28 August, 2015

video mpya ya Young Dee Ft Ben Pol ‘Do It’ itazame hapa.

young dHii video mpya ya Paka Rapa Young Dee aka Young Dar es salaam ft  Ben Pol ‘Do It’ itazame hapa na nipe mtazamo wako hapo chini ukiweza.

DE BRUYNE HUYOOO EPL YAMEBAKI MASAA TU, KUJIUNGA NA WAKALI HAWA…

De Bruyne KelvinMachester City wamemuwekea mezani bonge la mshahara kiungo wa Wolfsburg Kevin De Bruyne, mkurugeni wa michezo wa timu hiyo Klaus Allofs amewaambia waandishi wa habari.
Akizungumza mjini Monaco wakati wa kupanga makundi ya UEFA Champions League, amesema makubaliano kati yao na Man City yanakaribia kukamilika. Amefafanua kuwa dili hilo litakalovunja rekodi ya klabu hiyo kwa kumuuza De Bruyne kwa kitita cha pauni milioni 54 linaweza kukamilika ndani ya masaa 48 baada ya makubaliano ya pande mbili kufikiwa.
Mgurugenzi huyo wa Wolfsburg amesema, ofa kutoka Man City imekuwa kubwa mno na wao hawawezi kupambana kuwazuia.
“Tumekuwa kwenye mazungumzo na sasa tumekaribia kukamilisha lakini dili bado halijakamilika. Lakini nadhani tutafikia muafaka muda si mrefu”.
Allofs amesema, timu yake haiwezi kushindana na matajiri hao wa EPL ambao wameahidi kumpa De Bruyne mshahara wa pauni 200,000 kwa wiki kiungo huyo mwenye miaka 24.

STARS YASHINDWA KUTAMBA UTURUKI MBELE YA LIBYA, BOCCO AFUNGA GOLI LA KUFUTIA MACHOZI

Kikosi cha Stars kilichoanza leo dhidi ya Uganda 
Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeshindwa kutamba mbele ya Libya baada ya kufungwa kwa goli 2-1 kwenye mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu kuelekea mechi yake dhidi ya Nigeria kuwania kufuzu kucheza mashindano ya Mataifa ya Afrika yatakayofanyika mwaka 2017 huko Gabon.
Mchezo huo uliochezwa nchini Uturuki ambako Stars imeweka kambi, ulikuwa ni wa mazoezi na ulikuwa hautambuliwi na CAF wala FIFA ila ulikuwa unatumiwa na makocha wa timu zote mbili kwa ajili ya kutathmini vikosi vyao kuelekea michuano ya kutafuta tiketi ya kushiriki michuano hiyo ya Afrika.
Kwenye mchezo huo, goli pekee la Tanzania limefungwa na John Bocco ‘Adebayor’ kwa mkwaju wa penati baada ya Simon Msuva kufanyiwa madhambi kwenye eneo la hatari na mwamuzi kuamuru ipigwe penati ndipo Bocco akaipatia Stars goli la kufutia machozi.
Stars bado inaendelea na kambi yake nchini humo ambapo ikirejea jijini Dar es Salaam itafanya maandalizi kwa siku chache kabla ya kuivaa Nigeria Septemba 5 mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa.

USAJILI : BAADA YA DI MARIA HUYU NDIYE MCHEZAJI ANAYEFUATA KUSEPA UNITED KWA KIPINDI HIKI.

logo
Huu ni muda wa kuhama na kuhamia kutoka kwenye club mbalimbali duniani. Di Maria alihama kutoka Manchester united na kujiunga na PSG. List ya wachezaji walihama na kuhamia ni wengi na pesa iliyotumika ni nyingi.
Jina jipya linalotajwa kutoka Manchester united ni la kipa Victor Valdes ambae anategemewa kujinga na club ya Besiktas. Taarifa inasema kwamba Rais wa Besiktas yupo Le Meridien Beach Plaza hotel huko Monte Carlo kwa ajili ya kukamilisha dili la mchezaji huyo.
Hadi sasa taarifa zinasema kwamba Valdes amepewa ofa ya mkataba wa miaka 2 na option ya kongeza mwaka mmoja wa ziada kama akitaka.
valdes

MOURINHO ALAUMU MAREFA, AKATAA KUMZUNGUMZIA JOHN STONES

momo

Story hii inamuweka tena kwenye vyombo vya habari JM kwa kuendeleza tabia yake ya kulaumu watu kutokana na club yake kufanya vibaya.
Kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho amewalaumu waamuzi kua ndio sababu ya timu yake kua na mwanzo mbaya wa ligi.Amewalaumu marefa kwa kitendo cha kuwapa red card wachezaji wake John Terry pamoja na kipa Thibaut Courtois na kuwazawadia penati West Bromwich na Swansea city.
Mourinho amesema “Kitu ambacho sio cha kawaida katika mwanzo wa msimu huu ni kua na mechi tatu alafu kati ya hizo mbili mnacheza watu kumi uwanjani na kupata adhabu ya penati mbili kutokana na maamuzi”
“Sio kitu tunachokitaka ila kua na point nne sio masihara, itabidi tusonge mbele,tujiimarishe.Tunajua tutaimarika na tutaimarika ili tupate matokeo mazuri zaidi”
Vile vile Mourinho amekataa kuzungumzia suala la mlinzi wa Everton John Stones kwa kusema anafuraha na kikosi alichonacho.
“Sipendi kuzungumzia wachezaji wa timu nyingine, nina furaha na kikosi chang ,kama tukipata mchezaji mwingine kabla ya dirisha la usajili kufungwa ni vizuri kama tukikosa nitaendelea na kikosi nilichonacho” alisema Mourinho

UPDATE: KOCHA WA REAL MADRID AMEPIGILI MSUMALI WA MWISHO KUHUSU BENZEMA NA ARSENAL

real

Real Madrid imezidisha msumali kwenye ndoto ya Arsenal kutaka kumsanjili Benzema kwa msimu huu. Mipango ya Arsenal ya kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid karim Benzema inazidi kutibuka baada ya meneja wa Real Madrid kuonyesha kutaka huduma yake kwa msimu huu.
Wakiwa wanajiandaa na mchezo wao wa jumamosi dhidi ya Real Betis, Rafael benitez alisema“Benzema ni mchezaji mzuri na tunamuhitaji ili tuzidi kupata mafaniko. Yeye ni silaha tosha kwetu katika safu ya ushambuliaji”.
Karim Benzema mwenye umri wa miaka 27 ana mkataba na Real Madrid ambao utamalizika mwaka 2019 na ameonekana kua chaguo la mashabiki wa arsenal na club pia lakini kwa sasa imeonekana ni ngumu kumpata. Kushindwa kuhamia msimu huu haimaanishi ndio over.

Hii ndio kamati mpya yaShindano la Miss Tanzania, Jokate na yeye yupo


Kamati mpya ya Miss Tanzania imetangazwa Leo ikiwa ni wiki moja baada ya Baraza la sanaa la Taifa ( BASATA) kulifungua shindano hilo lililokua limefungiwa miaka miwili.
Jokate ambaye ndio msemaji wa kamati hiyo mpya amesema “Kwa niaba ya kamati mpya ya Miss Tanzania tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa uongozi wa kampuni ya Lino International Agency Limited kwa kutuamini na kututeua kuwa wajumbe wapya wa kamati ya Miss Tanzania yenye majukumu ya kuandaa, kuratibu ns kusimamia mashindano ya urembo ya Miss Tanzania”
“Kwa leo hatutakuwa na mengi ya kusema kwa sababu ndio kwanza tumekabidhiwa jukumu hili hivyo kamati yetu itakutana kupanga mipango na mikakati endelevu ya kuendeleza sanaa hii ya urembo ndani hadi nje ya mipaka yetu  ya Tanzania” Aliongeza msemaji wa kamati hiyo.
Hii ndio orodha ya wajumbe wa kamati hiyo
1.Juma Pinto – Mwenyekiti
2.Lucas Rutta – Makamu Mwenyekiti
3.Doris Mollel – Katibu Mkuu
4.Jokate Mwegelo – Msemaji wa Kamati
5.Hoyce Temu – Mjumbe
6.Mohamed Bawazir – Mjumbe
7.Gladyz Shao – Mjumbe
8.Magdalena Munisi 0 Mjumbe
9.Shah Ramadhani – Mjumbe
10.Hamm Hashim – Mjumbe
11Khalfani Saleh – Mjumbe
12.Ojambi Masaburi – Mjumbe
Wajumbe wa Sekretarieti :
1.Dr.Ramesh Shah
2.Hidan Ricco
3.Yasson Mashaka
4.Deo Kapteni

Source: Millardayo.com

Wapenzi wa jinsia moja wadai kunyanyaswa


Kundi la kuteta haki za kibinadam nchini Tanzania la LGBTI Voice of Tanzania imetangaza kuwa imeanzisha kampeini ya kuchangisha pesa za kututea haki za wapenzi wa jinsia moja, watu walio badili jinsia zao.
Shirika hilo limesema kuwa sheria za Tanzania zinawakandamiza watu wanaoshabikia mapenzi ya jinsia moja.
Mkurugenzi wa shirika hilo James Wandera amesema wamechangisha zaidi ya dola elfi thelathini, has kutoka wa wafadhili kwa njia ya mtandao.
Amesema wanapanga kutumia fedha hizo kuzuia uwezekano wa wabunge kuidhinisha mswada uliowasilishwa bungeni.
Mswada huo haujajadiliwa bungeni lakini unapendekeza adhabu ya dhidi ya wapenzi wa jinsia moja kuimarisha zaidi.Sheria za Tanzania zimeharamisha mapensi ya jinsia moja na wale wanaopatikana na hatia hupewa adhabu ya kifungo cha hadi miaka 20 gerezani.

Mshukiwa wa kike wa ugaidi asakwa-Kenya


Serikali ya Kenya imetoa zawadi ya $20,000 wa mtu yeyote atakaye toa habari za kukamatwa kwa mshukiwa mmoja wa ugaidi wa kike, Rukia Faraj.
Idara ya polisi imesema kuwa Rukia anasakwa kwa madai ya kuwasajili na kuwasafirisha watu wachanga kujiunga na mme wake nchini Somalia kwa mafunzo ya ugaidi na pia kujiunga na kundi la kigaidi la Al Shabaab.
Mume wake Ramadhan Kufungwa pia anasakwa na polisi kwa madai ya kupanga mashambulio ya kigaidi nchini Kenya.
Rukia sasa anajumuika na washukiwa wengine ambao wanasakwa na serikali ya Kenya kwa madai ya kupanga mashambulio ya kigaidi.
Wengine ni pamoja na Mohammed Kuno anayejulikana kwa jina lingine Gamadere au Dhuliadein ambaye anatuhumiwa kupanga mashambulio ya kigaidi katika chuo kikuu cha Garisa, ambapo zaidi ya watu 148 waliuawa

Askofu aliyekabiliwa na kesi aaga dunia



Aliyekuwa Askofu wa kanisa la Katoliki kutoka Poland, ambaye alitarajiwa kufikishwa mahakamani kwa madai ya dhuluma za ngono amefariki.
Jozef Wesolowski alipelekwa hospitali mwezi uliopita, saa chache tu kabla ya kufishwa mahakamani.
Askofu huyo anatuhumiwa kuwapa watoto pesa na kuwadhulumu kingono wakati alikuwa balozi wa Vatican katika Jamuhuri ya Domincan.
Kamati maalum ya kanisa la Katoliki ilimpata na hatia na ikamsimamisha kazi mapema mwaka huu.
Wesolowski angelikuwa mtu wa kwanza wa ngazi ya juu katika kanisa hilo la Katoliki kufikisha mahakamani mjini The Vatican kwa madai ya kuwadhulumu watoto kingono.
BBC

sekunde 15 za video mpya ya Chris Brown: ‘Liquor’ (VideoTeaser)

c breezy2

Headlines za Chris Brown ni mpya kila siku mtu wangu… siku  chache zilizopita Chris Brown alitangaza kuwa anaipa Album yake mpya jina la mwanae ‘ROYALTY’ ikiwa zawadi kwa mwanae ambaye amechangia kwa kiasi kikubwa sana kubadilisha maisha yake.
Ninayo nyingine kutoka kwa C Breezy mtu wangu, nimepita kwenye page yake ya Instagram na nimekutana na video ya sekunde 15 ya wimbo wake mpya ‘Liquor’, wimbo ambao unapatikana kwenye album yake mpya tunayoisubiria.
c breezy
Ukitembelea pia ukurasa wa Chris Brown wa Twitter utakutana na post nyingine kutoka kwake ikisema; “Coming soon. Directed by yours truly”… so good news kwa wewe shabiki wa Chris mtu wangu ni kwamba video wa wimbo huu mpya Chris anasimama pia kama Director!
Nimeisogeza kwako kipande cha video kutoka kwa Chris Brown niliyoweza kuinasa kupita ukurasa wake wa Instragram @chrisbrownofficial.

HABARI NJEMA INAYOMUHUSU MSANII ‘PATORANKING’ WA NIGERIA


Kwa mujibu wa taarifa zilizo tufikia zinazo muhusu msanii Patoranking wa Nigeria zinasema kuwa msanii huyo anategemea kufanya ngoma na msanii wa mkubwa kimataifa ambaye ni DJ and producer maarufu kwa jina la Dre Skull, aliyewahi kufanya kazi na wasanii kama Snoop Dogg, Pusha T, Popcaan and Beenie, Man taarifa hizi zilianza kusambaa mara baada ya Dre Skull kuwekwa wazi kwenye Twitter Monday (24 August).
dre


Ulikua unafahamu kama Chris brown anamiliki migahawa 14 ? Soma hii



Pamoja na kupata mafanikio makubwa kwenye music akiwa kama mmoja ya wasanii wanaouza zaidi, Christopher Maurice Brown au maarufu kama Chris Brown pia ni mjasiliamali na anamiliki migahawa 14 inayouza Burger na vyakula vya haraka (burger kings).
Chris brown ameshare mambo 25 ambayo watu hawafahamu kuhusu yeye  “25 Things You Don’t Know About Me” ya mtandao wa US Weekly na moja ya mambo hayo ni kuwa anamiliki migahawa 14 au maarufu kama Burger Kings.
Kumiliki migahawa inayouza vyakula vya haraka ni moja ya biashara yenye mafanikio makubwa Marekani lakini sio rahisi, kwa mujibu wa Burger kings mtu yoyote mwenye nia ya kufanya biashara hiyo anatakiwa awe na mtaji wa dolla  1,500,000 na nyinine dolla 500,000 kwa ajili ya vinywaji (Hii ni kwa mgahawa mmoja)  Chris brown anamiliki migahawa 14, unaweza piga hesabu.

25 August, 2015

NEW AUDIO:Harmonize--‘Aiyola’

aiyolacoverfinal (1)Harmonize ni msanii chipukizi ambaye yupo chini ya label ya ‘Wasafi Classic’ inayoongozwa na Diamond Platnumz a.k.a Dangote ameachia wimbo wake mpya ‘Aiyola’. Huo ni wimbo wa kwanza kuachiwa kwa wasanii waliopo chini ya label hiyo ya Wasafi Classic na producer wa wimbo huo ni Max.Sikiliza hiyo ngoma hapa;

Drake na Selena williams ni wapenzi? Tazama hizi picha


Tetesi za kuwa rapper  Drake na mcheza tenisi Serena williams ni wapenzi zinaweza zikawa zimethibitishwa na hizi picha zinazowaonesha pamoja wakishikana na kupiga busu.
Picha hiziz zilipigwa kwenye mgahawa mmoja huko huko Cincinnati, Marekani.
drake-serena-kissing-photos-04-480w

drake-serena-kissing-photos-03-480wTetesi za Uhusiano wao zilianza baada ya Drake kuonekana akimshangilia serena williams kwenye mashindano ya Wimbledon.

24 August, 2015

Elizabeth Michael rocks an Eve Collection for TMT Finale

Looking amazingly beautiful,Tanzanian actress Elizabeth Michael a.k.a Lulu decided to rock this Eve Collection design for the TMT finale
From the color to the lace details and of course,the mermaid fitting...we love it!

Je unataka ndoa yako iwe na mvuto?


Je ungependa kuwa na ndoa thabiti ?
Jifunze kugawanya majukumu na mumeo ama mkeo hapo nyumbani.
Utafiti uliofanyika nchini Marekani umebaini kuwa kugawanya majukumu ya kuwalea watoto kati ya mume na mke kunaimarisha joto la mapenzi nyumbani.
Utafiti huo uliofanyika miongoni mwa familia 487 nchini Marekani umebaini kuwa kugawanya majukumu ya kuwalea watoto na mahitaji mengine hapo nyumbani kati ya mume na mke kunasaidia kuimarisha uhusiano baina yao na hivyo pia kupalilia cheche za mahaba kati ya wanandoa.
Katika nyumba ambamo baba na mama wanasaidiana kuwalea watoto kuwalisha kuwavisha kugharamia mahitaji yao utafiti uligundua walikuwa wakishiriki tendo la ndoa kwa kiwango kikubwa zaidi ya wale ambao majukumu yote yaliwachiwa mwanamke.
Hata hivyo waligundua kuwa iwapo majukumu yote aliyatekeleza mume tofauti ilikuwa ndogo sana.
Utafiti huo wenye jina '' 2006 Marital and Relationship Study'', ulitolewa kwa kongamano la wanasaikolojia nchini Marekani na kuonesha kuwa katika ndoa ambazo mwanamke alitelekezewa majukumu na akasalia kuwajibikia asilimia 60% ya majukumu ya kuwalea watoto, wanawake hao hawakuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu yao binafsi katika ndoa.
Hii ni kumaanisha kuwa iwapo mama mzazi ndiye anayewalinda wavisha walisha na kutunga sheria za hapo nyumbani mara nyingi ifikapo wakati wa kuwa mwanamke huwa hawezi kujituma kumridhisha mumewe katika hali ya maisha ya unyumba.
Dr Daniel Carlson, naibu profesa katika chuo kikuu cha Georgia State , anasema;
"jambo ambalo tulishangaa hata nasi ni pale tulipogundua kuwa wanawake walishindwa kutekeleza majukumu ya unyumba wakiwachiwa asilimia kubwa ya majukumu ya malezi ya watoto''
Sasa wasomi hao wameanza kuweka mikakati ya kuendelea na sehemu ya pili ya utafiti wao ilikujibu swali kwanini ndoa zenye wachumba waliogawanya majukumu yana mshiko zaidi haswa ikija katika swala la unyumba na hususan tendo la ndoa ?Profesa Sir Cary Cooper, wa kitivo cha Biashara cha chuo kikuu cha Manchester anasema kuwa uchunguzi huu unatilia pondo dhana iliyokuwepo tangu miaka ya nyuma kuwa mwanaume mwenye kujali watoto wake anatunukiwa penzi la ziada na mwanamke.

Sarafu ya Afrika Kusini yaanguka


Sarafu ya Afrika Kusini ,Rand, imeporomoka hadi kiwango cha chini zaidi ikilinganishwa na ile ya dola na hivyobasi kusababisha hasara kubwa katika miezi 19 huku kukiwa na wasiwasi kuhusu ukuwaji mdogo wa uchumi wa China.
Sarafu hiyo ilishuka na kubadilishana kwa 14 dhidi ya dola .
Ni sarafu ambayo imeathiriwa vibaya zaidi miongoni mwa masoko 25 yanayoinuka baada ya wawekezaji kuuza mali zao zilizo hatarini zaidi kutokana na wasiwasi wa ukuwaji wa uchumi wa taifa la uchina ambao ni wapili kwa ukubwa duniani.

Waliotibua shambulizi watuzwa Ufaransa


Rais wa Ufaransa Francois Hollande amatoa tuzo la juu zaidi nchini Ufaransa kwa Waamerika wanne ambao walitibua shambulizi la kigaidi kwenye treni ya mwendo wa kasi kwenda mjini Paris siku ya Jumamosi.
Mwanajeshi Mmarekani ambaye alijeruhiwa Spencer Stone alipomuangusha mwanamgambo huyo sakafuni , alipewa tuzo hilo pamoja na Waamerika wengine na Muingereza mmoja ambao wote wametajwa kuwa mashuja.
Bwana Hollande alisema kuwa kungetokea maafa kwenye treni hiyo iwapo abiria hao hawangechukua hatua.
Waziri mkuu wa Ubelgiji Charles Michel na balozi wa Marekani nchini Ufaransa Jane Hartley walishudhuia sherehe hizo.

HAYA NDIO MAJIBU YA VAN GAAL KUHUSU MSHAMBULIAJI MPYA

gaal
Baada ya vyombo mbalimbali vya habari pamoja na baadhi ya wachambuzi wa soka nchini England kusema kwamba Manchester United inahitaji mshambuliaji mpya ili kumsaidia Wayne Rooney, kocha wa klabu hiyo mholanzi Louis Van Gaal haoni sababu ya kufanya hivyo.
Akizungumza mara baada ya mchezo wa timu yake na Newcastle United, uliomalizika kwa sare tasa isiyo na magoli, Van Gaal amesema timu yake ilionesha mchezo mzuri zaidi na kwamba walishindwa tu kutumia nafasi walizotengeneza.
Katika mechi hiyo, Manchester United walipiga mashuti sita golini katika dakika 20 za kwanza huku pia Rooney akikataliwa bao na mshika kibendera kwa madai ameotea.
Van Gaal amesema, haoni sababu ya kusajili straika mpya kwani timu yake ilifanya vizuri katika michezo dhidi ya Spurs, Aston Villa, Club Brugges na Barcelona pia katika michezo ya preseason.
Kuhusu Wayne Rooney, kocha huyo amemkingia kifua na kusem, “Wayne alifunga goli. Bahati mbaya lilikataliwa. Sihitaji mshambuliaji mpya” alijiamini Van Gaal.
Katika michezo mitatu ya ligi kuu England, Manchester United wameshinda miwili na kupata sare mechi moja huku wakifikisha points 7 na kufunga magoli 2 moja likiwa ni la kujifunga.
Hata hivyo wachezaji wengi wa Manchester United, wameonekana kuridhika na performance yao uwanjani, lakini wakasikitishwa na matokeo.
Wayne Rooney alikataliwa goli la mapema, huku kipa wa Newcastle mholanzi Tom Krul akimkatalia Javier Hernandez goli la wazi wakibaki wawili. Chris Smalling naye akagongesha mwamba akipiga kichwa mpira wa kona.

Manchester City ilipata ushindi wa mabao 2-0 ugenini, Goodson Park dhidi ya wenyeji Everton

Ni ushindi wa Tatu mfululizo kwa kikosi cha Manuel Pellegrini na sasa wanashikilia kilele cha msimamo wakiwa na alama tisa. Mlinzi wa Kushoto, Alexandar Kolarov alifunga bao la kungoza dakika ya 60 kisha Samir Nasri akamaliza mechi dakika ya 88 kwa kuzamisha goli la ushindi.
City imeanza msimu tofauti na matarajio ya wengi, kasi yao ni ya kiwango cha timu inayohitaji hasa ubingwa. Walianza na ushindi mkubwa wa 3-0 ugenini The Hawthoms Stadium dhidi ya West Brom iliyo ‘ ienyesha’ Chelsea siku ya Jumapili. Kiungo na nguzo kuu ya timu hiyo, Mu-Ivory Coast, Yaya Toure ndiye mfungaji wa goli la kwanza la City msimu huu, ambalo alilifunga dakika ya 24’ kwa umbali wa ‘ yard 20’.
nasri
Nahodha, Vicent Kompany akafunga kwa mpira wa kona ya David Silva na kuwa mlinzi wa kwanza kufunga katika klabu hiyo msimu huu. Silva alifunga pia katika gemu hiyo ya kwanza na kuthibitisha uimara, kuanzia katika safu ya ulinzi ambayo iliweza kuwazima washambuaji Saido Berahino na Lickie Lambert.
Ilikuwa ni timu mpya tofauti na ile iliyomaliza katika nafasi ya Tatu msimu uliopita. Akiwa tayari amemsaini Muargentina, otamedi kutoka Valencia ya Hispania kama ingizo jipya katika safu ya ulinzi wa kati, Pellegrini ameshuhudia safu yake ya ulinzi ikicheza gemu Tatu mfululizo pasipo kuruhusu nyavu zao. Bacary Sagna tayari ameoneka ‘ ku-hodhi’ nafasi ya beki ‘ 2’ wakati Alexandar Kolarov akishika nafasi ya beki ‘ 3’.
Kompany na Eliaquim Mangala wamekuwa imara katika beki ya kati. Bado ‘ Wanne’ Hao wana safari ya kuthibisha ujio wa safu ya ulinzi ya City ambayo imetajwa mara kwa mara kama sababu ya kuanguka kwa timu hiyo anapokosekana, Kompany. Pellegrini sasa ana wigo mpana katika beki ya kati na ile ya pembeni. Gael Clichy, Martin Demichelis ni namba zaidi katika idara hiyo. Demichelis tayari amecheza kwa dakika kumi msimu huu ( aliingia kuchukua nafasi ya Yaya dakika ya 80 dhidi ya West Brom).
Silva, Yaya na kiungo Mbrazil, Fernandinho walianza katika idara ya kiungo katika mechi ya kwanza. Wilfried Bonny ambaye alishiriki katika utengenezaji wa goli la Yaya Toure, Raheem Sterling na Jesus Navas walianza katika safu ya mashambulizi. Sergio Aguero aliingia dakika ya 63 kuchukua nafasi ya Bony, Samir Nasri akaingia kuchukua nafasi ya Sterling dakika ya 74’.
Hiki ni kikosi kikubwa, kilikosa nguvu Fulani ya hamasa ya kuhitaji mafanikio zaidi msimu uliopita hasa baada ya kufeli katika malengoya kuingia miongoni wa klabu Nane Bora za ulaya. Asilimia kubwa ya wachezaji wa City ni wale walioshinda mataji mawili ya ligi kuu ndani ya misimu minne iliyopita hivyo suala la uzoefu wa kushinda kitu kigeni upande wao.
Mechi Tatu bila kuruhusu nyavu zao?
Ndiyo, City ilichapa Chelsea 3-0 katika gemu yao ya Pili nay a kwanza katika uwanja wa Etihad. Aguero ( mfungaji bora wa msimu uliopita) alifunga goli lake la kwanza msimu huu akiwa katikati ya mabeki wanne wa Chelsea, dakika ya 31’, Kompany akafunga tena kwa stahili ya kuunganisha mpira wa kona ya Silva kisha kiungo, Fernandinho akafunga goli maridadi la mpira wa kiki ya moja kwa moja na kuwamaliza mabingwa watetezi.
nasri 2
City ilitengeneza nafasi kumi ( 18) katika gemu na Chelsea ambao walimumudu kufanya hivyo mara Kumi ( 10). Dhidi ya West Brom walitengeneza nafasi 20. Nafasi ( 8) za hari walitengeneza dhidi ya Chelsea, na ( 7) dhidi ya West Brom siku ambayo walimiki mchezo kwa asilimia 69. West Brom walitengeneza jumla ya nafasi ( 9) na kumfanya kipa Joe Hart ‘ ku-save’ mara mbili.
Dhidi ya Chelsea, Hart ‘ ali-save’ mara tatu na timu ilizidiwa kwa asilimia moja katika umiliki wa mpira. Safu ile ile ya ulinzi iliyo anza dhidi ya West BroM, Chelsea ndiyo ilitumika katika gemu ya Tatu na Everton. Iliendeleza ubora wao, safari hii dhidi ya kina Arouna Kone na Romelu Lukaku. Chelsea ilikuwa na Eden Hazard, Diego Costa katika mashambulizi lakini walizimwa.
Silva, Yaya na Fernandinho wameanza pamoja katika gemu zote msimu huu na walikutana na wachezaji wa ‘ Kingereza’, Tom Cleverley, Gareth Barry, Ross Barkley na James McCarthy na kutengeneza mchezo moja ya michezo migumu katika wiki ya Tatu.
Aguero, Navas na Sterling walianza pamoja dhidi ya Chelsea, watatu hao walibanwa mno dhidi ya Everton lakini mlinzi wa kushoto, Kolarov dakika ya 60’ akiwa katika ‘ angle’. Nasri akafunga akiunganisha mpira wa faulo dakika ya 88’ na kukamilisha asilimia 100 ya ushindi.
Licha ya kutoruhusu nyavu zao safu ya ulinzi ya City tayari imefunga mara Tatu kati ya magoli Nane waliyokwisha funga hadi sasa. Kopany katupia kambani mara mbili wakati Kolarov amefanya hivyo mara moja.
Wachezaji waliotakiwa kubeba majukumu hayo kimsingi ( washambuaji) wamefunga mara moja tu ( Aguero) lakini bado timu imefanikiwa kupata alama Tisa katika gemu Tatu tena wakifunga mara Nane. Yaya, Silva, Nasri, Fernandinho, viungo hawa wanne kila mmoja afunga goli moja. Hii inaonesha kuwa wachezaji wa kila idara hawako tayari kupoteza gemu kwa sababu ya kutofunga magoli.
RAHEEM STERLING……
Usajili ghali hadi sasa msimu huu katika ligi ya England. Sterling ameanza vizuri katika timu hiyo huku kasi yake ikisaidia safu ya mashambulizi kutengeneza nafasi nyingi katika kila mchezo. City walitengeneza nafasi ( 16) huku ( 9) zikiwa za hatari katika gemu na Everton. Kama si uimara wa mlinda lango, Tim Howard ( ali-save mara 7) bila shaka City ingeibuka na ushindi mkubwa zaidi.
Everton walitengeneza nafasi ( 10) tu huku Moja pekee ikiokolewa na Hart haikuwa na kasi pindi walipokuwa na mpira na viungo wa kati walisumbuliwa na uwezo wa kukimbiza mpira wa Navas na Sterling katika wings. Kuwa na mchezaji kama Sterling kisha ndani yake una Navas na Silva ni ishara mbaya kwa timu nyingine.
Sterling anaifanya City itengeneze nafasi nyingi katika gemu zake licha ya kwamba hajafunga wala kupiga pasi ya mwisho mchezaji huyo wa England ameongeza kasi, nguvu na maarifa katika timu ya Pellegrini. Kilichobaki ni kusubiri nini ataendelea kufanya. Watacheza na Watford mwishoni mwa wiki hii katika uwanja wa Ethad, kisha Cystal Palace ugenini, West Ham United nyumbani, Spurs ugenini……

HIKI HAPA KIKOSI CHA STARS KILICHOENDA UTURUKI

Stars 1Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ tayari imeondoka kuelekea Uturuki ambako itaweka kambi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Nigeria kuwania kufuzu kucheza michuano ya Mataifa ya Afrika mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa Taifa Septemba 5 mwaka huu.
Kikosi cha Taifa Stars kilichosafiri kuelekea Uturuki kimejumuisha wachezaji wa Azam na Yanga waliokuwa wakisubiri kumalizika kwa mchezo wa Ngao ya Jamii ambao ulipigwa siku ya Jumamosi na Yanga kuibuka kidedea kwa kutwaa ngao hiyo kwa mikwaju ya penati 8-7.
Hiki hapa kikosi kamili cha Stars kilichosafiri kuelekea Uturuki, Walinda mlango: Ali Mustafa (Yanga), Aishi Manula (Azam FC ) na Said Mohamed (Mtibwa Sugar)
Walinzi: Shomari Kapombe (Azam FC ), Abdi Banda, Mohamed Hussein, Hassan Isihaka (Simba), Juma Abduli, Mwinyi Haji Mngwali, Kelvin Yondani na Nadir Haroub (Yanga).
Viungo: Mudathir Yahya, Himid Mao, Frank Domayo (Azam FC), Salum Telela, Deusi Kaseke (Yanga) na Said Ndemla (Simba).
Washambuliaji: John Bocco, Farid Musa (Azam FC), Rashid Mandawa (Mwadui FC), Simon Msuva (Yanga), na Ibrahim Ajibu (Simba).
Kocha wa Stars Charles Boniface Mkwasa amesema wachezaji wakulipwa wa Tanzania wo watajiunga na Stars kulingna na kalenda ya FIFA pindi itakapohitaji wachezaji wa vilabu kwenda kuzitumikia timu zao za taifa.

USAIN BOLT AWEKA REKODI MPYA BEIJING

Hatimaye binadamu mwenye kasi zaidi duniani hivi sasa mjamaica Usain Bolt amethibitisha uwezo wake baada ya kushinda ubingwa wa dunia wa riadha za mita 100 mjini Beijing, China.
bolt
Usain Bolt alitumia sekunde 9.79 kumshinda mwanariadha mwenye kashifa mbili za matumizi ya dawa za kuongeza nguvu ‘doping’ aitwae Justin Gatlin ambaye wiki yote hii alikua akitajwa kama mpinzani wa kweli wa Bolt kutokana na kuwa na rekodi nzuri sana katika riadha.
Akizungumza mara baada ya ushindi huo, Usain Bolt amekiri kuwa hiyo ilikua ni mechi ngumu kuwahi kukutana nayo lakini hakusita kusifia uwezo wake na ufalme wake katika riadha.
Aidha akizungumza kuhusu kashifa zinazochafua mchezo huo hivi sasa za matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu ‘doping’ Bolt ameuthibitishia ulimwengu kwamba mazoezi na kujituma ndio siri pekee ya kufanya vizuri na kwamba madawa hayana tija yeyote mbele ya kujituma mazoezini.
Wawili hao sasa watapambana tena katika mbio za mita 200 jumatano hii huku Bolt akisema pamoja na kujiandaa vya kutosha lakini anatarajia ushindani mkubwa kutoka kwa Gatlin aliyekuwa kifungoni kwa matumizi ya dawa tangu 2011.

Diamond na Diva warushiana maneno hewani,


Msanii wa Kizazi kipya Diamond Platnumz na Mtangazaji wa Clouds Fm, Diva Loveness love wamejikuta wakirushiana maneno hewani kwasababu ya ugomvi wao chinichini ambao unaonekana ni wa muda mrefu.
Vita hiyo ya maneno ya watu hao ambao waliwahi kuimba wimbo wa pamoja ‘Piga simu’ imeanza baada ya Mtangazaji wa kipindi cha XXL, Bdozen kuwauliza kama washamaliza tofauti zao (hazijulikani) ndio Diamond akadakia na kumuuliza mtangazaji huyo kwanini huwa anamsema vibaya baada ya hapo ndio wakaanza kurushiana maneno makali.
Diamond alisikika akisema anawaza kwanini hakumk*za labda ndio heshima ingekuwepo lakini Diva alijibu hilo haliwezekani kwasababu Diamond sio Type yake. Mtangazaji wa kipindi cha XXL Bdozen alilazimika kuzima Mike kwasababu hakukuwa na dalili za watu hao kupatana licha ya kujaribu kuwapatanisha hewani.
Hatujui kilichoendelea lakini baada ya Muda kidogo, Diva aliamia kwenye mtandao wa Twitter, akialalamika kuwa Diamond alimtishia kumpiga

Icheki ndinga mpya ya bondia Floyd Mayweather

may
Bondia wa kimataifa Floyd Mayweather  haishiwi Headlines, mara nyingi Stori zake nyingi zinahusiana na utajiri alionao.
Niliwahi kuandika Stori kuhusu Floyd Mayweather kutojua kiasi cha pesa zake zilizopo benki kutokana na kuwa na kiasi kikubwa cha fedha nyumbani kwake.
ndani
Hii nyingine ya leo ni kuhusiana na gari la kifahari alilonunua bondia huyo aina ya Koenigsegg CCXR Trevita lenye thamani ya dola milioni 4.8.
injin
Aina hii ya gari yapo mawili tu duniani kote mpaka sasa.
Hivi ndivyo alivyoandika kwenye ukurasa wake wa @Instagram
The American boxer couldn't help bragging about his latest acquisition on Instagram (above and below)

Baada ya kuachana na Lewis Hamilton sasa Nicole Scherzinger yuko na huyu Muingereza.

eddy 5
Staa wa Rnb Nicole Scherzinger ’37’ aliyekuwa na kundi la The Pussy Cat Dolls amehusishwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na msanii wa Uingereza Ed Sheeren ’24’.
Nicole Scherzinger amekuwa na Ed Sheeran baada ya kuachana na mpenzi wake wa muda mrefu Lewis Hamilton.

Dk. John Pombe Magufuli ataja vipaombele 25 nakusema kuwa anayatambua matatizo ya watanzania

magufuli
Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana Kimezindua rasmi Kampeni zake za Uchaguzi wa Mwaka 2015 huku Mgombea wake Dk. John Pombe Magufuli akisema kuwa anayatambua matatizo ya watanzania na kutaja vipaumbele 25 vikiwemo Mapambano dhidi ya Rushwa, Elimu na Ajira.
Mgombea wa Urais kupitia tiketi ya CCM Dk Magufuli ajinadi kushughulikia rushwa. Aahidi kujenga mahakama maalum ya wala rushwa asema serikali yake itakuwa ya viwanda, Lakini pia adai anayajua matataizo ya watanzania na kusema yeye ndiye mwenye kuweza kuleta mabadiliko.
1. Umoja wa Taifa
2. Kulinda Muungano wa Tanzania.
3. Ulinzi na usalama
4. Kuheshimu mihimili ya Dola.
5. Mahakama maalum ya mafisadi na majizi
5. Utawala bora
7. Ataheshimu mawazo yote ya kuleta maendeleo hata yakitoka upinzani
8. Ataimarisha vyombo vya usalama
9. Vita dhidi ya ubadhirifu
10. Kodi ilipwe na wote
11. Ataongeza ajira kwa kuimarisha viwanda
12. Sekta ya kilimo itaimarishwa
13. Sekta ya mifugo itaimarishwa ili iwe na tija kwa kujenga viwanda
14. Madini yatadhibitiwa ili yalete maendeleo
15. Maji yatapelekwa Vijijini na mijini
16. Zahanati kila kijiji, Hospitali ya rufaa kila mkoa, kuboresha maslahi ya wauguzi
17. Elimu bure hadi kidato cha nne, nyumba za walimu zitajengwa.
18. Wanafunzi wa vyuo vikuu, atahakikisha mikopo inakwenda mapema ili wasome
19. Kujenga hostel za mwana vyuo
20. Maslahi ya watumishi, kila mtu anayefanya kazi atapata haki yake.
21. Gesi itasimamiwa vyema ili isaidie nchi
22. Barabara zitaboreshwa, flyovers kujenga ya kwanza salander, tazara
23. Msongamano Dsm utashughulikiwa
24. Reli itajengwa upya
25. Bandari, anga zitaboreshwa
26. Maslahi ya maliasili yataboreshwa ili watalii wengi waje ili tupate pesa
27. Serikali itakuwa rafiki kwa wawekezaji wenye nia njema
28. Maslahi ya wafanyakazi yatalindwa
29. Walemavu watalindwa na haki zao zitalindwa
30. Uhuru wa Habari utalindwa na atakuwa na waandishi karibu
31. Wasanii na wanamichezo haki zao zitalindwa, kutakuwa na Mfuko maalum kwa ajili hiyo

23 August, 2015

KAMPUNI YA APPLE YAZINDUA APP MPYA YA MUZIKI

Kampuni ya Apple imetangaza kubuni programu tumizi mpya inayojumuisha maktaba ya kupeperusha muziki moja kwa moja kwenye internet, programu ya kusikiliza redio kwenye internet na njia maalum ambayo wasanii wataweza kubadilishana vibao vya miziki ambayo bado haijachapishwa rasmi.
App hiyo mpya inajumuisha mfumo wa kubashiri na kupendekeza utakaotumia mwelekezo wa binadamu kuchagua pamoja na sheria ya hisabati ya kutegua kitendawili kwa mifumo au algorithms.
150608221644_2
App hiyo mpya inalenga kuzipa upinzani Spotify, Tidal na app nyinginezo za muziki.
Kadhalika Apple imefichua kwamba Uingereza ndiyo itakayokuwa nchi ya kwanza kupata huduma ya kulipia ya Apple Pay nje ya Marekani. Watumiaji wa simu pamoja na vifaa vingine vya apple kupaa njia mpya ya kusikiliza muziki pamoja na redio.
” Watu wengi katika sekta hii wanachukulia kuzinduliwa kwa huduma hii ya muziki kama jambo kubwa, na matumaini yao ni kwamba hii itasaidia kubadili upokeaji wa huduma kwa usajili wa malipo kuwa bure,” amesema Chris Cooke, kutoka tovuti ya maswala ya muziki Complete Music Update.
“Lakini Spotify ina mbinu yenye matangazo ya kibiashara inayotolewa bure kuisadia kutangaza bidhaa zake jambo ambalo Apple haina.”
Huduma hii mpya ya Apple inazindua kituo cha radio cha Beats 1, mtangazaji katika kituo hicho ni aliyekuwa DJ wa BBC Zane Lowe miongoni mwa watangazaji wengine mashuhuri.
150608203311_apple_music_640x360_apple.com_nocredit
App hiyo vile vile ina uwezo wa kufanya kazi pamoja na programu tumizi ya Siri inayotoa msaada wa maelekezo kwa sauti na kuwawezesha watumiaji kuiamuru icheze wimbo kutoka sauti ya filamu au mwaka bila kuhitaji kujua jina la wimbo huo.

Manchester United haifungiki.

LVG
Ukiwa umepita mwaka mmoja tangu Manchester United ilipoanza kuwa chini ya kocha Mdachi Louis Van Gaal dalili za kocha huyo kuanza kuielekea njia ya mafanikio zimeanza kuonekana baada ya timu yake kuanza kufanya vizuri .
Hivi karibuni United imejikuta ikishika nafasi ya tatu kwenye ligi kuu ya England baada ya michezo miwili ikiwa imeshinda michezo dhidi ya Tottenham na Aston Villa na kujikusanyia pointi sita huku ikiwa haijaruhusu bao hata moja.
Moja ya mambo ambayo yamezungumzwa sana kwenye vyombo vya habari ni jinsi ambavyo United wanahitaji kuongeza nguvu kwenye eneo ya ulinzi ambapo wamekuwa sokoni wakiwasaka mabeki bora kama Sergio Ramos na Nicolas Otamendi .
Kauli ya United kuhitaji kuboresha idara ya ulinzi imepata nguvu zaidi baada ya kocha Louis Van Gaal kumchezesha kiungo wa kati Daley Blind kwenye eneo la ulinzi hali ambayo imewafanya wengi waamini kuwa anahitaji mtu kwenye nafasi hiyo.
United iliendeleza rekodi ya kufungwa mabao machache katika mchezo wake wa jana(jumamosi) dhidhi ya Newcastle .
United iliendeleza rekodi ya kufungwa mabao machache katika mchezo wake wa jana(jumamosi) dhidhi ya Newcastle .
Hata hivyo takwimu zinaongea kinyume na yale yanayozungumzwa na wachambuzi ambapo United inaonekana kuwa timu yenye safu borra ya ulinzi katika michezo iliyochezwa tangu mwezi Novemba .
United imeongoza kwa kufungwa idadi ndogo ya mabao ambapo tangu mwaka jana imefungwa mabao 23 pekee ikiwa mbele ya Chelsea ambayo Imeruhusu mabao 27 , takwimu hizi zimeanzia kwenye michezo 12 ya mwisho ya msimu uliopita mpaka michezo mitatu ya msimu huu ambapo katika michezo ya msimu wa mwaka 2015/2016 bado United haijaruhusu wavu wake kuguswa.
Chelsea ndio timu ya pili kwa idadi ya mabao ya kufungwa katika michezo ya ligi ya England tangu mwezi novemba mwaka jana.
Chelsea ndio timu ya pili kwa idadi ya mabao ya kufungwa katika michezo ya ligi ya England tangu mwezi novemba mwaka jana.
Chelsea imejikuta ikianza Ligi vibaya baada ya kufungwa kwenye mchezo mmoja huku ikitoka sare kwenye mchezo mwingine na hii leo (jumapili) vijana hawa wa Mourinho wanaingia uwanjani kucheza na West Bromwich Albion katika mechi ambayo matokeo yoyote tofauti na ushindi kwa Chelsea yatakuwa mabaya.

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...