13 August, 2016

Download Music: Jah Prayzah Ft. Diamond Platnumz – Watora Mari

https://youtu.be/U8Ogqf9P2qIMwanamuziki Diamond Platnumz anazidi kufanya collaboration na wanamuziki kutoka nje ya nchi ambapo wakati huu amefanya na mwanamuziki kutoka Zimbabwe , anayefahamika kwajina la  Jah Prayzah. Kumbuka kushare ngoma hii na wana kitaaa kwa kadiri uwezavyo. 
>>>Bofya ku Download Music: Jah Prayzah Ft. Diamond Platnumz – Watora Mari.<<<<

Sababu kwanini Paul Pogba amefungiwa kucheza vs Bournemouth

Kiungo mpya wa Manchester United Paul Pogba amesimamishwa kuitumikia timu yake kwa mchezo wa kwanza wa Premier League,  chama cha soka cha England kimethibitisha
Pogba, 23, alirejea Old Trafford kutoka Juventus kwa ada ya uhamisho iliyovunja rekodi ya £89.3 million, miaka 4 baada ya kuhamia klabu ya Turin kwa ada ya £800,000 kufuatia kukosa muda wa kucheza na mgogoro wa mkataba mpya. 
Hata hivyo Pogba itambidi asubiri mpaka wiki ijayo kucheza mchezo wake wa kwanza na klabu yake mpya kwa sababu amefungiwa kucheza mchezo wa Jumapili dhidi ya Bournemouth.

Kiungo huyo wa Ufaransa amesimamishwa kwa kosa la kupata kadi mbili za njano katika msimu uliopita wa mashindano ya Coppa Italia, na adhabu yake imehamia katika michezo inayosimamiwa na Chama cha soka cha England

12 August, 2016

Download Music: Dully Sykes Ft. Harmonize – Inde

Kutoka Wasafi Rec, Dully Sykes anakuja na Inde ngoma ambayo amemshirikisha Harmonize. Bofya hapo chi kupata wimbo huo. Kisha kumbuka kuwashirikisha wana kitiaa kwa kadiri uwezavyo,

DOWNLOAD HAPO CHINI:

10 August, 2016

Africa ina medali mbili tuu mpaka sasa michuano ya Olimpiki huko Rio.

Chad Le Clos
Kufika sasa Afrika imeshinda medali mbili kupitia waogeleaji wa Afrika Kusini, Chad Le Clos na mwenzake Cameron van der Burgh.Wote wamepata medali za fedha.

Clos alikuwa wa pili shindano la mita mia mbili mtindo wa freestyle la wanaume, mshindi akiwa ni Sun Yang wa China..
Burgh amefuzu kwa fainali ya mita 200 mtindo wa Butterfly baadaye leo hii anakonuia kutetea taji lake aliloshinda London miaka minne iliyopita lakini anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa nyota wa Marekani Michael Phelps anayelenga kupata dhahabu yake ya 20.
Kwa jumla Afrika Kusini ni ya 21 kwenye msimamo wa medali pamoja na Indonesia na New Zealand.Timu ya Kenya ya Raga ya wachezaji 7 kila upande
Bingwa mtetezi, Marekani inaongoza ikiwa na jumla ya medali 19 ikifuatiwqa na China 13 na Australia ni ya tatu na medali saba.
Kwa upande wa dhahabu Marekani na China wote wana dhahabu tano na Australia dhahabu nne.
Tukiangazia mataifa ya Afrika Mashariki, mabondia wa Kenya wanazidi kunawiri kwani jana Peter Mungai ameanza vyema kwa kumshinda Bin Lv wa China kwa pointi uzani wa light-flyweight.
Bondia mwingine wa Kenya Rayton Okwiri naye pia alishinda pigano lake la kwanza Jumapili uzani wa welter na siku hiyo hiyo Kennedy Katende wa Uganda akashindwa kwa TKO raundi ya kwanza na Joshua Buatsi wa Uingereza uzani wa light-heavy.
Mabondia wa Afrika Mashariki ambao bado hawajacheza ni Ronald Serugo wa Uganda uzani wa 'fly' na Benson Gicharu wa Kenya uzani wa bantam.Timu ya Kenya ya Raga ya wachezaji 7 kila upandeNigeria inafanya vyema kwenye mchezo wa tenisi ya meza huku Angola ikiwika kwa mpira wa mikono upande wa wanawake kwani kufikia sasa wameshinda mechi zao zote mbili na wako nafasi ya kwanza kundi A pamoja na Brazil. Jumla ya mataifa 206 yanashiriki michezo ya Olympiki ya mwaka huu

J. Cole’s Top 10 Rules For Success

Do you need to get Success in your life? do u need awesome life so far? here we go...Check out some words of wisdom from J. Cole on achieving success. Don't forget to share this article to all of friends any where through social medias as much as you can.

Tizama hapa Trailar ya Movie mpya inayokwenda kwa jina la Netflix’s Luke Cage

Marvel’s Luke Cage, which premieres globally on September 30, 2016 at 12:01am PT is the third show in the Defenders series to launch on Netflix. The series follows the releases of Marvel’s Daredevil and Marvel’s Jessica Jones, leading up to the future release of Marvel’s Iron Fist, and ultimately, Marvel’s The Defenders/

Drake amtaja J-cole kama Legendary wa kizazi cha sasa

Drake Rapper anae zidi kufanya poa katika game ya muziki nchini marekan Drake amemtaja  Mwanamuziki J.Cole kama Legendari wa kizazi cha sasa, Akiwa katika show ya Fainali za MSG ambazo zilihudhuriwa na wasanii kibao kama vile Julez Santana, Cam’ron, Fat Joe, na Remy Ma , Drake alisema  
"You are looking at one of the smartest, greatest, most legendary artists of our generation.".
Tizama video fupi ya show hiyo hapo chini

Video mpya: Bonge la Nyau ft Q Chillah-'Aza'

Msanii wa Bongo Fleva, Bonge la Nyau time ameachia hii video mpya ya single iitwayo Aza aliyomshirikisha Q Chillah, video hiyo imetayarishwa na Kwetu Studio. Tizama video hiyo hapo chini kisha washirikishe wana kitaa kupitia mitandao yako ya kijamii kadiri uwezavyo.

Serena williams atupwa nje katika michuano ya Olimpiki

Bingwa huyo wa dunia alionekana na kufanya makosa mara tano mfululizo
Bingwa mtetezi Serena williams ametupwa nje ya mashindano ya michezo ya Olimpiki baada ya kushindwa na mchezaji wa Ukraine Elina Sitoniva katika hatua ya tatu ya tennis ya mashindano ya wanawake.

Williams ameshindwa kwa seti 6-4-6-3 na Sitovia ambae anashika nafasi ya 20 duniani.
 Bingwa huyo wa dunia alionekana na kufanya makosa mara tano mfululizo katika raundi ya saba kipindi cha pili.
"haikua kama nilivyokua nataka iwe lakini angalau nimweza kufuzu kuja Rio, hilo lilikua kati ya malengo yangu" amesema William.Serena Williams

" Mchezaji mzuri leo ameshinda leo lakini najua kuwa wakati mwingine utakua mchezo mzuri sana na nasubiri wakati huo"
William na mdogo wake Venus wametolewa katika mashindano ya wawili ya wanawake siku ya jumapili na raia wa jamhuri ya watu wa Cze, Lucie Safarova na Barbora Strycova.

09 August, 2016

New Video: Usher – No Limit Feat. Young Thug

Kutoka kwenye album yake ya nane aliyo ipa jina la Flawed Usher Raymond kaachia video ya single yake mpya iliyopewa jina la No Limit akiwa kamshirikisha vyema rapper Young Thug. Tizama video hiyo hapo chini kisha kumbuka kuwashirikisha wana kitaa kwa kadiri uwezavyo.

Sababu ya samaki kupungua Ziwa Tanganyika

Ziwa Tanganyika
 Utafiti mpya umebaini kupungua pakubwa kwa idadi ya samaki katika Ziwa Tanganyika, mojawapo ya  maziwa muhimu zaidi kwa uvuvi duniani, kumetokana na ongezeko la joto duniani katika karne moja iliyopita.

Ziwa Tanganyika ndilo la kale zaidi Afrika na samaki wake huwa muhimu sana kwa lishe katika mataifa yanayopakana na ziwa hilo.
Lakini idadi ya samaki imepungua sana, huku wavuvi wakiendelea kuongezeka.
Ongezeko hili la wavuvi lilidhaniwa kuwa chanzo kikubwa cha kupungua kwa idadi ya samaki.
Lakini utafiti mpya unaonesha chanzo hasa ni ongezeko la joto duniani kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.
Ziwa Tanyanyika ndilo la pili kwa ukubwa duniani miongoni mwa maziwa yenye maji yasiyo na chumvi na maji yake huwa katika mataifa manne: Burundi, Jamhuri ya KIdemokrasia ya Congo, Tanzania na Zambia.
Samaki kutoka kwa ziwa hilo hutoa asilimia 60 ya protini zitokanazo na wanyama ambazo huliwa na watu eneo hilo.
Aidha, ni eneo lenye aina nyingi ya wanyama na mimea.


Ziwa Tanganyika 

Ili kufahamu mabadiliko yanayotokea katika ziwa hilo, watafiti wamechukua sampuli za mchanga kutoka kwenye kina cha ziwa hilo.
Baada ya kufanya utathmini wa mchanga huo na visukuku, wamepata viashiria kwamba idadi ya samaki imekuwa ikishuka sambamba na ongezeko la joto duniani.

Wanasayansi wanasema katika maziwa yanayopatikana maeneo yenye joto karibu na ikweta, ongezeko la joto katika maji hupunguza kuchanganyikana kwa maji kutoka sehemu ya juu ya ziwa ambayo huwa na oksijeni pamoja na maji yenye virutubisho vingi sehemu ya chini kwenye ziwa.

Kutochanganyikana vyema kwa maji haya husababisha virutubisho vinavyofika juu kwenye ziwa kupungua, hili hupunguza ukuaji wa miani (mimea ya rangi ya kijani, kahawia au nyekundu inayoota chini ya bahari) na hili hupelekea kupungua kwa lishe ya samaki.

Ziwa Tanganyika

Watafiti waliohusika katika utafiti huo wanasema ongezeko la joto limepunguza kuchanganyikana kwa maji, kupungua kwa ukuaji wa miani pamoja na kupungua kwa maeneo ambayo viumbe waishio chini ya bahari wanaweza kuishi na kustawi.

"Wazo letu lilikuwa kuchunguza visukuku na kubaini kushuka kwa idadi ya samaki kulianza wakati gani," anasema Prof Andrew Cohen kutoka Chuo Kikuu cha Arizona.
"Iwapo hili lilifanyika kabla ya kuanza kwa uvuvi wa kiviwanda miaka ya 1950, basi ungekuwa na ushahidi mkubwa kwamba hili halitokani na ongezeko la uvuvi na hivi ndivyo tulivyobaini."

Wanasayansi hao hata hivyo hawajapuuzilia mbali athari za ongezeko la uvuvi katika miongo sita iliyopita.
Wanasema kumekuwa an ongezeko la watu tangu miaka ya 1990, hasa kutokana na wakimbizi waliotoroka mizozo na kuhamia maeneo yaliyo karibu na ziwa hilo.Ziwa Tanganyika
"Ukizingatia mtindo wa sasa wa kuendelea kugawika zaidi kwa maji kwenye ziwa, idadi ya samaki itaendelea kupungua. Watu wanaosimamia sera wanafaa kuanza kufikiria kuhusu chanzo mbadala cha mapato na lishe kwa watu wanaoishi eneo hilo."

Matokeo ya utafiti huo yamechapishwa katika jarida la kisayansi la Proceedings of the National Academy of Sciences.

CHANZO: BBC SWAHILI

Music: Ruby – Je Utanipenda(Cover)

Helen George 'Ruby' Mwanadada mwenye sauti murua na Hit-maker wa Na yule, Forever na nyingine kibao, safari hii katuletea Je Utanipenda ikiwa ni cover song yake Diamond. Sikiliza hapa alafu toa maoni yako na Kumbuka kuwashirikisha wana kitaa kwa kadiri uwezavyo.

Rapper Bow Wow kustaafu akiwa na miaka 29

Mwanamuziki maarufu wa nyimbo za 'hip hop' Bow Wow, ambaye jina lake halisi ni Shad Moss, ametangaza kuwa atastaafu kutoka kwenye fani ya muziki, akiwa na umri wa miaka 29, mwaka huu 2016.
Ametoa tangazo hilo kwenye mtandao wa Twitter.


Bow Wow alitoa albamu yake ya kwanza akiwa na umri wa miaka 13, mwaka 2000.
Baadhi ya nyimbo zake maarufu ni "Like You" akimshirikisha Ciara na "Let me hold you" akimshirikisha Omarion.

08 August, 2016

Video:Gentriez, Belle 9 na Young Dee-‘Chapaa’

 
GentrIez, Belle 9 na Young Dee wanatualika kwa pamoja kuitazama video mpya ya ‘Chapaa‘ ya kwake Gentriez video ambayo imeongozwa na  director Hanscana kutoka Wanene Entertaiment,Kumbuka pia kuwashirikisha wana kitaaa kupitia mitandao yakijamiii.

Bofya Download Hapo chini Kupakua Audio

loading...

07 August, 2016

Mwanasayansi anyongwa kwa kosa la usaliti huko Iran

Mwanasayansi kutoka Iran Shahram Amiri ameuawa
Iran imethibitisha kwamba imemuuwa mwanasayansi wa nyuklia, ambaye alituhumiwa kwamba aliipa Marekani habari muhimu kuhusu mpango wa kinyuklia wa Iran.

Shahram Amiri alitoweka mwaka wa 2009 alipokwenda kuhiji katika mji mtukufu wa Mecca .
Alipojitokeza mwaka uliofuatia alikuwa nchini Marekani , akisema kuwa alitekwa nyara na CIA.
Kupitia kwa mitandao ya kijamii alidai kuwa alikuwa ametekwa na kuwa aalikuwa akijificha kutoka kwa majasusi wa Marekani.
Lakini alidai kwamba aliweza kutoroka, na alikaribishwa kama shujaa aliporudi Iran.

Video tatu za Shahram Amiri

Lakini baadaye, Bwana Amiri alifikishwa mahakamani.
Marekani imesema bwana Amiri alikwenda Marekani mwenyewe, na kwamba aliwapatia habari muhimu.
Habari za kuuawa kwake ziliibuka jumamosi mamake mzazi aliposema kuwa alipokea mwili wake uliokuwa na alama za kunyongwa shingoni.

Msemaji wa mahakama aliwaambia waandishi wa habari kuwa ''Shahram Amiri alikuwa amewapa maadui wa Iran habari nyeti kuhusiana na mpango wake wa kinyuklia.''
Gholamhossein Mohseni Ejei alinukuliwa akisema.

Awali Amiri alipokewa kwa shangwe na taadhima aliporejea nyumbani.
Iran imekuwa ikitafuta maarifa ya kuunda silaha za kinyuklia japo imekuwa ikipinga kufanya hivyo na badala yake ikisema kuwa inatafuta nguvu mbadala za umeme.

ata hivyo majuzi ilikubaliana na mataifa yenye nguvu zaidi duniani kusitisha mpango huo wa kisiri na badala yake ipokee msaada kutoka kwa mataifa hayo yenye nguvu za kinyuklia.

loading...

Meneja timu ya taifa ya Kenya ya riadha atimuliwa huko Rio.

Mkurugenzi wa shirika la kupambana na madawa ya kuongeza nguvu mwilini ADAK Japhter Rugut ameahidi kuchunguza madai hayo kikamilifu.
Meneja wa timu ya taifa ya Kenya ya riadha katika michezo ya Olimipiki Meja mstaafu Michael Rotich, atahojiwa na kitengo cha jinai pindi atakapowasili Nairobi.

Waziri wa michezo wa Kenya Dr. Hassan Wario, aliyeko mjini Rio de Janeiro amethibitisha kuwa meneja huyo wa timu ya riadha ameamrishwa kurejea nyumbani mara moja.
''kwa hakika hatutavumilia mtu yeyote ambaye anaonesha dalili za kuyumbisha kampeini yetu dhidi ya madawa ya kusisimua misuli''

Gazeti la Sunday Times la jijini London, limetoa ukanda mpya wa video unayoonyesha Meja Michael Rotich, akiahidi kuwaonya wanariadha wa kikosi chake kuhusu ziara ya maafisa wa mamlaka kuu ya kudhidbiti matumizi ya dawa ilizopigwa marufuku , madamu tu alipwe mlungula wa pauni elfu kumi £10,000.
Meja Rotich ni meneja mkuu wa kikosi cha wanariadha wa Kenya.
Ilani ya mapema anasema ,itawapa wanariadha muda wa kusafisha chembechembe za dawa hizo kutoka mwilini mwao.

Meja Rotich anaripotiwa kukanusha kuwa hajafanya lolote baya, huku akiongeza kuwa alizungumza na maripota hao wa kujificha, ili kutaka kuwafahamu ni akina nani hasa na nini walichokuwa wakikitafuta.

Meneja wa Kenya aliyeitisha hongo afurushwa Rio
Ritaa Jeptoo mmoja kati ya zaidi ya wanariadha 40 wa Kenya waliopigwa marufuku


Gazeti hilo la Sunday Times na runinga ya Ujerumani ARD zilimrekodi afisa huyo bila yeye kujua kuwa alikuwa akirekodiwa.

Mkurugenzi wa shirika la kupambana na madawa ya kuongeza nguvu mwilini ADAK Japhter Rugut ameahidi kuchunguza madai hayo kikamilifu.
Madai hayo yanatokea siku mbili tu baada ya shirika la kupambana na madawa duniani WADA kuiondoa Kenya kwenye orodha ya mataifa ambayo yanakiuka kanuni za vita dhidi ya udanganyifu michezoni na utumizi wa madawa ya kusisimua misuli.

Kwa mujibu wa mwandishi mpekuzi Hajo Seppelt, Meja Rotich amekuwa akishirikiana na watu wanaoendesha mpango huo wa siri wa kutoa dawa za kusisimua misuli.

Meja huyo alikuwa miongoni mwa kikosi cha kenya kilichoshiriki katika guaride la ufunguzi wa michezo ya Olimpiki ijumaa iliyopita. 

CHANZO: BBC SWAHILI.

New Music: Chin Bees – Zuzu

Kwa siku kadhaa za hivi karibuni, msanii huyu amekua akisikika vilivyo kwenye ngoma mbali mbali akiwa ameshirikisha kama vile ngoma ya Sweet Mangi yake Nick wapili. Safarii hii jamaa kausimamia mzigo peke yake na ngoma inakwenda jina la Zuzu iliyotayarishwa na Young Keezy na Luffa katika studio za Switch Records. Bofya HAPA kuushusha wimbo huo.
 AU 
loading...

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...