30 April, 2016

New Music: BenPol & Baraka ft Mr.blue. MWAMBIE

Ngoma mpya kutoka kwa wakali hawa katika muziki wa bongo flava.. nawazungumza Benpol na Baraka Da-Prince wakimshirikisha Mr.Blue, ngoma inakwenda kwa jina la MWAMBIE na imefanyika katika studio za Dully "studio 4.12"

Bofya HAPA kuipakua nyimbo hiyo.


PITIA NA HIZI PIA
>Mambo 8 unayopaswa kufahamu juu ya Ujio mpya wa iPhone 7
> Oliver Mtukudzi picha Halisi ya Muziki wa Kiafrica.
>Wafahamu madancer Albir Rojas na Sara Lopez wakali wa 'Kizomba dance' 
>ELIMU YA TANZANIA YENYE MFUMO WAKIKOLONI

29 April, 2016

Download Music: Ruby Ft. Allice & Nandi - Mama

post-feature-imageRuby ambaye alianza kutikisa kwenye game la muziki baada ya kutoa ngoma ya Nayule kisha akaja juu hadi leo kila ngoma ambayo anaitoa imekuwa hit ameungana na Allice pamoja na Nandi wakakuletea wimbo wa Mama.

28 April, 2016

New video: Sajna – Ndoto Yako

Ni yule yule aloimba Mganga na Iveta, kutokea pande za Rock-city Sii mwingine bali ni Sajna. Leo katuletea video inayokwenda kwa jiana la Ndoto Yako baada ya kimya cha mrefu tangu kutoka katika mikono ya aliekua Maneger na producer wake aliye-fahamika kama Kid-Boy .Angalia hapa video hiyo..

Mambo 8 unayopaswa kufahamu juu ya Ujio mpya wa iPhone 7

iPhone with sakuraKila mwaka, kampuni ya Apple inay-tengeneza simu za i iPhone 7 huwa wanatoaga toleo jipya la simu hizo ambazo huvutia watumiaji weengi ulimwenguni. Tangu kutolewa kwa iPhone 6 na iPhone 6 Plus kampuni hiyo wameweza kuboresha simu hizo kwa maana kwamba katika mfumo wa kiuendeshaji(operating system) na pamoja na kuongeza  ukubwa wa Screen. Kumekuwa na kukosolewa kwa design mbaya ya simu hizo hasa katika upande wa camera.
Uvumi ulioko sasa ni ujio mpya wa  iPhone 7, watu ulimwenguni kote wamekuwa wakijiuliza maswali je,nn hasa kitakua kimebadilika na kuboreshwa? Leo nitakupatieni angalo mambo 8 muhimu juu ya ujio mpya wa iPhone 7, na mambo hayo ni kama yafuatayo:-

1.Inatazamiwa kuachiliwa mwezi September.
Ifahamike tangu kutolewa kwa Phone 5, iPhone 5S, iPhone 6 na iPhone 6 plus zimekua ziktolewa katika mwezi September hivyo wataalamu wa mambo wametazamia Simu hiyo itatoka mwezi September. Na kutokana na kuvuja kwa Email kutoka Vodafone kwenda  kwa wafanya-kazi wake, imefahamika kua  iPhone 7 itatoka tarehe 25 mwezi September. Aidha Email hiyo iliyo vuja ime eleza kua watu wataanza ku-order Simu hizo kuanzia September18.

2.Itakuja na Toleojipya la  iOS 9.
Bila hata kuuliza ni kwamba simu hiyo itakuja na toleo jipya la mfumo wa  iOS 9 na hii ilitangazwa na kampuni hiyo kweny Worldwide Developers Conference (WWDC) 2015 mnamo June 8, 2015. Imekua ikizoeleka na kufahamika kuwa kampuni ya Apple imekua ikitoa new iOS version kabla hata ya officially releasing the final version. Na imekua ni kawaida kwamba new iOS is always prepared for a new iPhone release event.

3. Front camera: full 1080P at 240fps
 “iOS 9 is hinting at future device front cameras having: 1080p resolution, 240fps slow mo, panoramic capture, flash” Taarifa hii ilitolewa na developer Hazma Sood ikielezea kwamba  Simu hiyo itakuwa na Camera ambayo itakuwa na uwezo wa kuchukua panoramic images, 1080p video and slow-motion clips at 240 frames kwa Sekunde. This is a big improvement tangu kutolewa kwa iPhone 6 and iPhone 6 Plus only support 720P video shooting for FaceTime talking. Na inavyo onekana ni kwamba main camera itakuwa na uwezo wa mega-pixel 12 tofauti na iPhone 6 yenye mega-pixel 8 tuu( wale wa instagram mjiandae).

4.Flash light kwenye camera ya mbele.
Kama tunavyo fahamu ni kwamba hakuna toleo lolote la iPhone lililo wahi kutoka likiwa na Flash light kwenye camera ya mbele, hivyo kwenye iPhone 7 jambo hilolitakuwepo. Wale wapenzi wa zile mambo za selfie this is good news for you!

5.Force Touch screen design
 According to the report from Macotakara, Apple’s next iPhone would be 0.15mm longer and 0.2mm thicker than existing ones (iPhone 6 and iPhone 6 Plus) because it’s adopting the Force Touch screen board, which has been adopted by Apple Watch. From the tech blog 9to5mac report released last month, Apple would apply this touchscreen board to enhance iMessage, keyboard and Apple Pay performance.

6. Itakuja na processor yenye nguvu zaidi.
Toleo hilo jipya la iPhone litakuja na Apple’s A9 processor, ambayo itakua na uwezo wa 2GB RAM ikiwa na mara mbili zaidi ya ile ya iPhone 6. “Additional RAM would allow iOS to leave background tasks and tabs in Safari open for longer without a need to reload or refresh,” it says. “But additional RAM can also come with costs to battery life, as memory constantly consumes power.”.

7.Haitakuwa na  sehemu ya kuchomeka head-phone.
Ifahamike kwamba toleo hili litakua ni toleo la aina yake kuwahi kutolewa na Apple maana itakuwa ni simu nyembaba kuwahi kutokea. (0.15mm longer and 0.2mm). Kwa maana hiyo itakulazimu kununua Bluetooth headphones, jambo ambalo lita wachukiza watu wengi.

8.Utakua na uwezo wa kuichaji kwa wireless.
 Apple is apparently testing a prototype with wireless charging, a rumour that comes straight from Chinese social network Weibo.
But that’s not the only model Apple is testing. Other prototypes include multi-Force Touch, a fingerprint scanner in the screen, and USB-C connector.
No one knows which of these will make it to the market... if any.

Hayo ndio mambo unayopaswa kuyafahamu wewe mpenzi na mtumiaji wa iPhone. unaweza kununua iPhone 6 kwa bei poa kabisa leo kwa wauzaji maarufu duniani, Hapa na wazaungumzia Amazon. Fuata picha inayofuata hapo chini kufahamu namna ya kujipatia simu hiyo kwa bei poa .




Jiunge nami leo

* indicates required

Music: Madee – Migulu Pande


Kutokea Tip-Top connection Madee katoa ngoma yake mpya  leo inayokwenda kwa jina la “Migulu Pande” ambayo imetengenezwa na Producer Tspice kutoka Nigeria na Tuddy Thomasi kutoka ngoma record.
Jipakulie ngoma hiyo kwa kubofya HAPA.



27 April, 2016

Cellebs 10 maarufu waliogundulika kuwa na HIV/AIDS nchini Marekani.

Wapo mastar wengi mno duniani waliyo endekeza bata na mwisho wa siku kuishia kukanyaga miwaya (Kupata UKIMWI.) ila wamekua mstari wa mbele kuhamasisha jamii zao juu ya Gonjwa hili hatari ambalo limemeza wengi na ndio hasa chanzo cha ongezeko la watoto wa mitaani na Yatima.
Leo nitakupa angalao mastar 10 walio kugundulika kua wameambukizwa Virusi vya UKIMWI.

1.Kevin Peter Hall

Kevin Peter Hall Kwa wale wapenzi wa movies mtakua mnamfahamu huyu jamaa, alicheza kwenye movie ya 'Predator'. Aliambukizwa Virusi vya UKIMWI kwa njia ya kuwekewa damu(blood transfusion) na baadae aliugua Homa ya Mapafu(pneumonia) na kuiga Dunia.





2.Magic JohnsonNo. 17 Magic Johnson Mcheza kikapu maarufu nchini marekani "Magic Johnson" aligundulika kua ana virusi vya UKIMWI mnamo mwaka 1991 hali iliyo mfanya kuacha Kikapu katika ligi ya NBA, na hakufahamu kuwa ni nani hasa alimpa ugonjwa huo sababu alikua ana wapenzi wengi (Michepuko).

3.Rick WilsonRick Wilson Mpiga guitar wa bendi ya B-52's ambae pia alikua shoga maarufu alifariki dunia mnamo mwaka 1985 akiwa na umri wa miaka 31 sababu ya AIDs.

4.Michael Jeter
 Michael Jeter unaweza ukamfahamu mr.Jeter kwenye movie ya 'The Green Mile.' Huyu nae aligundulika ana virusi ila hakufariki kwa ngoma na badala yake kilicho muua ni kifafa akiwa na umri wa miaka 50.

5.Eric "Eazy-E" Wright
 Easy E of NWA in Torrance, CA. 1989 Rapper na mwanzilishi wa kundi la N.W.A aligundulika na maambukizi ya virusi vya UKIMWI mwaka 1995. Alikua ni mtu wa totoz( madem) na alikua na watoto 7 kila mmoja na mama yake(doh!). Alifariki mwezi mmoja baadae.

6.Arthur Ashe
 Arthur Ashe Mcheza tenis maarufu duniani Arthur Ashe alipata maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa njia ya Kuongezewa damu Kipindi alipokua amefanyiwa operation ya moyo kwenye miaka ya 80. Alipokua na miaka 49 tuu alifariki Dunia.

7.Gia CarangiGia Carangi Huyu alikua ni mwana mitindo katika miaka ya 70 na 80 na aligundulika kuwa na maambukizi ya virusi vya UKIMWI akiwa na umri wa miaka 26 tuu. Na alifariki kwa magonjwa nyemelezi ingawa katika kipindi cha miaka mitano ya mwisho alisubuliwa na heroin addiction.

8.Timothy Patrick MurphyTimothy Patrick MurphyAn original cast member of 'Dallas,' Murphy alifariki kwa HIV mnamo mwaka 1988.

9.Tim Richmond
Tim RichmondNASCAR driver Tim Richmond Alifariki kwa Ugonjwa Huo na hakuna aliyekua anafahamu kua jamaa huyo ni muathirika mpaka ilipokuja kugundulika siku 10 baada ya kifo chake.

10.Charlie Sheen
No. 1 Charlie Sheen Kama ni mfuatiliaji wa 'The Today Show', basi nyota huyo kuna kipindi alitangaza kua Amepata maambukizi na hii ilikua ni siri aliyo kaa nayo kwa miaka minne huko nyuma na watu walio kuwa wanaifahamu siri hiyo walikua wakitaka pesa nyingi kutoka kwa jamaa huyu ili wasitangaze hivyo jamaa akaona atangaze tuu kuondoa Usumbufu.
"I'm here to admit that I am in fact HIV-positive. And I have to put a stop to this onslaught, this barrage of attacks and of sub-truths and very harmful and mercurial stories that are about the [alleged] threatening the health" he told Matt Lauer.





New Music: Ferooz – Nimejifunza

CgESMWmUsAA2k3tKumekua na kimya kirefu mno kutoka kwa  Ferooz na leo hii katoka alipokua amejificha na hatimae kaja na nyimbo yake inayokwenda kwa jina la  "Nimejifunza" inavyo onekana humu ndani kaongea juu ya Ujio wake mpya na Ugumu alopitia kipindi alichokua kimya.
Jipakulie ngoma hiyo kwa kubofya >>>HAPA<<

Oliver Mtukudzi picha Halisi ya Muziki wa Kiafrica.


Linapotajwa jina la wimbo wa "Neria" basi kila mmoja wetu atakua na mawazo mawili tofauti ambayo yote humuongelea Nguli wa muziki wa Kiafrica na sio mwingine ni Oliver Mtukudzi kutoka kule Zimbabwe kwa mbabe Robert Mugabe.
Jina la utani huwa wanamuita "TUKU" ambapo jina hilo limetokana na jina Mtukudzi hivyo akaamua kufupisha jina lake hilo na kupata hiyo a..ka. amezaliwa mnamo 22 Septemba 1952 mjini Highfield, Harare) ni mwanamuziki wa Kizimbabwe. Oliver ni miongoni mwa wanamuziki walio maarufu kwa muda mrefu sana katika nchi hiyo ya Zimbabwe. Na alianza shughuli za muziki kunako miaka ya 1977 pale alipojiunga na bendi ya Wagon Wheels, ambayo pia alikuwemo na mwanamuziki wa zamani Bw. Thomas Mapfumo.

   Nyimbo ya kwanza ilikuwa "Dzandimomotera" iliyoheshimika sana, na hapo ndipo Tuku alipotoa albamu yake ya kwanza, nayo pia ilileta mafanikio makubwa kabisa. Mtukudzi nae pia ni mmoja wa wanakundi la Mahube, kundi la muziki la nchi za Afrika ya Kusini.

Oliver pia ni baba wa watoto watano na wajukuu wawili, wawili hao pia ni wanamuziki. Ana dada zake wanne na kaka mmoja ambaye tayari amekwisha fariki. Anafurahia kuogelea katika bwawa lake la kuogelea (swimming pool) ambalo lina umbo la gitaa. Oliver ametoa zaidi ya albamu 40 na amepata kushinda tuzo nyingi mno na hata zingine hawezi kuzikumbuka.
   
Filamu alizoshiriki:
  • Jit (mwong. Michael Raeburn , 1990)
  • Neria (mwong. Goodwin Mawuru, imetungwa na Tsitsi Dangarembga, 1993). Mtukudzi ndiyo alikuwa nyota wa filamu na yeye ndiye aliotengeneza nyimbo ya filamu.
  • Shanda (mwong. John na Louise Riber, 2002, rev. 2004)
 Tuzo alizowahi kushiriki na kushinda.
  • Tuzo ya KORA kwa ajili ya matayarisho mazuri ya nyimbo yake ya Ndakuwara mnamo mwaka wa 2002
  • Tuzo ya National Arts Merit (NAMA) mnamo mwaka wa 2002 na 2004 kama kundi bora la muziki/ mwanamuziki bora wa kiume
  • Tuzo ya KORA kama mwanamuziki bora wa kiume wa Africa na tuzo ya Lifetime Achievement mnamo mwezi Agosti wa mwaka wa 2003
  • Tuzo ya Reel kama lugha bora ya Kiafrica mnamo wamaka wa 2003
  • An honorary degree from the University of Zimbabwe in Desemba 2003
  • Tuzo za M-Net Best kama nyimbo bora ya filamu mnamo 1992, kwa ajili ya filamu ya Neria.

Tafadhali pitia na Hizi zifuatazo.
 1.Wafahamu madancer Albir Rojas na Sara Lopez wakali wa 'Kizomba dance'
 2. Sababu tano ni kwa nini Bongo flava ya Awali ilikuwa bora kuliko ya bongo 








Music: Nuh Mzinda Ft Ali Kiba – Jike shupa

Kimekua kimya cha muda tangu Nuh mziwanda kuachia ngoma yake ya Mwisho ilokwenda kwa jina la hadith na baada ya hapo jamaa huyu alikaa tena kimya kirefu hali ilowapa mashabiki wake mashaka, ila leo katuletea kitu cha  Jike shupa akiwa kamshirikisha Alikiba. Ni muziki muzuri kwa watu wazuri..
Bonyeza >>>HAPA<< kuupakua wimbo huo







26 April, 2016

New Music: Barnaba - Wanifaa

post-feature-image Baada ya kuonekana picha mitandaoni kwa muda mrefu sasa ikionyesha Barnaba Class akiwa amepoz na mtoto wa kike hatimae leo Barnaba katuletea kitu, ni Audio  yake mpya inayokwenda kwa jina la "Wanifaa" ni ngoma nzuri kwa watu wazuri wanaopenda muziki mzuri.
Bonyeza >>>HAPA <<< kuupata wimbo huo.



Video: Sugu – Freedom

Joseph Mbilinyi (Mr. II Sugu) ambaye ni Mbunge wa Mbeya mjini ni msanii wa kitambo wa hiphop baada ya kimya kirefu kwenye bongo fleva, ameachia video mpya ya wimbo unaitwa ‘Freedom‘ ikiwa ni kazi ya MJ Records video imeongozwa na Hanscana. I mekua kitambo  sana tangu Mr. II Sugu kuacha kutoa kazi na kuingia katika siasa na kiukweli mashabiki wake tuliukosa uhondo.







24 April, 2016

Wafahamu madancer Albir Rojas na Sara Lopez wakali wa 'Kizomba dance'

Well! well! well!.. Leo nmepanda hapa MTOKAMBALI kivingine kabisa japo bado niko kule kule kwenye Burudani na Leo nitawapatia angalao Biography ya wakali hawa wa dance ulimwenguni. Linapotajwa jina la 'Kizomba' basi kila mmoja haachi kumfkiria Albir Rojas  na Sara Lopez maana wakali hawa ndio wenye KIZOMBA DANCE.

Nianze na Albir Rojas:-
Ni  dancer, choreographer, actor na ni professor.
 Alizaliwa mnamo 25th mwezi October 1979 huko PANAMA na mama yeke kumpatia jina la Albir ambalo hakutaka mwanae kuchakachua jina hilo kamwe, na mama yake aliamua hivyo sababu kuna siku mama yake huyo alikwenda nchini India nakumkuta mama mmoja akimwita mwanae wa kiume "Albir" kisha akamuuliza mama huyo wa kihindi jina hilo lina maana gani? basi mama yule wa kihindi akajibu "BRAVE" na ndipo mama yake dancer huyu akaamua kumpatia jina hilo.

Wakati akiwa mdogo wa umri mika 12, mama yake alikua akimfundisha dancing japokua wakati huo jamaa huyu alikua havutiwi na dancing na badala yake alikua akivutiwa na Video games na akaendelea na video games pamoja na dancing mpaka akiwa na umri wa miaka 14 wakati alipokuwa High school.
Akiwa high  school alialikwa kushiriki kwenye choreography na hapo ndipo Albir akaamua kuikubali DANCING na kuanza kuifanyia kazi. Akiwa na umri wa mika 16, alijiunnga na darasa ladance katika funky dance school na huko alikua akijifunza mambo mengi kuhusiana na choreography.
 Albir alimaliza high school akiwa na umri wa miaka 18 na lifanikiwa kutoka na Bachelor of Commerce degree (Accounting).

Baada ya kumaliza masomo yake alipata kazi akiwa kama accountant na huku alikua pia akisoma masomo yake ya shahada ya uzamivu katika maswala hayo hayo ya biashara. Albir alikua akiutesa mwili wake kwa kazi mno maana hasubuhi alikua akienda kazini na jioni alikua akihudhuria darasani na usiku alikua akifanya mazoezi ya dance jambo ambalo mwili wake kuna muda uluonekana kuchoka.
Licha ya hivyo jamaa huyo hakukata tamaa na aliamua kuacha kazi ofisini na kuamua Kuifanya sanaa kwa ujumla kipindi chote cha cha maisha yake.

Albir alikua katika dancing mwaka hadi mwaka na aliwahi kuonekana katika kazi kama Grease, the King and I, Fame, West Side Story na Fantastics, kote huko alikua kama Actor na dancer.
Aliamua kwenda  Madrid kwa ajili ya masomo yahusuyo Communication, Advertising, Film making and Sound Technician na alimaliza na akamua kuishi Madrid tangu mwaka 2001 mpaka leo.

Albir amekua akifundisha dancing styles kama cuban salsa, salsa in line, bachata dominicana, bachata madrid, hip hop, popping, KIZOMBA, TARRAXINHA, SEMBA and ballroom dances ambazo yeye ni MASTER wa Style hizo.
Albir anapenda anachokifanya na hua anapenda kushirikisha feelings zake kwa watu wapenda dancing mfano Mimi ( ha ha ha haa).

Nije kwa bibie Sara López:-
AlbirRojas2Mwana dada huyu ni mzaliwa  Madrid, Spain na alizaliwa mnamo mwaka 1986. Alianza dancing akiwa na umri mdogo wa miaka 5 na alitumia miaka 7 kujifunza dance katika ballet, contemporary dance, modern dance, hiphop. na akiwa na umri wa miaka 16 alinza na Latin dances, Salsa, Bachata pamoja na Kizomba.

Akiwa na umri wa mika 18 tuu, akawa amemaliza elimu yake ya  Sekondary na akaamua kwenda Madrid kwa ajili ya kujifunza classical ballet. Huko alikaa kwa muda wa mika mitatu zaidi akiwa akijifunza tena Latin rhythms.
Alipata dancing partner wake wa kwanza nchini humo aliyejulikana kama Ronald Jara ambaye alionekana nae katika mashindano ya dancing Madrid in Africadançar (Lisbon Ureno) mnamo mwaka 2012.
na baadae akatambulishwa kwa Mkali Albir ambaye walionekana kufanya kazi kwa pamoja hadi mwaka 2014 walipo achana.

Ikumbukwe kuwa Dancers hawa hawakuwahi kuwa wapenzi kamwe licha ya watu wengi ulimwenguni kufahamu kuwa walikua wapenzi. Nikupatie angalao video moja ya wakali hawa wakifanya vitu vyao katika KIZOMBA.

Mpaka hapo sina la ziada nikutakie siku njema na tukutane tena Juma lijalo hapa hapa MTOKAMBALI,







Mtokambali |

Video MPYA: Mafikizolo na Diamond- COLORS OF AFRIKA

Baada ya muda mrefu tangu kurekodiwa Audio ya ngoma hii hapa mnamo June 2014 Johannesburg South Afrika, hatiae leo video ya wimbo huo imetoka. Video inakwenda kwa jina la  COLORS OF AFRIKA ambayo ndani yuko Diamond Plutnum akiwa sanjari na Mafiki Zolo kutoka kule bondeni kwa madiba.
Chukua nafasi hii kuitizama video hiyo 'COLORS OF AFRIKA' na kumbuka kuwashirikisha wana kitaa.






Mtokambali

New Video: Lady Jaydee – Ndindindi

post-feature-imageBaada yaluachilia Audio ya NDINDI, mwana dada Lady Jaydee katuletea video rasmi ya wimbo huo ambayo imeongoza na director Justin Campos. Chukua time yako kuitazama video hiyo ya mwana dada komandoo hapo chini kwa kubonyeza PLAY. Pia usisahau kuwasharikisha wana kitaa.





Mtokambali

Music:Maarifa Nac ft Barakah Da Prince – Sielewi

 IMG-20160423-WA0002
Msanii wa muziki wa Hip Hop, Maarifa Nac, ameachia wimbo wake mpya, ‘Sielewi’ ambao amemshirikisha Barakah Da Price msanii ambae anazidi kufanya poa katika game ya bongo flava. Chukua time yako kuidownloa na kuisikiliza ngoma hiyo kisha usisahau kuwashirikisha wana kitaani .
Download ngoma hiyo HAPA 

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...