kuwachezesha Wenzie
neymarhighs_sf6ly9x16vcg10w421p262n2m-1425743415Baadhi ya wachezaji  bora duniani wamekuwa bora kutokana na ukweli kwamba wana uwezo wa kuwachezsha wachezaji wenzao. Mchezo wa Neymar huko nyuma ulikuwa umeegemea katika uwezo wake binafsi zaidi na kuna muda alifanya iwe rahisi kwa wapinzani kuzuia dhidi ya timu yao. Lakini kadri siku zinavyozidi kwenda amekuwa sehemu muhimu ya timu, Neymar ameuelewa zaidi mfumo na sasa anawachezsha mpaka wachezaji wenzie. Takwimu zinaonyesha hivi sasa anapiga sana pasi kuliko ilivyokuwa zamani, hili la kupiga pasi limeongeza kutokutabirika kwa mchezo wake na kuzidi kuwapa wakati mgumu wanaomzuia kumkaba. Hili limeleta mabadiliko makubwa katika staili ya uchezaji wa Neymar – pia limemletea mafanikio kuliko mwanzoni.
  1. Influence in the International side :
Neymar of Brazil celebrates his second goal against Turkey during their international friendly soccer match at Sukru Saracoglu stadium in Istanbul November 12, 2014. REUTERS/Murad Sezer (TURKEY  - Tags: SOCCER SPORT)Wanaompinga Neymar wana utetezi wao kwamba mchezaji huyo anafanya vizuri Barcelona kutokana na sapoti ya Messi na Suarez lakini kiwango cha Neymar kinapoangaliwa kwenye level ya timu ya taifa – ushahidi unaonyesha Neymar ndio msingi mkuu wa mashambulizi ya timu ya Selecao. Nahodha huyo wa Brazil ameitawala safu ya ushambuliaji ya timu hiyo na ameiongoza kimafanikio mpaka sasa akiwa na miaka 23 tu. Bado ana safari ndefu kuendelea kuwa na kiwango kikubwa alichonacho. Ameyabeba majukumu ya unahodha vizuri sana na anaamini hivi karibuni ataipa mafanikio Brazil.
5. Kawaacha Mbali Waliokuwa Wanashindanishwa Nae

5Mbrazil huyu amekuwa kiwango cha juu sana msimu uliopita na zaidi msimu huu. Unapojaribu kumlinganisha na wachezaji wa kizazi chake kama Eden Hazard, Antoine Griezmann, Gareth Bale utofauti wa uelewa wa mchezo na kukua kwa Neymar. Anausoma mchezo vyema zaidi kuliko alivyokuwa Santos, anajua wapi anatakiwa kukimbia na mpira na wapi kwa kupasia na hazidishi manjonjo kama ilivyokuwa mwanzoni. Uhamisho wake kwenda Barcelona umemsaidia katika kukua kiuchezaji na kuboreka zaidi katika mchezaji hatari zaidi, hizi ni ishara halisi za mchezaji mwenye ubora wa kuwa bora duniani.

14 October, 2015

KIJANA BADILI MTAZAMO WAKO NA JENGA MAISHA BORA



      Kwanza nipende kukusalimu ewe mtanzania mwenzangu kwa kwakusema uu hali gani? Ni matumaini yangu yakwamba uu mzuima na buheri wa afya ingawaje sii asilimia mia moja ni jambo lakumshukuru  MUNGU kwani hapa tulipo sii kwa akili zetu wala kwa ujanja wetu bali ni kwa neema tuu.
       Basi kwa kuyasema hayo ambayo ni salamu zangu kwako wewe mtoka mbali , twende moja kwa moja kwenye mada yetu ambayo teyari nimeiwasilisha kupitia kichwa cha habari hapo juu yakwamba KIJANA BADILI MTAZAMO WAKO NA JENGA MAISHA BORA.
   Ni wazi kwamba neno MAISHA sii neno geni masikioni mwetu yakwamba kila mmoja wetu amekua akihangaika hapa na pale, usiku na mchana hii yote ni sababu ya maisha. Nuliwahi kumsikia mzazi mmoja akimweleza mwanae yakwamba ” Mwanangu kuwa uyaone” name nikajiuliza, Je akue ayaone nini? Magari au majumba? Kumbe alikua akimaanisha  MAISHA.
     Maisha ya kijana Mtanzania wa leo yamekua kama kitendawili ambacho kimekosa mtu wakukitegua. Je tumpe nani mji ili aweze Kukitegua?  Yapo mamba mengi yanayo sababisha maisha kuwa magumu au yasiyo na mwelekeo kwa vijana walio wengi na mambo hayo yanatokana na vijana wenyewe na mifumo mibovu ya elimu wapewazo nijana hawa huko mashuleni hasa hasa katika shule za msingi na zile za sekondari.
Kijana mwenyewe anawezaje kuyaharibu maisha yake?
   Yapo mambo mengi mno ambayo kijana akishindwa kuyazingatia wakati wa makuzi yake yanampelekea kija moja kwa moja kupoteza mwelekeo wake katika masha. Mambo hayo ni kama vile : kuto kuweka malengo sahihi katika maisha, Kufuata mkumbo,  tamaa mbaya,  na mtazamo hasi tuliyo nayo vichwani mwetu.  Hayo ni mambo baadhi ambayo kijana mwenyewe anaweza kujisabishia maisha yake kuharibika.
    Kutokuwa na malengo. Kati ya makosa makuu ambayo vijana wengi wanafanya ni kutokuwa na malengo katika maisha yao, na ni wazi yakwamba vijana wengi tumejikuta hatuna malengo sahihi katika maisha yetu ya kila siku, unakutana kijana mtaani amekaa magengeni kwanzia mwanzo wa siku hadi mwisho wa siku hana lolote. Kuwa na malengo ni jambo muhimu mno katiaka maisha ya kila mwanadamu na tambua yakwamba kila aliefanikiwa katika maisha alijiwekea malengo thabiti na akayafuatilia vilivyo kuhakikisha yanatimia. Kumbuka yakua malengo yanendana na ndoto ulizo nazo wewe kama kijana. Ili ndoto yako itimia ni lazima uwe na malengo. Sasa pale kijana anaposhindwa kuwa na malengo ya kweli ndipo anapojikuta akihangaika huku na kule bila mafanikio yeyote.  Ikumbukwe kuwa maisha ni vile unavyoishi  na wewe mwenyewe ndiye utakae hamua yakua maisha yako yawe mazuri au mabala “hatma ya maisha yako ipo mikononi mwako kijana”.
   Labda ni kwa nini kijana anashindwa kuwa na malengo hai katika maisha?
Mara nyingi kijana anakua na tamaa na vishawishi visivyokua na maana. Kama nlivyosema malengo yanawekwa kutokana na ndoto alizo nazo kijana sasa kama huna ndoto na msimamo yakwamba usimamie nini hasa katika maisha ili aweze kujikwamua katika hali ngumu yaki maisha. Tama za hapa na pale na kufuata mkumbo ni vitu ambavyo hupoteza ndoto za vijana wengi, inafika pahala kijana anakuwa anatamaini vitu vingine ambavyo vipo njee ya uwezo wake na kumpelekea kuachana na ndoto zake za mwanzoni na kujiingiza katika vitendo viovu ili kuvipata vitu hivyo.
Kutokuweza kufahamu thamani ya muda; Nipende kuchukua nukuu ya mtu mmoja aliye kuwa maarufu duniani kwa kupitia filamu na huyu sii mwingine ni BRUCE-LEE ambae aliwahi kusema “if you truly love life never play with time coz there is your life originate” vijana wengi tumekuwa tukijikuta tukipoteza muda katika mambo yasiyokuwa na tija katika maisha yetu. Jiulize huko kwenye mitandao yakijamii unapokuwa muda wote huo unafaidika vipi?  Ndio  yawezekana kuna kitu unafaidika nacho lakini kiuhalisia jambo hilo halikusaidii kukukwamua huko ulipo kama unvyotarajia. Kati ya mali tulizo nazo hapa duniani moja wapo ni Muda. Muda ukiutumia vizuri hakika utafanikisha malengo kwa wakati unao taka wewe lakini pindi ukiutumia vibaya hakika utajuta kwan muda ukisha kwenda haurudi nyuma kamwe.  Sasa nacho taka kusema hapa ni kwamba muda sio rafiki ndugu yangu.
    Kutokujiami kama tunaweza peke yetu: katika swala lakujiamini, nimekua nikiliona katika vijana tulio wengi yakua tunakua tukishindwa kujiamini kama peke yetu hatuwezi kabisa. Nipende kuwaambia vijana wenzangu kua tukiishi katika misingi yakutokujiamini tutakua tumeshindwa nakuanguka kimaisha. Unakuta mtu ana fursa katika jamii lakini kijana huyo anaogopa kuichukua fursa ile nauifanyia kazi ili iweze kumwokoa hapo alipo. Watu maarufu duniani waliziona fursa kati yao na wakajaribu na hatimae wakafikia kilele cha mafanikio. Ondoa dhana ya uoga na thubutu kufanya na nakuhakikishia utafikia lengo lango. Acha kujiona huna nguvu wala akili na ukifanya watu watakuonaje. We unadhani Mwalimu JK Nyerere angekua na uoga mbele ya wakoloni leo hii tungekua wapi? Ni mfano tuu ambao tunautoa kutoka kwa baba wa taifa Mwalimu JK Nyerere kwani aliionoa fursa yakudai uhuru wa Tanganyika ndipo akajaribu bila uoga na mwisho wa siku leo hii Tanzania tunatembea vifua mbele.
      Kukataa shule; Niliwahi kuulizwa swali na Mtu mmoja swali ambalo liliniumiza kichwa wakati nlipokua natafuta jibu lake na swali hilo ni “do you think education is certificate in your life?” nikuachie nami hili swali ujibu mwenyewe lakini sintokupatia jibu nlililomjibu mtu Yule. Nipende kuambia kijana mwenzangu ambaye una kataa shule katika dunia ya leo tuna kufananisha na kipofu. Leo hii nani atakuajiri kama hauna elimu? Ndio unaweza kwa namna moja ama nyingine ukajiajiri lakini ukweli ni kwamba hata kujiari kunahitaji elimu. Ubongo wa mwanadamu una ujazo wa lita moja na nusu lakini kalamu na karatasi vina weza kuujaza ubongo huo kwa muda mchache mmno. Nakushangaa sana kwani hata maandiko ya MUNGU yametuambia “mshike sana elimu usimwache aende zake maana yeye ndiye mkombozi wa maisha yako”  ni maandiko yakutoka katika vitabu takatifu na sio maneno yangu mimi Mtokambali. Nipende kukuambia kijana mwenzangu Elimu iwe msingi wa maendeleo yako wewe kijana.
          Hayo niliyo yasema hapo juu ni baadhi tuu ya  mambo ambayo yanaweza kukufanya wewe kijan kuharibu maisha yako kwa ujumla. Nakuahidi katika mwendelezo wa makala hii katika mfululizo wa makala zetu hapa MTOKA MBALI nitakuelezea mambo zaidi yatakayoweza kukuangusha wewe kijana katika maisha yako na jinsi gani utaweza kujikwamua kaitika hayo mambo na kutoka katika UTUMWA wa fikra.
Nipende kukushukuru wewe ulie chukua muda wako ulio wa thamani na kusoma makala hii. Nina amini umepata kitu hapo. Nikusihi kaa hapa hapa kwa vitu moto moto.

Makala hii imeandikwa na FRANCI S MAWERE Kwa udhamini wa MAWERE MEDIA GROUP  Limited (MMGLtd),Kwa mawasiliano nasi tafadhaili piga simu namba 0767322193, au tutumie  barua pepe  mtokambali2015@gmail.com.

22 August, 2015

MAKALA: WAKO WAPI MAN DOJO NA DOMOKAYA?

Awali ya yote nipende Kutoa Shukrani zangu za kipekee kwa mwenyezi Mungu kwa kunilinda wiki nzima hata nmepata nafaSi yakuwepo tena leo hii hapa mtoka mbali. Pia nichukue nafaSi hii kuku Shukuru we kamanda kwa kutembelea makala zetu na kuziSoma pia.
   
     Katika makala yetu leo tuna angaza jicho kwa wakali hawa wa bongo fleva ambao miaka ya nyuma waliweza kuzikonga nyoyo za maShapiki  wao vilivyo, na hawa si wengine ni MAN DOJO NA DOMO KAYA. Naweza sema kwamba vijana hawa sii wageni kuwaskia maskioni mwako kwani waliweza kuziteka media tofauti tofauti zenye ukubwa hapa Tanzania na hata nchi za njee kwa vibao vyao vilivyo kua vimejaa ujumbe tele kwa jamii mfano DINGI, BARUA, na NIKUPE NINI. Hivyo ni baadhi ya vibao walivyopata kutesa navyo kipindi cha miaka ya mwanzoni mwa 2000.
    Jambo lakujiuliza ni je wakali hawa wamepotelea wapi?
Ni wazi kwamba leo hii ukipata nafasi yaku onana nao, swali utakalo wauliza ni mbona siku hizi hatuwasikii? Hicho ndicho kilichomo katika fikra za mashabiki wa hawa wakali au ukipenda waite manguli wa bongo fleva. Yawezekana kabisa kwamba hawa jamaa wanatamani kurudi katika game ya muziki nakuwika tena kama ilivyokua mwanzini laki inakua ni vigumu kwani muziki wa bongo fleva unazidi kukua siku baada ya siku na kwa vile ukimya wao kwa muda mrefu bila kusikika, imefanya hata mashabiki wao kuwasahau kabisa. Lakini tukumbuke yakua wahenga walisema "hakuna marefu yasiyo na ncha" yawezekana katika game hii ya muziki wakizazi kipya imekua ngumu na wala sii rahisi kama ilivyokua kipindi cha nyuma ambapo muziki huu haukua na soko ki vile, na kwakusema hivyo ni dhahiri yakua wakali hawa wamepotea kabisa.
 Waliweza kutengeneza vibao vingi ambavyo nimeweza kuvitaja baadhi hapo juu na vingine ni kama vile HISTORIA, WANA KNOCK KNOCK, NIZIKWE HAI, na TASWIRA. Kama kweli wewe ni mpenzi wa muziki wa bongo ni wazi kua vibao hivi vilikukonga moyo ipasavyo na hadi leo unawakumbuka hawa jamaa vilivyo.
      Siwezi sema yakwamba hawa jamaa hawawezi kurudi katika umahiri wao kama mwamzo ila jitihada na juhudi zao ndizo zitawaleta tena kwatika game ya muziki na kuwika tena mbele ya wadogo zao katika muziki huu wa bongo fleva.
  Ni malizie kwa kusema, "Yatupasa kuwakumbuka vijana kama hawa ambao mchano wao katika jamii ni mkubwa mno, tuwape shime pale wanapo anguka ili waweze rudi katika hai zao za kawaida masha kusonga mbele"

 Nipende kukushukuru wewe ulichukua muda wako adhimu na wenye dhamani kwa kukaa kitako nakusoma makala zetu. Endelea kutembelea MTOKA MBALI ili uweze kupata kile unachokitaka.

MAKALA hii imeandikwa na Francis Mawere kwa hisani ya MAWERE MEDIA GROUP Ltd
TUTUMIE email yako kupitia mtokambali2015@gmail.com au piga simu namba 0767322193

16 August, 2015

MAKALA: LIFAHAMU KABILA LA HADZABE KABILA PEKEE LINALOISHI KWA KUTEGEMEA UWINDAJI

Wahadzabe au Wahadza hili ni kabila la Tanzania, linalopatika Kaskazini ya kati ya Tanzania, Wanaoishi karibu na Ziwa Eyasi kwenye bonde la ufa, katika uwanda wa Serengeti.
Kwa mujibu wa takwimu zilizopo zinaonesha wahadzabe wapo watu chini ya elfu moja, huku ikiwa watu 300-400 huishi kama wawindaji. Katika dunia ya sasa wahadzabe ndio watu wanaoishi kwa kutegemea shughuli za uwindaji.
 Historia
Hadza (pia inajulikana kama Wahadzabe, Hadzapi, Watindiga, au Kindiga) wanajiita Wahadzabe - na suffix -Kuwa akimaanisha "watu" katika lugha yao, Hadzane (-ne kuwa suffix kwa "lugha"). Tu Hadza kusema Hadzane, kwa hiyo lugha ni muhimu katika kuamua nani wa kuainisha kama Hadza.

Kwa kutumia ushahidi kutoka chombo jiwe middens, malazi mwamba na mwamba sanaa, zinaonyesha kwamba kabla ya miaka 3,000 iliyopita, watu walioishi katika Tanzania muundo wao wakujikimu na muundo wao wakijamii sawa kabisa na ile ya Hadza. Takriban miaka 2500 iliyopita, watu walionge lugha ya Cushitic walihamia Kaskazini mwa Tanzania; Miaka 1,500 iliyopita, Wabantu kutoka Afrika Magharibi alianza walianzakumiliki Tanzania, na karibu 300 miaka iliyopita,wa wazungumzao Kinailoti kutoka Sudan kuhamia katika kaskazini mwa Tanzania na Hadza wilaya. Kuna makundi kadhaa ya kikabila tofauti kwamba wanaishi katika maeneo yanayopakana kandokando na Hadzabe, ni pamoja Datoga, Iraqw, Wamasai, Isanzu, na Sukuma. 
Lugha
Lugha ya Hadzabe, iitwayo Hadzane, ni jadi inayofananishwa kama lugha ya Khoisan sababu ina Clicks. Hadzane ina variants tatu ya click konsonanti: meno, alveopalatal, na imara. Wataalamu wa lugha wamesema kuwa ingawa inaweza kuwa na ushiriki mchache wa kufanana na lugha ya Sandawe, Hadzane ina cognates chache hivyo ni mara nyingi inachukuliwa kama lugha inayojitenga. Hadzabe Wengi kuongea Kiswahili kama lugha yao. Nafasi ya Kabila ili katika Utalii 
Leo kabila ya Hadzabe ilikuwa kabila maarufu sana, kama iliyo kabila la wamasaii, watalii kutoka nchi mbalimbali hufanya safari zao na kuelekea hadi katika vijiji vya wahadzabe ili tu kujifunza na kujionea namna gani wawindaji hao wanavyoishi.

Shughuli za kitalii ambazo hufanyika katika kijiji cha Wahadzabe
Pamoja na kwenda kuwinda na wahadzabe
  • Kuvua katika Ziwa Eyasi
  • Safari za mtubwi katika Ziwa Eyasi
  • Kutembelea mapango ya wahadzabe
  • Kupata nafasi ya kuijua mimea ambayo wawindaji hawa huitumia kuweka katika mikuki yao.
  • Kutembelea maboma waishio na kupata kusikiliza stori zinazohusu maisha yao  
Ni matumaini yangu umepata kufahamu kabila hili pekee lililobaki TANZANIA. 
Endelea kutembelea mtoka mbali ili uweze kufurahia makala tofauti tofauti zinazochapishwa hapa hapa nyumbani MTOKA MBALI.

 
PITIA NA HIZI PIA
>Mambo 8 unayopaswa kufahamu juu ya Ujio mpya wa iPhone 7
> Oliver Mtukudzi picha Halisi ya Muziki wa Kiafrica.
>Wafahamu madancer Albir Rojas na Sara Lopez wakali wa 'Kizomba dance' 
>ELIMU YA TANZANIA YENYE MFUMO WAKIKOLONI


Makala hii imeandikwa na  FRANCIS MAWERE
PHOTO CREDITS: MANIFESTER BRAND

Jiunge nami na watu 3000 walio chagua kujiunga na MTOKAMBALI ili Kupata Makala zetu kila Week-End

* indicates required

15 August, 2015

MAKALA : MUZIKI WA DANCE TANZANIA UNAKWENDA WAPI?

Ni jambo lakumshukuru Mwenyezi Mungu Muumba wa ulimwengu yakwamba bado ninaishi na nazidi kudunda. Kwani uliwahi kujiuliza Mungu angetudai kulipia PUMZI tunayotumia tungelipia kiasi gani cha fedha? Hakuna mtu angeweza kulipia ADA hiyo.
   Baada yakusema hayo, leo tuje kwenye MAKALA yetu na Leo nitazungumzia MUZIKI WA DANCE TANZANI. Ni wazi kwamba miaka ya nyuma MUZIKII huu ulitamba sana na kila mahali ulipokua ukikatiza basi sikio lako haikosi kusikia muziki huu ila miaka hii yakizazi kipya MUZIKI WA DANCE umeonekana ukipotea licha ya BENDI tofauti tofauti kuendelea kurudishia uhai muziki huu.
    MARA nyingi nimekuwa nikijiuliza maswali mengi yasiyo na majibu pale ninapowasikia watu ambao naamini hasa ni mashabiki wa muziki wa dansi wakilalamika juu ya kupotea kwa muziki huo, licha ya kuwepo kwa bendi ambazo zinajinadi kupiga aina hiyo ya muziki hivi sasa.

   Pengine wafuatialiji hasa wa muziki huu wanaweza kutambua ukweli wa jambo hili hasa kwa kulinganisha zama hizi na zile za Dar International, Moro Jazz, Cuban Marimba Bend ,Kimulimuli JKT, Tabora Jazz, Nyanyembe Jazz na nyingine nyingi ambapo wanamuziki mahiri kama Marijani Rajabu, Mbaraka Mwinshehe, Juma Ubao,Salum Abdalah, walitamba na kuufanya muziki wa Tanzania kujulikana kimataifa.
   Jambo la kujiuliza hapa ni kwa nini muziki wetu wakati huo ulikuwa unakubalika na jamii yote licha ya kuwa kulikuwa na upinzani mkali kutoka kwa muziki wa Zaire (sasa DRC Congo) ambayo nayo wakati huo ilikuwa na wanamuziki vigogo kama Tabu Ley, Luambo Lwanzo Makiadi (Franco) , Abeti Maskini, Mbilia Mbel, Mpongo Love, n.k.

Ukweli wa hili utaujua ukigundua kuwa wanamuziki wa Tanzania kipindi hicho walikuwa hawapendi kuiga kutoka kwa wageni badala yake walisimama imara kupiga na kuulinda muziki wao, ndiyo maana ilikuwa vigumu kutekwa kimuziki na wageni.

Ukirudi nyuma kidogo miaka ya 80 na 90 kulikuwa na msururu wa bendi za muziki huo hapa nchini ambapo licha ya wingi wake, zilisimama imara na kuendelea kutangaza muziki huu kimataifa zaidi ya ilivyokuwa mwanzo.
   Hakuna asiyefahamu ubora wa Bendi za Vijana Jazz wakati huo ikiwa na Hemed Maneti , Super Matimila chini ya gwiji la muziki Dk Remmy Ongara, DDC Mlimani Park ya Cosmas Chidumule, Juwata Jazz ya TX Moshi William, Tancut Almasi ya Kasaloo Kyanga na Kyanga Songa, Bima Lee ya kina Jerry Nashon ‘Dudumizi’ n.k, bendi ambazo kila moja ilipiga muziki wa dansi wa Tanzania kwa mtindo wa wake lakini bado ukawa juu kuliko ule wa kutoka nje.

Lengo letu hapa si kuzitaja bendi hizo lakini kiukweli nyingi kati ya hizo zilikuwa hazifanyi hata matangazo ya barabarani, lakini wapenzi wake walikuwa wanajua mahali ambapo zilikuwa zinafanya maonyesho na kwenda kufurahia burudani ya muziki halisi wa dansi ambao leo haupo tena.

Iko wapi leo Njata Njata , au ni wapi iliko Mwenge Jazz ‘Paselepaa’, Bantu Group ‘Kasimbagu’, Tancut Almas ‘Kinyekinye kisonzo’ ni wazi ukikumbuka haya kama ulikuwa mpenzi wa kweli wa burudani wakati huo lazima chozi litakutoka hasa ukiiona Sikinde ya sasa iliyobaki jina tu, huku ikishuhudiwa muziki wake kumezwa na aina ya muziki kutoka Congo DRC.

Kwa sasa asilimia kubwa muziki wa Tanzania imemezwa na muziki wa Kikongo, kwani kila bendi hivi sasa baada ya wimbo kuisha kinachofuata ni rap ambazo zinachukua nafasi kubwa huku zikiwa hazina ujumbe wowote zaidi ya kusifia watu

Hii ni tofauti na siku za nyuma ambapo mbali na kupata wimbo wenye mashairi mazuri yenye mafunzo kilichokuwa kinafuta baada ya wimbo kumalizika ni kuachia ufundi wa wapiga vyombo kumalizia burudani na kuwafanya mashabiki walioshiba ujumbe vichwani mwao kujimwaga ukumbini kuserebuka.

Hakika hii ilikuwa maana halisi ya dansi. Hebu tuambizane ukweli ni nani ama ni bendi ipi leo inafanya haya niende ukumbi gani ambapo sitakutana na makelele ya rapu za kumsifia mfanyabiashara fulani wa magari ambaye hana anachokijua katika muziki zaidi ya kumwaga hela ukumbini ah ah! Kazi kwenu mnaojiita vijana!

Hakika miaka hiyo ilikuwa ya ukweli kwa dansi la Tanzania kwani mbali na ubora wa bendi na wanamuziki waliokuwa hodari wa utunzi na upigaji vyombo wakati huo pia kulikuwa na Mashindano ya kutafuta bendi bora Tanzania yaliyojulikana kama (MASHIBBOTA), mashindano ambayo kwa kiasi fulani yalikuwa nguzo ya muziki huo ambayo kwa sasa yamebaki historia.

 
Wako wapi waimbaji wa kike muziki wa dansi nchini?

09 August, 2015

MISITU YETU TANZANIA TUNAFAIDIKAJE NAYO?



Kwanza napenda kuchukua fursa hii kumshukuru sana Mwenyezi Mungu, muumba wa mbingu na dunia na vyote vilivyomo tukiwamo sisi wanadamu, kwa mema mengi mno anayonitendea na hasa kwa kutujalia uhai hadi leo hii.
Kwa vyovyote vile bila ya Mwenyezi Mungu kutuwezesha na kututia nguvu sisi wenyewe hatuwezi, bali hali ilivyo ya kimazingira na kimaumbile tutakwama tu, hata hao wanaokwenda angani na kufanya wanayoyafanya huko si kwa uwezo wao tu, bali pia ni kwa mapenzi yake Mola

Nipende kuchua nafasi hii kukukaribisha katika makala yetu leo Juma pili  tarehe 9 mwaka 2015. Leo nitapenda kuzungumzia shwala hili la Rasilimali ya Misitu tuliyojaliwa na Mwenyezi Mungu.
Katika hali ya kawaida ni kwamba Misitu tulionayo inatosha kukidhi mahitaji yetu sote tuliopo karibu na Misitu katika mambo ya uhifadhi wa wanyama pori, kupata vyanzo vya maji, upatikanaji wa mbao kwa ajili ya ujenzi na hata kupatikana kwa kuni kwa ajili ya kupikia kwa wale wengi wetu tunayotumia nishati hii ya kuni.
 Misitu ya asili ni matokeo ya kazi nzuri iliyofanywa na Mwenyezi Mungu tangu alipouumba ulimwengu, ikiwamo sayari hii tunayoishi sisi wanadamu. Kwa maneno mengine, misitu au maliasili zote tulizonazo ikiwa ni pamoja na madini, wanyamapori, samaki na viumbe wengine waishio baharini, ardhi (kwa maana ya udongo), maji (kwa maana ya vijito, mito, maziwa, mabwawa, bahari na ardhioevu), nishati mafuta na gesi asilia ni zawadi tuliyopewa na Mwenyezi Mungu.
   Kwa bahati nzuri Tanzania Bara imebahatika kuwa na eneo kubwa lenye misitu ya asili pamoja na mapori mazuri yenye utajiri mkubwa wa wanyamapori. Kwa takwimu za mwaka 1998 (ambazo sasa zimeboreshwa na matokeo ya mradi wa kitaifa wa kupima na kutathmini misitu ya asili), Tanzania ilikuwa na eneo la misitu ya asili la takribani hekta milioni 33.5.

Kati ya hizo, hekta milioni 13 ni eneo la misitu lililohifadhiwa kisheria (misitu ya hifadhi ya Serikali Kuu (Central Government Forest Reserves) takribani misitu 600 na misitu 200 ikimilikiwa na Serikali za Mitaa (Local Authority Forest Reserves) chini ya halmashauri za wilaya); na zaidi ya hekta milioni 20 ya misitu ya asili bado haijahifadhiwa na kusimamiwa kisheria.

Kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita, vijiji vichache vimeweza kutenga sehemu ya misitu katika vijiji vyao na kuitangaza kuwa misitu ya hifadhi ya vijiji yenye jumla ya hekta zaidi ya milioni saba. Hatua hiyo ni ya kupongezwa maana vijiji husika sasa vina nguvu ya kisheria kusimamia na kutumia misitu husika ipasavyo na hatimaye kunufaika na usimamizi huo, kwa kuongozwa na Sheria ya Misitu na kanuni zake.
Vilevile, vijiji vinayo fursa ya kujiwekea sheria ndogo ndogo kwa lengo la kuimarisha zaidi utekelezaji wa shughuli za kulinda msitu kwa faida yao na Taifa kwa jumla. Pamoja na mafanikio hayo, bado sehemu kubwa ya misitu ya asili ambayo haijahifadhiwa kisheria inapatikana katika maeneo ya vijiji na haitumiki ipasavyo kuviletea vijiji maendeleo endelevu.

Miaka zaidi ya 20 Serikali imekuwa ikitekeleza mpango wa Usimamizi Shirikishi wa Kutunza na Kuendeleza Misitu nchini (Participatory Forest Management-PFM). Dhana ya Ushirikishwaji ni mbinu ya uongozi inayowezesha kupata mchango wa mawazo na ushiriki mzuri kutoka kwa wadau mbalimbali, hasa katika utekelezaji wa shughuli za kujiletea maendeleo endelevu kwa kutumia rasilimali za asili tulizonazo.

Ushirikishwaji husaidia watu kubadilishana mawazo na kufahamu vizuri nini kinaendelea au kinatekelezwa kwa faida yao. Hivyo kwa kuwashirikisha wanavijiji katika masuala yanayohusu maendeleo yao vijijini ni suala muhimu sana na huondoa lawama, pia huongeza motisha wakati wa kutekeleza jambo lililoamuliwa.

Isitoshe, ni wajibu wa kila mdau kuhakikisha kuwa anawajibika ipasavyo katika kutoa mawazo na kufikia uamuzi sahihi ili lengo na madhumuni ya mipango ya maendeleo katika sehemu yao iweze kufanikiwa. Ili wanakijiji au jamii katika ujumla wake waweze kufanya hivyo, ni lazima waelimishwe vya kutosha na kuwajengea uwezo (capacity) wa kusimamia na kutumia kwa misingi endelevu rasilimali na fursa zilizopo ikiwamo misitu ya asili.

Swali lililopo ni je tunafaidika vyema na hizi faida zitokanazo na misitu tulio nayo?
Zipo faida nyingi zitokanazo na Misitu hii tuliyo nayo na faida hizo na kama vile kutumika katika maswala ya ufugaji wa nyuki, hifadhi za wanyama, upatikanaji wa nishati ya kuni na upatikanaji wa mbao ambazo tunatumia katiaka maswala ya ujenzi na maendeleo hapa nchini.
Ni ukweli ulio wazi na usiopingika ya kwamba rasilimali hii haitufaidishi ipasavyo na nathibitisha ukweli huu kwa kutumia mfano mdogo tuu wa upungufu wa MADAWATI mashuleni mwetu hasa zile za msingi. Kimsingi tusingetarajia kuona fedheha na aibu hii kubwa inayotukumba  sisi leo hii Hapa nchini Kwetu. Kuna wakati nilikua natazama taarifa ya habari nikaona habari inayo onyesha watu wa Jamhuri ya watu wa SWITZILAND wakitoa msaada wa MADAWATI katiaka shule Fulani ya msingi huko Dar-es-salaam. Jamani hivi ni kweli tumekosa miti yakuweza kutupatia hayo madawati ambayo watoto wetu wanalizimika kukaa kwenye sakafu na juu ya mawe wakati wakiwa madarasani waifundishwa?
Ufugaji wa nyuki.
  Huo ni mfano mdogo tuu unaonyesha ni jinsi gani bado rasilimali za misitu hapa nchini hatufaidiki nazo ipasavyo.Maoni yangu na mapendekezo yangu ni haya juu ya swala la ukosefu wa madawati mashuleni.
Kwa sasa zipa shule nyingi za UFUNDI hapa Tanzania ambazo zinamilikiwa na serekali na baadhi ya nyingine zinamilikiwa na taasisi binafsi na point ni kwamba Kuna baadhi ya misitu mikubwa ambayo imekomaa na ambayo inaweza kutupatia mbao kwa ajili ya kutengeneza madawati yakutosha.
Kwa nini serekali isivune miti hiyo kwa mujibu washeria na ki sha kutumia ile sera ya “KATA MTI PANDA MITI”  ili kurudisha miti ambayo imevunwa kwa ajili yakutengeneza madawati?
    Inawezekana kabisa kufanya hivyo na kisha mbao kupatikana ambapo mbao hizo zitipelekwa katika vyuo vya ufundi ambapo wanafunzi wanaojifunza ufundi seremala watatengeneza madawati hayo kama sehemu ya  somo  lao darasani. Ni matumaini yangu kila mkoa vyuo hivi vya ufundi vinapatikana na jambo hili linaweza kufanikiwa kwa kiasi Fulani.
Serekali Kwa kupitia wataalamu wa mambo ya misitu waandae miche yakutosha kwa ajili yakupanda sehem zitakazokua zimevunwa miti hiyo.
 Kwakufanya hivyo tutaondoa aibu na tatizo hili la ukosefu wa madawati Katika shule zetu.
 Yasije yakawa yale ya “Penye miti mingi hapana wajenzi.”
  Nichukue nafasi hii kukushukuru wewe ulie chukua nafasi na muda wako kupitia makala zetu. Tafadhali ungana nami tena katika makala zetu zinazotoka kila Mwisho wa wiki.
  
      MAKALA HII IMEANDIKWA NA:-
              Francis Mawere
KWA HISANI YA MAWERE MEDIA GROUP Ltd (MMGLtd)
MAWASILINO:
Email: mtokambali2015@gmail.com Phone no: 0767322193

01 August, 2015

Zama za ujasiriamali zilizoufukia ujamaa (MAKALA)

Nyerere2
Na FRANCIS MAWERE
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliamua kuanzisha mfumo wa kiuchumi wa Ujamaa na Kujitegemea miaka michache baada ya Tanganyika kujipatia uhuru wake.
  Kwa kufanya hivyo alikuwa ameamua kufuata mawazo ya akina Adam Smith, David Ricardo, Milton Friedman, Fredrich Hayek, Ayn Rand Robert Owen, Pierre Leroux na Karl Marx kwa kuwataja kwa uchache; ambao wanatajwa kama waasisi na watetezi wa Ujamaa.
Hii ni kwamba aliamua kusimama kinyume na mawazo ya ubepari ya akina  Stuart Mill, Albert Einstein, George Bernard Shaw, Leo Tolstoy na Emma Goldman ambao katika anga za uchumi wanaheshimika kuwa waasisi na watetezi wa ubepari.
Mwalimu Nyerere alitumia muda, akili na nguvu nyingi sana kuwasilisha na kuwashawishi Watanzania kuupokea na kuukubali Ujamaa na Kujitegemea.
Mambo hayakwenda vizuri katika pande mbili. Mosi, kutokana na hali ya uchumi wa kidunia na nafasi ya Ujamaa kwa wakati huo duniani; utekelezaji wa sera za Kijamaa ulikuwa ni wa kutoa jasho mno. Pili, Watanzania wengi waliupokea Ujamaa na Kujitegemea kwa shingo upande na wale walioupokea kwa moyo mweupe inaonekana hawakumuelewa vizuri Mwalimu Nyerere.
 Upande wa kwanza ni nafasi ya Ujamaa duniani wakati Mwalimu Nyerere alipokuwa anauleta Ujamaa uliokolezwa mapambo (Ujamaa na Kujitegemea) hapa Tanzania. Ukweli ni kwamba hadi kufika miaka ya 1950 tayari Ujamaa ulishakuwa kwenye hali mbaya ya kumalizikia kuanguka. Hii ina maana Mwalimu Nyerere alikuwa anajaribu “bahati” ya kuijenga Tanzania imara kiuchumi kwa kutumia mfumo wa uchumi ambao ulishakuwa katikati ya changamoto kali sana za kushindwa.

 Ushahidi wa kushindwa kwa Ujamaa katika miaka hiyo, tunaupata kutoka kwa mataifa ambayo tunaweza kuyaita waasisi na miamba wa Ujamaa duniani. Gazeti la Urusi liitwalo Pravda, Mei 1988 liliandika habari ya kitafiti kuhusu hali tete ya uchumi wa Umoja wa Nchi za Urusi (USSR) kutokana na kufuata sera za Ujamaa.
 Katika habari hiyo, Pravda ilithibitisha kuwa matarajio ya Wajamaa yanazidi kuyeyuka kutokana na matokeo mabaya kwenye uchumi. Kwa mfumo, ilielezwa kuwa kati ya sekta 170 zilizoainishwa kuboreshwa na Ujamaa wao hakukuwa hata na moja iliyofanikisha malengo walau kiasi cha kuridhisha. Gazeti hilo lilihitimisha kwa kusema kuwa mfumo wa Ujamaa ni sawa na machafuko yaliyokusudiwa.

 Si hivyo tu, bali nyuma kabisa hapo mwaka 1920 wakati wa utawala wa Lenins Bolsheviks kule Urusi, tayari wanauchumi wengi akiwamo mwanauchumi wa Kiaustralia, Ludwig von Mises, walieleza kwa kina kuwa Ujamaa ulishakuwa umeanguka.
 Kwenye machapisho yake mawili maarufu sana, Economic Calculation in the Socialist Commonwealth  na Socialism, An Economic and Sociological Analysis, Mises anasema kuwa kutokana na tabia, tamaduni, mazoea na asili ya mwanadamu; kufanikisha Ujamaa ni sawa na kutengeneza sanamu kisha kutaka uipe uhai.

 Tunafahamu kuwa vita kubwa ya wafuasi wa Ujamaa na wale wa ubepari chimbuko lake kubwa ni mgawanyo wa rasilimali zilizopo katikati ya wanajamii. Ubapari wenyewe unasifa ya kuruhusu watu binafsi kuendesha uchumi kwa watu binafsi kumiliki njia kuu za uzalishaji.
 Kwenye ubepari, serikali inatakiwa kubaki kama mwangalizi tu na inapaswa kuliacha soko kuamua. Wakati Ujamaa wenyewe unasisitiza kuwa njia kuu za uchumi ni lazima zimilikiwe kwa pamoja na serikali iwe na mamlaka kamili ya kuingilia chochote katika mwenendo wa kiuchumi.
 Hapa ndipo penye kasheshe kubwa. Wale wapinzani wa Ujamaa huwa wanaenda mbali na kumnanga Karl Marx na kusema kuwa hakuwa na sababu za kiuchumi kuasisi Ujamaa. Marx yeye aliona kuwa ubepari ulikuwa ukilinyonya tabaka la wafanyakazi hivyo alipofikiria Ujamaa alisema utakuwa ni mfumo ambao utamlipa kila mtu kwa kadiri ya anavyofanya kazi.

Pengine tuanzie hapa kuutazama Ujamaa wa Mwalimu Nyerere hasa tukiangalia ule upande wa pili wa namna ambavyo ulipokewa kwa shingo upande na namna ambavyo haukueleweka. Mwalimu Nyerere alipoibuka na mfumo wa Ujamaa aliuongezea viungo kwa kuuita “Ujamaa na Kujitegemea”, lengo lake lilikuwa ni kuona Tanzania kama taifa likisimama na kumudu mahitaji yake na ya watu wake pasipo kutegemea fadhila, kuombaomba ama misaada.

Yakafanyika mambo mengi lakini makubwa mawili ni kuanzishwa kwa Vijiji vya Ujamaa na kutaifishwa kwa mali binafsi kuwa za umma. Nia ilikuwa nzuri lakini matokeo ya hatua hizi mbili hayakuwa mazuri pengine kwa sababu wananchi hawakuuelewa vema huu Ujamaa na Kujitegemea.
Kutokana na hili, maelfu ya wananchi hasa wale waliohamishwa makazi, waliopoteza mifugo yao, waliotakiwa kuacha mashamba na mazao yao na kwenda kwenye vijiji vya ugenini waliuchukia Ujamaa na Kujitegemea katika hatua za awali kabisa. Hata ubinafsishaji wa mali binafsi zikiwamo hospitali, shule, viwanda, kampuni na mashirika ulileta kizaazaa kwa sababu wamiliki wake walikuwa na wafuasi wengi na kama hawakuridhika basi na wafuasi wao waliuchukia Ujamaa na Kujitegemea ungali unaanza.

Pamoja na hilo inaonekana wananchi walioupokea Ujamaa na Kujitegemea walielewa kipengele kimoja tu cha Ujamaa lakini hiki cha Kujitegemea inaonekana hakikueleweka kabisa. Ili useme taifa linajitegemea ina maana kuwa wananchi wanajitegemea. Kwenye Ujamaa na Kujitegemea serikali ilihodhi njia kuu za uchumi na miundombinu ya kijamii, huku wananchi wakibaki kufanya kazi “kijamaa”.
 Suala hili lilisababisha wananchi wengi kama si wote kuitegemea serikali kwa mambo mengi ikiwamo upatikanaji wa elimu, huduma za afya, miundombinu na mengineyo. Serikali iliendelea kufurukuta kuwapa wananchi bure huduma za kijamii hadi ikafika mahali ikajikuta haina ujanja tena. Ndipo pale mahali Mwalimu Nyerere alipoamua kung’atuka na ghafla bin vuu nchi ikawa haina ujanja zaidi ya kujisalimisha kwenye makucha ya Benki ya Dunia (WB) na Shirika na Fedha (IMF).
 Ilikuwaje Taifa la Ujamaa na Kujitegemea likashindwa kujitegemea? Jibu ni rahisi. Ni kwa sababu wananchi wake katika ngazi ya mtu mmoja mmoja walikuwa hawajitegemei. Badala yake walikuwa wakiitegemea Serikali kwa kila kitu. Jambo hili halikutokea kwa bahati mbaya na wala halikutokana na ubovu wa uongozi wa Mwalimu Nyerere, isipokuwa una chimbuko lake kutoka katika saikolojia na tabia za kibinadamu kama alivyosema mwanauchumi Mises.

Kosa kubwa lililofanyika katika mfumo wa Ujamaa na Kujitegemea ilikuwa ni kutafuta usawa wa kijamii na kiuchumi kwa watu wote. Kiasili kila mwanadamu ameumbwa tofauti na kupewa upeo, vipawa, karama, uwezo, matarajio na maono yanayotofautiana. Tena kiasili mwanadamu hutafuta kuwa tofauti, kufanya lile alipendalo na kutambuliwa na kujulikana kwa yale ayafanyayo.
Hapa kwenye karama, maono, vipawa ndipo mahali ambapo humuwezesha mwanadamu kusoma mazingira yake, kuangalia matatizo yaliyopo na kuyatafutia ufumbuzi kwa kutumia karama, vipawa, maono na uwezo wake. Namna hii ya utatuzi wa matatizo na changamoto ndiyo msingi na chimbuko la ujasiriamali (Intrinsic Entrepreneurship).

 Mchumi na mwanasaikolojia wa kale, John Stuart Mill, katika kitabu chake cha Principles of Political Economy (1848) anasema, “Ukimlazimisha mwanadamu awe sawa na wengine, afanye kila kitu kwa kuamuliwa na mamlaka, basi atakuwa na hulka zifuatazo: Atakuwa mtu anayefanya mambo nusunusu (passive), hatafanya mambo makubwa zaidi ya yale wanayofanya wenzake hata kama ana uwezo na kubwa kabisa hataona umaana wa kujipambanua katika kazi kwa sababu iwe atafanya sana ama atafanya kidogo, maslahi anapata yale yale.”
Hapa ndipo mahali Ujamaa na Kujitegemea ulipoua vipawa vingi vya kijasiriamali. Wafanyakazi hawakuona umuhimu wa kufanya zaidi, wananchi hawakuwa na sababu ya kufanya zaidi kwa sababu Serikali ilitoa kila kitu na vile vile ilikuwa na utaratibu unaobana unapotaka kufanya biashara. Mathalani, ule mtindo wa kumbana mtu na kutaka ajieleze namna alivyofanikiwa hata akajenga nyumba ama kununua kitu cha thamani ulizalisha woga miongoni mwa Watanzania wengi.
 Kivuli cha woga ule kinatutafuna hadi sasa, ndiyo maana nchi hii mtu anapofanikiwa kiuchumi watu hawamuamini, wanamtilia shaka; eidha watasema ni fisadi ama ni mshirikina ama ni mwizi. Ujamaa na Kujitegemea ingawa haukuandika katika maandishi ya sera zake, lakini ulihesabu mtu kuwa na utajiri kama “dhambi na unyonyaji”.

 Kule Magharibi walianza kutumia msamiati wa ujasiriamali miaka ya 1700! Sisi Tanzania msamiati huu ndiyo kwanza unavuma miaka hii ya 2000. Dhana ya ujasiriamali iliasisiwa na ubepari. Tulipokuwa tunacheza ngoma ya Ujamaa na Kujitegemea tuliuita ubepari ni unyama. Kwa lugha nyepesi ni kuwa Ujamaa na Kujitegemea ulipenyeza imani vichwani mwa Watanzania; ya kuamini kuwa “ujasiriamali ni unyama”.
 Hili tunaweza kulithibitisha kwa kutazama kile ambacho Watanzania tunafahamu kuhusu ujasiriamali. Wengi wa Watanzania bado wanashangaa-shangaa, wanasikiasikia tu lakini wanahisi kuwa ujasiriamali si kitu kinachowahusu. Jirani zetu Wakenya ambao wamekuwa wabepari nyakati zote; hadi watoto wa shule za msingi wananunua hisa katika soko lao la hisa Nairobi. Sisi hapa Tanzania wasomi wetu wanahitimu vyuo vikuu hawajui hata ABC hisa achilia mbali uwezo wa kutumia maarifa waliyopata kujiajiri.

 Nihitimishe kwa kusema kuwa kushindwa kwa Ujamaa na Kujitegemea hakuwezi kuhesabiwa moja kwa moja kama ni kushindwa kwa Mwalimu Nyerere; kwa sababu Ujamaa ulishakuwa umeshindwa kabla hata Mwalimu Nyerere hajabuni Ujamaa na Kujitegemea.
Wachumi wanatuthibitishia kuwa miundombinu ya Ujamaa ndiyo chimbuko la kuanguka kwake. Na moja ya sababu za kudondoka kwa viwanda na mashirika mengi ya umma ilikuwa ni kushindwa kuzalisha kwa kuangalia mahitaji na matakwa ya watumiaji (soko).
Watanzania tunahitaji ushindi wa kiuchumi tunapoendelea kumuenzi Mwalimu

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...