04 July, 2015

YALIYOJIRI HUKO BUNGENI LEO: Wabunge wengine 35 nao wamepigwa stop kuingia Bungeni kwa siku tano

stop
Kumekuwa na story nyingi tofauti toka ndani ya Kikao cha Bunge Dodoma, kwa muda wa siku tatu mfululizo zimetokea vurugu, Kikao kikaahirishwa kwa siku mbili mfululizo.
Alhamisi July 02 2015 Mbunge John Mnyika aliomba mwongozo kuomba Bunge lisiendelee kwa vile ishu ya kujadili Miswada mitatu kwa siku moja ilikuwa inakiuka Kanuni za Bunge, ukatokea mvutano na baadae Spika AnneMakinda akaahirisha Bunge.
Dada Anne
Spika wa Bunge, Anne Makinda.
Ijumaa July 03 2015 hali ikawa hivyohivyo tena, wakati Waziri George Simbachawene anasoma Muswada, ikatokea mvutano mwingine, zikaanzishwa kelele Bunge likaahirisha tena.. Kikao cha Jioni Spika Anne Makinda akarudi na list ya majina ya Wabunge ambao wamesimamishwa Bungeni kutokana na maamuzi ya Kamati ya Maadili ya Bunge.
01-Mtifuano+Bungeni
Leo July 04 2015 Kikao kimeanza tena saa tatu asubuhi, Mbunge Ezekiel Wenje akaomba Spika atoe ufafanuzi wa kwanini Mbunge Silinde hayuko kwenye list ya waliotajwa kusimamishwa lakini Askari wa Bunge wamemzuia asiingie kwenye Kikao?
Majibu ya Spika hayakuwaridhisha baadhi ya Wabunge, zikaanza tena kelele… Spika akataja list ya Wabunge wengine ambao wanasimamishwa kuhudhuria Vikao vya Bunge kwa siku tano kila mmoja.
List ya Wabunge wote iko hapa.
Ezekiel Wenje
Mussa Kombo
Masoud Abdallah Salim
Rebecca Ngodo
Sabrina Sungura
Khatib Said Haji
Dr. Anthony Mbassa
Maulidah Anna Valerian Komu
Kulikoyela Kahigi
Cecilia Pareso 
Joyce Mukya
Mariam Msabaha 
Grace Kiwelu
Israel Natse 
 Mustapha Akonaay
Konchesta Rwamlaza
Suleiman Bungura 
Rashid Ali Abdallah 
Ali Hamad
Riziki Juma
Rukia Kassim Ahmed
Azza Hamad
Khatibu Said Haji
Kombo Khamis Kombo
Ali Khamis Seif
Haroub Mohammed Shamisi 
Kuruthum Jumanne
Mchuchuli
Amina Mwidau
Mkiwa Kimwanga
Salum Baruhani 
Marry Stellah Malaki
Rashid Ally Omary
Mwanamrisho Abama
Lucy Owenya
Hiyo stori iko kwenye hii sauti hapa, utasikia mwanzo mpaka mwishon ilivyokuwa mpaka majina ya Wabunge walipotajwa.

Usisumbuke Mawerenewz.blogspot.com ndio mtandao wako wakipekee unaokupa habari za BURUDANI,MICHEZO, SIASA, na HABARI MBALIMBALI ZA KIMATAIFA pamoja na KITAIFA Endelea kutembelea MTOKA MBALI pia nifuate twitter>>>@mawere3, facebook>>>Mawere Mtoka Mbali, Instagram>>>mawere_mtoka_mbali,

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...