28 June, 2015

Steve Nyerere: Sijakurupuka Kugombea Ubunge

Steve  Nyerere: Sijakurupuka Kugombea Ubunge Staa wa Bongo Movies na aliyekuwa mwenyekiti wa Bongo Movie Unit, Steve Mengere ‘Steve Nyerere’ ambaye wiki iliyopita alitangaza niua yake ya kugombe ubunge mwaka huu wa uchaguzi amedai kua hajakurupuka kuutaka ubunge kupitia jimbo la Kinondoni na kuwa ataendeleza sanaa hata akiwa mbunge.Akizungumza na millardayo.com alisema..’Kwanza ninataka kuwahakikishia watanzania sijakurupuka, nimekuwa  mwanachama wa chama cha Mapinduzi  umoja wa vijana almost miaka 25 na sasa hivi nina miaka 29 naelekea 30 lakini vilevile nimekuwa kamanda wa vijana miaka 10 tawi la bwani kinondoni, nimekuwa mwamasishaji  wa chama cha mapinduzi kitaifa kwa muda wa miaka 10Kwa hiyo nataka kusema sijakurupuka na wala sijatamkia sifa kwasababu labda nimeona mtu Fulani amegombea na mimi basi tu  nigombee hapana  nimeona  katika wilaya yangu ya  kinondoni kuna matatizo kadhaa  nani anaweza kuyatetea hayo matatiizo  basi mimi ndio nitakuwa mtetezi wa wilaya wa Kinondoni pamoja na matatizo ya wasanii wetu, kuhusu kazi zangu za filamu nitakuwa nafanya kama kawaida huku nikiwa natumikia kazi za Bungeni’alisema 

Usisumbuke Mawerenewz.blogspot.com ndio mtandao wako wakipekee unaokupa habari za BURUDANI,MICHEZO, SIASA, na HABARI MBALIMBALI ZA KIMATAIFA pamoja na KITAIFA Endelea kutembelea MTOKA MBALI pia nifuate twitter>>>@mawere3, facebook>>>Mawere Mtoka Mbali, Instagram>>>mawere_mtoka_mbali,

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...