Baada ya miaka nane tangu aondoke Barcelona, staa wa zamani wa klabu hiyo, Ronaldinho amerudi katika klabu hiyo huku akikabidhiwa jukumu lingine tofauti na kucheza soka.
 ronadinho
Ronaldinho ambaye aliichezea Barcelona msimu wa 2003-2008 na kufunga magoli 91, kutoa pasi za magoli 52 katika michezo 198 kwa sasa atakuwa balozi wa dunia wa Barcelona.

Taarifa zinaeleza kuwa sababu ya Barcelona kumtumia Ronaldinho kuwa balozi ni kutokana na umaarufu alionao maeneo mbalimbali na lengo lao ni kukuza jina la Barcelona zaidi ya ilivyo sasa ili kuiwezesha kufahamika zaidi na hata kufungua milango mipya ya kibiashara.

Baada ya kupewa nafasi hiyo Ronaldinho amepost picha katika ukurasa wake wa Instagram akiwa nje ya uwanja wa Nou Camp unaotumiwa na Barcelona na tayari amehudhuria uzinduzi wa ofisi za Barcelona za New York, Marekani.