26 October, 2016

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthibitisha manunuzi yake. 

Taarifa iliyotolewa jana na SEEA ilisema urejeshaji wa fedha baada ya kuthibitika kwa manunuzi ni moja ya njia mbili za nafuu kwa wateja wa Samsung Note 7.

 Mbali na urejeshaji fedha, SEEA imesema katika taarifa yake, wateja wenye simu za Samsung Note 7 wanaweza pia kuamua kuzibadilisha na kupatiwa simu mpya za Galaxy S7 au Galaxy S7 Edge, au Galaxy Note 5, pamoja na chenji itokanayo na tofauti ya bei.

SEEA imesema katika taarifa yake kuwa inafahamu kwamba simu za Note 7 zilikuwa hazijaanza kuuzwa katika soko la nyumbani, lakini kwa kuwa imeweka mbele usalama wa wateja wake ipo tayari kuchukua jukumu hilo.

Note 7 zimegundulika kuwa na tatizo katika betri ya simu hiyo ambayo husababisha kulipuka, lakini hata baada ya kubadilishwa baadhi ya wateja waliopata simu za toleo la pili pia wameelezea kuwapo kwa tatizo hilo pia.

SEEA imesema ofa yake ni kwa wateja wa aina zote mbili, walionunua mara ya kwanza katika msoko nje ya Afrika Mashariki na wanaomiliki Note 7 baada ya kubadilishiwa walizonunua mara ya kwanza.

Video mpya ya Taylor Gang Ft Wiz Khalifa na Tuki Carter ‘Sleep At Night’.

Wiz Khalifa na kundi lake la Taylor Gang wametoa video ya wimbo wao mpya “Sleep at Night” kutoka kwenye album ya TGOD Volume 1. yenye nyimbo 23 ikiwa na wasanii kama Ty Dolla $ign, Juicy J, Berner, Chevy Woods, na Raven Felix.

Aliyekuwa beki wa Brazil Carlos Alberto afariki

Aliyekuwa mchezaji mashuhuri wa timu ya Brazil Carlos Alberto ,ambaye alikuwa nahodha wa kikosi kilichoshinda kombe la dunia mwaka 1970 amefariki akiwa na umri wa mika 72.

Alifunga mojawapo ya mabao mazuri zaidi duniani katika historia ya kombe la dunia katika mechi ya fainali dhidi ya Italy mwaka 1970,baada ya kuwachenga mabeki na kufunga kupitia mkwaju mkali.

Beki wa kulia Alberto alichezeshwa mara 53 na Brazil na kushinda mataji ya nyumbani dhidi ya Fluminense na Santos ambapo alishiriki mara 400.
Alifariki mjini Rio de Janeiro kufuatia mshtuko wa moyo.

Gambia kujiondoa katika mahakama ya uhalifu ICC

Serikali ya Gambia imesema kuwa itajiondoa kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC mara moja.
Hatua hiyo imekuja kutokana na madai kuwa ICC hushughulika na Waafrika pekee.


Maamuzi ya kujitoa katika mahakama hiyo yanafuatia baada ya Burundi na Afrika ya Kusini kutangaza kujiondoa
Rais wa nchi hiyo Yahya Jammeh amekua madarakani tangu mapinduzi nchini humo mwaka 1994.

Uchaguzi ujao unatarajiwa kufanyika desemba lakini mapema mwaka huu viongozi nane wa upinzani walikamatwa na kuhumiwa miaka mitatu jela kwa kuhusika katika maandamano ambayo hayakua na kibali.
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty limesema kuwa maamuzi hayo ni sehemu ya muendelezo wa ukandamizaji wa haki za binadamu nchini Gambia.

Mkongo amvuruga Kadjanito, abadili na dini

Msanii wa Bongo fleva Khadija Said Maige maarufu kama Kadjanito amefunguka na kusema kuwa amepagawa na mapenzi ya Tresor Lisimo mchezaji wa mpira ambaye ndiye anataka kufunga naye ndoa tarehe 29 mwezi wa 10 mwaka huu. 

Kadjanito kupitia kipindi cha eNewz kinachorushwa na kituo cha Tv EATV anasema aliona amekaa peke yake kwa muda mrefu hivyo ameamua kuwa mke wa mtu ili na yeye awe mwanamke aliyekamilika sababu amempata mtu anayependana naye na mtu ambaye wanaelewana.

"Nimeamua kufunga ndoa kwani nilikaa muda mrefu peke yangu nikatafakari nikaona siyo kitu kizuri nikiwa kama msichana ambaye nina 'Inspire' watu wengi lazima kuna vitu nifanye ili niwe mwanamke kamili, maana ukiwa peke yako mtu anaweza kukuchukulia labda huyu mtu muhuni lakini mimi nimeamua kuwa mke wa mtu, najua ni kitu kikubwa lakini haitanifanya mimi niache kazi zangu za muziki"

Ameendelea kusema "Nimeamua kufunga ndoa sababu nimeona nimepata mtu ambaye tunapendana, ninaendana naye na ninampenda sana. Aisee mimi nafunga ndoa ya Kikristu yaani jamaa nimemzimia mpaka nimeamua kumfuata katika imani yake, kiukweli ninamfuata" alisema Kadjanito

25 October, 2016

Mmiliki wa Mtandao wa Wikileaks afariki Dunia

Mwanzilishi wa mtandao maarufu wa Wikileaks, Gavin MacFadyen (76) amekutwa amefariki Jumamosi ambapo  chanzo cha kifo chake bado hakijajulikana.

Mtandao wa Wikileaks umekuwa ukiibua mambo mbalimbali ya siri ya mgombea  urais wa Marekani, Hillary Clinton. 

Wengi hawajayaamini kifo chake ambacho kimewastua na kuumiza mioyo ya watu wengi hasa pale wanapomkumbuka marehemu kama mwanzilishi wa kituo cha habari za uchunguzi (Centre for Investigative Journalism) mwaka  2003 ambapo wanahabari wengi wakubwa duniani wamejifunza hapo.

List ya Wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji Bora wa Dunia

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limetangaza majina ya wachezaji 30 ambao wanataraji kuwania tuzo ya Mchezaji Bora wa Dunia kwa mwaka 2016 maarufu kama Ballon d’Or.

Majina ya wachezaji ambao wanawania tuzo hiyo kwa mwaka huu imeongezeka kutoka 23 hadi 30 na Disemba 13 yatatangazwa majina ya wachezaji watatu ambao wataingia katika kinyang’anyiro kwa kupigiwa kura na mshindi kupatikana.

Wachezaji 30 ambao wametajwa kuwania Ballon d’Or 2016 ni kama Ifuatavyo
Sergio Aguero (Manchester City), 

Pierre-Emerick Aubameyang (Borussia Dortmund), 
Gareth Bale (Real Madrid), 

Gianluigi Buffon (Juventus),

Cristiano Ronaldo (Real Madrid), 

Kevin De Bruyne (Manchester City), 

Paulo Dybala (Juventus),

Diego Godin (Atletico Madrid),

 Antoine Griezmann (Atletico Madrid), 

Gonzalo Higuain (Juventus),

Zlatan Ibrahimovic (Manchester United), 

Andres Iniesta (Barcelona),

Koke (Atletico Madrid),

 Toni Kroos (Real Madrid),

Robert Lewandowski (Bayern Munich).

Music: PHARRELL – ‘RUNNIN”

Pharrell Williams ameachia ngoma mpya ambayo itatumika katika movie ya  Hidden Figures, ndani ya wimbo huo Pharrell amezungumzia juu ya wanawake na haki zao.

New Video: Qboy ft Rayvanny & Shetta – Mugacherere [Official Music Video]

Stylist wa mkali wa Bongo Fleva, Diamond na kutoka kambi ya WCB, Q boy ameachia video ya single yake mpya ‘Mugacherere’ aliyowashirikisha Ray Vanny na Shetta.

Pluijm: Mzambia kuinoa Yanga?

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mholanzi Hans van der Pluijm,amesikitishwa na kitendo cha uongozi wa klabu kuleta kocha mpya, Mzambia George Lwandamina, bila kumtaarifu, akisema "huko ni kunivunjia heshima".


 Pluijm alisema alipaswa kutaarifiwa na uongozi juu ya jambo lolote kuhusu nafasi yake kazini, lakini cha ajabu anajua kupitia vyombo vya habari.
“Sijaambiwa chochote. Uongozi umenivunjia heshima sana, kwa klabu kama Yanga hawakupaswa kufanya hivyo,”alisema Pluijm.
Pamoja na hayo, Pluijm amesema anasubiri kukutana na uongozi wa klabu kujua mustakabali wake rasmi na baada ya hapo atakuwa na ya kuongea zaidi. “Labda nitachukua hatua ya kupumzika kwanza kabla ya kuamua mustakabali mpya,”alisema.  

Aidha, kuhusu uwezekano wa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi, Pluijm alisema:“Sipendelei sana hiyo kazi. Nataka kufanya kazi na wachezaji kila siku kwa matakwa ya moyo wangu. Ila nitakwenda kuwasikiliza, tunaweza kuafikiana kwa lolote, ikiwamo kubaki kama Mkurugenzi wa Ufundi,” alisema.

Pluijm pia akagusia maandalizi ya mchezo ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya JKT Ruvu kesho akisema wachezaji wake wote wapo fiti kuelekea mechi hiyo na hana majeruhi.

Yanga imerejea jana kutoka Mwanza, ilikopita ikitokea Bukoba mkoani Kagera ambako Jumamosi ilishinda 6-2 dhidi ya wenyeji Kagera Sugar katika mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

 Uongozi wa Yanga unataka kumuondoa Pluijm na wasaidizi wake wote, Juma Mwambusi, kocha wa makipa Juma Pondamali na Meneja Hafidh Saleh na kumpa nafasi Mzambia Lwandamina atakayekuwa Kocha Mkuu, akisaidiwa na Boniface Mkwasa, Manyika Peter kocha wa makipa na Meneja, Sekilojo Chambua.

CHANZO: Nipashe

Sipendi 'bifu' na msanii yeyote - Joh Makini

Msanii wa miondoko ya Hip Hop nchini Joh Makini amesema katika vitu ambavyo hapendi kwenye kazi zake za kisanii ni kuwa na 'bifu' na msanii mwenzake katika tasnia ya sanaa nchini.
Makini ameyasema hayo alipokuwa akijibu maswali ya wapenzi wa muziki wa Bongo Fleva waliokusanyika kushuhudia program maalumu ya Kamatia Kitaa katika  kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio.
“Sipendi kuwa na bifu na msanii yeyote , mimi naamini katika muziki wangu na kuheshimu kila mmoja katika kazi yake” Amesema Makini
Aidha Makini ameongeza kuwa katika mambo ambayo humuumiza sana ni kuona kazi za wasanii zikiwa zimezagaa mtaani na kuuzwa bila wasanii kunufaika na chochote.
“Jambo hili inabidi serikali iingilie kati kwa sababu ugumu wa maisha mtaani umefanya vijana kuanza  kudurufu kazi zetu na kuziuza bila sisi kunufaika na chochote na jambo hili linatokana na jamii kutokuwa na elimu ya kutosha “ Amesema Joh Makini.

Pamoja na hayo Makini amewataka mashabiki kuendelea kuwaunga mkono kwani kundi la weusi limejipanga vyema katika kutoa burudani ya uhakika kwa mashabiki.

CHANZO: eatv.tv

Kelele zamuondoa Justin Bieber jukwaani kwa hasira

Justin Bieber aliondoka katika jukwaa la tamasha yake mjini Manchester baada ya kuwataka mashabiki kutopiga kelele wakati anapoimba.

Wakati wa tamasha zake tatu zilizopita katika mji huo ikiwa miongoni mwa ziara yake ya dunia nzima mwanamuziki huyo alisema : Nathamini msaada ninaopata, nathamini mapenzi munayonipa na nathamini ukarimu wenu.Lakini kelele munazopiga wakati ninapoimba lazima zisitishwe.Tafadhali na ahsanteni.Sidhani ni muhimu ninapojaribu kusema kitu na nyinyi munapiga kelele.

Na mashabiki hao walipokataa kusitisha kelele zao aliangusha kipaza sauti na kuondoka katika jukwaa,huku baadhi ya mashabiki wakimzoma.
Baadaye kijana huyo wa miaka 22 alirudi kuendelea na tamasha yake na kuelezea kwa nini aliondoka kwa hasira.

''Nahisi kwamba nataka wasiliana nanyi.Lengo hapa ni ninapowaangalia katika macho ,munajua kwamba tuko katika wakati muhimu na kwamba tunawasiliana''.

Utafiti: Betri zinazotumiwa katika simu zina sumu

Zaidi ya gesi 100 zinazoweza kusababisha kifo hutolewa na betri zinazopatikana miongoni mwa mabilioni ya vifaa vinavyotumiwa na raia wengi duniani kama vile simu aina ya smartphone na vipatakilishi kulingana na utafiti mpya.


Utafiti huo ulibaini gesi 100 zenye sumu zinazotolewa na betri za Lithium, ikiwemo ile ya kaboni monoksaidi, ambayo inaweza kusababisha kujikuna katika ngozi, macho na pua mbali na kuathiri mazingira.

Watafiti kutoka taasisi ya ulinzi ya NBC nchini Marekani pamoja na chuo kikuu cha Tsinghua nchini China wamesema kuwa watu wengi huenda hawajui hatari ya betri kupata moto, kuharibika ama kutumia chaji isiofaa katika vifaa hivyo, jarida la Science Explorer limeripoti.

Katika utafiti huo mpya,walichunguza betri moja ya kuchaji inayojulikana kama Lithium-ion,ambayo huwekwa katika vifaa vinavyotumika kila mwaka.

''Siku hizi,Betri za Lithium-ion hukuzwa na serikali nyingi duniani kama kawi inayopatikana kwa haraka ili kuviwasha vifaa vyote ikiwemo magari ya kielektroniki hadi simu," alisema Jie Sun, profesa mkuu katika taasisi ya ulinzi ya NBC.

Sun na wenzake waligundua sababu kadhaa ambazo zinaweza kuongeza gesi zenye sumu zinazotolewa.
Betri zilizopata chaji zaidi hutoa gesi zaidi za sumu ikilinganishwa na betri ilio na asilimia 50 ya chaji.

CHANZO: BBC.

24 October, 2016

Beki wa Manchester United Eric Bailly aumia vibaya

Beki wa Manchester United anayetoka Ivory Coast Eric Bailly alipata jeraha mbaya ya goti wakati wa mechi ambayo timu yake ililazwa 4-0 na Chelsea Jumapili.

Mchezaji huyo wa miaka 22 aliumia baada ya kukabiliana na Eden Hazard wa Chelsea.
ALiondolewa uwanjani dakika ya 52.

"Nina wasiwasi kwamba ni jeraha mbaya," meneja wa United Jose Mourinho alisema. "Ameumia kwenye goti, eneo lenye kano. Anahisi kwamba ni jeraha mbaya sana."

Bailly alikuwa amechezea United mechi zote walizocheza msimu huu ligini.
Alijiunga nao kutoka klabu ya Villarreal ya Uhispania kwa £30m kabla ya kuanza kwa msimu.

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...