Katika makala yetu leo tuna angaza jicho kwa wakali hawa wa bongo fleva ambao miaka ya nyuma waliweza kuzikonga nyoyo za maShapiki wao vilivyo, na hawa si wengine ni MAN DOJO NA DOMO KAYA. Naweza sema kwamba vijana hawa sii wageni kuwaskia maskioni mwako kwani waliweza kuziteka media tofauti tofauti zenye ukubwa hapa Tanzania na hata nchi za njee kwa vibao vyao vilivyo kua vimejaa ujumbe tele kwa jamii mfano DINGI, BARUA, na NIKUPE NINI. Hivyo ni baadhi ya vibao walivyopata kutesa navyo kipindi cha miaka ya mwanzoni mwa 2000.
Jambo lakujiuliza ni je wakali hawa wamepotelea wapi?
Ni wazi kwamba leo hii ukipata nafasi yaku onana nao, swali utakalo wauliza ni mbona siku hizi hatuwasikii? Hicho ndicho kilichomo katika fikra za mashabiki wa hawa wakali au ukipenda waite manguli wa bongo fleva. Yawezekana kabisa kwamba hawa jamaa wanatamani kurudi katika game ya muziki nakuwika tena kama ilivyokua mwanzini laki inakua ni vigumu kwani muziki wa bongo fleva unazidi kukua siku baada ya siku na kwa vile ukimya wao kwa muda mrefu bila kusikika, imefanya hata mashabiki wao kuwasahau kabisa.
Waliweza kutengeneza vibao vingi ambavyo nimeweza kuvitaja baadhi hapo juu na vingine ni kama vile HISTORIA, WANA KNOCK KNOCK, NIZIKWE HAI, na TASWIRA. Kama kweli wewe ni mpenzi wa muziki wa bongo ni wazi kua vibao hivi vilikukonga moyo ipasavyo na hadi leo unawakumbuka hawa jamaa vilivyo.
Siwezi sema yakwamba hawa jamaa hawawezi kurudi katika umahiri wao kama mwamzo ila jitihada na juhudi zao ndizo zitawaleta tena kwatika game ya muziki na kuwika tena mbele ya wadogo zao katika muziki huu wa bongo fleva.

Nipende kukushukuru wewe ulichukua muda wako adhimu na wenye dhamani kwa kukaa kitako nakusoma makala zetu. Endelea kutembelea MTOKA MBALI ili uweze kupata kile unachokitaka.
MAKALA hii imeandikwa na Francis Mawere kwa hisani ya MAWERE MEDIA GROUP Ltd
TUTUMIE email yako kupitia mtokambali2015@gmail.com au piga simu namba 0767322193