Wiki moja baada ya ofa ya kwanza ya Manchester United kumsajili Sergio
Ramos kukataliwa na Real Madrid, hatimaye mchezaji huyo ambaye yupo
mapumzikoni ametoa kauli yake United walituma ofa ya kwanza ya paundi millioni 28.3 kwa Madrid ili
kupata saini ya beki huyo wa kimataifa wa Spain, lakini Madrid waliikata
ofa hiyo.
Hata hivyo baada ya Ramos kugundua Madrid wameikataa ofa hiyo,
alichukua uamuzi wa kuwaweka wazi viongozi wa Madrid kupitia wakala wake
kwamba – Anataka kuondoka na kujiunga na United na kuiomba Madrid
ikubaliane bei na Manchester United. Uamuzi huo wa Ramos umeishtua Madrid, ambao walitegemea wangefanya makubaliano ya mkataba mpya na beki huyo. Madrid wanategemewa kujaribu kumtuliza Ramos na mkataba mnono mpya
lakini kaka na meneja wa mchezaji huyo – Rene Ramos ameshaifahamisha
Madrid lengo la mteja wake kutaka kuanza maisha mpya sehemu nyingine.
Rene ameripotiwa kusema kwamba Ramos anataka kuhamia Old Trafford
wakati huu wa dirisha la usajili na klabu pekee ambayo anataka Madrid
ifanye nayo makubaliano ni United.
Usisumbuke Mawerenewz.blogspot.com ndio mtandao wako wakipekee unaokupa habari za BURUDANI,MICHEZO, SIASA, na HABARI MBALIMBALI ZA KIMATAIFA pamoja na KITAIFA Endelea kutembelea MTOKA MBALI pia nifuate twitter>>>@mawere3, facebook>>>Mawere Mtoka Mbali, Instagram>>>mawere_mtoka_mbali,
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment