Stonebwoy msanii wa Ghana aliebuka mshindi wa Best International Act: Africa kwenye tuzo za BET Awards 2015 alichukua time na kufanya interview na Live Fm jijini Accra kutoa shukurani zake kwa watu waliompigia kura na pia kuongelea suala ya Fuse ODG kutokushiriki kwenye tuzo hizo siku ya
Jumapili.
>>> “kuna
mapungufu kila kona na hakuna mtayarishaji wa tuzo anayepatia kila kitu
kwa asilimia mia. So ilikua ni suala la kuangalia kama binafsi
ungependa kwenda kwenye tuzo au la. Wewe kama msanii uliyechaguliwa una
sababu ambazo haziwezi kupingwa na mtu yoyote za kuamua kama utaweza
kuja kweye tuzo husika ama kupotezea”.
>>> “Mimi
nilienda kwa sababu nilikua na sababu zangu za msingi za kuenda na
naamini hata yeye alikua na sababu zake za msingi za kwa nini hakutokea
siku ile. Licha ya hayo, kuchaguliwa hakumanishi kuwa utapokea tuzo, na
hiyo haimanishi sisi wasanii hatu ujui mchango wetu kama wasanii”. <<< Stonebwoy.
Stonebwoy anajulikana kwa wimbo wake wa Baafira ambao ndani yake ameshirikisha Sardokie kutoka Nigeria. Nimekusogezea wimbo huo hapa chini unaweza kuusikiliza hapa mtu wangu.
No comments:
Post a Comment