14 October, 2016

Video: “How long” Davido Ft Tinashe

Mawere Mtokambali, Davido Tizama hapa Video mpya Kutoka kwa Davido alomshirikisha Tinashe . Enjoy the Video.Baada ya kutangaza kuachia video ya wimbo wake mpya wa “How long” aliomshirikisha Tinashe kutoka ijuma hii, hatimaye kichupa kimetoka..

Kocha wa Uingereza asema kikosi chake ni kibovu

Kocha wa muda wa timu ya taifa ya Uingereza, Gareth Southgate amesema alirithi kikosi kibovu baada ya kutoka sare ya bila kufungana na Slovenia katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia juzi. 
 Kocha wa Uingereza Gareth Southgate kushoto
Southgate alichukua mikoba ya Sam Allardyce mwezi uliopita kwa ajili ya kuisimamia timu hiyo katika mechi zake nne ambapo mpaka sasa ameshinda mchezo mmoja dhidi ya Malta kabla ya sare ya jana waliyopata. 

Uingereza ambao wanaongoza kundi F, walipata alama hiyo moja jana kufuatia juhudi za hali za juu zilizoonyeshwa na kipa wake Joe Hart. 

Southgate amesema wakati alipoichukua timu haikuwa sawa lakini taratibu anaona kama kikosi hicho kinaimarika.

Ligi kuu ya England inaendelea tena wikiendi hii kwa michezo saba kuchezwa

Leicester City
Mabingwa watetezi wa ligi hiyo Leicester City, watakua ugenini Stanford Bridge, kuwakabali wenyeji Chelsea.Washika bunduki wa London Arsenal wao watakua nyumbani katika dimba la Emirate kuwalika Swansea City.

Matajiri wa jiji la Manchester Man City, watawakaribisha Everton mchezo utakaopigwa katika dimba la Etihad, Fc Bournemouth wao watakipiga na Hull city.

Stoke City watakua nyumbani katika dimba la Britania kucheza na Paka Weusi wa Sunderland, West Bromwich Albion watapima ubavu na Tottenham.West HamWagonga nyundo wa London West Ham United watakua na kibarua pevu kwa kupepetana na Tai wa Crystal Palace.

13 October, 2016

Mbio Za Kilimanjaro Marathon 2017 Zazinduliwa Dar Es Salaam.....Kufanyika Februari 26, 2017

Mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2017 ambazo ni za 15 tangu Kuanzishwa kwake, zimezinduliwa rasmi  leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na wanahabari, wadhamini na Chama Cha Riadha Tanzania.

“Tumeona matunda ya udhamini huu kwa mfano mwaka huu tumeshuhudia mshiriki wa Kili Marathon akishiriki katika michezo ya Olimpiki kule Brazil na kumaliza katika nafasi ya tano katika mbio za kilomita 42. Tunaweza kuwapata akina Simbu wengi kutoka kili Marathon na ndicho hasa wadhamini wengi wanakitafuta,” alisema Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Group, Kushilla Thomas

Aidha Mkurugenzi huyo alisema  wadhamini wengine wa mashindano hayo ni Tigo ambao wanadhamini 21km, Gapco kwa 10 km-viti vya magurudumu na baiskeli ya kunyonga kwa mkono na Grand Malt-5km. Wadhamini wengine ni pamoja na KK Security, TPC Limited, FNB, Kibo Palace, Kilimanjaro Water, CMC Automobile,Keys Hotel, Air Rwanda na Anglo Gold Ashanti.
 
Aliishukuru pia  wizara yenye dhamana ya michezo kwa kuhakikisha miaka yote kwamba tukio hili linafanikiwa,pia amewapongeza waandaaji, Wild Frontiers, waratibu wa kitaifa-Executive Solutions, Chama cha Riadha Tanzania (RT), Kilimanjaro Marathon Club, Mkoa wa Kilimanjaro na Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) kwa kuwa wenyeji wa mashindano hayo.
 
Kwa upande wake, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli zawadi kwa 42km Kilimanjaro Premium Lager Marathon ni pamoja na – jumla ya Tsh milioni 20 kwa washindani wanaume na wanawake watakaoshika nafasi 10 za juu. Mshindi wa kwanza kutoka kila kundi atapata Tsh milioni 4 kila mmoja.

 “Hatuwezi kuwasahau wanariadha wote wa hapa nchini walioshiriki kwenye mashindano haya na kuipa fahari nchi yetu na kuwa watashinda zawadi zote hizi tunazozitoa. Tunaamini kwamba mashindano haya ya marathon pia yatafungua milango kwa wanariadha wetu kwa ajili ya kushiriki mashindano ya kimataifa ya marathon nje ya nchi yenye zawadi kubwa,” alisema Pamela Kikuli.

Janet Jackson,athibitisha ni mja mzito akiwa miaka 50

Mwana-Muzik Janet Jackson amethibitisha rasmi kwamba anatarajia kujifungua mtoto wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 50.

Ameliambia jarida la People: "Tunashukuru Mungu kwa baraka tuliyonayo", na akapigwa picha na tumbo lake linalozidi kuwa kubwa kudhihirisha uja uzito.
Fununu kuhusu uja uzito wake zilizuka Aprili alipojitokeza kuahirisha shughuli zake na tamasha la kimataifa 'Unbreakable' akisema anataka kupanga uzazi na mumewe Wissam al-Mana.

Ameonekana hivi karibuni London akinunua vitu katika duka la watoto.
Jarida la The People limenukuu duru iliyo karibu na familia ya Jackson aliyesema: "Ana furaha sana kuhusu uja uzito wake na anedelea vizuri sana. Ana raha kuhusu kila kitu."

Katika video iliowekwa kwenye Twitter mwezi April, amewaambia mashabiki wake kuwa ana ahirisha shughuli zake, kwasababu "kumekuwa na mabadiliko ya ghafla".Janet Jacket katika video ya Twitter
"Nilidhani ni muhimu mujue kwanza. Mimi na mumewangu tunapanga familia yetu," alisema, na kuongeza: "Tafadhali iwapo munaweza, jaribu muelewa kuwa ni muhimu nifanye hivi kwa sasa."
Aliendelea kusema: "Ni lazima nipumzike, ni agizo la daktari."

Janet Jackson ni nani:Janet Jackson (Mei 2010)
  • Janet Damita Jo Jackson alizaliwa Mei 16 1966 Gary, Indiana Marekani
  • Ni mdogo katika ndugu tisa na ni dadake muimbaji nyota Michael Jackson
  • Alitoa albamu yake ya kwanza Janet Jackson mnamo 1982
  • Ana albamu 11 ya hivi karibuni ikiwa ni Unbreakable, iliotolewa 2015
  • Ni mshindi mara 7 wa tuzo ya Grammy
  • Alianza taaluma yake kwa kushiriki katika kipindi cha televisheni The Jacksons mnamo 1976 na ameshiriki katika filamu kadhaa ikiwemo ya Tyler Perry 'Why Did I Get Married'
  • Muimbaji huyu ameolewa na mumewe wa tatu, Bilionea raia wa Qatari Wissam al-Mana, 2012.
Janet Jackson sio mwanamke maarufu wa kipekee kuzaa katika umri mkubwa.
Mshindi wa tuzo ya Oscar Halle Berry amezaa mtoto wake wa pili akiwa na miaka 47, miaka mitatu iliyopita.
Mkewe John Travolta, Kelly Preston amezaa mtoto wake wa tatu akiwa na miaka 48.

CHANZO:BBC

Rwanda yapiga marufuku simu za Galaxy Note 7

Serikali ya Rwanda imepiga marufuku uagizaji na usambazaji wa simu za kampuni ya Samsung aina ya Galaxy Note 7.

Hatua hiyo imechukuliwa siku chache baada ya kampuni hiyo ya Korea Kusini kutangaza kwamba ingesitisha uundaji na uuzaji wa simu hizo kutokana na kuongezeka kwa visa vya simu hizo kushika moto au kulipuka.

>>>>> Samsung yasitisha utengezaji wa simu za Galaxy Note 7

Mamlaka inayosimamia bidhaa na matumizi nchini Rwanda imesema hatua ya kupiga marufuku simu hizo imechukuliwa kwa sababu za kiusalama.

"Kwa sababu za kiusalama, wateja ambao huenda walinunua simu hizi binafsi nje ya nchi wanatakiwa kuzizima na kuzirejesha eneo walizozinunua," imesema taarifa ya kaimu mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo Meja Jenerali Patrick Nyirishema.

 Samsung pia imewashauri walio na simu hizo kuzizima na kutozitumia tena.

Liverpool v Man Utd: Uteuzi wa refa Anthony Taylor wakosolewa

Anthony Taylor
Mkuu wa zamani wa marefa Uingereza Keith Hackett amekosoa uteuzi wa refa kutoka Manchester Anthony Taylor kuwa mwamuzi wa mechi ya Ligi ya Premia kati ya Liverpool na Manchester United.

Taylor huishi maili sita kutoka Old Trafford, na Hackett anaamini huenda hilo likasababisha madai wa kupendelea upande mmoja.

"Hakuna anayetilia sana uadilifu wake," Hackett alisema.

"Lakini je, kitu kikienda mrama? Itakuwa vigumu kwa baadhi kuvumilia."
Taylor hana uhusiano wowote na United lakini hushabikia klabu ya Ligi ya Taifa ya Kaskazini ya Altrincham.

Hackett anasema inashangaza ikizingatiwa kwamba Mark Clattenburg angepatikana siku hiyo ya Jumatatu.

Badala yake Clattenburg, ambaye ni shabiki wa Newcastle United, ataudumu kama mwamuzi wa nne mechi nyingine wikendi.
Tayari mashabiki wa Liverpool wameanza kulalamika mitandao ya kijamii kuhusu uteuzi wa Taylor.

Uchaguzi Marekani 2016: Trump 'alipapasa wanawake kama pweza'Wanawake wawili wameambia gazeti la New York Times kwamba mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump aliwashika kimapenzi bila idhini yao.

Mwanamke mmoja amesema mgombea huyo alimshika matiti na kujaribu kuingia mkono wake chini ya sketi yake wakiwa kwenye ndege miongo mitatu iliyopita.

Wa pili anasema Bw Trump alimpiga busu bila yeye kutaka katika jumba la Trump Towers mwaka 2005.
Maafisa wa kampeni wa Trump wamesema "makala hii yote ni hadithi ya kubuni".

Gazeti la New York Times limeanzisha kampeni "ya uongo, na iliyoratibiwa kumharibia jina kabisa", taarifa ya maafisa wa Trump imesema.

Jessica Leeds, 74, kutoka Manhattan, ameambia gazeti hilo kwamba alikuwa ameketi karibu na Bw Trump sehemu ya abiria wa hadhi ya juu kwenye ndege wakielekea New York pale alipoinua sehemu ya kupumzishia mkono kitini na akaanza kumshika.

Mwanamke huyo alikuwa na umri wa miaka 38 wakati huo.
"Alikuwa kama pweza .... mikono yake ilinishika kila pahali," anasema. "Ulikuwa ni unyanyasaji."

Rachel Crooks alikuwa mpokezi wa wageni katika kampuni ya kuuza ardhi ya nyumba katika jumba la Trump Tower, wakati huo akiwa na miaka 22.
Anasema alipigwa busu la lazima na Bw Trump nje ya lifti ya jengo hilo.
"Ilikuwa vibaya sana," Bi Crooks ameambia New York Times.
"Niliudhika sana kwamba alidhani nilikuwa sina maana kiasi kwamba angefanya hivyo (bila hiari yangu)."

Wawili hao hata hivyo hawakuripoti visa hivyo kwa maafisa wa serikali.
Hata hivyo, wanasema waliwaambia marafiki na jamaa zao yaliyojiri.Trump Tower in Manhattan
Bi Leeds anasema alikasirika sana na alitatizika kimawazo baada ya Bw Trump kumgusa.

Anasema mara moja aliondoka eneo la abiria wa hadhi na kwenda kuketi eneo la abiria wa kawaida.Maafisa wa kampeni wa Clinton wamesema simulizi hizo za kuogofya kwenye New York Times zinatilia mkazo "kila kitu ambacho tunajua kuhusu jinsi Donald Trump huwachukulia wanawake".

Kumshika makalio'

Hayo yakijiri, Mindy McGillivray naye ameambia gazeti la Palm Beach Post kwamba akiwa na miaka 23 , Bw Trump alimshika makalio katika kilabu chake cha Mar-a-Lago club jimbo la Florida mwaka 2003.

Anasema alikuwa amesimama karibu na mchumba wake wa wakati huo Melania Knauss.

Bi McGillivray, ambaye kwa sasa ana miaka 36, anasema hakuripoti kisa hicho kwa polisi.

Lakini mwenzake, mpiga picha Ken Davidoff, aliambia gazeti hilo kwamba mwanamke huyo alimwita kando siku hiyo na kumwambia: "Donald amenishika makalio sasa hivi".

Maafisa wa Trump wanasema madai ya Bi McGillivray hayana ukweli wowote.
Wanawake wote watatu wamesema wanaunga mkono Bi Clinton.

Ijumaa wiki jana, video iliyopigwa mwaka 2005 ilitokea na kumuonyesha Bw Trump akinena maneno ya kuwadhalilisha wanawake na kuongea kuhusu kuwapapasa wanawake.

Aliomba radhi kuhusu matamshi hayo, lakini akasema yalikuwa mazungumzo ya mzaha faraghani.
Viongozi wengi wakuu wa Republican, akiwemo Spika Paul Ryan, wameshutumu matamshi hayo. Bw Ryan alisema hatamtetea tena Bw Trump.CHANZO: BBC

Picha: Nicki Minaj akava jarida la Marie Claire la mwezi Novemba

Rapper wa kike wa Marekani, Nicki Minaj amefanikiwa kukava jarida la Marie Claire la mwezi Novemba, mwaka huu.

Ndani ya jarida hilo mchezaji huyo amezungumzia vitu vingi ikiwemo kushindanishwa na rapper wa kiume, kufanya kolabo na Beyonce, na mengine.

“I don’t need to read a book about [business]. I can look at someone’s career and just pinpoint the dos and the don’ts, and the one person I’ve done that with for my entire career was Jay Z. He did such a great job being an authentic street guy and a businessman, and I was like, Why aren’t there women doing that, taking the success from rap and channeling it into their empire? I felt like anything he could do, I could do.”


14719071_1597745170529194_1503146289112547328_n

“Every time Bey and I do something together, I see how women are inspired, and it has nothing to do with how we look. It has to do with how we are owning who we are and telling other women you should be the boss of your own career and the brains behind your life or your decisions or your art. I just love that feeling.” 

Tazama picha zaidi hapa chini.
14716413_1828933283992686_2188140156316286976_n
14624365_893519087448818_3752921712912498688_n
14561746_222878581462421_6771207673779060736_n

12 October, 2016

Steve Bruce kuwa kocha mpya wa Aston Villa

Steve Bruce
Klabu ya soka ya Aston Villa ya England inatarajiwa kumtangaza Steve Bruce kuwa meneja mpya wa timu hiyo leo jumatano baada ya kumtimu kocha wake Roberto di Matteo.

Bruce mwenye umri wa miaka 55 alikua kocha wa Hull City, kabla ya kubwaga manyaga mwezi Julai mwaka huu.

Mmiliki na mwenyekiti wa Aston Villa, Dr Tony Xia, ameandika katika mtandao wa Twita, kuwa kocha huyo atatambulishwa na ni wakati wa kuwa pamoja na kuirejesha timu katika sehemu nzuri.

Villa wako katika nafasi ya 19 katika ligi daraja la kwanza (Champinship).Bruce amewahi kuvinoa vilabu vya Birmingham City, Wigan Athletic na Sunderland.

10 October, 2016

Mwanamuziki raia wa Rwanda aliye na hofu ya kurudi nyumbani

Corneille alipoteza familia yake yote mwaka 1994
Mwaka 1994 alikuwa na umri wa miaka 17 akiishi nchini Rwanda kwenye familia moja tajiri na ndoto yake ilikuwa ni ya kuwa muimbaji maarufu.

Lakini maisha ya Corneille Nyungura yalichukua mkondo mwingine kwa ghafla wakati yalitokea mauaji ya kimbari ya mwaka mwaka 1994 wakati takriban watu 800,000 wa kabila la watusi na wahutu wachache wenye msimamo wa wastani waliuawa.

Wakati kundi la wauaji lilipowasili nyumbani kwao, Corneille alijificha nyuma ya sofa wakati familia yake yote ilichinjwa.Takriban watu 800,000 waliuawa nchini Rwanda mwaka 1994
Sasa yeye ni raia wa Canada na mmoja wa wanamuziki bora zaidi wa RnB kutoka nchini Rwanda na amekuwa akiimba kwa miaka 20 iliyopita
Akijaribu kukubaliana kile kilichotokea nchini mwake mwaka 1994, Corneille anasema kuwa na uoga wa kurudi nyumbani kwao.

Music: Matonya – Sugua Benchi (Download)


Baada ya kimya cha muda mrefu msanii Matonya ameamua kurudi kwa nguvu zote baada ya kuachia Audio na Video za ngoma hii yakwake mpya inayoitwa “Sugua Benchi”.

Exclusive |Download Kosa Sina - Linah

Ngoma mpya kutoka kwa mwanadada huyu mwenye Sauti yake almaarufu kama Ndege Mnana Linah Sanga. Wimbo huu una jina la Kosa Sina. Bofya Kitufe Cha DOWNLOAD hapo chini kuupakua wimbo huo..
PAKUA NYIMBO MKITO JALI WASANII WETU.

50 Cent kuachia Mix-tape yake mpya Hivi karibuni.

Mashabiki wa 50 Cent wamekua wakiuliza maswali mengii ambayo yanatokana na Kimya cha huyu jamaa katika social media tofauti tofauti. Kuna kila dalili kwamba Mashabiki wa 50 watapata kitu roho inapenda hivi karibuni maana DJ Whoo Kid yupo studio akifanya mixing ya ngoma za Mixtape ya nne ya 50 Cent.

Mix-tape hii itahusisha ngoma zote za 50 ambazo bado hazijatoka kama vile Young Buck, Lloyd Banks, Tony Yayo na Kidd Kidd.

Matokeo ya Barani Afrika kufuzu kombe la dunia

Barani Afrika kumepigwa michezo minne ya kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la dunia zitazofanyika nchini Urusi Mwaka 2018.Nigeria
Nigeria Super Eagle wakicheza ugenini wamewatambia wenyeji wao Zambia chipolopolo kwa kuiwachapa kwa mabao 2-1. 

Mabao ya Nigeria yakifungwa na Alex Iwobi na Kelechi Iheanacho, goli la Zambia likifungwa na Collins Mbesuma

Algeria wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani wametoshana nguvu na Cameroon kwa kufungana bao 1-1.

Mafarao Misri wamewatambia Congo kwa kuwachapa kwa mabo 2-1 huku Tunisia nao wakishinda nyumbani kwa mabao 2 - 0 dhidi ya Guinea.

Samsung yasitisha utengezaji wa simu za Galaxy Note 7

Kampuni ya Samsung imesitisha utengenezaji wa simu za Galaxy Note 7 baada ya hofu kuendelea kuwepo kuwa hata zile simu za mara ya pili zilizodaiwa kurekebishwa zinaweza kulipuka.

Mtu anayefahamu uamuzi huo kwa ukaribu, amethibitisha kupitia CNN usitishwaji wa muda wa simu hizo baada ya shirika la habari la Korea Kusini, Yonhap kuripoti kwanza kuhusiana na taarifa hizo.

Tangazo hilo limekuja baada ya makampuni ya Marekani na Australia kusema yataacha kufidia simu hizo kwa walionunua mwanzo kutokana na wasiwasi kuwa simu hizo nazo ni vimeo kama za awali.

Mapema baada ya Galaxy Note 7 kuingia sokoni mwezi August, baadhi ya watumiaji walidai kuwa simu zao zilikuwa zikishika moto. Kampuni hiyo ililazimika kuziondoa sokoni simu zote kwa kudai zina tatizo la betri linalopeleka zichemke na hivyo kuwaka moto.

Simu mbadala zilikuwa zimalize tatizo hilo na tayari baadhi ya watumiaji walipewa zingine. Lakini baadhi ya wateja bado wamekuwa wakiripoti kuwepo kwa tatizo hilo hatari kwenye simu zao mpya.

CHANZO:BONGO5

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...