15 October, 2015

Kisa cha Santos kutaka Neymar afungiwe miezi 6 hiki hapa

Klabu ya Santos ya Brazil imeripotiwa kutuma maombi FIFA imfungie miezi sita mchezaji wao wa zamani Neymar kwa miezi 6 kama sehemu mambo yao ya kisheria dhidi ya mshambuliaji huyo na klabu yake mpya ya FC Barcelona.
  Kwa mujibu wa Sport, Santos wanahisi kusalitiwa na nahodha wa Brazil ambaye kwa mujibu wao alikiuka mkataba baina yao alipojiunga na Barca mwaka 2013. Pia inasemekana wanataka malipo ya fidia ua kiasi cha €55million katika adhabu ambayo wanataka FIFA itoe.
Haijafahamika lini FIFA itatoa maamuzi katika kesi ya Santos dhidi ya Neymar ya kutaka shirikisho hilo limfungie kwa miezi 6.
  Mashtaka ya Santos’ yanaelezea katika toleo la gazeti la Sport: “Neymar anatuhumiwa na Santos kuvunja kanuni namba 63 ya nidhamu. Katika jalada lao la mashtaka pia Santos wamezungumzka namna mchezaji alivyokosa utii wa sheria za uhamisho za FIFA za namba 17(3) and 17(5).”
Neymar amekanusha kuvunja sheria/kanuni yoyote kama anavyotuhumiwa na waajiri wake wa zamani, akisisitiza alihamia Barcelona mara tu baada ya kukubaliana kimsingi na Santos. Kwa mujibu gazeti la Sport, Neymar ana barua ya kutoka kwa Raisi wa Santia Luis Alvaro de Oliveira ambayp ilikuwa inampa ruhusa ya kuanza kuzungumza na Barcelona.
Santos walitangaza kwamba wangemchukulia hatua mchezaji wao wa zamani, baba yake Neymar na Barcelona mwanzoni mwa mwaka huu, wakiwatuhumu kufanya udanganyifu katika majadiliano ya uhamisho wa Neymar. Santos wanasema Barca walifanya udanganyifu katika malipo halisi ya waliyolipa na waliyoyatangaza.
  Ada waliyoripotiwa kulipa Barcelona mwanzoni kwa ajili ya Neymar ilikuwa €57 million (£42 million), lakini uchunguzi wa baadae ulionyesha bei halisi ni €86.2 million (£63.5 million).
Mpaka sasa Raisi wa zamani wa Barca Sandro Rossell na wa sasa Joseph Maria Bartomeu wana kesi mahakamani juu ya udanganyifu huu.

Kizza Besigye akamatwa Uganda


Kiongozi wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) nchini Uganda, Kizza Besigye amekamatwa pamoja na wanachama wengine wa chama chake.
Kukamatwa kwao kunajiri wakati ambapo chama hicho kilikuwa kinaanza kampeni zake kwa uchaguzi mkuu wa mwaka ujao kulingana na mwandishi wa BBC Patience Atuhaire katika mji mkuu wa Kampala.
Watu wengine wawili pia walikamatwa pamoja na bwana Besigye wakati maafisa wa polisi walipovamia nyumba yake mapema leo kulingana na vyombo vya habari.
Mbunge wa chama hicho Ssemujju Nganda ambaye pia ni msemaji wa chama hicho pia alikamatwa nyumbani kwake na amepelekwa katika kituo cha polisi cha Naggalama,karibu na mji mkuu wa Kampala.
Besigye amepoteza mara tatu kwa rais Yoweri Museveni katika uchaguzi uliokumbwa na utata.

Upinzani wapinga matokeo ya uchaguzi Guinea


Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Guinea amejiondoa katika uchaguzi uliofanyika nchini humo akisema kuwa kulikuwa na udanganyifu mkubwa uliotekelezwa na serikali kulingana na kiongozi wake wa kampeni.
Uamuzi huo wa Cellou Diallo wa kujiondoa unajiri wakati ambapo matokeo yanaonyesha kwamba rais Alpha Conde anaongoza kwa wingi wa kura akitafuta kushinda awamu ya pili ya miaka mitano.
Wachunguzi kutoka muungano wa Ulaya wanasema kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa haki licha ya matatizo makubwa ya vifaa.
Matokeo kamili ya uchaguzi huo yanatarajiwa mwishoni mwa wiki hii.

Lil wayne ajichanganya baada ya Lamar Odom kuzidiwa, aandika ‘R.I.P’

Mchezaji wa zamani wa timu ya kikapu ‘LA Lakers’ na mume wa zamani wa Khole kardashian, Lamar Odom yupo hoi kitandani baada ya kudaiwa kutumia kiwango kikubwa cha dawa za kulevya Cocain kiasi cha kupaatwa na kiharusi na figo zake kushindwa kufanya kazi.Lil wayne ni mmoja ya mastaa wakubwa waliopokea habari hiyo tofauti na ukweli halisi, alitweet “R.I.P LO,Dam man. My blessings to ur fam and friends.” lakini baada ya muda aligindua kuwa alikua amejichanganya, na kuwa mcheza kikapu huyo bado yupo hai, Alitweet tena  “Woop.”

Vyanzo mbalimbali vimedai kuwa Odom aliamua kubwia unga kwa kiasi kikubwa baada ya kupokea simu iliyomuudhi inayohusiana uhusika wake kwenye show ya Keeping up with the Kardashians hata hivyo wanafamilia hao wa The kardashians walifika Hospitalini hapo kumjulia hali.

I am The Black Gold of the Sun


These are random picks of pictures i came across today and had to share

 Celebrate the Black Gold in you,everyday...because You and I ARE the Black Gold of the Sun
Pictures from Arteide's Album on The Human Race

Huu hapa mchongo mpya wa P.diddy..kuanzisha kipindi cha Comedy kinachohusiana na Maisha ya kweli ya Msaidizi wake


Rapper, Producer, Muigizaji na mjasiliamali Sean Combs amejiunga na kituo cha runinga cha ABC kuandaa kipindi cha vichekesho kitakachohusu maisha ya kweli ya aliyekua msaidizi wake Sarah Snedeker.
Kipindi icho cha Vichekesho  ambacho kitarekodiwa na kamera moja tu tayari kimeandikiwa Script kitaonesha maisha ya binti aliyetoka kwenye maisha duni lakini anapata bahati ya kuwa msaidizi wa Billionaire mkubwa lakini anajikuta akiangukia kwenye maisha machafu ya ubadhirifu na ufisadi na vitu vingi vinavyomsahaulisha alipotoka.

Ulishawahi kujiuliza kuna maneno gani mengine ya kumwambia mpenzi wako tofauti na ‘I love you’ ?


‘Nakupenda’ ni  neno tamu ambalo unaweza mwambia  hivyo  mpenzi wako mara kwa mara lakini si neno pekee ambalo watu wengi wanapenda kusikia mara kwa mara. Yapo mambo mengi ya kumwambia mpenzi wako apate amani, hii inajenga upendo na  Heshima kati yenu.
 1. Mwambie Anaweza:
Kuna wakati tunapitia mambo magumu sana katika maisha na watu wanakata tamaa ya maisha wanakosa uthubutu wa kujaribu tena na tena, kama amefeli mtihani,amepata ajari ya gari, amepata hasara ya kibiashara mwambie “baby you can” mwambie anaweza kuendelea na maisha yataendeleea mtie moyo hii itamfanya ajiamini na kuona thamani yake kwako.

 1. Unanivutia
Mwambie ni kiasi gani anakuvutia, mwambie alivyo mrembo/mtanashati  mueleze ni kiasi gani unakuwa  na furaha akiwa karibu nawe, hii itamsaidia mpenzi wako kujiamini.  Msifie mpenzi wako  kwa suti au tai yake mpya , msifie msichana  kwa kiatu chake na gauni lake zuri kabla hajatoka nyumbani sababu anaweza akasifiwa na wengine, kwahiyo kuwa wa kwanza kumpa sifa hizo atajisikia wa fahari.

 1. Unajivunia kuwa Nae
Mambo yanaweza yasiwe vile mnavyotaka wakati wote, kuwa karibu na mwenza wako  na umuelezee ni kwa kiasi gani unajivunia kuwa nae, nafasi yake katika maisha yako na umuhimu wake ni faraja kwako, mueleze na umuonyeshe pia matendo yanaongea zaidi ya maneno.  Mwambie “am proud of you”

 1. Omba Kutoka Nae.
“Let’s go out”  hapa wasichana wengi huwa wanasubiri watoke na wapenzi wao mpaka waambiwe au mpaka mpenzi wake apange kutoka nae, chukua nafasi ya kumtoa  mpenzi wako mara moja moja na ugharamie huduma zote za siku hiyo, kama ni safari ufukweni, hotelini au migahawa mjini. Kama msichana kuwa tofauti na wale wasichana wanaosubiri kila siku ofa za mpenzi, kuwa tofauti usisubiri mpenzi wako akutoe, mtoe wewe siku moja.

 1. Msamaha
Uwe mwepesi wa kusema neno samahani kila mara, kuna kukoseana mara kwa mara kuwa wa kwanza kuomba msahama hii itapunguza hasira za mapenzi wako na malumbano pia hayatapata nafasi, hii itasaidia kuhimarisha mahusiano ya muda mrefu.

HONGRA DIAMOND PLUTNUM imetangazwa hivi na MTV BASE..


Hii good news imekuja siku chache baada ya ushindi wa tuzo za AFRIMMA 2015 ambazo zilitolewa Dallas Texas Marekani ambako Diamond Platnumz alishinda tuzo tatu.
Sasa kupitia twitter page ya MTV BASE leo October 15 2015 yameandikwa maneno ya kumpongeza Mtanzania Diamond Platnumz kwenye ushindi wa MTV Europe Music Awards yakisomeka >>> ‘ | Congratulations to who is the ‘Best African Act
MTV 5
Kwa time hiyohiyo kundi la Sauti Sol la Kenya lilimpongeza Diamond kupitia Instagram page yao na kuandika ‘MTVEMA imebaki Afrika Mashariki, ilikua yetu mwaka 2014 na sasa ni ya Diamond mwaka 2015, tumpongeze #BestAfricanAct2015 Diamond Platnumz, usisahau kuendelea kumpigia kura sasa hivi anaiwakilisha Afrika kwenye kipengele cha #WorldwideACT, mshindi atatangazwa tarehe 25 October 2015 Milan, Italy
MTV 3
MTV 4
Bonyeza kwenye hii link inayofata hapa ili kumpigia Diamond kura >>> VOTE
mtv 7
mtv 6

14 October, 2015

Hii ndio orodha kamili ya washindi wa Tuzo za BET HipHop 2015


Tuzo za BET Hiphop 2015 zimeoneshwa rasmi usiku wa jana, Big sean na Kendrick Lamar wametawala tuzo hizo kwa kushinda tuzo 3 kila mmoja, wakifuatiwa na Drake aliyeshinda Tuzo mbili ikiwa ni pamoja na ‘MVP of the Year’ na Fetty wap aliyeshinda tuzo ya  “track of the year” na  tuzo ya “who blew up”
Hii ndio orodha kamili ya washindi
Best Hip Hop Video: Kendrick Lamar “Alright”
Best Collabo, Duo or Group: Big Sean feat. Drake and Kanye West – “Blessings”
Best Live Performer: J. Cole
Lyricist of the Year: Kendrick Lamar
Video Director of the Year: Benny Boom
DJ of the Year: DJ Mustard
Producer of the Year: DJ Mustard
MVP of the Year: Drake
T rack of the Year: “Trap Queen” – Produced by Tony Fadd (Fetty Wap)
Album of the Year: J. Cole “2014 Forest Hills Drive”
Who Blew Up Award: Fetty Wap
Hustler of the Year: Dr. Dre
Made-You-Look Award (Best Hip-Hop Style): DeJ Loaf
Best Club Banger: Big Sean feat. E-40 – “IDFWU”
Best Mixtape: Future – 56 Nights
Sweet 16: Best Featured Verse: Drake – “My Way (Remix)” (Fetty Wap feat. Drake)
Impact Track: Kendrick Lamar – “Alright”
People’s Champ Award: Big Sean feat. Drake and Kanye West – “Blessings

Je, unayafahamu haya kuhusu wanawake?


Kuna usemi mmoja nimezoea sana kuusikia “I can’t understand women” hii ni nyimbo kila mwanaume anaimba, inawezekana ikawa kweli, kutokumuelewa mwanamke, inawezekana ikawa inasababishwa na wewe kutokuelewa mambo kadhaa yanayowahusu wanawake, hapa tafiti wa  kisayansi  na zisizo za kisayansi  zitakusaidia kumuelewa mwanamke kisaikologia na kitabia.
 1. Mapigo ya moyo ya mwanamke hupiga haraka kuliko mwanaume.
Maumbo ya wanawake huwa si makubwa kama ya wanaume , kwahiyo mioyo yao huwa inapiga mara nyingi, moyo wa mwanamke unapiga mapigo 78 ndani ya dakika moja.

 1. Mwanamke anaongea maneno 20,000 kwa siku wakati mwanaume anaongea maneno 13,000 tu kwa siku. Inawezekana ni watu wa maneno mengi na stori nyingi pia.

 1. Mwanamke hulia mara 30-64 kwa mwaka. Inasemekana tatizo la homoni, kuna asilimia 60% ya homoni inayoitwa prolaktini kwa wanawake kuliko kwa wanaume

 1. Mtaalamu wa Kwanza wa Program za Kompyuta (computer programmer) ni Mwanamke. Nani kasema wanawake hawawezi hesabu , Ada Lovelace (1815 -1852 ) ndio mwanamama  wa kwanza kufanya program za kompyuta.  Na inasemekana  katika rekodi zilizowahi kuwekwa  mtu wa kwanza kugundulika kuwa na  Uwezo mkubwa wa kufikiri (IQ)  ni Mwanamke.

 1. Wanawake wanapenda sana Chokoleti kuliko Tendo la ndoa. Utafiti unaonyesha wanaume wanapenda sana kufanya mapenzi kuliko wanawake, wanaume hutumia sana akili wakati wanawake ni watu wahisia zaidi,(emotions) hisia gani wanazipata wanawake wakila chokoleti hilo ni kwa wanaume kujiuliza.

 1. Asilimia 30 tu ya wanawake huwa wana furahia tendo la ndoa, wanawake wengi huwa hawatimiziwi haja zao za mwili na wengi wao hudanganya kama wameridhika, ila ukweli ni kwamba wachache kufikia haja zao kikamilifu. Inaweza ikawa ni matatizo ya kisaikologia au wanaume kutokujua wapenzi wao wanaridhika na nini.

 1. Kila mwanamke ana kitu kimoja hapendi juu ya mwili wake. Inaweza ikawa ni ukubwa wa matiti yake, tumbo lake au miguu yake hii inategemaa na mtu na mtu

 1. Akili ya mwanamke ni safi kuliko ya mwanaume, hii ni kwasababu mwanamke ni mtu wa vitu vingi akili ya mwanamke inaweza kuwa safi mara nyingi kuliko wanaume, akili chafu au wanaita Dirty mind hii ni kwa wanaume zaidi.

 1. Wanawake wana uwezo mkubwa wa kusikilizaa, wanaume wanasikiliza na upande mmoja tu wa ubongo,upande wa kushoto wa ubongo wao katika kusikiliza wakati wanawake wanatumia pande zote mbili katika kusikiliza .

 1. Wanawake wanaishi miaka mingi kuliko wanaume Dunia . Hii inaweza kuelezwa na sababu mbalimbali , kiwango cha homoni (Testosterone na estrogen) wanawake wana  uwezo mkubwa wa kuzoea mazingira kuliko wanaume . Hata hivyo, kuwa na muda mrefu wa kuishi haina maana wanawake wana  afya bora  kuliko wanaume.  Ila mazingira ambayo wanaume wanaweza yakawashinda wanawake wanayaweza.

Chris Brown atangaza tarehe ya kuachia Album yake mpya ‘Royality’

Album mpya ya Chris brown ‘Royality’ itatoka rasmi tarehe 27 November mwaka huu.
.

Staa huyo wa RnB alitoa taarifa hiyo siku ya jana (Oct. 13)  kwenye kipindi cha ‘Nessa and Camilo’ cha  Hot97, Album hiyo imepewa jina la mtoto wake wa kwanza mwenye umri wa mwaka mmoja ‘Royality’
Hadi sasa ameachia nyimbo mbili kutoka kwenye Album hiyo “Liquor” na “Zero”

Picha: Davido akutana na Trey songz na Young Jeezy

davido and trJumamosi iliyopita tarehe 10 Oktoba, Staa wa muziki wa Naija, Davido alienda kuparty kwenye club ya ‘Compound Night Club’ huko Atlanta na Mastaa wakubwa wa Marekani Trey songz na rapper Young Jeezy.
Kwa mujibu wa Boss wa HKN, Davido amesema Nimekua nikiwaona kwenye TV lakini sasa tunachangia bill moja club’. Trey songz ni moja ya wasanii wa kimataifa walioshirikishwa kwenye Album mpya ya Davido, ameshirikishwa kwenye wimbo unaoitwa ‘Wetin you Say‘.
davido and joel katz
Pia Davido alikutana na Mwanasheria namba moja kwenye Entertainment kwa mujibu wa Billboard, Joel Katz kwahiyo tunaweza tegemea chochote kati ya hawa watu wawili, Joel Katz pia huwa anaitwa ‘the deal maker who thinks outside the box’

KIJANA BADILI MTAZAMO WAKO NA JENGA MAISHA BORA      Kwanza nipende kukusalimu ewe mtanzania mwenzangu kwa kwakusema uu hali gani? Ni matumaini yangu yakwamba uu mzuima na buheri wa afya ingawaje sii asilimia mia moja ni jambo lakumshukuru  MUNGU kwani hapa tulipo sii kwa akili zetu wala kwa ujanja wetu bali ni kwa neema tuu.
       Basi kwa kuyasema hayo ambayo ni salamu zangu kwako wewe mtoka mbali , twende moja kwa moja kwenye mada yetu ambayo teyari nimeiwasilisha kupitia kichwa cha habari hapo juu yakwamba KIJANA BADILI MTAZAMO WAKO NA JENGA MAISHA BORA.
   Ni wazi kwamba neno MAISHA sii neno geni masikioni mwetu yakwamba kila mmoja wetu amekua akihangaika hapa na pale, usiku na mchana hii yote ni sababu ya maisha. Nuliwahi kumsikia mzazi mmoja akimweleza mwanae yakwamba ” Mwanangu kuwa uyaone” name nikajiuliza, Je akue ayaone nini? Magari au majumba? Kumbe alikua akimaanisha  MAISHA.
     Maisha ya kijana Mtanzania wa leo yamekua kama kitendawili ambacho kimekosa mtu wakukitegua. Je tumpe nani mji ili aweze Kukitegua?  Yapo mamba mengi yanayo sababisha maisha kuwa magumu au yasiyo na mwelekeo kwa vijana walio wengi na mambo hayo yanatokana na vijana wenyewe na mifumo mibovu ya elimu wapewazo nijana hawa huko mashuleni hasa hasa katika shule za msingi na zile za sekondari.
Kijana mwenyewe anawezaje kuyaharibu maisha yake?
   Yapo mambo mengi mno ambayo kijana akishindwa kuyazingatia wakati wa makuzi yake yanampelekea kija moja kwa moja kupoteza mwelekeo wake katika masha. Mambo hayo ni kama vile : kuto kuweka malengo sahihi katika maisha, Kufuata mkumbo,  tamaa mbaya,  na mtazamo hasi tuliyo nayo vichwani mwetu.  Hayo ni mambo baadhi ambayo kijana mwenyewe anaweza kujisabishia maisha yake kuharibika.
    Kutokuwa na malengo. Kati ya makosa makuu ambayo vijana wengi wanafanya ni kutokuwa na malengo katika maisha yao, na ni wazi yakwamba vijana wengi tumejikuta hatuna malengo sahihi katika maisha yetu ya kila siku, unakutana kijana mtaani amekaa magengeni kwanzia mwanzo wa siku hadi mwisho wa siku hana lolote. Kuwa na malengo ni jambo muhimu mno katiaka maisha ya kila mwanadamu na tambua yakwamba kila aliefanikiwa katika maisha alijiwekea malengo thabiti na akayafuatilia vilivyo kuhakikisha yanatimia. Kumbuka yakua malengo yanendana na ndoto ulizo nazo wewe kama kijana. Ili ndoto yako itimia ni lazima uwe na malengo. Sasa pale kijana anaposhindwa kuwa na malengo ya kweli ndipo anapojikuta akihangaika huku na kule bila mafanikio yeyote.  Ikumbukwe kuwa maisha ni vile unavyoishi  na wewe mwenyewe ndiye utakae hamua yakua maisha yako yawe mazuri au mabala “hatma ya maisha yako ipo mikononi mwako kijana”.
   Labda ni kwa nini kijana anashindwa kuwa na malengo hai katika maisha?
Mara nyingi kijana anakua na tamaa na vishawishi visivyokua na maana. Kama nlivyosema malengo yanawekwa kutokana na ndoto alizo nazo kijana sasa kama huna ndoto na msimamo yakwamba usimamie nini hasa katika maisha ili aweze kujikwamua katika hali ngumu yaki maisha. Tama za hapa na pale na kufuata mkumbo ni vitu ambavyo hupoteza ndoto za vijana wengi, inafika pahala kijana anakuwa anatamaini vitu vingine ambavyo vipo njee ya uwezo wake na kumpelekea kuachana na ndoto zake za mwanzoni na kujiingiza katika vitendo viovu ili kuvipata vitu hivyo.
Kutokuweza kufahamu thamani ya muda; Nipende kuchukua nukuu ya mtu mmoja aliye kuwa maarufu duniani kwa kupitia filamu na huyu sii mwingine ni BRUCE-LEE ambae aliwahi kusema “if you truly love life never play with time coz there is your life originate” vijana wengi tumekuwa tukijikuta tukipoteza muda katika mambo yasiyokuwa na tija katika maisha yetu. Jiulize huko kwenye mitandao yakijamii unapokuwa muda wote huo unafaidika vipi?  Ndio  yawezekana kuna kitu unafaidika nacho lakini kiuhalisia jambo hilo halikusaidii kukukwamua huko ulipo kama unvyotarajia. Kati ya mali tulizo nazo hapa duniani moja wapo ni Muda. Muda ukiutumia vizuri hakika utafanikisha malengo kwa wakati unao taka wewe lakini pindi ukiutumia vibaya hakika utajuta kwan muda ukisha kwenda haurudi nyuma kamwe.  Sasa nacho taka kusema hapa ni kwamba muda sio rafiki ndugu yangu.
    Kutokujiami kama tunaweza peke yetu: katika swala lakujiamini, nimekua nikiliona katika vijana tulio wengi yakua tunakua tukishindwa kujiamini kama peke yetu hatuwezi kabisa. Nipende kuwaambia vijana wenzangu kua tukiishi katika misingi yakutokujiamini tutakua tumeshindwa nakuanguka kimaisha. Unakuta mtu ana fursa katika jamii lakini kijana huyo anaogopa kuichukua fursa ile nauifanyia kazi ili iweze kumwokoa hapo alipo. Watu maarufu duniani waliziona fursa kati yao na wakajaribu na hatimae wakafikia kilele cha mafanikio. Ondoa dhana ya uoga na thubutu kufanya na nakuhakikishia utafikia lengo lango. Acha kujiona huna nguvu wala akili na ukifanya watu watakuonaje. We unadhani Mwalimu JK Nyerere angekua na uoga mbele ya wakoloni leo hii tungekua wapi? Ni mfano tuu ambao tunautoa kutoka kwa baba wa taifa Mwalimu JK Nyerere kwani aliionoa fursa yakudai uhuru wa Tanganyika ndipo akajaribu bila uoga na mwisho wa siku leo hii Tanzania tunatembea vifua mbele.
      Kukataa shule; Niliwahi kuulizwa swali na Mtu mmoja swali ambalo liliniumiza kichwa wakati nlipokua natafuta jibu lake na swali hilo ni “do you think education is certificate in your life?” nikuachie nami hili swali ujibu mwenyewe lakini sintokupatia jibu nlililomjibu mtu Yule. Nipende kuambia kijana mwenzangu ambaye una kataa shule katika dunia ya leo tuna kufananisha na kipofu. Leo hii nani atakuajiri kama hauna elimu? Ndio unaweza kwa namna moja ama nyingine ukajiajiri lakini ukweli ni kwamba hata kujiari kunahitaji elimu. Ubongo wa mwanadamu una ujazo wa lita moja na nusu lakini kalamu na karatasi vina weza kuujaza ubongo huo kwa muda mchache mmno. Nakushangaa sana kwani hata maandiko ya MUNGU yametuambia “mshike sana elimu usimwache aende zake maana yeye ndiye mkombozi wa maisha yako”  ni maandiko yakutoka katika vitabu takatifu na sio maneno yangu mimi Mtokambali. Nipende kukuambia kijana mwenzangu Elimu iwe msingi wa maendeleo yako wewe kijana.
          Hayo niliyo yasema hapo juu ni baadhi tuu ya  mambo ambayo yanaweza kukufanya wewe kijan kuharibu maisha yako kwa ujumla. Nakuahidi katika mwendelezo wa makala hii katika mfululizo wa makala zetu hapa MTOKA MBALI nitakuelezea mambo zaidi yatakayoweza kukuangusha wewe kijana katika maisha yako na jinsi gani utaweza kujikwamua kaitika hayo mambo na kutoka katika UTUMWA wa fikra.
Nipende kukushukuru wewe ulie chukua muda wako ulio wa thamani na kusoma makala hii. Nina amini umepata kitu hapo. Nikusihi kaa hapa hapa kwa vitu moto moto.

Makala hii imeandikwa na FRANCI S MAWERE Kwa udhamini wa MAWERE MEDIA GROUP  Limited (MMGLtd),Kwa mawasiliano nasi tafadhaili piga simu namba 0767322193, au tutumie  barua pepe  mtokambali2015@gmail.com.

Aliyekuwa mchezaji NBA Lamar Odom, apatikana amezirai katika danguro

OdomAliyekuwa mchezaji wa mpira wa vikapu nchini Marekani Lamar Odom anatibiwa hospitalini baada ya kupatikana amezirai katika danguro mjini Nevada ,kulingana na mamlaka. Maafisa wa polisi waliitwa katika danguro la Love Ranch huko Crystal mjini Nevada baada ya kupatikana akiwa hana fahamu siku ya jumanne.

M'marekani huyo alibebwa na gari na kupelekwa hadi hospitalini kwa kuwa alikuwa mrefu mno kubebwa katika ndege. Bwana Odom mwenye umri wa miaka 35 amezichezea Miami,Dallas na Los Angeles Lakers pamoja na Clippers.

Pia aliichezea Marekani katika michezo ya Olimpiki ya mwaka 2004 na kushinda medali ya shaba.
Ugonjwa wake haujulikani lakini wasamaria wema walituma ujumbe wao kwa mtandao wa twitter baada ya habari hizo kusambaa.

Bwana Odom ambaye alikuwa amemuoa nyota wa kipindi cha Keeping up with the Kardashians, Khloe Kardashian amekuwa mnywaji mkubwa wa pombe na dawa za kulevya.

Alihusishwa na kuendesha gari akiwa mlevi mwaka 2013 na kupigwa marufuku katika shirikisho la mchezo wa mpira wa vikapu nchini Marekani NBA kwa kukiuka sheria dhidi ya dawa za kulevya ya mwaka 2000.

Odom na Kardashian waliowana mwaka 2009 katika sherehe ambayo ilionyeshwa katika kipindi cha runinga ya Marekani E.

Walitalakiana mwaka 2013.Odom alishinda ubingwa wa NBA akiwa na klabu ya Lakers mwaka 2009 na 2010 na alitajwa kuwa mchezaji wa sita bora mwaka 2011. Mara ya mwisho kucheza katika NBA ni mwaka 2013 alipokuwa akiichezea Clippers.

Huu hapa mtizamo wa T.I kuhusu mgombea Urais wa Marekani, Hillary Clinton


CEO kutoka kwenye lebo ya Hustle Gang T.I ameingia kwenye headlines baada interview yake na Dj Whoo Kid kwenye moja ya radio nchini Marekani… akiwa kwenye interview hiyo T.I alizungumzia mipango yake ya kufanya collabo na Usher Raymond, Young Thug na B.O.B pia alizungumzia changamoto alizokumbana nazo kwenye kufanya kazi na rapper Travis Scott.
TIPP3
Baada ya kutumia dakika 12 kuongelea vitu vyote hivyo T.I akaulizwa swali linalohusiana na hali ya Siasa sasa hivi nchini Marekani haswa wagombea nafasi ya Urais nchini humo wakiwemo Donald Trump na Hillary Clinton ambae mume wake Bill Clinton alishawahi kuwa Rais wa Marekani pia…
>>> ” Sio kwamba nina ubaguzi wa kijinsia ama nini ila kusema kweli siwezi kumchagua mwanamke kuwa kiongozi wa nchi ya Marekani… kwa sababu nawajua wanawake na mara nyingi wanafanya maamuzi yasiokuwa ya msingi kwa kufuata mioyo na hisia zao. Huwa wanafanya maamuzi ya mambo mazito kwa vile wanavyojisikia wakati huo alafu badaae wanasema hawakudhamiria kufanya maamuzi hayo… nisingependa kumchagua mwanamke alafu aje kufanya haya..” <<< T.I.
Baada ya interview hii T.I alishambuliwa na watu mbalimbali wengi wakimuuita mbaguzi wa jinsia, wengine wakisema anachukia wanawake… kila mtu alisema lake!
TIPP

Magufuli azungumzia samaki, Lowassa ageukia madini


Magufuli azungumzia samaki.

Mgombea wa urais kupitia Chama Cha mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema akiwa rais ataendelea kukamata meli za kigeni zinazovua samaki kwenye bahari ya Tanzania kinyume cha sheria kama alivyowahi kufanya akiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi.

Alisema hatakubali kuona samaki wa Tanzania wanageuzwa shamba la bibi, hivyo samaki watakaokamatwa kwenye meli zinazovua kiholela watagawiwa kwa wananchi kama kitoweo. Dk. Magufuli alisema hayo kwenye mikutano yake ya kampeni katika majimbo ya Mchinga na Kilwa Kusini mkoani Lindi na pia Kibiti mkoani Pwani.

Mgombea huyo alisema kuna watu wanamchonganisha na wavuvi kwa kudai kwamba akiingia madarakani atachoma nyavu zao na hawatakuwa na fursa za kuendesha shughuli zao.

Alisema yeye atakuwa rafiki mkubwa wa wavuvi wadogo na atawawezesha kwa mikopo na zana bora za uvuvi ili wavue kisasa na kuondokana na umaskini. Alisema atapambana na meli kubwa za uvuvi ambazo zimekuwa zikiiba samaki ambao ni mali ya Watanzania.

Sitaruhusu samaki walio kwenye bahari yetu wawe shamba la bibi. Wanaojijua kuwa wanaiba samaki wetu arobaini zao zimefika, mimi nitakamata na kugawa bure kwa wananchi, maana samaki ni mali yao…. kama niliweza kufanya hivyo nikiwa waziri wa kitoweo, siwezi kushindwa nikiwa rais,” alisema.

Lowassa ageukia madini

Mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, amesema iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25 atahakikisha mikataba yote mibovu ya madini inapitiwa upya ili kujenga uchumi imara kwa manufaa ya taifa.
 
Lowassa ambaye alishaahidi kuifumua pia mikataba ya mafuta na gesi wakati akiwa mkoani Mtwara, aliyasema hayo jana kwenye mwendelezo wa mikutano yake ya kampeni katika kata ya Katoro, Jimbo la Busanda mkoani Geita.
Iwapo nitashinda na kuwa rais, nitahakikisha mikataba mibovu ya madini na gesi inapitiwa tena ili kulinufaisha taifa,” alisema na kushangiliwa na maelfu ya watu waliojitokeza kwenye mkutano huo.
 
Mgombea huyo anayeungwa mkono pia na vyama vingine vinavyounda muungano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), alisema mbali na kupitia mikataba ya madini na gesi, pia atahakikisha kuwa anaibadili Tanzania na kulikabili kwa ukamilifu tatizo la umaskini linalowakabili mamilioni ya wananchi. 
 
Kadhalika, alisema serikali atakayoiongoza itaboresha elimu na kilimo, ikiwa ni njia mojawapo ya kuwakwamua Watanzania kutoka kwenye lindi la umaskini.
-Nipashe

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...