19 December, 2015

Lubanga na Katanga wahamishiwa DR Congo

Katanga
Viongozi wa zamani wa waasi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Thomas Lubanga na Germain Katanga wamepelekwa DR Congo wakakamilishie vifungo vyao huko.
Wawili hao walifungwa jela na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) baada ya kupatikana na makosa ya uhalifu wa kivita.
Hii ni mara ya kwanza kwa ICC kuwatuma wafungwa nje wakatumikie vifungo vyao.
Afisi ya Rais wa mahakama ya ICC ilitangaza DR Congo kuwa taifa litakalotumiwa kutekeleza vifungo vya wawili hao Desemba 8.Lubanga
Afisi hiyo ilisema Thomas Lubanga Dyilo na Germain Katanga wenyewe walikuwa wameeleza mapenzi ya kwenda kutumikia vifungo vyao taifa lao la kuzaliwa.
Mahakama ya ICC itaendelea kufuatilia kufungwa kwao kuhakikisha wanawekwa katika “mazingira yafaayo kimataifa ya kuwazuilia wafungwa”.
Wawili hao wamehamishiwa DR Congo kupitia ushirikiano wa karibu kati ya maafisa wa DR Congo, Uholanzi na Ufaransa.
Lubanga alihukumiwa kifungo cha miaka 14 jela tarehe 10 Julai, 2012 baada ya kupatikana na makosa ya kuwaandikisha watoto kwenye jeshi na kuwatumia vitani.
Mahakama ya rufaa ilidumisha hukumu hiyo Desemba 2014. Lubanga amekuwa kizuizini The Hague tangu 16 Machi 2006 na ukizingatia muda aliokaa kizuizini kabla ya kuhukumiwa, basi huenda akaachiliwa huru kabla ya 2020.
Katanga alihukumiwa kifungo cha miaka 12 jela kwa maoksa ya kushiriki kosa la uhalifu dhidi ya binadamu na makosa manne ya uhalifu wa kivita ya kuua, kushambulia raia na kuharibu mali kijiji cha Bogoro, Ituri mashariki mwa Dr Congo.
Anatarajiwa kukamilisha kifungo chake tarehe 18 Januari 2016.

For the Stylish Grown Men

 

As we get near to Christmas and New Year...and the Holiday Season has kicked in...let me gift you my Male Readers with a lil' something from the amazing Samuel L. Jackson. Stylish by his own right,quite good looking and one hell of an actor


 The trend of rocking that jamper with a good pair of jeans is still a hot trend that will get into 2016...don't forget to accessorize the look with a watch or bracelet
 As a stylish man,do not be afraid to rock polka dots, prints and other patterns that brighten you up...
 For my readers from cold areas,this is an ideal Christmas look to keep you warm while containing your cool. And if you are at the hot Da'Slam as I am...then you can replace the heavy coat with a shear long shirt with great jeans as well
At the end, keep your style regardless of the trends.

Check out the new movie "The Hateful Eight" in which Samuel L. Jackson shows off his great acting experience

RATIBA YOTE YA EPL IKO HIVI

Chelsea vs Sunderland
Leo timu ya Chelsea inaingia uwanjani kukipiga dhidi ya Sunderland kwenye mchezo wa ligi kuu England ikiwa ni mchezo wa kwanza baada ya kocha Jose Mourinho kutimuliwa kwenye kikosi hicho.
Kwenye mabano ni muda halisi (kwa saa za Afrika Mashariki) ambao mechi zitaanza kuchezwa.
Chelsea vs Sunderland (saa 18:00)
Everton vs Leicester (saa 18:00)
Man Utd vs Norwich (saa 18:00)
Southampton vs Tottenham (saa 18:00)
Stoke vs Crystal Palace saa (18:00)
West Brom vs Bournemouth (saa 18:00)
Newcastle vs Aston Villa (saa 20:30)

BAADA YA KUFUKUZWA MOURINHO, VAN GAAL AHOFIA KIBARUA CHAKE

Van Gaal +Mourinho
Baada ya kocha Jose Mourinho kutupiwa virago na klabu ya Chelsea, presha ni kubwa kwa kocha wa Manchester United Louis Van Gaal ambaye anasema anahofia kibarua chake na kwamba hajui kwamba inaweza kuwa ni zamu yake kuondoka kama hatopata matokeo haraka.
Van Gaal ambaye amesikitishwa kufukuzwa kazi kwa kocha wake huyo msaidizi wa zamani wakiwa wote Barcelona, na kusema hawezi kudadisi zaidi chanzo cha kufukuzwa kocha huyo aliyemzungumzia kuwa bora zaidi wa kizazi chake na mwenye rekodi ya kipekee.
Kocha huyo amesema anahofia kumalizia career yake ya ukocha kwa kufukuzwa na kwamba anahitaji kupata matokeo kuepusha hilo mara baada ya kuenda mechi tano bila ushindi huku wakifungwa na Vfl Wolfsburg na Bournemouth mfululizo.
Tayari wachambuzi wa soka duniani wanaona ni wakati Manchester United inatakiwa kuachana na Louis Van Gaal na badala yake kumnasa kocha Pep Guadiola ambaye anamaliza muda wake Bayern Munich ama Jose Mourinho ambaye ni chaguo la mashabiki, huku ikielezwa pia kuwa bado Van Gaal anapata sapoti kubwa kutoka katika bodi ya klabu hiyo.
Wakati huo huo, kocha Manuel Pellegrine wa Manchester City akizungumzia sakata hilo amesema kuwa yeye binafsi hawezi mkumbuka Jose Mourinho lakini akakiri kuwa ni pengo kubwa katika ligi kuu England kutokana na uwezo wa mreno huyo. Pellegrine akiendelea zaidi amesema katu hana presha yeyote ile pamoja na mazungumzo yanayoendelea hivi sasa ya kumuhusu Gadiola kurithi mikoba yake msimu ujao.

RATIBA YA MECHI ZOTE ZA VPL JUMAMOSI DECEMBER 19

VPL-Tanzania
Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara inaendelea tena leo kwa michezo sita kupigwa kwenye viwanja vya miji sita tofauti ikishuhudia timu 12 zikishuka uwanjani kusaka pointi tatu muhi kwa ajili ya kujiimarisha kwenye msimamo wa ligi hiyo ambayo imeanza kushika kasi tena baada ya kusimama kwa muda.
Hii hapa ni ratiba kamili ya michezo yote itakayopigwa December 19, 2015 kwenye viwanja sita vya mikoa tofauti;
Yanga vs Stand United (Uwanja wa Taifa-Dar es Salaam) 
Mwadui FC vs Ndanda FC (Mwadui Complex-Shinyanga) 
Kagera Sugar vs African Sports (Ali Hassan Mwinyi-Tabora)
Tanzania Prisons vs Mtibwa Sugar (Sokoine Stadium-Mbeya)
Toto Africans vs Simba SC (CCM Kirumba-Mwanza)
Majimaji FC vs Azam FC (Majimaji Stadium-Ruvuma)
Azam TV ndiyo sehemu pekee ya kushuhudia ligi kuu Tanzania bara live. Jiunge na Azam TV ushuhudie mastaa wa VPL, magoli pamoja na uchambuzi wa kina.

Miaka 9 ya Wayne Rooney na Man United

Nahodha wa Manchester United Wayne Rooney leo anatarajia kutimiza mechi yake ya 500 tangu alipoanza kuitumikia klabu hiyo mnamo 2004.
 
Rooney anatarajiwa kurejea dimbani leo baada ya majeruhi ya enka yaliyomuweka nje katika mechi 3 dhidi ya  West Ham, Wolfsburg na Bournemouth.
Rooney alijiunga na  United kutoka Everton mwaka 2004 kwa ada ya uhamisho ya £25.6m akiwa na miaka 18 na katika mechi yake ya kwanza tu alifunga hat trick yake ya kwanza katika ushindi wa 6-2 vs Fenerbahce.
 
Mshambuliaji huyo mpaka sasa ameshashinda makombe matano ya EPL na moja la Champions League, na tuzo kadhaa zake binafsi.

Wayne Rooney ameshacheza mechi 499 akiwa na jezi za mashetani wekundu, akishika nafasi ya 10 katika listi ya wachezaji waliocheza mechi nyingi zaidi katika historia ya klabu hiyo.


Mpaka kufikia sasa Rooney ameshafunga jumla ya magoli 237 katika mechi 499, katika magoli hayo – amefunga hat trick mara 8.
 Klabu ya Aston Villa ndio timu ambayo Rooney ameifunga magoli mengi zaidi tangu alipoanza kuitumikia United. 
Wayne Rooney amefunga magoli 11 katika mechi 24 vs Manchester City. Idadi hii inamfanya kuwa mchezaji aliyefunga magoli mengi zaidi kwenye Manchester Derby – Baba Kai pia ana rekodi ya kutoa assists 82 katika premier league tu.

Hii Video mpya ya French Montana Ft Puff Daddy ‘First Time’, itazame hapa.

092013-shows-hha-2013-french-montana-press.jpgRapa French Montana amekutana na Puff Daddy na kukamilisha video ya wimbo wake “First Time”. Montana anajitayarisha kutoa album mpya mwakani Mac & Cheese 4 ikiwa na wasanii kama Kanye West, Miguel, Big Sean, na Travis Scott.

Video: Ben Pol Ft. Avril & Rossie M - 'Ningefanyaje'.

post-feature-imageBen Pol amerejea tena na kichupa cha Ningefanyaje alicho shirikiana na Avril mwanamuziki kutoka Kenya pamoja na Rossie M.

Video: Chege Ft. Runtown & Uhuru - 'Sweety sweety'

post-feature-image
Watch and share , brand new music video "Sweety sweety" by Tanzania bongo flava artist Chege Featuring artist from Nigeria Runtown and Uhuru from South Africa xelimpilo.
Directed by Justin Campos | Produced by Dj Maphorisa.

Soulja Boy ataka kuwa na muonekano mpya kimaisha

Rapper wa marekan Soulja Boy sasa anatazama kumairisha maisha yake na kuwa na muonekano mpya;
rapper huyo anatoa tatoo zote usoni mwake na kuacha uso wake wazi. Kwenye instagram page yake kaandika haya
“Recently I’ve been going through this process to get my tattoos removed, wanted to share the actual procedure. I appreciate all my friends, fans, and family. We have to strive to be a better person everyday.”

17 December, 2015

Arsenal itachukua ubingwa EPL na Leicester itacheza UEFA msimu ujao

covvvv
Leicester ni club ambayo inafanya vizuri hivi sasa kwenye EPL ambapo imekua tishio kwa club kubwa kwenye mechi zao mbalimbali. Kama sio kutoka suluhu basi lazima washinde mechi dhidi yao.
Arsenal itachukua ubingwa EPL na Leicester itacheza UEFA msimu ujao ni ripoti kutoka ECI ambacho ni kirefu chake ni Euro Club Index. Hawa jamaa wametoa listi yao ambayo imetoa matokeo jinsi ligi ya EPL itakavyoisha.
Matokeo hayo yanaonyesha kwamba Arsenal ndio itakua bingwa kwa msimu huu ikifuatiwa na Manchester City, Manchester United then Leicester City. Chelsea itamaliza kwenye nafasi ya 9 na Sunderland, Aston Villa na Norwich zitashuka daraja.
Concept ya ECI ili kupata matokeo haya ni kwamba wanatumia mechi za zamani za club hizo, performance ya wachezaji kwenye timu za taifa, mechi zao za sasa kwenye ligi na nyinginezo.
Mahesabu yao yanaendelea kuwa complicated sana hadi kufanya mahesabu ya mechi walizoshinda, walizofungwa hadi kwenye draw. Baada ya hapo wanachanganya na kupata matokeo kwa formula zao na ndio wakapata hii listi.
Mwisho wa siku mpira hauamuliwi kwa kutumia mahesabu ya kwenye karatasi bali kila kitu ni uwanjani. Huu hapa ni msimamo wa ligi jinsi ligi itakavyoisha kwa msimu huu
2F6CDF4700000578-3362345-image-m-47_1450276423863

Guardiola Akiondoka Bayern: Je atakwenda Etihad, Old Trafford au Darajani?

Kocha huyo mwenye sifa kubwa miongoni mwa makocha bora duniani ameiambia Bayern Munich kwamba hana mpango wa kuongeza mkataba wake mwishoni mwa msimu.
Vilabu tofauti ulimwenguni ikiwemo Barcelona, ambapo kocha hugo alishinda mara mbili  Champions League pamoja na makombe matatu ya La Liga, wapinzani wao Real Madrid nao pia wanaonekana kuvutiwa baada ya kuonekana wana nia ya kuachana na Rafa Benitiez.
  Lakini inaonekana hatma ya Kocha huyo itaamuliwa na vilabu vya England, Chelsea, Manchester United na Manchester City wote wanaonekana kumtaka kocha huyo mwenye rekodi nzuri ya makombe.
Arsenal pia inaweza kuhusika ikiwa Guardiola ataamua kupumzika mpaka mkataba wa Wenger utakapomalizika mwishoni mwa msimu ujao.
Guardiola alitoboa siri kwenye kitabu chake   “Pep Confidential” kwamba, baada ya kuondoka Barcelona na kabla hajaamua kujiunga na Bayern, alikuwa na nafasi ya kujiunga na City na Chelsea.
Manchester United pia walidhaniwa kwamba walikuwa wanamtaka Guardiola kabla ya kumuajiri  Louis Van Gaal.
Sasa inaonekana  United wanaweza kuachana LvG, na wanapewa nafasi ya kumtwaa Guardiola ambaye anatajwa kuvutiwa na utamaduni wa United hasa katika matumizi ya kutumia academy yao.
Kadri siku zinavyoenda ndivyo inavyoonekana ngumu kwa Van Gaal kuweza kumaliza misimu yake mitatu ya mkataba wake – mashabiki na inaripotiwa baadhi ya wachezaji wameanza kumpinga.
  Guardiola pia amekuwa akihusishwa kwa muda na kuhamia Etihad, wengi wakitoa sababu ya uhusiano wake na CEO wa City Ferran Soriano na mkurugenzi wa soka Txiki Begiristain ambao walifanya nae kazi Barcelona.
Lakini baadhi ya vyombo vya habari Uingereza vinaeleza kwamba Guardiola ataichagua United mbele City ikitokea United wakionyesha nia ya dhati ya kumhitaji.
Carlo Ancelotti anatajwa kwamba ndio mrithi wa Guardiola ndani ya Allianz Arena

MH. ZITTO AFUNGUKA KUHUSU PROF. SOSPETER MUHONGO!

http://habarikwanza.com/wp-content/uploads/2015/12/zitto-663x445.jpg
Mbunge wa Kigoma Mjini Mh. Zitto Kabwe amefunguka na kuandika ujumbe mrefu unao muhusu Prof. Sospeter Muhongo kwenye ukurasa wake wa Facebook, kama ifuatavyo:
“Prof. Sospeter Muhongo alikuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati wa sakata la ‪#‎TegetaEscrow‬. Kamati ya Bunge ilipendekeza na Bunge kuazimia kuwa Muhongo avuliwe madaraka yake ya Uwaziri. Prof. Muhongo alijiuzulu. Akafanyiwa uchunguzi na Kamishna wa Maadili kutamka kuwa hakukutwa na kosa la kimaadili. Unajengaje hoja kuwa hana haki ya kuteuliwa kuwa Waziri? Keshaadhibiwa kwa kosa la awali, kwa kujiuzulu. Sheria ipi inasema hana haki ya kuteuliwa tena?
Niliongoza Kamati ya PAC.
Nina uhakika Waziri muhongo kwenye sakata lile alishauriwa vibaya na kujikuta anatetea ubadhirifu. Lile nifunzo kubwa kwake na ninavyomuona sasa hatarudia tena makosa yale. Kuna mambo ya msingi lazima afanye sasa
1) Azuie kuanzia sasa malipo ya ‘capacity charges’ kwa kampuni ya kitapeli ya IPTL na atumie sheria kutwaa mitambo ya IPTL na kumilikisha TANESCO
2) Amtake Waziri wa Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi kumkamata mara moja anayejiita mmiliki wa IPTL na afunguliwe mashtaka ya utapeli, wizi wa udanganyifu na uhujumu uchumi; huyo mmiliki na washirika wake ambao ni raia wa Tanzania
3) Amtake Gavana wa Benki Kuu na FIU kuichukulia hatua za kisheria Benki ya Stanbic ikiwemo kupiga faini ya kurejesha fedha zote zilizokua kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.
Hizo ndio hoja za msingi na sio uteuzi wa Prof. Muhongo. Mwenye ushahidi dhidi ya Muhongo si aende Mahakamani? Tuache siasa za porojo porojo”

BEI YA MENO YA TEMBO YASHUKA NCHINI CHINA

http://habarikwanza.com/wp-content/uploads/2015/12/YAO-MING.jpg
Pamoja na kupanda kwa bei za pembe za ndovu kuanzia mwaka 2010 kufikia mwaka 2014, thamani ya meno ya tembo imeshuka kwa kiasi kubwa nchini China jambo ambalo ni habari njema kwa Tanzania katika harakati zake kukomesha ujangili wa pembe za ndovu. 
Taarifa mpya ya utafiti uliofanywa na watafiti Esmond Martin na Lucy Vigne wa shirika la Save the Elephants na kutolewa wiki hii imeainisha kwamba bei za meno ya tembo ghafi nchini China zimeshuka kwa zaidi ya nusu katika kipindi cha miezi 18 iliyopita kutoka dola za Marekani 2,100 kwa kilo moja hadi kufikia dola 1,100. Katika utafiti wao uliofanya katika majiji nane nchini, watafiti hao wamegundua kwamba mahitaji ya meno ya tembo na bidhaa zitokanazo na pembe za ndovu yanaendelea kushuka kwa kasi kubwa kuliko ilivyowahi kutokea. 
Viwanda vinavyotengeneza bidhaa mbalimbali zitokanazo na pembe za ndovu vimeripoti kuwepo na uhaba wa pembe za ndovu na vibali vinavyotolewa na serikali kuwaruhusu wafanyabiashara kuuza pembe za ndovu kihalali vimecheleweshwa. Matokeo ya utafiti huu mpya yanaenda sanjari na ongezeko kubwa la uelewa wa watu nchini China ambapo sasa sehemu kubwa ya jamii inaelewa madhara ya tatizo la ujangili kwa tembo wa Afrika na uelewa huu umeongezeka maradufu kati ya mwaka 2012 na 2014 kwa mujibu wa taarifa ya Wildaid, Save the Elephants na African Wildlife Foundation. 
 ‘Wakati hali hii ikijitokeza, serikali ya China imepiga hatua kubwa katika kudhibiti soko la pembe za ndovu tangu mwezi Septemba ambapo Rais wa nchi hiyo Xi Jinping alitangaza kwamba China na Marekani zitashirikiana kukomesha biashara ya pembe za ndovu. Akizungumza kuhusu utafiti huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Wildaid, Peter Knights amesema: 
“Kuanguka kwa bei ya pembe za ndovu nchini China ni habari nzuri tuliyotaka kusikia japo bado kuna kazi kubwa hii ni hatua muhimu sana katika kukomesha janga la ujangili. Kupigwa marufuku biashara hii nchini China na Marekani vitatoa shinikizo kwa Hong Kong, Thailand na Japan nazo kupiga marufuku biashara hii. Pia hii itazipa moyo nchi za Kenya na Tanzania kuendelea kupambana na ujangili.” 
Tangu mwaka 2012, mashirika ya WildAid, Save the Elephants na African Wildlife Foundation yaliungana kufanya kazi ya uhamasishaji juu ya ujangili nchini China kwa kuwatumia watu maarufu nchini humo kama Yao Ming mcheza mpira wa kikapu NBA zamani na muigizaji Li Bingbing ambao kupitia matangazo mbalimbali wamekuwa wakihamasisha jamii kuacha kununua, kugawa au kupokea pembe za ndovu kama zawadi. Mashirika makubwa ya habari nchini China ya CCTV na Xinhua nayo yametoa msaada mkubwa katika jitihada hizi kwa kutoa matangazo yenye thamani ya dola za Marekani milioni 42 bure ambapo matangazo hayo yamewafikia mamilioni ya wananchi wa China. 
Vilevile jitihada hizi pia zimesaidiwa na Mwanamfalme wa Uingereza Prince William ambaye alitoa hotuba ya kihistoria mwezi Oktoba na kuwaomba wananchi wa China kukataa kabisa biashara ya pembe za ndovu. Akizungumza kuhusu anguko hilo la bei ya meno ya tembo Balozi wa WildAid Jacqueline Mengi amesema:
“Upunguaji wa mahitaji ya pembe za ndovu huko nchini China ni ishara kwamba jitihada za Wildaid pamoja na serikali za nchi tofauti zinaendelea kuzaa matunda. Mwaka jana tulizindua kampeni maalum ya kuongeza ufahamu na kuielimisha jamii kuhusu tatizo la ujangili linaloikabili Tanzania. Kwa matokeo ya utafiti huu ni dhahiri kwamba mwamko wa kulinda tembo wetu umeongezeka.”
 Mashirika ya WildAid, African Wildlife Foundation na Save the Elephants yamekuwa yakiipa shinikizo kubwa Hong Kong nchi inayodaiwa kuwa kituo kikubwa cha biashara hiyo duniani. Baada ya mashirika hayo hivi karibuni kutoa filamu iliyochukuliwa kwa siri ikionyesha jinsi ambavyo Hong Kong imeshindwa kudhibiti biashara hiyo haramu, maafisa wa serikali hiyo wameonyesha dalili za kuwa tayari kukomesha biashara hiyo jambo ambalo linaungwa mkono na Baraza a Sheria la Hong Kong.

Ripoti mpya ya UNICEF yashtua


Zaidi ya watoto milioni 16 duniani, wamezaliwa katika mazingira ya kivita katika kipindi cha mwaka mmoja pekee.
Ripoti mpya ya shirika la Umoja wa mataifa linaloshugulikia maswala ya watoto UNICEF imesema kila baada ya sekunde mbili mtoto mmoja huzaliwa katikati ya mizozo ya kivita.
Ripoti hiyo inasema pia katika maeneo hayo hakuna huduma za afya.
Idadi ya watu wasio na makao imeongezeka maradufu tangu vita vya pili vya dunia.

Magufuli amfuta mkuu wa kupambana na rushwa

Magufuli
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Dkt Edward Hoseah, na pia akawasimamisha kazi maafisa wa nne wa taasisi hiyo.
Rais Magufuli amesema hajaridhishwa "na namna taasisi hiyo ilivyokua ikitekeleza wajibu wake katika kukabiliana na rushwa hususani kwenye upotevu wa mapato ya serikali katika bandari ya Dar es salaam.”
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema Dkt Magufuli amemteua aliyekuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru Bw Valentino Mlowola kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru.
Kwa mujibu wa Bw Sefue, Dkt Magufuli amechukua hatua hiyo baada ya kujiridhisha kuwa "utendaji kazi wa Takururu chini ya Dkt Edward Hoseah hauwezi kuendana na kazi anayoitaka”.
Rais Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa watumishi waandamizi wanne wa Takururu ambao walisafiri nje ya nchi licha ya Rais Magufuli kupiga marufuku safari za nje kwa watumishi wa umma.
Watumishi hao ni Mary Mosha, Ekwabi Mujungu, Doreen Kapwani na Rukia Nikitas ambao walisafiri nje ya nchi licha ya kunyimwa kibali cha safari kutoka kwa Rais ama Katibu Mkuu Kiongozi.
Bw Sefue amesema atakayekiuka agizo la rais "atachukuliwa hatua kali”.
Hii si mara ya kwanza kwa Dkt Magufuli kuwachukulia hatua maafisa wa Serikali tangu achukue madaraka mwezi uliopita. Siku chache baada ya kuingia afisini, a libadilisha usimamizi wa hospitali ya taifa ya Muhimbili baada ya kufanya ziara ya kushtukiza huko na kutoridhishwa na utoaji huduma.
Majuzi alivunja bodi inayosimamia bandari.

Millen Magese kuonekana kwenye video mpya ya Diamond na Mafikizolo?


Mwanamitindo mkubwa wa Tanzania, Millen Magese ataonekana kwenye video mpya ya Diamond Platnumz na Mafikizolo.
Millen
Millen anaweza akawa mmoja ya watu wataoonekana kwenye video hiyo, kupitia Instagram muimbaji wa kundi la Mafikizolo, Nhlanhla Nciza ameweka picha akiwa na mrembo huyo wakati wa kushoot video
“On set for the Mafikizolo @diamondplatnumz @djmaphorisa music video shoot, surrounded by my beautiful honeys Tanzania’s international supermodel @ladivamillen @blackbarbiellish and makeup boss @nthatomashishi East meets south #OneContinentOneLove #EpicnessAllAround”
Millen salam
Video ya wimbo huo unaoitwa ‘Colours of Africa’ imekamilika  na imeshootiwa Afrika kusini.

Mtandao mkubwa wa Marekani waisifia Cover ya Hello iliyoimbwa kwa kiswahili, wasema ni bora kuliko original

Zimetoka Cover nyingi za wimbo wa Adele ‘Hello’ lakini hii iliyoimbwa na msanii wa Kenya, Dela Maranga kwa lugha ya Kiswahili inaweza kuwa bora zaidi.
Mtandao wa Perez Hilton umesema Cover ya wimbo wa Adele ‘Hello’ iliyoimba kwa kiswahili ni bora kuliko Original iliyoimbwa na Adele mwenyewe. “Dela Maranga is a singer from Nairobi, Kenya, and her Swahili version of the 25classic may actually be better than the original. Her voice is powerful like Adele’s, but she also has this soulful tone that makes the lyrics even more painful — in the best way possible.” Wameandika kwenye mtandao huo Isikilize hapa

Nicki Minaj aiomba mahakama isimpeleke Meek Mill jela tena,ajitolea kumnyosha.

minajNicki Minaj ametoa ushahidi juu ya maisha ya Meek Mill na kwanini jaji hatakiwi kumpa athabu kubwa ya kurudi jela kwa kosa la kuvunja masharti ya mahakama.
Nicki Minaj amesema ” mimi ndio ntakaye kuwa na lala mwenyewe akienda jela,najua Meek Mill is Not Perfect ila huta amini jinsi alivyobadilika sasa”
Nicki Minaj ameomba mahakama impe nafasi ya kumsaidia Meek Mill kufata masharti ya mahakama. Wakili wa Meek Mill amesema biashara ya muziki ina mpa msongo wa mawazo msanii huyu.

AY Ft Diamond Platnumz kwenye remix ya 'Zigo'

post-feature-imageSiku hizi watu wanafanya mambo kimya kimya! Inaonekana kuwa AY amemjumuisha Diamond Platnumz kwenye remix ya hit single yake, Zigo na tayari wanafanya video nchini Afrika Kusini.

AY na Diamond hawajasema kitu. Lakini kampuni inayotengeneza video yake imeumwaga ubuyu kwenye Instagram. Kampuni hiyo iitwayo Studio Space Pictures ya Afrika Kusini, imeweka picha hiyo juu ya wakali hao na kuandika: Earlier today with @aytanzania @ @diamondplatnumz #ZigoRemix #studiospacepictures.”

Haijulikani kama ni Diamond pekee ndiye aliyemo kwenye remix hiyo lakini kuna uwezekano mkubwa wasanii wengine wakali kuipandia beat hiyo ya Nahreel.

Hii si mara ya kwanza Diamond na AY kukutana kwenye kazi ya pamoja. Diamond amewahi kuweka ladha kwenye wimbo wa AY ‘Asante.’

CV ya Studio Space Pictures si haba. Imefanya video kali zikiwemo Phumakim ya Casper Nyovest, Sim Dope ya AKA, Marry You ya Ice Prince, Easy to Love ya Bucie, Show ya Victoria Kimani na zingine.

15 December, 2015

MOURINHO ALIA KUSALITIWA

Mo 4
Kocha Jose Mourinho wa Chelsea amewatupia lawama wachezaji wake kwa kile anachosema anasalitiwa. Akiongea mara baada ya kupokea kichapo cha goli 2-1 toka kwa Leicester City jana usiku, kocha huyo anasema haelewi kitu gani kinawasumbua wachezaji wake hasa ikizingatiwa kuwa amekua akijitahidi sana kama mwalimu kuwaandaa lakini haoni hilo kwa wachezaji.
Mourinho anasema kuwa, alifanya kitu kikubwa sana msimu uliopita na kuwapandisha wachezaji katika viwango ambavyo wameshindwa kuvirudia tena msimu huu, na kwamba anaona kama anasalitiwa.
Kipigo hicho cha jana kimeifanya Chelsea wawe tayari wamepoteza michezo 9 ya ligi kuu hadi hivi sasa wakishika nafasi ya 16 na points zao 15 tofauti ya point moja tu na yule aliye katika mstari wa kushuka daraja.
Aidha Mourinho ameshangazwa na kitendo cha mchezaji wake Eden Hazard kuamua kujitoa mwenyewe uwanjani baada ya kugongana na mshambuliaji Jamie Vardy wa Leicester katika dakika ya 30, kitu kilichotafsiriwa kama uvivu na ukosefu wa uzalendo.
Lakini pamoja na matokeo hayo, kocha huyo wa Chelsea anasema hana wasiwasi na kibarua chake kwakua anaamini mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich hatomtimua na badala yake atamsapoti katika kuokoa jahazi la mabingwa hao watetezi.
Ushindi huo wa magoli 2-1 wa Leicester City yaliyopachikwa na washambuliaji wao hatari Jamie Vardy na Mahrez yameipandisha Leicester hadi nafasi ya kwanza na sasa wanaongoza ligi hiyo wakiwa na alama 35.
Angalia video Mourinho akiwachana wachezaji wake kwa kile anachokiita wanamsaliti.

UNAJUA JULIO AMESEMA NINI KUHUSU UTEUZI WA NAPE NNAUYE? HAJAISHIA HAPO, KACHIMBA MKWARA WANAOMCHONGANISHA…

Nape Nnauye, Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo
Siku chache mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DR. John Pombe Magufuli kumteuwa Nape Nnauye kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, wadau wa michezo wameendelea kumpongeza Nnauye kwa kuteuliwa kwake kushika nafasi hiyo.
Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ kocha wa Mwadui FC ambaye timu yake itashuka uwanjani December 19 kuikabili Ndanda FC amesema amefurahishwa na uteuzi huo huku akisema sekta ya michezo imepata Waziri kijana.
Julio ameweka wazi story hiyo wakati akizungumza na kituo cha Radio One cha jijini Dar es Salaam kupitia kipindi chake cha michezo.
“Rais Magufuli kumteuwa Nape Nauye kuwa Waziri atakaeshughulikia michezo mimi ninaupongeza uteuzi huo, alichofanya ni sahihi, isipokuwa ninamasikitiko makubwa nimepata taarifa kwenye magazeti yameandika mimi nimesema Mh. Nape aanze na TFF ambayo inauozo kuna kuna watu wanamdanganya Malinzi. Habari hizi si za kweli mimi sikusema na sikutaka mtu anisemee, mimi nina akili timamu ninapotaka kusema langu hakuna mtanzania asiyejua kuwa Julio ni muwazi na anaweza kusema dakika yoyote”, alifunguka Julio.
“Nakumbuka kuna mwandishi aliniuliza kuhusu Nape, sasa atakapokuwa anasema kitu ambacho kitanigombanisha na kunichonganisha na watu wengine sipendi na nakemea kwa nguvu kubwa na waandishi wa aina hii nitawapeleka mahakamani haraka sana”.
Julio ametoa pongezi kwa Nape Nnauye juu ya uteuzi wake wa kuwa Waziri atakaeshughulikia pia masuala ya michezo lakini pia amesema hapendi kuchonganishwa wala kugombanishwa na watu.
Jumamosi ya December 12, Julio alikiongoza kikosi cha Mwadui kupata ushindi wa bao 2-0 dhidi ya wapinzani wao wa mji mmoja Stand United na kukisaidia kikosi chake kufikisha pointi 18 kwenye ligi ya Vodacom Tanzania bara

WACHEZAJI 6 WATARUDI KWENYE TIMU ZAO ZA ZAMANI KWENYE MICHEZO YA UEFA CHAMPIONS LEAGUE HATUA YA 16 BORA

zamani
Jumatatu December 14 draw ya UEFA Champions League hatua ya mtoano ilitangazwa. Ratiba hiyo imezua gumzo kubwa mitaani pamoja na kwenye mitandao ya kijamii huku michezo kadhaa ikipewa uzito wa juu. Michezo inayozikutanisha timu za Bayern Munich vs Juventus, Chelsea vs PSG, na Arsenal vs Barcelona inatazamwa kama ni fainali ambazo zitakuwa zikichezwa kwenye hatua ya mapema.
Michezo hiyo ya hatua ya 16 bora itaanza kuchezwa February 2016, kuelekea kwenye michezo hiyo mtandao huu umeangalia baadhi ya wachezaji ambao watakuwa wakirejea kwenye klabu zao za zamani ambazo waliwahi kuzitumikia katika nyakati tofauti.
6. Kingsley Coman-Bayern Munich
Arsenal's Mathieu Debuchy, left, holds Bayern's Kingsley Coman during the Champions League Group F soccer match between Bayern Munich and Arsenal FC in Munich, southern Germany, Wednesday, Nov. 4, 2015. (AP Photo/Matthias Schrader)
Bayern Munich itakutana na Juventus kwenye hatua ya mtoano, Kingsley Coman atakuwa mchezaji ambaye anakutana na klabu yake ya zamani. Kwasasa yupo kwa mkopo kwenye kikosi cha Bayern Munich akitokea Juventus. Amekuwa kwenye kiwango kizuri tangu alipotua Bayern na kocha Pep Guardiola amekuwa akimuamini na kumpa nafasi ya kucheza.
5. Mario Mandzukic-Juventus
zamani 2
Striker wa Juventus Mario Mandzukic atakua akicheza dhidi ya klabu yake ya zamani Bayern Munich wakati klabu hizo zitakapokutana kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora. Alitwaa taji la UEFA Champions League akiwa na The Bavarians alipokuwa akikitumikia kikosi hicho mwaka 2013.
4. Thomas Vermaelen-Barcelona
zamani 3
Beki wa Barcelona Thomas Vermaelen pia atakuwa akikutana na timu ya Arsenal, timu ambayo aliitumika miaka kadhaa iliyopita. Alijiunga na miamba ya Catalan majira ya kiangazi msimu wa mwaka 2014 na msimu uliopita ametwaa mataji matatu (treble) akiwa na kikosi hicho.
3. Aturo Vidal-Bayern Munich
zamani 4
Kiungo wa Bayern Munich Aturo Vidal atakuwa akicheza dhidi ya Juventus wakati klabu hizo mbili zitakapomenyana kwenye raundi ya 16 bora mwaka ujao. Vidal alikosa taji hilo wakati Juventus ilipopoteza mchezo wake wa fainali dhidi ya Barcelona mwezi May mwaka huu lakini wiki kadhaa baadaye akajiunga na wakali wa Allianz Arena.
2. David Luis-PSG
zamani 5
Mlinzi wa Paris Saint Germain David Luiz aliifunga timu yake ya zamani Chelsea na kuisaidia timu yake ya sasa kuitupa nje Chelsea kwenye michuano ya UEFA mapema mwaka huu lakini timu hizo zitakutana tena kwenye hatua ya 16 mwezi February mwaka ujao.
1. Alexis Sanchez-Arsenal
zamani 6
Star wa Arsenal Alexis Sanchez aliondoka Barcelona baada ya muda mwingi kuishia kukaa kwenye benchi. Kwasasa ni moja ya  wachezaji tegemeo kwenye kikosi cha Arsenal na anakutana na timu yake ya zamani ambayo haikuonesha kumuamini. Wakati huu Sanchez atapata nafasi ya kuwaonesha Barcelona kuwa walimwacha mchezaji bora timu hizo zitakapokutana kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora.

Ijue smartphone inayokaa chaji siku 15.. (+Video)


Mawasiliano muhimu sana mtu wangu, ndio maana watu wengi wanaona umuhimu wa kuwa na smartphone ili mawasiliano ya njia nyingi yaweze kumfikia.
Wataalam wa mambo wakaingia kazini na kubuni kitu kinaitwa powerbank… ambayo kama smartphone yako ikiisha chaji basi hiyo inakusaidia uendelee kubaki hewani, lakini simu+powerbank ni sawa na mizigo miwili ya kubeba mkononi, usijali… Wachina wanajali mahitaji yako.
CHINA
Kwa sababu unahitaji kitu nafuu, usipitwe na stori kwamba Wachina wameingia chimbo na kuja na mzigo wa smartphone ambazo zinaweza kukaa chaji kwa siku 15, hesabu hiyo kwa lugha nyingine ni kwamba inakaa na chaji kwa wiki mbili kamili !!
Simu yenyewe inaitwa Oukitel K10000 ambayo Wachina wenyewe wamesogezewa tayari sokoni ndani ya nchi yao na pia inapatikana Marekani kwa bei ya kama dola 239 ambazo kwa TZ inasomeka kwa shilingi 515,000/=…. Kaa tayari mtu wa nguvu, mzigo unaweza kugusa sokoni Afrika pia.
Unaweza kuiangalia simu yenyewe hapa, kama huna imani na vitu vya kichina cheki na hiki

Wabunge walioukataa Uwaziri, Mapigano ya wakulima, wafugaji, aliyevamia kwa MWINYI bila taarifa…#MAGAZETINI

MTANZANIA
Wabunge wanne wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wametajwa kukataa uteuzi wa nafasi ya uwaziri ili kujaza nafasi za wizara nne zilizokuwa wazi, imebainika.
Hatua hiyo imetokana na kile kilichoelezwa kuwa ni hofu ya wabunge hao kushindwa kwenda na kasi ya Rais Dk. John Magufuli, ambaye aliwaapisha mawaziri wapya Desemba 12, mwaka huu.
Wabunge hao ambao hawakupenda kutajwa majina yao gazetini walidai kuwa kasi ya Rais Magufuli inawatia hofu.
“Kasi ya Rais Dk. John Magufuli ni nzito na kwangu ni ngumu na nilifikiri niko mimi peke yangu kumbe baada ya taarifa hizi nasikia na wenzangu wawili nao walikataa uteuzi.
“Niliarifiwa juu ya uteuzi lakini baada ya kupima nikaona hapana siwezi kazi ya uwaziri, bora ni baki na ubunge wangu,” alisema mbunge huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe.
Wakati akitangaza Baraza la Mawaziri, Desemba 10, mwaka huu, Rais Magufuli alisema kuna baadhi ya wizara hazina mawaziri kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo unyeti wa wizara hizo na kwamba anaendelea kuwatafuta.
Kutokana na hali hiyo Rais Magufuli aliteua manaibu waziri wa wizara hizo, huku akitoa ahadi kuwa atawatangaza mawaziri wake baadaye atakapomaliza mchakato.
Wizara hizo ni pamoja na Ujenzi, Uchukuzi na Miundombinu ambayo naibu wake ni Mhandisi Edwin Ngonyani na Wizara ya Fedha na Mipango, ambayo naibu wake ni Dk. Ashatu Kijaji.
Wizara nyingine ni Maliasili na Utalii, ambayo naibu wake ni Mhandisi Ramo Makani, Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi ambayo naibu wake ni Mbunge wa Jimbo la Nyasa mkoani Ruvuma, Stella Manyanya.
MTANZANIA
Mkazi wa Ilala Mtaa wa Lindi, Hafidhi Ally, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo Kinondoni akikabiliwa na tuhuma za kuvamia kisha kuingia nyumbani kwa Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi.
Mbele ya Hakimu Ester Kihiyo, karani wa mahakama hiyo, Mosses Mchome, alidai kwamba mtuhumiwa alifanya kosa hilo Desemba 10, mwaka huu saa 7:30 usiku nyumbani kwa Mzee Mwinyi,  Mikocheni B, Dar es Salaam.
Karani Mchome aliiambia mahakama hiyo kwamba, Hafidhi aliingia hadi ndani ya nyumba hiyo bila ruksa kutoka kwa mlinzi aliyekuwapo kwenye lindo, Nuru Saidi, ambapo alimweleza kwamba hana mahali pa kuishi.
“Mtuhumiwa ulikaidi amri ya mlinzi aliyekuwepo zamu siku hiyo, aliyekutaka urudi ulipotoka, kisha ulisisitiza kwamba huna sehemu ya kuishi, lakini pia wewe ni mtoto wa rais huyo mstaafu wakati huo ukielekea ndani kitu ambacho ni kinyume cha sheria,” alidai Mchome.
Mtuhumiwa alikana kosa hilo na upelelezi bado unaendelea.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 28, mwaka huu na mtuhumiwa alirejeshwa mahabusu baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambapo alitakiwa apeleke wadhamini wawili waaminifu wenye barua kutoka kwa ofisa mtendaji wa kata anakoishi.
MTANZANIA
Mtu mmoja amefariki dunia na wengine wanne wamejeruhiwa, akiwamo askari polisi mmoja baada ya kutokea mapigano kati ya wakulima na wafugaji katika Kijiji cha Dihinda, Kata ya Kanga, Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro.
Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Dihinda, Hariri Kilama, alisema tukio hilo lilitokea Desemba 11, saa 11 jioni.
Kwa mujibu wa Kilama, tukio hilo lilisababishwa na mfugaji mmoja aliyejulikana kwa jina la Shaban Ramadhan, kuingiza ng’ombe wake katika shamba la mkulima aliyetambuliwa kwa jina la Bakari Mlunguza ambao waliharibu mazao.
“Baada ya uharibifu wa mazao hayo, uongozi wa kijiji ulimwita Bwana Shamba wa Kijiji, Mathew Limbanywa, kwa ajili ya kufanya tathimini ya  mazao yaliyoharibiwa na mifugo hiyo.
“Baada ya tathmini hiyo, ilibainika, kuwa uharibifu uliofanyika ulikuwa mdogo na bwana shamba huyo aliomba suluhu ifanyike ili kutatua mgogoro huo.
“Pande hizo zilipokaa pamoja, mkulima aliomba alipwe fidia ya shilingi laki tatu, lakini mfugaji alikataa na kusema yupo tayari kulipa shilingi laki mbili.
“Makubaliano hayo yalipofanyika saa nane katika ofisi ya Ofisa Mtendaji wa Kijiji, Wiliam Masanyika, mfugaji aliondoka na saa 11 jioni alirudi na kundi la wenzake na kuanza kupiga miruzi ya kuita ng’ombe wake waliokuwa chini ya ulinzi ofisini hapo.
“Wakulima walipoona kuna dalili za mapigano, nao walijibu mapigo, ambapo wafugaji walimpiga mkulima mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Mohamed ambaye alifariki dunia wakati akipelekwa katika Hospitali ya Mission ya Bwagala wilayani humo.
“Pamoja na mauaji hayo, ng’ombe 71 nao waliuawa na wengine 120 walijeruhiwa vibaya na wakulima hao,” alisema Kilama.
Waziri wa Kilimo, Chakula na Mifugo, Mwigulu Nchemba, aliliagiza Jeshi la Polisi mkoani Morogoro kuimarisha ulinzi katika eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuwakamata waliohusika katika vurugu hizo.
Naye Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Morogoro, Leonard Paul, alisema polisi mkoani hapa wanawashikilia watu 19 wakiwamo watatu wanaodaiwa kuwaua ng’ombe hao kwa kuwakatakata kwa mapanga
MWANANCHI
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema watu wanaomiliki mashamba bila kuyaendeleza huku wakiyatumia kama dhamana ya kukopea fedha benki watanyang’anywa.
Lukuvi, akizungumza kwa mara ya kwanza baada ya kuripoti kazini jana pamoja na naibu wake, Angelina Mabula, alisema kuna watu wamehodhi mashamba makubwa lakini hawayaendelezi, hawayalipii kodi, na mbaya zaidi wanayatumia kukopa fedha benki.
“Mkuu wa idara anayehusika na ardhi ninaomba Jumatatu ijayo orodha ya watu tuliowapa ardhi lakini wameitumia kuombea mikopo ambayo wanaitumia kwa shughuli nyingine.
Hao nitalala nao mbele,” alisema Lukuvi baada ya kujitambulisha kwa wakuu wa idara za wizara hiyo.
“Nipeni pia orodha ya watu wanaotakiwa kulipa kodi ya ardhi lakini hawalipi na tukikutana wiki ijayo nielezeni taratibu zinazotakiwa kuchukuliwa dhidi yao,” alisisitiza.
Akisisitiza kuhusu hilo, Lukuvi alisema wiki ijayo atakwenda kuchukua shamba lililohodhiwa na mwekezaji lenye ekari 1,600 huko Mbarali mkoani Mbeya na kuwarudishia wananchi.
Japokuwa Lukuvi hakumtaja mwekezaji atakayenyang’anywa shamba hilo wilayani Mbarali, lakini shamba la ukubwa huo lililokuwa na mgogoro kwa muda mrefu ni la Kapunga.
Akiwa kwenye kampeni mkoani Mbeya, mgombea urais wa CCM ambaye sasa ni Rais John Magufuli, aliahidi kurejesha shamba hilo kwa wananchi ili kumaliza mgogoro wa muda mrefu.
Aidha, Lukuvi aliwaagiza maofisa hao kuwasiliana na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ili kuangalia wawekezaji waliopewa ardhi kama wanaitumia kwa malengo yaliyokusudiwa.
“Tukikutana Jumatatu ijayo nipewe taarifa za kila mwekezaji na ukubwa wa ardhi aliyopewa; aliomba kwa madhumuni gani, na je, anaitumia ardhi hiyo kwa madhumuni aliyoombea?” alihoji. Kuhusu upimaji wa ardhi,
Lukuvi alisema asilimia 10 ya ardhi nchini ndiyo imepimwa na kwamba juhudi zinahitajika ili kupima ardhi zaidi. Tunataka tukikutana wiki ijayo, ofisa anayehusika na upimaji aje na mpango wa upimaji ardhi na umilikishaji na atueleze utagharimu kiasi gani ili tuweze kuona serikali itawekeza vipi katika upimaji wa ardhi nchi nzima,” alisema.
Kuhusu ujenzi wa nyumba za kupangisha, Lukuvi alisema kumeibuka kampuni nyingi zinazofanya biashara ya kujenga nyumba kubwa na kuzipangisha lakini hakuna chombo chochote cha serikali kinachosimamia sekta hiyo. “Hii ni biashara kubwa ambayo inakua siku hadi siku, hivyo ni lazima sasa wizara isimamie kwa kuweka chombo maalumu. Hivi sasa biashara inafanyika lakini hatupati kodi kwa sababu si rasmi,” alisema.
Waziri Lukuvi alimtaka mkurugenzi wa nyumba wa wizara hiyo kuandaa mpango wa namna ya kuwasaidia watu maskini ili kuwa na nyumba bora.
“Tunataka atueleze serikali ifanye nini ili kuwasaidia wananchi maskini kuwa na nyumba bora ili waondokane na nyumba zilizoezekwa kwa nyasi,” alisema.
MWANANCHI
Wizara ya Nishati na Madini, imezindua matumizi ya mfumo mpya wa malipo ya ada za leseni za madini kwa njia ya kielektroniki (OMCTP) Kaimu Kamishna Mkuu wa Madini, John Nayopa jana alisema mfumo huo ulianza kutumika wiki iliyopita na utawawezesha wateja kutuma maombi ya leseni na taarifa za utendaji kazi kwa njia ya mtandao.
“Mfumo huu ni salama kwa fedha za wateja na kuanzia sasa malipo ya ada za leseni yatafanyika kwa njia ya mtandao pekee. Ofisi zetu za madini zitatoa msaada kwa wateja wanaohitaji maelekezo,” alisema.
Alisema utawawezesha pia wateja kupata ramani za kijiolojia, takwimu mbalimbali za madini na kufanya malipo kwa njia ya miamala ya simu za mkononi, Maxmalipo na kupitia benki (EFT).
Nayopa amewataka wadau kuchangamkia fursa za uwekezaji zilizopo katika sekta ya madini ikiwa ni pamoja na kuongeza thamani ya madini na kuchakata mchanga wenye madini ili wanufaike na Serikali iongeze mapato kwa kupitia ulipaji wa kodi.
Mfumo huo unalenga kurahisisha utoaji wa leseni wachimbaji wadogo, kupunguza mlundikano wa maombi ofisi za madini, kurahisisha mawasiliano kati ya wizara na wamiliki, kujua taarifa za leseni na utoaji wa taarifa za madini kwa wakati
MWANANCHI
Mradi wa kuchakata gesi asilia kutoka Madimba Mtwara­Songosongo hadi Dar es Salaam umekamilika na kuwezesha uzalishaji umeme katika mitambo ya Kinyerezi, Ubungo, Tegeta na kuingizwa kwenye gridi ya Taifa.
Kwa sasa mradi huo unazalisha asilimia 70 ya umeme wote unaotumika nchini kupitia Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC), Dk James Matagio alisema jana kuwa nchi inaelekea katika uchumi wa gesi kutoka katika uzalishaji wa umeme kwa kutumia mafuta na maji. Alisema ujenzi wa bomba jipya la gesi umeongeza uzalishaji kwa asilimia 30.
Dk Matagio lisema mradi wa usambazaji gesi asilia katika mikoa ya Mtwara, Lindi na Dar es Salaam pia unalenga kusambaza gesi katika nyumba 30,000 na magari 8,000.
Alisema upembuzi yakinifu na usanifu wa michoro umekamilika na kwa sasa wanatafuta fedha kutekeleza mradi unaotarajia kugharimu Dola 150 za Marekani.
Meneja wa Mawasiliano wa TPDC, Maria Msellemu alisema kutokana na ugunduzi wa mafuta nchini Uganda, Serikali ya nchi hiyo ilitia saini makubaliano na Tanzania kwa kushirikiana na TPDC na Kampuni ya Total.
Alisema makubaliano hayo yanalenga kuangalia uwezekano wa kusafirisha mafuta ghafi kutoka nchini humo kupitia Bandari ya Tanga hadi kwenye soko la nje.
“Tumeanzisha kampuni tanzu za Gaso ambayo inashughulikia gesi, Copec uagizaji wa mafuta na Kampuni ya International Business biashara za kimataifa,” alisema Msellemu.
MWANANCHI
Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo (KMKM), kimekamata shehena ya makonyo na karafuu kavu iliyodaiwa kusafirishwa kwenda nje ya nchi kwa njia ya magendo katika Bandari ya Milango Mikavu kisiwani hapa.
Kamanda wa KMKM Pemba, Silima Haji Haji alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 2:30 usiku. Alisema watu waliokuwa wakivusha shehena hiyo walikimbia na kutelekeza magunia 31 za makonyo na manne ya karafuu kavu baada ya kuwaona askari wa kikosi hicho wakienda kuwakamata.
Alisema kabla ya tukio hilo, askari waliokuwa doria waliwatilia wasiwasi na walipowafuatilia watuhumiwa hao walikimbia.
Kamanda Silima alisema katika kipindi hiki ambacho karafuu zinaendelea kuchumwa, askari wake wameongeza ulinzi baharini na nchi kavu ili kuwadhibiti watu wanaotaka kuhujumu uchumi wa nchi kwa masilahi yao binafsi.
Mdhamini wa Shirika la Biashara la Taifa (ZSTC) Pemba, Abdalla Ali Ussi amepongeza juhudi zinazochukuliwa na kikosi cha KMKM kupambana na biashara ya magendo ya karafuu.
Aliwataka wananchi kujiepusha na biashara hiyo haramu inayowanufaisha kwa kuwa inadhoofisha uchumi wa nchi. Alisema wananchi wameitikia wito wa Serikali wa kuuza karafuu katika vituo vya ZSTC na kwamba fedha zinazopatikana hutumika katika kukuza maendeleo.
Baadhi ya wananchi wanaouza karafuu katika Kituo cha Shirika Bandarini Wete, wameviomba vyombo husika kufanya uchunguzi ili watuhumiwa wakamatwe.
Mmoja wa wakazi hao, Yussuf Said Rashid alisema ni vema Serikali kupitia ZSTC kuandaa utaratibu maalumu wa kuwakagua wananchi wenye mikarafuu ili kujiridhisha kama wanaziuza kwenye vituo vya shirika hilo.
Alisema vitendo vya magendo vinatakiwa kukomeshwa kwa kuweka mikakati kabambe ya kuvidhibiti ikiwamo wananchi kutoa taarifa wanapoona matukio kama hayo.
MWANANCHI
Maandalizi ya upangaji wa ada elekezi kwa shule binafsi nchini yameibua mvutano kati ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi na Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi (Tamongsco) baada ya kulalamikia kutopewa nafasi ya ushiriki katika hatua za awali.
Katibu Mkuu wa Tamongsco, Benjamini Nkonya alisema jana kuwa chama hicho kiliwachagua mawakili wake wanne kwa ajili ya kutoa ushirikiano kwa wizara hiyo katika upangaji na uchambuzi wa ada elekezi, lakini haijawatumia.
Alisema Serikali imekuwa ikiwatumia wamiliki wa shule binafsi wasiokuwa na uwakilishi wa mawazo ya chama hicho. Waliochaguliwa na chama hicho kuwakilisha maoni yao ni mwenyekiti wake, Mrinde Mnzava, makamu mwenyekiti Jeremiah Bwegenyeza, Katibu mkuu, Benjamin Nkonya na mhasibu, Mapenzi Yona.
Hata hivyo, Kamishina wa Elimu Wizara hiyo, Profesa Eusella Bhalalusesa alipinga ofisi yake kupokea majina ya wawakilishi wa chama hicho.
Alisema utafiti bado unaendelea, hivyo wanayo nafasi ya kuwasilisha maoni yao. “Sijapata majina yao, lakini kwa nini tugombanie fito wakati nyumba ni moja? Wadau ni wengi na siyo rahisi kumfikia kila mmoja, wataalamu watakapokamilisha ripoti yao kabla ya mwaka wa masomo 2016, tutaichambua na wadau wote kabla ya kuanza majaribio yake.
“Lakini katibu huyo wa Tamongsco (Benjamini Nkonya) nilimuona kwenye televisheni akisema wameshiriki vizuri kutoa maoni yao,” alidai Profesa Bhalalusesa.
Profesa Bhalalusesa alitaja baadhi ya vigezo vitakavyotumika kupanga ada elekezi kuwa ni huduma zinazotolewa na shule, eneo la shule inakopatikana na mmiliki wa shule husika.
Alipoulizwa kuhusu kutenganisha mtoa huduma na mfanyabiashara ili kutoza kodi alisema: “Ndiko tunaelekea huko, tutaangalia shule inayotoa huduma na inayofanya biashara ili iweze kutozwa kodi.”

Obama: Tumeipiga IS kwa nguvu Novemba


Rais wa Marekani, Barack Obama amesema vikosi vya Marekani vinawashambulia wanamgambo wa Islamic State kwa nguvu kuliko wakati mwingine.
Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari katika wizara ya ulinzi nchini humo, Obama amesema mashambulizi zaidi ya anga yametekelezwa dhidi ya kundi hilo mwezi Novemba kuliko mwezi mwingine wowote.
Muungano wa ndege za mashambulizi ya anga, wapiganaji, ndege za mashambulizi ya mabomu na ndege zisizo na rubani vimeongeza kasi ya mashambulizi ya anga na kufikia 9,000 mpaka sasa.
''Mwezi uliopita wa Novemba, tuliangusha mabomu zaidi kwenye maeneo ya ISIL kuliko mwezi mwingine wowote tangu kampeni hii ilipoanza, pia tunawaua viongozi wa IS, makamanda wao na wauaji mmoja baada ya mwingine," amesema Obama.
Hata hivyo amekiri, kuwa kutokana na mashambulizi ya kigaidi ya hivi karibuni, jitihada zaidi zinahitajika.
''Tunatambua kuwa jitihada zinahitajika haraka. Hakuna anayejua raia wangapi wa Syria na Iraq wanaoathirika kutokana na vitendo vya kigaidi vya IS pia na familia za San Bernardino na Paris na kwingine ambako wanaomboleza vifo vya wapendwa wao,'' amesema Rais Obama.

Hoteli iliyoshambuliwa Mali kufunguliwa

Mali
Hoteli iliyoshambuliwa katika mji mkuu wa Mali, Bamako, mwezi jana itafunguliwa tena leo.
Watu wenye silaha walishika mateka wageni 170 kwa saa tisa katika hoteli ya Radisson Blu, na kuua watu 22 na kujeruhi wengine 14.
Polisi na wanajeshi wa Mali, wakisaidiwa na vikosi vya usalama kutoka nje, waliingia kwenye hoteli hiyo na kuwaua washambuliaji.
Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita ametangaza kupitia Twitter kwamba hoteli hiyo itafunguliwa.

Afrika kujadili nafasi yake katika uchumi wa dunia


Mawaziri kutoka Mataifa 160 wanakongamana hii leo jijini Nairobi ikiwa siku ya kwanza ya Kongamano la Shirika la Biashara Dunani, WTO.
Ni mkutano wa kwanza ya aina yake barani Afrika.
Mjadala mkuu unatarajiwa kuwa mwelekeo mpya kwa mataifa ambayo hayajanawiri, hasa baada ya maafikiano ya Kongamano ka Doha kutotimizwa baada ya zaidi ya miaka kumi.
Zaidi ya wawakilishi 7,000 wanakongamana katika ukumbi wa mikutano ya KICC kuanzia hii keo kujadili jinsi ya kufanya biashara kote ulimwenguni kwa usawa.
Licha ya kuwa bara afrika lina wanachama wengi zaidi katika WTO, kumekuwa na malalamishi kuwa shirika hilo limetawaliwa sana na mataifa yalionawiri tayari, kama Uchina na Marekani.
Bwana Robert Azevedo , ambaye ni mkurugenzi Mkuu wa WTO, umuhimu wa WTO kwa wanachama kutoka afrika.
Naye akasema Afrika inapata Fursa ya kujieleza na kuweka bayana matakwa yake kibiashara. ''Afrika inapewa Meza ya kusema matarajio yake,
Mahala pa kuketi.
Kipaza sauti ya kusema nacho. Mataifa haya hayezi kupuuzwa.
Hayawezi kusahaulika.
Na hali hii huenda likatimika ikiwa WTO haitendi kazi yake vizuri, au haizingatii maswala yote muhimu, kama vile biashara ndogo ndogo na zile wastani, na vile zitawiana na msururu wa biashara za kimataifa.
Ni jinsi gani ya kusaidia mataifa ya Afrika kunawiri kiviwanda?
Njia bora zaidi ni kuyapa mataifa jukwaa ya kushiriki, kutoa maoni, na kusema ni njia gani tuwaweza kuwasaidia.''Alisema Azevedo
Kwa zaidi ya miaka ishirini shirika la WTO imefanya majadiliano bila kuafikiana jinsi mataifa masikini yatasaidiwa kufanya biashara.
Kwenye Kongamano la Doha ya Mwaka 2001, mataifa masikini yaliomba ruzuku katika biashara za sekta ya Kilimo wanayotegemea sana bila mafanikio.
Mataifa mengi sasa yanafanya makubaliano ya makundi madogo, kwa mfano jumuiya ya Afrika Mashariki au Muungano wa Kenya, Uganda na Rwanda, ambao umerahisisha usafiri wa raia wa nchi hizo pamoja na bidhaa kutoka bandari ya Mombasa.
Bw Azevedo anasema ni wakati wa WTO kuinuka sambamba na miungano kama hii.
Azevedo''Na hii ndio sababu kongamano la Nairobi ni muhimu sana. Ni wakati wa kutafakari, Nadhani wanachama watazungumza na kujadili maswala haya nyeti kama mawaziri, kwa hivyo ni mjadala muhimu kisiasa''
Azevedo hatarajii makubaliani katika maswala yote tata, ila ana matumaini kuwa mjadala utazua angalau msimamo mmoja kuhusu mwelekeo wa pamoja wa siku za usoni.
Kati ya mataifa arobaini na tatu kutoka Afrika ambayo ni washiriki wa WTO, 33 zinatambulika kama mataifa masikini, ikiwemo Tanzania, Uganda na Sudan Kusini.
Ethopia haijajiunga na WTO ingawa imewasilisha ombi. Katika kongamano la mwaka huu wanachama watapiga kura kuamua ikiwa mataifa ya Liberia na Afghanistan watakubaliwa kuwa wanachama.
Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf yuko Kenya kushuhudia uamuzi huo.

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...