26 October, 2016

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthibitisha manunuzi yake. 

Taarifa iliyotolewa jana na SEEA ilisema urejeshaji wa fedha baada ya kuthibitika kwa manunuzi ni moja ya njia mbili za nafuu kwa wateja wa Samsung Note 7.

 Mbali na urejeshaji fedha, SEEA imesema katika taarifa yake, wateja wenye simu za Samsung Note 7 wanaweza pia kuamua kuzibadilisha na kupatiwa simu mpya za Galaxy S7 au Galaxy S7 Edge, au Galaxy Note 5, pamoja na chenji itokanayo na tofauti ya bei.

SEEA imesema katika taarifa yake kuwa inafahamu kwamba simu za Note 7 zilikuwa hazijaanza kuuzwa katika soko la nyumbani, lakini kwa kuwa imeweka mbele usalama wa wateja wake ipo tayari kuchukua jukumu hilo.

Note 7 zimegundulika kuwa na tatizo katika betri ya simu hiyo ambayo husababisha kulipuka, lakini hata baada ya kubadilishwa baadhi ya wateja waliopata simu za toleo la pili pia wameelezea kuwapo kwa tatizo hilo pia.

SEEA imesema ofa yake ni kwa wateja wa aina zote mbili, walionunua mara ya kwanza katika msoko nje ya Afrika Mashariki na wanaomiliki Note 7 baada ya kubadilishiwa walizonunua mara ya kwanza.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...