30 January, 2016

Video: J. Cole – Love Yourz

Fresh off the release of his surprise album Forest Hills Drive: Live From Fayetteville, NC, J. Cole debuts a video for “Love Yourz” taken from his sold-out show at Crown Coliseum, which aired as part of his HBO concert special J. Cole Forest Hills Drive: Homecoming earlier this month. The three-and-a-half-minute clip includes candid backstage moments, live show footage, and cameos from his Dreamville crew as well as Pusha T and No I.D.

“2-6, Fayetteville, Fayettenam, I fu**in’ love ya’ll,” Cole tells the hometown crowd. “This been some legendary shit.”

Forest Hills Drive Live was recorded on the last date on Cole’s “Forest Hills Drive” tour and features music from his platinum-selling album, plus a medley of “Lights Please,” “In the Morning,” and “Nobody’s Perfect.”

Watch Cole pay homage to his hometown.

Video: Godzilla - Get High

Baada ya kimya cha muda mrefu, Godzilla anakuja na video ya Get High.

Chelsea imemchukua mshambuliaji wa Brazil Alexandre Pato kwa mkopo hadi mwisho wa msimu.

Alexandre Pato
Mshambuliaji huyo wa umri wa miaka 26 ambaye amekuwa akichezea klabu ya Corinthians ya Ugiriki amechezea taifa lake mechi 27 na kuwafungia mabao 10.
Alichezea Brazil katika Michezo ya Olimpiki mwaka 2008 na 2012.
“Nina furaha sana kujiunga na Chelsea,” alisema Pato baada ya kujiunga na klabu hiyo ya Stamford Bridge. “Ni klabu niliyoitamani sana, na nasubiri kwa hamu kuwafahamu wachezaji wenzangu wapya na kucheza nao pia.
"Naishukuru Chelsea kwa kuniunga mkono na natumaini nitawafanyia hisani kwa sababu ya kuwa na Imani name.”
The Blues, walioshinda Ligi ya Premia msimu uliopita, wametatizika sana msimu huu na wamo nambari 13 ligini, ingawa bado wanacheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Kaimu meneja Guus Hiddink amesema licha ya hali kwamba Pato ametatizwa sana na majeraha, hadhani kwamba kumchukua ni kucheza bahati nasibu.
"Si kubahatisha. Kuja kwake hapa kwa mkopo kunatuwezesha kumfuatilia na kujua iwapo anaweza kuzoea ligi hii,” amesema Hiddink.
Chelsea pia wanakaribia kumnunua difenda wa New York Red Bulls Matt Miazga, 20.
"Hatuna haraka, lakini atakuwa kwenye kikosi chetu siku za karibuni,” ameongeza Hiddink.

Stephane Mbia amejiunga na klabu ya Hebei China Fortune nchini Uchina

Stephane Mbia
Nahodha wa timu ya taifa ya Cameroon Stephane Mbia amejiunga na klabu ya Hebei China Fortune nchini Uchina.
Mbia amekuwa akichezea Trabzonspor ya Uturuki.
Mchezaji huyo wa zamani wa Marseille mwenye umri wa miaka 29 sasa atajiunga na nyota wa Ivory Coast Gervinho katika klabu hiyo ya Uchina.Gervinho alijiunga na Hebei China Fortune akitokea AS Roma Jumatano.Mbia
"Twamsubiri sana beki kamili Mbia afike hapa na kuonyesha ustadi wake,” klabu hiyo iliandika kwenye Twitter.Mbia aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter: “Najivunia kujiunga na Hebei China Fortune, niko tayari. Twende kazi."

Magazeti ya leo January30,2016



29 January, 2016

De Bruyne kukaa nje wiki sita


Kiungo wa Manchester City, Kevin de Bruyne, atakua nje ya dimba kwa muda wa wiki sita baada ya kuumia goti siku ya Jumatano.
De Bruyne aliumia goti la kulia katika mchezo kombe la Capital, ambapo Man City, waliwakabali Everton, na kushinda kwa mabao 3-1.
Wakala wa mchezaji huyu Patrick de Koster, amesema" Nimezungumza na Kevin, amesema atarudi uwanja kwa nguvu zaidi."
Mchezaji huya atakosa michezo muhimu ya timu yake ukiwemo ule wa fainali ya kombe la Capital, dhidi ya Liverpool, hapo Februari 28, pia atakosa mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi Dynamo Kiev.
Kulikua na wasiwasi huenda nyota huyu asingeweza rudi dimbani mpaka mwisho wa msimu.

Ligi kuu ya Bara kuendelea wikiendi


Ligi kuu ya Tanzania bara itaendelea tena kushika kasi wikiendi hii kwa nyasi za viwanja saba kuwaka moto siku ya jumamosi.
Wagosi wa kaya Coastal Union watakua wenyeji wa Yanga, Wekundu wa msimbazi Simba sport klabu wao watakua wenyeji wa Afrikani Sport mchezo utaochezwa kwenye uwanja wa taifa Dar Es Salaam.
Maafande wa Jkt Ruvu watawaalika wana lizombe Majimaji ya Songea, Tanzania Prison watashuka dimbani kuwakabili Azam FC.
Mtibwa Sugar watacheza na Stand United,huku Mwadui Fc ya Shinyanga watakipiga na majirani zao wa Mwanza Toto Afrikans. Kagera Sugar watapima ubavu na Mbeya City.
Yanga na Azam wanafukuza kileleni wote wakiwa na alama 39, mshambuliaji wa Yanga Amis Tabwe ndie kinara wa kuzipasia nyavu akiwa na mabao 13.
Ligi hiyo itaendelea tena siku ya jumapili kwa mchezo mmoja kuchezwa kwa Mgambo Jkt kucheza na Ndanda FC.

Kutana Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa Ya Januari 29



Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...